Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, May 18, 2012

Hujafa hujaumbika-38Mwanadada wakili alikuwa wa kwanza kufika eneo la tukio, na moja kwa moja aliingia ndani, na kukuta watu wa huduma ya kwanza wakifanya kazi yao, hakupewa nafasi kabisa, akaona haina, akasogea pembeni kuwapa nafasi, …na haikuchukua muda mara ule mwili ukainuliwa kwenye machela tayari kwa kukimbizwa hospitalini,….

Hakuana na jinsi, alitaka kumuona kuwa ni nani, lakini haikuwa rahisi hivyo, askari hawakumpa nafasi hiyo, walisema kazi yao ni kujaribu kuokoa maisha ya huyo mtu hawawezi kumchelewesha hapo zaidi, ikabidi atulie na akawa anaangaza macho huku na kule mara mara akamuona, jamaa kakaa pembeni, huku kainamisha kichwa chini,akamsogelea na kumgusa kwenye bega kwa nyuma.

‘Vipi …ooh, ni wewe, umefikaje huku….?’ Akamuuliza kwa kushangaa alipogundua kuwa ni mtu anayemjua.

‘Oh,…afadhali umefika, hapa nilitaka nikupigie simu,  kumbe na wewe umekuja, afadhali maana hawa polisi hawana dogo, Mimi ndiye niliyewapigia simu polisi,lakini nawajua wanaweza wakanigeuka , wema wangu uanweza ukaniponza….’akasema.

‘Imekuwaje wewe uwapigie simu, ulifikaje huku, Ina maana hapa unapajua….hebu niambia kwa ufupi na kwa hara…’akasema wakili mwanadada, na kabla hajaongea kitu, mkuu na kundi lake wakaingia na walipoona watu wakimalizia kazi mbali mbali mle ndani, akawaona wapenafasi kwanza,ili awaulize kila mmoja kwa wakati wake.

‘Imebidi awahishwe hospitaliu haraka,…huenda tukaokoa maisha yake,….’akasema askari kumwambia mkuu.

Mkuu akamsogeza huyo askari pembeni, karibu na tuliposimama, huyo askari ndiye aliyefika hapo mapema na kundi lake baada ya kupigiwa simu, akamuuliza swali la kwanza;

`Hebu niambie,ulifikaje hapa..?’ akauliza swali la utata.

‘Tulipigiwa simu na jamaa mmoja,…..mmh, yule pale,…’akanyosha kidole kunielekeza mimi.

‘Huyu jamaa kwenye simu alituambia kuwa amefika hapo baada ya kupigiwa simu na …..huyo aliyefikwa na hayo maafa,….mapaak sasa hatujamjua ni nani, huyo mwanadada, alisema kuwaanamuhitaji huyo jamaa kwa haraka , hayo ni kwamaeelzo yake ya haraka, sijamuhoji vyema, nimemuweka pembeni kwanza ili tumalize hayo ya muhimu…’akasema huku wote wawili wakiniangalia mimi

‘Tutamuhoji baadaye, wewe elezea kuhusu kazi yako,nini ulikiona uligundua nini…’akasema mkuu.

‘Nilipofika hapa, nilifika na kikosi kamili, maana nashukuru huyo jamaa alitupa maelezo safi kabisa, kwahiyo tulkuja tukiwa tumejiandaa, niliuagiza docta na kundi lake wafike hapo haraka, pia tulikuja na wataalamu wa alama za vidoela na wachukua picha, na wachunguzi wote niliwapata kwa haraka, kwahiyo tulipofika hapa kila kitu kilifanyika kwa haraka, hakuna kilichokosewa, tumewaachia sasa madocta wamalizie kazi yao ili watupe taarifa….kwasasa wamesha mchukua huyo ….eeh ,tuseme majeruhi hadi hospitalini’akasema huyo askari.

‘Kwahiyo unaweza kusema nini kuhusu hili tukio…?’ akauliza mkuu.

‘Ni tukio la kutaka kuua, kwa kutumia bunduki, …kwasasa tunaweza kusema ni majambazi, lakini hatuja wan a uhakika nalo,….siwezi kusema ni mauaji maana hatujapata taarifa ya docta, lakini huyo muathirika kapigwa risasi,…na ngoja tumsubiri docta atuambie wapi na athari yake, lakini mimi na wenzangu tuiimkuta akiwa bado hajapoteza fahamu….

