Siku hiyo sikuweza kulala, na kila nikilala, nikawa namuota
Kimwana, nashangaa kwanini , maana nilishamtoa moyoni ,lakini niliposiki kuwa
kafa, moyo ukawa unamuwaza yeye. Na kulipopambazuka, nikaamua kwenda kutafuta
ukweli na hata kujua taratibu za mazishi yake zitakuwa vipi.
‘Ndio…ni kweli,mkeo keshatangulia mbele za haki, …tulimkanya
sana lakini hakutaka kutusikiliza , na matokeo yake ndiyo hayo. Unajua hico
kifo chake alijitabiria mwenyewe, nakumbuka siku moja alisema kuwa yeye kufa
kwakwe itakuwa kwa risasi maana kutokana na matendo yake, kuna wengi wamakufa
kwa njia hiyo, sasa ndio hayo hayo yamemkuta…’ nikapata hizo taarifa kutoka kwa
mtu wake wa karibu.
‘Aaah, ina maana ulikuwa unajua kuwa yupo wapi, ….kipindi
kile nimekuja kukuulizia ukanikana na
baya zaidi ukawa unanikimbia, kwanini,….?’ Nikamuuliza.
‘We acha tu, hata ulipokuja hapa, sikuwa naamini kuwa upo
peke yako, mimi kwa macho yangu,nilikuwa ukiwa na sijui niite nini, ulikuwa na
jitu la kutisha nyuma yako…’akasema na kuniangalia kwa macho ya uwoga.
‘Mbona nyie watu mnanishangaza sio wewe tu, wengi walisema
hivyo, lakini mbona mimi nipo peke yangu…’nikasema.
‘Basi unamshetani….lakini wewe mwenyewe hujijui…’akaniambia.
‘Tuyaache hayo, sasa mbona ulinidanganya kuwa hujui wapi
alipokuwa mke wangu?’ nikamuuliza.
‘Wewe mwenyewe unajua kuwa yule alikuwa rafiki yangu mkubwa,…na
siri zake nazitunza, na alishaniambi kuwa anafanya hayo kwa ajlli ya usalaam
wako, kwa vile anakupenda na hataki uingie tena kwenye matatizo, na ili
akusaidie, ni bora kabisa msionane naye…alinkanya kabisa kuwa nimsimumabie wapi
alipo…’akasema huyo mtu wake wa karibu.
‘Sasa kwanini inaongeamambo yake…?’ nikamuuliza.
‘Hayo maswali ya mahakamani, kwa vileuemsahawahi
kusimamisshwa mahakamani na wewe unajifanya kuuliza maswali kama ya kwao, …nafanya
hivyo kwasababau hayupo duniani, tena,…na hutaweza kumpata tena, na kwahiyo
htaweza kuingie kwenye matatizo kwa kupitia kwake…’akaniambia.
‘Ina maana hata polisi uliwadanganya….?’ Nikamuuliza.
‘Hata polisi sikuwaambia lolote, walikuja wakaniuliza, wakijua mimi ni rafiki yao, lakini sikuwaambi awapi alipo, kuna muda polisi walikuwa wakimtafuta, sikujua kwanini,.....na pia hata yule wakili mtetezi wa wanawake,alinijia mara kwa mara….alijaribu sana
kunidadisi ili kama najua wapi alipo Kimwana,lakini sikuweza kutoa siri yake hata moja,…mimi alikuwa rafiki
yangu wa karibu,,nikikwama ananikwamua,….kwanini nimuumbue?’ akasema.
‘Sasa kwanini na wewe hukujiunga nay eye, au na wewe upo
unajifanya haupo kwa kuogopa askari?’ nikamuuliza.
‘Mimi aliwahi kunishawishi, nikamwambia bora nife na
umasikini wangu,…nilikataa kata kata, kwetu nimefundwa, nimekulia katika
maadili mema, usione kuwa nina bahati mbaya sijapata mume wa kunioa,lakini mimi
sipo kabisa katika uchafu huo….’akasema na kujiangalia.
‘Hongera, nakumbuka hata Kimwana aliingia kwangu kwa gia
hiyo, akajifanya kuwa yeye sas ani muadilifu, anataka kutulia na mume….akanihadaa,
nyie wanawake mnaaminika,mkitafuta kitu mtadanganya bila aibu..’nikasema.
