Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, May 17, 2012

Hujafa hujaumbika-37



Kesi ya Jangiri kama muuaji ilikuwa ya aina yake, maana kama ilivyotarajiwa huyu jamaa alikataa makosa yote ni kudai kuwa alitamka kuwa ndiye aliyemuua Kimwana kwasababu ya mateso na shinikizo la polisi, alifikia hadi kuonyesha alama za vidondoa eti vilivyotokana na mateso hayo, sijui aliteswa saa ngapi,…

Mara kwa mara wakili mwanadada alifika kwenye hiyo kesi na wakati mwingine alimuachia msaidizi wake,huku akiwa katika uchunguzi wake binafsi, alikuwa na mambo mengi ya kufuatilia, kiasi kwamba aliona muda haumtoshi, na leo akiwa ndani ya hii kesi, akapokea simu toka kwa mmoja wa wafanyakazi wake

‘Nipo mahakamani unasemaje?’ akauliza.

‘Kuna mtu kaleta barua hapa, na anasema hiyo barua ni ya muhimu sana, anataka wewe mwenyewe uipokee…ndani yake kuna mkanda wa CD’s,umeandikwa `confidential…’ na huyo mletaji anasema anahitaji jibu la harakakutoka kwako…’akasema.

‘Usiufungue huo mzigo, au huo mkanda ,inawezekana ikawa ni bomu, …nakuja…’akamsogelea msaidizi wake kwenye hiyo kesi na kkumnong’oneza jambo, rafiki yake akakunja uso, hakupenda abakie peke yake, lakini aliona hilo jambo alilokuja nalo rafiki yake ni la muhimu ….akakubali aondoke, nakesi ikaendelea,

Alipofika ofisini kwake,akaichukua ile barua na kuiangali kwa makini, akaichukua ile CD’s , na kuiweka kwenye mashine ya kuikagua na kugundua kuwa haina hatari, akaichukua na kuingia ndani ya chumba chake cha siri, na kuiangalia…halafu akamwambia huyo aliyeileta kuwa anaifanyia kazi,...

*****
Mkuu mimi nataka nionane na huyo mshitakiwa, faragha, bila ya kuwepo wakili wake, ….’akasema wakili mwanadada.

‘Kwanini, siunajau sheri zilivyo….’akasema mkuu.

‘Najua lakini wakati mwingine inabidi ufanye hivyo, ili kuweza kufanikisha sheria inayotaka kukiukwa…’akasema.

‘Kwani kuna nini umegundua…?’ akauliza mkuu.

‘Hayo ni maswala ya kimahakama, na mbinu za kisheria, kuna kitu nataka kuhakiki…nikifanikiwa nitakuja kukuambia, wewe jitahidi nionane na huyo mtu kwa faragha…’akasema na kuondoka.
Ilikuwa usiku na wakili mwanadada akaweza kukutansihwa na Jangiri, akamwangali kwa makini kabla hajamuuliza swali, nia ni kutaka kumjua hulka yake, kila mtu na hulka yake, ukiijulia unaweza ukamsoma na hata kumgundua kuwa anasema ukweli au uwongo,…

‘Mimi naamini kuwa kweli wewe sio uliyemuua Kimwana…’akasema na kumfanya Jangiri ashikwe na mshangao,akasema;

‘Wewe dada mjanja sana, ndani ya mahakama umekuwa ukinishinikiza mimi kuwa ndiye muuaji naua wanawake wasio na hatia…sasa unakuja na mbinu yako hii….hunipati ng’ooo, sawa mimi sio muujaji nimeshasema huko mahakamani sasa unataka nini kwangu…’akasema.

‘Ndio maana nataka ushirikiano wako, kama wewe sio muujai ni nanii aliyemuua Kimwana…nilikipaya fununu kutoka kwako, tutaweza kumshika huyo muuaji, nikuulize swali, wewe na kimwana mlijuana toka lini, ..’akauliza.