‘Naona pale dirishani, kumemeguka, ina maana ile ni sehemu risasi ilipopitia kutoka kwa nje, ….’mkuu akaangalia pale dirishani na kiyoo kilikuwa kimevunjika kidogo,….na alipokichunguza vyema akagundua kuwa kile kiyoo kilikuwa na matundu, na risasi ilipenye kwenye moja ya tundu, ilikosea kidogo ndio maana kiyoo kimemeguka…na kile kipende kilichomeguka kikaanguka chini na kusambaratika.

‘Ndio mkuu, pale ndipo risasi ilipopitia, wataalamu wamepapima, na huyo muuaji alikuwa kwa nje, akalenga shabaha kupitia kwenye moja ya matundu ya hicho kiyoo, akiwa anmuona huyo mwanadada kwa ndani tundu…’akasema huyo askari.

‘Kwahiyo huyo muuaji alikuwa kasimama kwa nje, au sio….?’akauliza mkuu.

‘Hapana kutokana na mtaalamu wetu wa silaha anasema mlengaji alikuwa mbali kidogo, na ukiangalia kule, kuna jengo ambalo lipo juu kidogo, ina maana mtu akiwa kule anaona huku kwa ndani, na kwa vile taa hapa zilikuwa zinawaka, kama unavyoziona, licha ya kuwa ni jioni jioni,….tulizikuta hivi hivi,….’akasema na kuangali juu, kweli taa zilikuwa zinawaka.

‘Ukiwa kwenye lile jengo unaweza kuona huku, ukitumia silaha yenye darubini unaweza ukaona vyema tumejaribu hilo kwa haraka….’akasema huyo askari.

‘Sijawaelewa , ina maana huyo aliyekusidia kuua alikuwa kwenye lile jengo, akatumia silaha yenye darubini kumlenga huyo …..mmh,muathirika,je alijuaje kuwa kuna tundu kwenye hili dirisha…na kweli unaweza kuona ndani ukiwa pale, mbana naona kama haiwezekani,kama ni usiku sawa,lakini jioni hii?’ akauliza.

‘Tumechunguza hilo, unaweza ukaona,taa hizi nikali sana, na viyoo vya nyumba hii vinaonyesha vyema,hata ukiwa pale unayaona haya matundu vyema..na hasa ukitumia silaha yenye darubini….’akasema huyo askari.

‘Hata hivyo ni kazi kweli kupenyesha risasi kwenye haya matundu, aliwezaje kufaya hivyo?’akauliza mkuu.

‘Yapo matundu mengi, labda alibahatisha tu, na bahati risasi ikapenya kwenye hilo tundu, licha ya kuwa ilikosea kidogo, ….sizani kuwa ni labda ni shabaha ya huyo mtu, kuwa alikusudia hiyo risasi ipenye kwenye tundu…kama itakuwa hivyo basi atakuwa mlenga shabaha mahiri…’akasema huyo askari.

‘Ehe, kwahiyo mumeshajua ni aina gani ya silaha iliyotumika…au mpaka risasi itokewe…?’ akauliza mkuu.

‘Kwa makisio ya mtaalamu wetu, baada ya kuchunguza jereja amesema ni risasi ya silaha kubwa,…na ni hizi zinazoweza kulenga toka mbali,….lakini pale kwenye jengo sio mbali sana..’akasema huyo askari, na kutlia kidogo, halafu akasema tena;

‘Naona ingekuwa ni bora tukasubiri hiyo risasi ikatolewa kwanza ndipo tukaweza kutoa maelezo yaliyo sahihi….kwasababu mengine yote yamekamlika imebania kazi ya madocta…’akasema huyo askari

‘Hiyo ni sahihi kabisa na je mumeshaongea na huyo aliyewapigia simu…?’akauliza mkuu na yule Askari  akageuka na kuangali huku tulikosimama na dada wakili, na kabla mkuu hajapata jibu alilolitaka akatusogelea pale tulipo na kuniangalia kwa mshangao, na baadaye akamwangalia dada wakili akatabasamu na kusema,…

‘Usiseme kuwa wewe ni wakili wake, hatajibu maswali mpaka umruhusu…’akasema kwa utani huku akitabasamu.

‘Na ndivyo ilivyo, mimi ni wakili wake toka siku nyingi, ila kwa wewe na kwa leo nakuruhusu umuhoji maswali yote unayotaka..’akasema wakili mwanadada.
Mkuu aliniangalia kwa makini, halafu akasema;

‘Naona tunakutana mara kwa mara, na kukutana kwetu inakuwa katika hali isiyo rasmi, vipi unataka kujiunga na polisi nini, maana kila ninapokwenda na kukuta upo, na kuwepo kwako kunakuwa  sio kwa heri, haya hebu nieleze ilikuwaje?’ akauliza mkuu.