‘Sio mimi, kwanza nijiunga ili iweje, ili kupata pesa, pesa
zanamna hiyo sizitaki, bora nife masikini, ndio maana umeona
nimejiajiri,sihitaji kuzalilishwa, ipo siku nitapata mume wangu , lakini sio
kwa kupitia njia hizo…’akasema na kutabasamu.
Kwakweli ukimkosa mtu ndio hapo unamuona ni wa maana kwako,
nilianza kumuwaza Kimwana, na moyo ukawa unasononeka,na kusemakwanini angalau
nisiengelikuatana naye angalau mara moja, kwanini amekufa kabla hatukakutana…nilikuwa
namengi ya kuongea naye, lakini ndio hivyo tena, sasa anaitwa marehemu.
‘Kwahiyo taratibu zipoje, maana alinikimbia siku nyingi,
….tangu nikiwa jela, …nilitazamia kuwa ndiye angelkuwa kija kunipa mawazo ,
lakini sikuwahi kumuona, na nilipotokka jela nikakuta hata ile nyumba kauza na
wala sikujua kaenda wapi….’nikasema na yule rafiki wa mke wangu akasema;
‘Alifanya hivyo kwa vile alikuwa akikupenda,…hakutaka
kuendelea kukuingiza kwenye matatizo, ndio maana akakumbia…’akasema.
‘Na taratibu za kumzika zitakuwaje,,?’nikauliza.
‘Hayo kwa sasa yapo mikononi mwa polisi,….na alishasema kuwa
akifa mwili wake usipelekwe huko kwao,kwasababu
kule alishaasi,hakuwa na mahusiano mema na wazazi wake….mtu wake wa karibu
kwa ajili ya taratibu za mazishi atakuwa huyo wanayemuita mama, ….’akatulia na
mimi nikamuuliza kwanini wanamuita mama.
‘Ni sifa tu, kwani sio mama kihivyo, bado msichana, ila kwa
vile ana pesa, kasoma,…nafikiri wanamuita hivyo kiheshima tu….’akasema
‘Kwani huyo mama hana mume?’ nikauliza.
‘Aolewe wapi muhuni yule…..hivi wanaume wamekosa mtu wa
kuoa,….ndio kwakweli kama alivyosema
Kimwana, anajua jinsi gani ya kuishi na
mume, ni mtaalamu hasa, lakini tabia zake…na mwalimu sio lazima awe mtaala wa kile anachokifundisha, mwalimu wa
udakitari anaweza asiwe dakitari, …hata hivyo tabia yake, hakuna wanaume
wangependa kumchukua kama mke,….wewe utachukuaje mabinti za watu na
kuwatumbukiza kwenye huo uchafu, ….je na watoto wake atakubali wafanyiwe hivyo…’akasema.
‘Unajue mimi na kumsikia kote, sijawahi kukutana naye uso
kwa uso, namuona tu kwa mbali, akiwa kwenye gari lake,….lakini sijawahi
kusimama na yeye kama hivi tukaongea…’nikasema.
‘Muda huo anao….ni mama shughuli yule…..na mambo yake ya
kisiri kisiri….nasiki sio Mtanzania, …’akasemahuku akionyesha wasiwasi.
‘Mbona uanogopa kumuongelea?’ nikamuuliza.
‘Ana masikio kama popo….anasiki kila kitu kinachoongeelwa
hapa jijini, ana watu kilakona wanaofanya kazi kwa ajili yake, anajuana na
wakubwa….kwahiyo ukimuongelea yeye uwe makini, na nakuomba tusiongee kabisa
kuhusu yeye, kama unataka kuniuliza maswala ya Kimwana, nipo tayari kwa
sasa,lakini sio kuhusu huyo mama…’akasema kwa uwoga.
‘Hayo yote uliyajuaje, nakuona kama unahusika na hilo kundi…?’nikamuuliza.
‘Kimwana alikuwa rafiki yangu wa karibu, ….akikwama kimawazo
anakuja kwangu ninampa ushauri, ….ni kikwamakipesanamtafuta yeye, lakini tukaja
kukosana pale nilipomshauri ajitoe kwenye hilo kundi,…nilipomshauri kuwa njia
nzuri ni kwenda kwenye vyombo vya usalama akawaambie ukweli,…’akasema huyo rafiki
wa mke wangu.