‘Hayakuhusu hayo , kama uantaak nijibu lolote, kwanza namuhitaji wakili wangu,….’akasema na kumwangali huyo wakili kwa mashaka.

‘Sikiliza nikuambia, …mimi napenda sana kuwa mkweli , na mtu mkweli kwangu ni rafiki mwema, na nikikuahidi kuwa nitakusadia, ujue kweli nitafanya hivyo…nataka nikusaidie, lakini pia nataka haki ikitendeke, ili tumjue aliyemuua Kimwana,….kwa uchunguzi wangu, ile risasi ilitoka kwenya bastola yako sio hiyo iliyomuua Kimwana….lakini kuna ujanja umetumika na huo ukweli umefutika,lakini kwa kupata maeezo kutoka kwako naweza kuufichua…’akasema wakili.

‘Una uhakika na hilo…..?’ akauliza Jangiri.

‘Nina uhakika ndio maana nikatafuta njia za kuongea na wewe, ili nipate maelezoo yatakayoniwezesha kulinda hoja ayangu….ukishirikiana na mimi, kesi ya mauaji juu yako itafutika,…siwezi kukuahidi makosa mengine, lakini hilo la mauaji ninaweza kukuahdi,ikiwa utaniambai ukweli….’akasema wakili.

‘Ukweli upi unaotaka kutoka kwangu…?’ akauliza.

‘Kwanza niambia jinsi gani ulivyomjua Kimwana….kama kweli ulivyodai kuwa ulikuwa ukipenda na isingelikwua rahis kwako kumuua…?’ akauliza, na yule jamaa alikaaa kwa muda kifikiria,akasema baadaye.

‘Ina maana kesi ya mauaji ianweza ikafutwa, na huenda kama nikufungwa sitafungwa kwa kesi ya mauaji na kweli sio mimi niliyemuua Kimwana…ni nani basi kafanya hivyo…inawezekanakabisa,nakumbuka vyema….’akatulia.

‘Hebu kumbuka vyema,….lakini kwanza niambia ulivyomjua Kimwana…?’akasema wakili.

‘Kimwana ni bosi wangu, lakini kabla ya kuwa bosi wangu, ….alikuwa rafiki yangu..’akatulia na kuwa kama anakumbuka jambo,…na baadaye ndio akaanza kuhadthia maisha yake na Kimwana…

*******

`Kimwana alikuwa rafiki yangu toka zamani sana, naweza kukiri mimi ndiye mwanaume wa kwanza kumjua, …na huenda naweza kukiri kuwa mimi ndiye niliyemuharibu. Nasema hivyo kwasababu, nyingi tu, achilia mbali kumuingiza mjini.

`Kipindi narudi nyumbani nikiwa na pesa za kumwanga kutoka na madili yetu ya hapa na pale, nilikutana na huyo msichana akiwa antokea shule, nikampla lifti , kipindi hicho nilikuwa na gari, maana pesa ilikuwa hainichezi mbali, nikamtamani huyu binti, licha ya kuwa alionekana mdogo,lakini alishakuwa msichana aliyevunja ungo.

`Nikaanza kumtongoza, na unavyojua wasichana wa kijijini, wanajifanay hawapendi kumbe wanapenda, na kumba huyo binti alishakuwa na hisi hizo zakimapenzi, labda kutokana na makundi rika au aliwahi kusimuliwa au kufundwa, kwahiyo hata nilipokuwa nikiongea naye, alionekana kujihami kikubwa….’akasema Jangiri.

‘Hata hivyo kumbe sifa zangu zilikuwa mdomoni mwa kila msichana, siku ya pili yake nilipomtamkia kuwa nampenda na nipo tayari kumpa chochote anchotaka ,akaniambai kwua na yeye ananipenda, ila yeye anachotaka ni mimi nimchkuea tukaishii naye mjini,kwani masiha ya kijijini hayataki…nikaona mambo sio ndiyo hayo.