‘Mimi nilikuwa nyumbani kwangu ninapokaa, na nikapokea simu , ….nilipoiangalia hiyo namba ilikuwa ngeni kwangu,….nilizarau kuipokea, lakini ilipoita mara ya pili  nikaipokea na mara nikasikia sauti ya kike, ilikuwa ikiongea kwa taratibu, labda ili watu wasisikie au ni kutokana na hali ya kiafya, sikujua ni kwanini, ila sauti ilikuwa ya kama kunong’ona….’nikasema.

‘Ilisemaje hiyo sauti….?’akauliza.

‘Ilisema, kuwa …niende nyumba na 512, mtaa huu  hapa Sinza, ….na nifike haraka, kwanza sikupaelewa, licha ya kuwa alinieleza , akanifafanulia nifikie wapi, na ni vyema nichukue boda boda ii nifike haraka, na akasisitiza kuwa ni muhimu, nikichelewa nitakuja kujuitia katika maisha yangu yote…nikamuuliza kwanini na yeye ni nani?’nikatulia kidogo.

‘Ehe elezea tu, tunataka kupata maelezo ya haraka haraka, ikawaje…?’ akauliza mkuu.

‘Alisema nitajua nikifika huko,…halafu nikasikia kama sauti ya kiyoo kikivunjika, au kama hicho, mara na na sauti ya `aaaaah’ na ikawa kimiya, lakin nilihisi hiyo simu bado ipo hewani’nikasema nikujaribu kukumbuka ilivyo kuwa…

*******

Siku hiyo nilikuwa nimepigika kweli, watu siku hizi husema nilikuwa nimefulia, na kila nilipojaribu kutafuta chochote sikuweza kupata, nikaenda kwa mama mmoja niliyomzoea, akanipa ukoko, na nikamsaidia kusafisha vyombo, basi tumbo lilipojaa, nikaaona nikajipumzishe chumbani kwangu,kwanza nilioga nikuwa nimenyoa jana , kwahiyo sikujusumbua kuangalia ndevu,kwani huko ninapokwenda kufanya kazi hotelini usiku wanahitaji uwe mtanashaji. Kuna mtu mmoja aliniwahi kunishauri nijiunge na wanamitindo.,....eti ninafaa sikupenda hilo wazo, 

Nikaona nijipumzishe tu, kwani unaweza ukatoka kutembea ukakutana na mabalaa, na mimi najaribu kuyakwepa,....sizitkai mbichi hizi,sina pesa, nitafanya nini, nikaamua nipige mbavu,maana nilikuwa na sehemu ya kufanya kazi, ni bora nikusanye nguvu.

Nikiwa ndani ya usingizi,nikaota ndoto kuwa nipo kijijini kwetu, lakini ndoto hiyo ilinirudisha siku nyingi nyuma, nikiwa natoka shuleni, nikakutana na msichana mmoja, sikuwa na mjua,msichana huyo akaniambai kuwa mimi ni mtu mbaya sana,

‘Kwanini unasema hivyo?’ nikamuuliza.

‘Kwasababuu wewe unaharibu watoto wa watu halafu unawaacha njia panda….akaniambia nimewaharibu hata kwenda shule hawawezi,….na wazazi wao wamewafukuza…’akasema huyo msichana mgeni kwangu.

‘Mbona mimi sijafanya hivyo, wapo wapi hawo watoto?’nikamuuliza

‘Wale pale….’akanionyesha kwa vidole,na kweli pale niliona watoto wamelazwa, lakini cha ajabu chini ni watoto, lakini kwenye vichwa vyaoo ni watu wazima,na mmojawapo niliyemuona ni Kimwana, yeye alikuwa kilia na machozi yake yalikuwa nii ya damu, na sura nyingine ambayo najaribu kuiwaza ,lakini siikumbuki vyema,… ilikuwa yenyewe inaniangalia kwa kushangaa,…

Nikamuuliza huyo msicahana mbona ni wana sura za namna hiyo, kichwani watu wazima lakini kiwili wili cha kitoto,akacheka na kusema, wewe hujioni, kichwani mnaonekana watu wazima, lakini mtendo yenu ya kimwili ni ya kitoto, aheri hata ya mtoto, utasema anafanya hayo kwasababu ni mtoto, hebu jiangalie wewe…’akasema na mimi nilipojiangalia, nikajikuta mwili wangu ni wa kitoto…

Nilishituka kwa hofu toka usingizini, na sikuweza kulala tena,nikiwazi hiyo ndoto, mara nyingi nikiota ndoto, huwa ina maana fulani, au inanieleekza jambo fulani, lakini ndoto hiyo haikuwezakunipa maana halisii ni nini, nikaamua kuipotezea na nikajinyosha kidogo na kabla sijamaliza kujinyosha simu ikalia.