‘Unafikiri kwanini alikataa kujitoa kwenye hilo kundi?’
nikamuuliza.
‘Alisema sio rahisi , alisema ukijiunga ni rahisi maisha
yako yatatengenezwa vyema, lakini unakuwa kama mtumwa, ambaye hana uhuru,
unatumikishwa hata kwa yale usiyoyataka,…na ole wako ukatae, na ole wako ujifanye
unachana na wao, ujue ndio mwisho wako wakuishi….’akasema.
‘Kwa mara ya mwisho mlionana lini?’ nikamuuliza.
`Karibuni tu alikuja kwangu,alipokuja sikumtambua kabisa,
alikuwa kajibadili, akasema bosi wao kakamatwa, na hivyo hata yeye anaweza
akakamatwa, kwahiyo anatafuta njia za kupotea hapa jijini, nikamshauri kuwa
hiyo ndio nafasi pekee ya kujitoa kwenye hilo kundi, ni njia rahisi ni kuwaambia
watu wa usalama…,’ akatulia kwa muda halafu nikamuuliza.
‘Halafu alisemaje?’
‘Alisema anavyomjua huyo bosi wake, aatatoka muda sio
mrefu,..hata hivyo akadai kuwa hajapata mtu wa usalama wa kumuamini, kwani wengi
wao anaowajua wameshatekwa na huyo mwanamama kimbinu, na wapo kisirisiri kwenye
hilo kundi…’akatulia kidogo.
‘Kwani una maana gani ukisema kundi, ni kundi kubwa sana,….au
lipoje?’ nikamuuliza.
‘Kundi hilo limejengwa kinamna, kwanza lilianza kama shule
ya kufundwa wanawali, na wanaume, waliotaka wasichana waliofundwa wakawa
wanawasilina na huyo mwanamama,kumbe hawo wanawali walikuwa kama chambo, ….na
ingelikuwa ni vyema kama wanaume hawo wangeliwachuku hawo wanawali kama wake,…..lakini
haikuwa hivyo…’akatulia na kuangalia huku na kule.
‘Kufundwa…kufundwa si kunafanyika ili mtu aolewe, su sio?’ nikauliza.
‘Ndivyo ilivyoonekana mwanzoni, lakini kumbe ilikuwa
tofauti, aliwafunda ili kupata pesa kwa kuwatumia hawo wasichana, ni kama
kuwauza kwa starehe za ngono,unanipata hapo, lakini mwisho wake hauishii hapo,
wanachukua picha kisiri, …..unasikia sana, hizo pica zinakuja kutumiwa kumbana
huyo mwanaume, kuwa kama asipotoapesa zitapelekwa magazetini….au kwa wake zao,
au serikalini,kama alikuwa mtu mashuhuri…’akatabasamu
‘Sasa wewe ulijuaje hayo yote…?’ nikamuuliza.
‘Nilijuaje hayo yote,….!’ …akasema kwa mshangao.
‘Kwani sasa ni siri……mbona watu hawo walipoazna kuhangaika
huku kule na hata kutishia kushitaki, ilienea sana,…..na hata ilifikia waheshimiwa
waliojiingiz ahuko, na hata kupooza miili yao kwa kushitulia na mambo hayo, …..wewe
fikiria yeye ni mtu mkubwa ana mke,leo analetewa mpicha michafu aliyofaya
kisiri, anaambiwa asipotoa mimilion aya pesa hiyo mpicha inafikishwa sehemu
nyeti, unafikiri itakuwaje…wengine wanapatwa na kiharusi hapo hapo…..wengine
kwa kufuatwa fuatwa wanaamua kujiua….’akasema.
‘Kwanini wajiue…kama imetokea hivyo kwanini wasiwashitaki
hao wahusika, au kuwakamatishia polisi…’nikasema.
‘Sio rahisi hivyo, kwanza hilo kundi wamajiandaa, wanajua
nini wanachokifanya, pilii hizo picha zinavyochukuliwa, zinakuwa chafu,kiasi
kwamba, hawatapenda zionakane,…..na hata hivyo utaenda kusema nini huko polisi,…..na
mke akijua itakuwaje, maana ukiamua kuwashitaki ina maana ,kila kitu hapo kinawekwa
hadharani, sasa huoni ndio kuumbukahuko, mzee mzima,muheshimiwa, tajiri wa
kuaminika, na hata…..na wengine wanakuja kudaiwa pesa na wakati huo hawana
zakutosha…..’akasema.