Tukasuka mpango,nikamtorosha huyo binti na kuja naye mjini,…kipindi hicho niliwahi hata kuwekwa ndani kwa ajili yake, maana wazazii wake walikuja kugundua kuwa mimi ndiye nilimyemtorosha wakanitumia maaskari, nikakamatwa na kuwekwa ndani.

Nilikaa siku tatu, na aliyewezesha mimi kutoka na huyo huyo binti,aliwaendea polisi na kuwaambia kuwa mimi ni mchumba wake, na hakunitosroha yeey, ila yeey ndiye alitoroka an kuja kwangu, kwahiyo kam ni kumshika wamshike yeye,…

Wazazi walikuja juu kweli, lakini Kimwana alikuwa kazimia kwangu, akawa hawajali wazazi wake, na kuwaambia kuwa hataniacha mimi kamwe kwasababu keshanipenda na huko kijijini harudi. Basiwazazi wangefanya nini, ikabidi wakubali shingo upande.

Nikawa naishi na huyu binti, lakini taarifa zangu zilifika hukoo kijijini kuwa mimii nafanya shughuli za kijamabzi, kwahiyo binti yao atapotea, na wakaja kunifuata kuwa wanamtaka binti yao kwasababu mimi ni jamabzi, nikawahamaki,nilihamaki kweli na Kimwana naye akinisadia na hata akawafukuza wazazi wake na kuwambai kuwa wasimfuate fuate kuhusu maisha yake….na ikawa mwishoo wa wazazi wake kumfuatilia.

Maisha yana kkupnda na kushuka, ikafikia mahli sina pesa, na dili hazipatikani, nikaona sas nitaumbuka na Kimwana ni mtu wa amtumizi, alikuwa mrembo, kama ulivyomuona na kila mwanaume alikuwa akimtaka, kwahiyo ilibidi niwe natumia ikiukweli,…sasa nikawa sina kazi ya maana nikawa sina pesa na kimwana akaniambai moja kwa moja kuwa yeye alinipednea kwasabbu yapesa, sina pesa, kwahiyo …

‘Ina maana alikuwa hakupendi ,alikuwa akipedna pesa zako tu….?’ Wakili akimuuliza.

‘Ndivyo ilivyokuwa,na kiukweli Kimwana hana habari na mapenzi haya ya kupenda eti, nakupenda kimoyoni, yeye anapenda matumizi, labda  niseme mpenzi wake ni pesa, kama huna pesa huna matumizii huna nfasi kwa huyo binti…’akaseam jangiri.

Basi nikaona nitamkosa, lakini nikabuni mbinu,, nikaoan kwa ajili ya urembo wake. Lazima nimtumie,nikamawambi nipo tayari kumuachie ajirushe na wanauem wengine,ilimradi tuapete pesa, lakini tufanye mbinu za kuishi, nikamsuka mapaka akakubali, tukaanza kazi ya kurubuni wanaume wa watu wenye pesa,…’

‘Kwa vipi….?’akauliza wakili.

‘Yeye kwasaabbu ya urembo wake, wapo matajiri waliokuwa wakimtaka, na hawo matajiri walikuwa na ndoa zao,tulichokuwa tukifanya ni yeye kukubali kwenda nao nyumba za wageni, na mimi nakuja baadaye nikiwa na cheti cha ndoa kuonyesha kuwa huyo ni mke wangu, na tunamshikilia huyo tajiri kuwa asipotupa kiasi fulani cha pesa tuankwenda kutoa taarifa polis na kwamkewake,….wengi walikuwa wakitoa pesanyingi tu, wengine walikuwa wakigoma…

Siku moja nikakutana na mama mmoja ,alikuwa akiendesha gari lakifahari, nikavutiwa nalo, mwanzoni nilitaka nifanye mpango na washikaji tuliibe, lakini siku ya pili yake nikakutana na huyo mwanamke akaniita na kuniambai kutokana na mwili wangu anaona nitafaa kuwa mlinzi wake, lakini kwanza anatka anaifundishe jinsi gani ya kuwa mlinzi….nikakubali na kwelii nikapitia chuo cha mafunzo ya ulizni ,kutumi asilaha,nilikuwa najua kutumia silaha kabla,lakini hapo nilifundishwa kutumiasilaha ya aian yoyote, silaha jisni ilivyo, na uliznii wa hali ya juu.