Nilipotizama ile namba, nikaiona ni ngeni kabisa machoni mwangu, nikaidharau na kuinuka kitandani,simu ileiliita mapaka ikakatika, nikasema hapigi tena, lakini mara akaanzakupiga tena, nikasema moyoni ni bora kusikiliza huenda ni simu ya pesa, nikaipokea;

‘Fika haraka hapa Sinza, ukifika hapa Kwaremi, ingia barabara inyofuata hadi nyumba namba SN X500, nipo ,fungua mlango utanikuta..’ikasema sauto ya kunong’ona. Nikamwambia kuwa huko sipajui na sina nafasi kwa sasa.

‘Ni muhimu sana,..usipokuja utajijutia masiha yako yote, nahitaji kukuona kwa jambo muhimu sana kwa ajili ya maisha yako ya baadaye….chukua boda boda, wengi wanapajua hapa mahali…nitamlipa huyo mwenye boda boda…’akasema kwa sauti hiyo hiyo ya kunong’ona.

‘Kwani wewe ni nani ….na umenijuaje….?’ Nikamuuliza.

‘Usiulize maswali mengi,unapoteza muda,weweukifikahapa utajua kila kitu na hata kie ambacho ulikuwa hukijui utakijua…njoo haraka…’mara nikasikia sauto ya kama `’kaaah’ naweza kusema ni sauti ya gilasi au kiyoo kilichovunjika, nasema hivyo baada ay kuona hivyo viyoo vilivyovunjika hapo, lakini kwa muda ule sikuweza kutambua ni sauti ya nini.

‘Ila nilichosikia cha wazi ni hiyo sauti ya `aaaah’na kutulia,nikabaki kusema `halooh, haloooh’ lakini sikusikia sauti nyingine sehemu ya pili, nikainuka kitandani haraka, na kutoka nje, ukumbuke sina pesa na ni nani angekubali akuchukue bure, ..bahati nilipotoka nje tu, nikamuona rafiki yangu mmoja,

‘Vipi broo, huna abairia leo…?’ nikamuuliza.

‘Kuna abiria mmoja kaniita nikamchukue huko Sinza, sasa najaribu kuliangali pikipiki langu maana huyo ni mtu wapesa…’akasema huyo rafiki yangu na moyoni nikasema mambo si hayo.

‘Hata mimi nafika huko, lakini sina pesa, kuna jamaa kaniambia nikifika huko atanipatia chochote, naomba lifti…’nikasema.

‘Wewe kila siku huna pesa….hujui nikikupakiza wewenitakosa abiria njiani,lakini twende tu, utanilipa tukifika…’akanimbia na mimi nikapanda kwenye hiyo pikipiki na haraka tukafika Sinza, na nilipomuulizia mitaa ya hapo, akasema Sinza anaijua sana kwani ndipo alipokulia na hata hiyo nyumba anaifahamu, ni nyumba nzuri, iliyojengwa kwa haraka sana…

Basi akanifikisha na kuniambia kuwa pesa nitampa huko nyumbani, name nikashukuru na kueleka kwenye hiyo nyumba. Kwakweli ilikuwa ni nyumba nzuri, imezungushwa geti la nguvu, nikafika kwenye geti na kukutata hakuna mlinzi, nikafungua mlango wa geti na kuingia ndani….nje kulikuwa na bsutani nzuri,nikaitamani ile nyumba.

Nikaharakisha kwenda kugonga mlango wa hiyo nyumba, lakini kulikuwa kimiya, nikafungua mlango na kuona upo wazi, nikaingia ndani. Macho yangu yalitua kwenye dirisha moja kwa moja, nikaona pale palivyomegeka, na kipande cha kiyoo kimedondoka chini na kuvunjika, nikaona ajabu,….sikuwa na mawazo ya kuangalia skafauni.