‘Sasa Kimwana yeye alikuwaje humo kundini,ni kiongozi au
alikuwa ni nani?’ nikauliza.
‘Yeye si kama mfanyakazi wao, yeye na mabinti wengine warembo,ndio
walikuwa chambo, na wakati mwingine hawajui kabisa jinsi hizo picha
zinavyochukuliwa…..’akasema
‘Lakini inavyoonekana watakuwa walishamweka kamamtu muhimu
katika hilo kundi,kwahiyo alikuwa akijua mengo ya hilo kundi,au sio?
nikamuuliza.
‘Sizani kuwa atakuwa anajua undani wa hilo kundi,hakuwa
kiongozi au mtu wa ndani sana, lakini yeye kwa urembo wake, na ustadi wake,…kwa
mambo fulani, walipenda sana kumtumia kama munganishaji, najua wewe unamfahamu
kwa makeke yake, maana wewe ni mmoja wa wahanga wake, siku zile nakutonya
unaniona nakuzibia riziki,….unapata vitu adimu,….bahati yako, maana wengi walioingia kwenye anga za
huyu dada, hawapo, na kama wapo wapo mbendembende…’akasema na kucheka.
‘We acha tu,…kama angelitulia kama alivyoniahidi,mmmh, ….
hata hivyo, nina uhakika kuwa hakutaka kunifanyia mabaya kiasi hicho ….ila najua
alifanya hivyo kwa sababu alilazimishwa…’nikasema.
‘Ni kweli, alishaniambai kuwa wewe ni mtu muhimu kwake,….ila
anafanya hayo kutokana na maagizo,.na alidai wakati mwingine alikuwa kikushauri
usifanye mamb fulani,lakini wewe ukawa huwezi kujizuia…na wewe bwana, ….halafu
unanihoji kama vile huji nini kilikuw akinaendelea kwenye hilo kundi.’akatulai
kidogo.
‘Alikuwa akipata maagizo kutoka kwa huyo mwanamama, au sio..na
nakushangaa, ina maana Kimwana laikuwa akikuhadithia kila jambo lililokuw
alikitendeka huko, maana naona unajau mengi?’ nikauliza.
‘Maagizo,ndio, kutoka kwa huyo, nani zaidi tena,….hayo
alinihadithia karibuni, wakati ananionye kuwa nisikuambie, kuwa yupo wapi,
hakuw aakitoa siri za watu hawo, alikuwa akiogopa,…’akasema na kuangalia huku
na kule., kama vile anagogopa kusikiwa.
‘Kimwana sasa kaondoka, na natumai kundi lina mashaka
sana,sio wao wameamua kumuua baada ya kumhisi kuwa atawasaliti..?’ nikauliza.
‘Mhh,sizani, ila kwakweli kifo cha Kimwana kimewaweka njia
panda, ….nasikia huyo mama kawa mbogo, katoa maagizo kwa polisi kuwa aliyemuua
huyo mtu wake, akamatwe haraka…eti anajulikana’akasema.
‘Anajulikana au wanajuana, sinasikia kuwa wamegeukana
wenyewe kwa wenyewe…, ndio hivyo wameanza kuuana?’ nikamuuliza.
‘Huyu mama anasema kuwa inasemekana aliyemuua ni mwanamke,….ambaye kwamudamrefu amekuwa akimsaka huyo Kimwana, wapo mashahidi waliomuona, anasema kuwa siku
hiyo, huyo mwanamke alikwenda akishirikiana na jamaa mmoja,na huyo jamaa
alianchwa getini na walinzi, huko ndani huyo mwanamama akamuua Kimwana,..’akasema
huyo mwanadada na kunifanay nianze kuogopa.
‘Haiwezekani, watakuwa wanajikosha tu, …ni ni mama gani huyo?.’nikasema kwa
wasiwasi nikauliza
‘Kwanini isiwezekane, Kimwana ana maadui wengi wenye kisasi na yeye, na hawo watu hawajui kuwa yeye ni kama kibarua tu, ...najua kiukweli mtu wakipta hiyo nafasi wataitumia tu…haijulikani kuwa ni mwanamke yupi, lakini wanahisi huenda ni wakili, sasa hatujui ni wakili yupi, maana wapo wengi,...'akasema nakutulia, halafu akaongezea kusema;
'Ndio Kimwana alikuwa rafiki yangu, lakini hata hivyo
sioni ajabu hilo likitokea, ….na kwakweli nitamkosa sana,maana kila nikikwama
nilikuwa nakwenda kwake,sasa…keshaondoka,…’akasema na kuonyesha uso wa huzuni.