‘Basi nikatulia an huyu tajiri mwanamke, na kumwambia Kimwana kuwa sasa nimepta kazi, atulie nyumbani, haat hivyo pesa niliyokuwa nikipta ilikuwa haitoshi, ikawa tunafananya dili zetu hizo hizo na siku moja huyu tajiri yangu akaniuliza Kimana ni nani wangu,..

‘Yule ni mpenzi wangu, kani vipi?’nikasema.

‘Nahitaji kufungua chuo cha warembo, na yeye namuona ni mrembo kweli, unaweza kumshawishi ajae kwenye hicho chuo,….’akaniamabii na mimi nikamwambai ahkuna shida, nikamwambia Kimana licha ya kwa mwanzoni aliktaa, lakini baadaye akakubali na ikawa mwanzo wa yeye kujuana na mama Docta.

Akiwa na mama Docta akapanda chati,nakuanza kunsiahau mimi,lakini sikujali, maana kazi ninayo, na kama ni wanawake nikiataka Napata,lakini kiukweli Kimwana nilipenda sana, na hata nikaja kumtamkia kuwa nataka nimuoe, alicheka sana sikuu hiyo….

‘Lakini mbona nasikia alikuwa lkiolewa na wanuem wengi, au ndio hiyo kazi aliyokuwa kapewa na huyu mama Docta.?’ Akauliza wakili.

‘Kimwana sio mke wa kuweka ndani, mtu amabye angeliweza kuishi naye na kuelewana naye, ni mimi peke yake, maaan namjua toka utotoni, najua nini anachokitaka, na tabia zetu zinaendena wengina wote waliomuoan zilikuwa ndoa  za kibiashara tu…hilo ninauhakika nalo…ila alipokuja kuolewa na huyo mwanaume,…nani huyu Msomali, pale niliona mabadiliko, inaonekana alimpenda kiukweli…lakini hata hivyo hata kama alimpenda kiukweli, badi alikuwa na kasoro, hakuna na pesa, na kiwamanamapenzi kwake ni pesa…’akasema.

‘Sasa ilikuwaje Kimwana akawa ndio bosi wako?’ akauliza.

‘Kutokana na utendaji wa kikazi, mimi nilikuwa mkali wa ulinzi na kutumia silaha, tulikuja kugudnu akwua Kiwamana ana maadui wengi sana, basi tukakubaliana kuwa kila anapokwenda niwe nayemimi,na kwa viletulikua tukijua kabla haikuw ashida kwangu,….

‘Haya sasa niambia ilikuwaje siku ile y atukio.

‘Siku ile ya tukio. …nilipata taarifa kuwa wewe unatakiwa uondoek duniani…kwa pesa nyingi tu’ akasema.

‘Ni nani alikupa hiyo taarifa au ni nani aliataka mimi niondoke dunianai?’ akauliza wakili.

‘Haina haja ya kumtaja mpaka hapo unaweza kujua ni nani, licha ya kuwa sikutaka kukuambia yote hayo,lakini kwa vile umenihakikishai kuwa mimi sio muuaji wa Kimwana nitakuambia kila kitu….

********

Baada ya kumaliza mazoezi ya kulenga shabaha, Wakili mwanadada alimwangalia mkuu kwa muda bila kusema kitu, hata mkuu akajikuta akijiuliza kwanini huyu mwanadada kila mara ananiangali sana , na ameligundua hilo mara nyingi, hakutaka kumuuliza, akasubiri, akijua kuwa subira huvuta heri , huenda kuna kitu anatka kuniambia;

‘Mkuu unajua sana kulenga shabaha,…’akasema wakili mwanadada.