Mara nikasikia sauti ya mtu akiguna kuonyesha maumivu,…haraka nikageuza kichwa kuangalia kule sauti ilipotokea, ooh, nikashikwa na mshituko, damu, zilikuwa zinavuja toka kwa huyo mtu aliyelala sakafuni, zilikuwa zikitoka eneo la bega,…karibu na kifua…mawazo yangu yalikuwa labda kapigwa kisu,lakini kulikuwa hakuna kisu,…nikamsogelea alikuwa mwanadada akiwa na nguo za kulalia, niakogopa hata kumgusa, nikujua sasa hilo ni balaa

‘Msoma…..mso….mali…naku….naku……’akawa anataka kusema kitu, lakini sauti ilikuwa hatoki vyema na wala hakuweza kumalizia hilo neno, alilotka kusema,  sikujua anataka kusema nini, na mara akaonyosha kidole nakunionyeshea kwenye kabati,…nikaangali sikuona kitu zaidi ya kabati la vitabu….nikamgeukia na kutaka kumuinua.

Lakini nikaona nitakuwa mjinga mtu kaumia badala ya kutoa msaada naanza mengine,nikapiga simu polisi na kuwapa maelekezo, na bahati nzuri,walisema kuwa wapo karibu na wanapajua hapo ninapowaelekeza, nikawapa hali halisi ilivyo.

Haikuchukua muda wakafika,…ndivyo ilivyokuwa mkuu,...'nikamaliza kujieleza.

Nb, leo najisikia hali sio shwari,....tuonane sehemu ijayo mungu akipenda.

WAZO LA LEO: Unaweza ukajikuta ukiandamwa na matatizo lukuki,hata kuwaza yasiyokuwepo, ooh, labda mkono wa mtu, ooh,kwanini mimi....cha muhimu ni kuvumilia na kujikabdihi kwa mungu, maana yote yameumbwa kwa ajili yetu wanadamu, yawe mazuri au mabaya. Jua kuwa mvumilivu hula mbivu.


Ni mimi: emu-three

8 comments :

Pam said...

pole kwa kutojickia vema... huyu aweza kuwa yule demu wa ahadi yz uttn!

Anonymous said...

NDUGU YANGU WEZAKO WANAKUIBIA KAZI YAKO, UNAUMIA WEWE WENZAKO WANAFAIDI, JARIBU KUTAFUTA NJIA YA KUMILIKISHA KAZI ZAKO, NI USHAURI TU

samira said...

m3 vipi unaumwa umesema leo hali sio nzuri au sijaelewa pole sana
daa yaani jamaa kila anapokanyaga ni balaa tu
muendelezo ni mzuri ,binadamu tunakutana na mengi kwenye maisha .la muhimu mtu kutokata tamaa hakuna lisilowezekana

emu-three said...

Pam na Samira, ni kweli afya ina migogoro, nashukuru kuwa leo ni Ijumaa, na kesho nipo nyumbani nitakuwa napumzisha mwili....siunajua tena kupigika, unatoka nyumbani usiku unarudi usiku.

Ama kwa mwenzangu uliyenishauri kuwa kazi zinaibiwa,...kwakweli hapo sina uwezo wa kuzia kwa sasa, kama kuna watu wa namna hiyo...mungu atawalipia...

Iliyobakia ni kumuomba mungu atusaidie, ipo siku tutajaliwa an kuweza kuwa na hiyo hati milki na kuchapa vitabu.

Na yule aliyeuliza kwanini siweki tangazo, ...natamani sana iwe ivyo, lakini sio rahisi kwa hapa kwetu bongo,....lakini yote tutaendelea kujaribu, ipo siku,...tuombeane heri.

Shukuru Hamisi said...

Tuko pamoja mpaka mwisho, hata kimya kimya....

emu-three said...

Shukuru nashukuru kuwa nasi na kuachana na kupita kimiya kimiya.
Unajua unapoandika jambo wenzako ndio wahakiki na washauri wakuu wakiwa kimia hutaweza kujua ujumbe umefika je ni safi

Rachel siwa Isaac said...

Ndugu wa Mimi,Pole sana kwa yoote, Mungu yu pamoja daima, ipo siku itabaki Story.

Asante kwa Wazo la leo pia.

Pamoja sana sana Ndugu wa mimi.

emu-three said...

Ndugu wa mimi Amin dua yako ipokelewe tupo pamoja
Nimesikitika leo yametokea mambo juu ya uwezo wangu, kuna tatizo la umeme kwenye sehemu ninapojishikiza.