Haraka haraka nikatoka hapo nikiwa na wasiwasi baada ya
kusikia hayo maneno, nikaona ni vyema nimtafute mwanadada wakili ili nijue nini
kinachoendelea, na kila nilipopiga simu yake ilisema kuwa inatumika, hapo
nikaanza kugopa, maana kwa hayo maelezo muda wowote naweza kukamatwa, na mimi
sitakubali kuingia tena jela,
‘Sasa nifanyeje…?’ nikajiuliza na wazo likanijia kuwa ni
bora niondoke kabisa hapa jijini.
Nilihakikisha kuwa sionekani maskani au sehemu ambazo wengi wanajua
kuwa napatikana huko,nikawa napiga chenga huku na kule, nikitafuta mwanya w a
kuonana na huyo mwanadada wakili, lakini hakuweza kupatikana.
Na mara nikapata taarifa kuwa natafutwa na polisi….hapo
nikachanganyikiwa na ndipo nikaamua kuwa vyema niondoke hapa jijini, na bila kuchelewa nikajindaa kuondoka, na harakawazo likaniji akuwa sio vyema kwenda huko kwetu kijijini, huko watanikamata kirahisi, nikaona niende hapo jirani, Morogoro,huko kuna marafiki zangu, nitajibana kwa muda, na bila kuchelewa, nikachukua dala dala hadi Ubungo.
Ilikuwa wakati nasubiri mabasi ya kwenda Morogoro, mara pembeni ya barabara, nikaona gari kimesimama, na macho yangu yakaona sura ya mtu, ambaye alinijia akilini, nikalisogelealile gari, lakini huyo jamaa alikuwa akiongea an simu, hakuwa kaniangalia moja kwamoja, ilionekana kuwa simu ilimteka akili, na alikuwa akongea kwahasira, akisisitiza jambo, nilipomtupia macho na yeye akaniangalia tukawa tunaangaliana, nikamkumbuka ….ooh, ndio yeye, ndio yule .muuaji wa Kimwana….
Je kilitokeanini..?
NB. Nimeona siku isipite hivi hivi, angalau niweke sehemu
hii ndogo kama nyongeza ya sehemu iliyopita kabla hatujaingia kwenye hitimisho, kwani mambo yenyewe mazito, tuombeane heri.....
WAZO LA LEO: Mara
nyingi utaona umuhimu wa mtu akishaondoka..Nawatakia Ijumaa njema.
Ni mimi:
emu-three
7 comments :
Kaka una moyo SANA,Mara nyingi unajitahidi kupost mapema,nadhani una karma Fulani hivi .MUNGU aendelee kukutunza
Nashukuru kwa kunipa moyo huenda ndio hivo, kwani nikianza kuandika wala sijajua nitaandika nini nakuta yanakuja yenyewe . Namuomba mungu iwe hivyo
inasikitisha sana binadamu hujuwi mbele mungu kaandika nini tuombeane kheri
jumaa karim
Samira ni kweli mjuzi wa yote hayo ni muumba pekee. Vipi Samira ulipotea kidogo!
kweli nilipotea kidogo yote nakimbizana na life lakini tupo pamoja
mkasa umenoga life life m3 ni ngumu sana
Ni kweli Samira, life ni ngumu sana, na je ukilinganisha huo ugumu wa huko ulipo na huku kwetu huoni ni aheri ya huko...lakini vyovyote iwavyo, yote ni maisha usikate tamaa, mungu yupo kwa wote wenye kusubiri..Tupo pamoja.
Pia kimiya kingi kwa wadau wengine kama akina Subira, Precious,elisa, Pam,Ammy na wengineo mpo wapi? Msinichoke mapema hivi...au kuna tatizo?
my dear ukweli bora huku sana kwani ukiwa si mvivu wa kazi kinaeleweka. utapiga hata kazi mbili kwa siku tofauti bidii yako tu .lakini huko unaweza kuwa na bidii ya kufanya kazi na kisieleweke jamani ,tuombeni mungu atuhifadhi
Post a Comment