‘Unanitania, katika walenga shabaha, mimi nipo mbali  sana, ….huoni hata wewe leo umenishinda kwa mbali sana, kwa ujumla mimi siwezi kujisfu kuwa nina shabaha, katika kundi letu sisi mwenye shabaha sana ni wakili wetu mkuu kwenye kitengo chetu cha sheria, kila tukifika hapa hakosi hata  mara moja, ana kipaji sana cha shabaha….

‘Mimi sijawahi kuja naye, nikamuona anavyplenga  shabaha,natamani nimuone,ili nijue siri ya uwezo wake huo…nasikia hali yake ni tete, huu ugonjwa wa shinikizo la damu, unawasumbua watu wengi sana siku hizii…’akasema wakili huku akijaribu kuwaza jambo.

‘Kwakweli yule ni mkali wa shabaha,…na ni mtu mwenye afya sana, nashindwa kuelewa hili shinikizo limemshindaje,…lakini ndio hivyo, mwili wa binadamu ni mwili tu, unawezwa ukalazwa kitandani kwa kuchomwa na sindani kwenye kidole,…unajua kama isingelikuwa haya matatizo yaliyomkumba, tungekuwa naye hapa, lakini natumai atayashinda yote,… …’akasema mkuu.

‘Kwani ana matatizo mengine, nilisikia ana matatizo ya kifamilia, …ilikuwaje….?’ Akauliza wakili mwanadada.

‘Ina maana wewe hujui hayo au unaniuliza kiubembe, hujui kuwa alikuwa na tuhuma nzito, iliyosukwa na hawa wahuni,…, na picha mbaya zikatolewa , …akaja kudaiwa pesa nyingi tu na hawo wahuni,  alihangaika na baadaye akaamua kulitoa hili jambo kwetu kisiri, tukasuka mpango ili kuwakamata hawo watu,lakini hatukufanikiwa,…hata hivyo lilikwisha, ila hapo ndipo afya yake ilipooanza kutetereka…’akasema mkuu.

‘Ina maana ndio maana hakutaka kushiriki kwenye hii kesi?’ akauliza wakili.

‘Haiwezi ikawa ndio sababu ya moja moja,….kwasababu tulishayamaliza mataizo yake , waliomfanyia hivyo ni vibaka wa kawaida tu,…Siku walipomletea hizo picha,alipatwa na mshituko mkubwa, na tangu siku hiyo anasema kuwa amekuwa akipata maumivu makali upande wa kushoto,…na limekuwa ni tatizo ambalo linamfanya ashindwe kutimiza wajibu wake, anahitaji mataibabu ya hali ya juu…’akasema mkuu.

‘Unajua hili tatizo halina asili kwa jamii zetu, na mtu anaweza akafumaniwa isiwe na tatizo, lakini jinsi uchumi unavyokuwa, na watu kuingia katika maswala ya kisheria katika kurithi mali, …na vitu kama hivyo, tatizo hilo linakuwa moja ya janga, maana unakuta labda utajiri upo kwenye familia ya mke, na mume kwao ndio hohe hahe, …..’akasema mwanadada na kutulia kwanza.

‘Kuna kesi moja iligubikwa na mambo hayo,…katika makubaliano ya ndoa ,mume aliambiwa kama atakutwa na tatizo,lakashifa hasa hiyo ya kuvunja sheria za ndoa, ya kufumaniana,au madawa ay kulevya, ….basi ndoa itakuwa imevunjika…sasa mke akampata mshikaji mwingine ,akaona njie pekee ya kuachana na mumewe, na kumtumbukiza kwenye kashfa, na alichofanya nii kumtegea mwanamke….’akatulia kwanza.

 Akasuka huo mpango ukiwashirikisha mke wa mtu na mshikaji wake, wakamtegea huyo mume wa huyo mke, …wakamtafuta msichana, hawa wanawake wanaojua hizo kazi, wanachohitaji wao ni pesa tu,…na wanaume mlivyo wazaifu, akategeka na tendo likafanyika na picha zikachukuliwa,….hutaamini hilo lakini lilitokea….

‘Sasa hapo tamaa ikatawala, huyo mshikaji alichokuwa akimpendeahuyo mke ni pesa, mengine yanakuja tu, kwasababu ya pesa, na tamaa ya huyo mshikaji ikamtuma afanye jambo jingine, kwasababu ule mpango wa kumkamatisha huyo mume wa huyo mke, huyo mshikaji, alikuwa  akiujua kiundani na ushahidii uliotakiwa ni picha ya tukio, yeye akaona kuwa kumbe anaweza kuzitumia hizo picha kuchuma pesa kirahisi,….’Yule wakili mwanadada akatulia na kumwangalia mkuu wake kama kweli anamsikiliza na kumuelwa akaendelea kusimulia hiyo kesi kwa kusema.

‘Baada ya lile tukio ushahidi ambayo ni picha akawa kabakia nazo huyo mshikaji, na wakapanga nini kitakachofuata…kwahiyo sasa ilibakia vitendo,…mke aanzishe chokochoko kuwa mume wake anatembea nje ya ndoa keshavunja mkataba,….kuna kitu kilitakiwa huyo mshikaji akifanye kwanza, lakini jamaa akawa hatimizi hiyo ahadi ili yule mke anze kashikashi, ingwaje kwa ndani ya familia, alishaanza kwa kumshutumu huyo mume kuwa anatembea nje ya ndoa,na mume akawa mkali na kukataa kata kata, na kudai ushahidi,….

‘Nia ya huyo mke ilikuwa ni hivyo,kuwa aachane na huyo mume ili aje baadaye aolewe na mshikaji wake, sababu ni kuwa mume wake ni mvivu katika maswala ya ndoa,…alimpenda kwa muonekano wa nje, kumbe mambo mengina hayatimiziki kihivyo, na siku alipokutana na huyo mshikaji kisiri akagundua kuwa kumbe kuna mambo ambyo hayapati kwa mumewe, yapo kwa waume wengine, kwa tamaa hizo  akaona kuwa huyo mshikaji ndiye anayefaa kuwa mume wake…’akatulia huyo mwanadada na kutizama chini.

‘Haya mambo yapo jamani, yanatesa jamii, usione watu wanatoka nakusema mume wangu ,au mke wangu, kuna watu hawana raha inapofikia katika hayo maswala, lakini yanapelekwa kimiya kimiya, watu wanaumia kimiya kimiya, kwa kuogopa kashifa, kwa kuogopa, kuwa atatoa siri ya ndoa,…ndoa zinalege lega, na wengine wanaachana kwa kisngizio kumbe chanzo ndio hicho  kisichoelezeka.

Sasa kumbe hata huyu mshikaji, hakuwa na upendo wa dhati na huyo mke wa mtu, ni kwasababu ya kutaka pesa na mali,..wapo wanaume wa namna hiyo wengi tu, kama walivyo wanawake wengi tu,..’akasema huyo mwanadada na mkuu akatikisa kichwa kukubali, akawa huku akiwa anasikiliza hicho kisa cha hiyo kesi anayoielezea wakili mwanadada.

‘Basi huyo mshikaji akawa anachukua nakala moja ya picha na kumpelekea yule mume wa mtu kwa siri, na kumwambia kuwa asipomlipa pesa nyingi atalifikisha hio swala kwa mkewe….hebu fikiri hapo jamaa alipoziona picha picha alikuwaje, alichanganyikiwa, …. akahaha, na kweli akampa hizo pesa, kwani pesa alikuwa nazo, kwa kupitia kwenye miradi ya familai ya mke, lakini muonja asali haonji mara moja, huyo mshikaji akafanya ndio sehemu ya kupatia kipato, ikawa ni kamchezo….’yule wakili mwanadada akacheka na kusema.

‘Unajua nimegundua jambo, ibilisi akishaingia akilini, anakuchezea kama mtoto mdogo, huyu mke,akawa anazitaka zile picha, lakini huyo mshikaji anamzungusha, na bila hizo picha ndoa haiwezi kuvunjika na yeye keshampenda huyo mshijaki, na mume kambana hapati mwanya wakwenda kuyapata yale ambayo hayapati toka kwa mume wake…akaona anawekewa kiwingu, akaamua kumtegea sumu mumewe….’akatabasamu tena huyo wakili na mkuu akasisimuka na hicho kisa, akasikiliza.

‘Sasa siku hiyo kaweka kinywaji chenye sumu, akitarajia kuwa mume wake akija atakinywa, yeye akwa akwa aktoka kwenda kazini, ….mume ana kawaida ya kurudi mchana kupata chochote, nay eye ndiye mwenye ufunguo wa nyumba, akasahau kuwa alishawahi kumpamshikaji wake ufunguo, ili wakija asipate shida ya kuingia ndani.

Sasa huyo mshikaji anajua kuwa huyo mume muda kama huo anakuwa nyumbani, na alihitaji pesa, akachukua nakala nyingine na kwenda huko kwa huyo mume wa mtu, alipofika kwa kujiamini,akafungua mlango na kuingia ndani….

 Alipoingia ndani akakuta mezani kuna  maandalizi,….yeye hakujali sana, akacukua kinywaji na kujimiminia, akajisaidia na chakula, hana wasi wasi, huku akisubiri, akaweka gilasi mojayakinywaji akanywa, akawa anakunywa taratibu, huku akisubiri, lakini jamaa siku hiyo akakutwa an foleni y magari akawa kachelewa kufika….mshikaji , akaongeza gilasi ya pili,….tumbo likaanza kuuma.

‘Mume anakuja anakuta mtu yupo chini mapofu yanamtoka mdomoni…hajiwezi kabisa, haraka akaita polisi na jamaa akakimbizwa hospitalini,…akafia njiani,  na yule mume akashikwa kuwa yeye ndiye kampa sumu huyo jamaa….sasa angali kesi kama hiyoilivyo,…inaumiza kichwa sana, unataiwa uwe makini, ukichukulia juu juu, utasema kweli, huyo mume ndiye kampa sumu huyo jamaa kwasababu ya hiyo tabia ya kumdai pesa kwa kutumia picha chafu…..’akatulia na kumwangaliwa mkuu .

‘Hapo ndipo uchunguzi ,akili na hekima inatakiwa kutumiwa, ukichukuliwa juu, juu ,….utafunga watu wasio na hatia,….ndio maana naogopa sana hizi kesi zinazofungamana na jamii na,…mahusiano,…usipokuwa makini utaumiza watu wengi wasio na hatia badala ya kuponya….’akasema wakili mwanadada.

‘Nikuulize hicho kisa kina maana gani kuhusiana na hii kesi yetu….?’akauliza mkuu.

‘Nilikuwa nataka kukuonyesha jinsi gani haya mambo ya kutishiwa kuwa usiponilipa pesa nitatoa siri yako jinsi sasa yanavyokuwa sumu kwa watu, ni kama uuaji wa namna fulani,inabidi jambo hili lifanyiwe kazi ya haraka na jamii ielimishwe,…’akasema huyo wakili mwanadada na alipoona mkuu katulia akamuuliza swali,

‘Na je tuhuma kwa huyu mama docta kuwa ana michezo kama hiyo imefikia wapi,?’ akauliza wakili.

‘Tatizo kubwa mambo kama haya hayana ushahidi, wale wanaotishiwa hawataki kuyaleta hayo mashitaka kwenye usalama, wakiogopa kuwa siri zao zitajulikana, na matokeo yake tunawapa nguvu sana hawa watu, nafikiri ndio silaha yao kubwa, kuwa wanafanya namna ambayo mtu waliyemlenga hataweza kutoa hiyo taarifa polisi

‘Huyu mama docta kaondoka muda sasa…..nafikiri karudi kwao Kenya….’akasema mkuu
Wakili akatulia kwa muda bila kusema neno, huku mara kwa mara akimwangalia mkuu huyo, alijua kabisa hisia zake zinaweza zikapingwa na mkuu, lakini kila mara alipowaza hilo jambo aliona inawezekana, kinachotakiwa ni kuhakikisha anakusanaya ushahidi, na ikiwezekana amshirikishe huyo mkuu kwa kila hatua, akageuka na kumwambia mkuu;

‘Samahani sana mkuu, usione kwanini nimetulia kimiya hivi bila kusema kitu, nilikuwa nikijaribu kujiuliza mwenyewe , na kutafakari kile ninachotaka kukuambia, najua unaweza usiniamini, lakini nahisi inaweza ikawa ndivyo hivyo, licha ya kuwa sijaweza kupata uhakika wa moja kwa moja…..’akasema wakili mwanadada na kutulia kwa muda.

‘Wewe ongea na kusikiliza…’akasema mkuu.

‘Mimi nina uhakika kuwa Jangiri siyo yeye aliyemuua Kimwana,…’akasema wakili.

‘Unasema nini,…mbona ushahidi upo, na yeye mwenyewe alikiri mbele yangu kuwa  yeye alikuwa na nia ya kukua wewe, lakini bahati mbaya risasi ikampiga Kimwana,amekuja kukana baada ya kumpata huyo wakili wao,….kama umjuavyo yule wakili anajua kucheza na sheria….’akasema mkuu.

‘Risasi iliyomuua Kimwana haikutoka katika bastola aliyokuwa nayo Jangiri,taarifa hii imebadilishwa kinamna, na ukweli kufichwa, kitu ambacho kinaonyesha kuwa kuna mtu ndani ya wanausalama anahusika na hiki kifo, au kafanya hivyo kwa shinikizo fulani, lakini hilo la kufanya kwa shinikizo halina nguvu, ….naoana kafanya hivyo makusudi ili kuhakikisha kuwa ukweli haujulikani,…’akasema wakili mwanadada.

‘Haiwezekani…’akasema mkuu na kumwangali wakili mwanadada.

‘Nakuomba leo twende kule Mbezi nikakuonyeshe ushahidi ambao huenda ukakufungua macho, lakini usiseme lolote kwanza kwa mtu yoyote, hili ni kati yangu mimi na wewe tu…kwasababu ikijulina nina uhakika kutakuwa janga kubwa…’akasema wakili mwanadada, na kumfanya Mkuu kumwangali huyu mwanadada kwamacho ya wasiwasi.

‘Usishangae mkuu, mambo hayo yapo, na usione kuwa labda u kiongozi, unafuatilia kitu, kuna mengine yanatokea nje ya uwezo wako, leo unayemuamini na yeye akajitahidi kuaminika kesho anaweza akahini huo uaminifu, huenda kajitihadi kikomo cha uwezo wake, akasema basi ngoje iwe hivi, akijua haitajulikana…hujafa hujaumbika, na ukistaajabu ya Musa ….’akasema huyo mwanadada na kabala hajamalizia huo usemi simu ikapigwa…..

NB: Sehemu hii nimeiandika kwa shida sana, sijui kama ipo sawa, tuzidi kuwepo kwenye sehemu ijayo..

WAZO LA LEO: Katika maisha haya usichukulie kila jambo kuwa ni sawa au si sawa, cha muhimu ni kuwa na uhakika nacho,maana ukiwa na pupa na hamasa ya kila jambo unalolisikia utaumia bila faida yoyote; Pupa huua,  na mwenye pupa hadiriki kula tamu.


Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Hongera mkuu,...nimeona hapo juu unatangaza watu waweke matangazo, ina maana hujapata hata moja, haiwezekani,mbona wenzako wana matangazo kibao,ya makampuni ya simu,na blog zao hazina mambo muhimu saaana.
Nikuambie kitu, huwezi kupata mpaka uwaendee.kwakweli inaniumiza sana, kuona muandishi mzuri kama wewe huna tangazo hata moja, likakusaidia.

Anonymous said...

Kufumaniwa sio mchezo kila kitu kinasinyaa.
Hongera mwaveja