Wakili mwanadada
alitizama saa yake na baadaye akamtupia jicho mkuu wa kituo ambaye alikuwa
kainama akisoma majarida mbali mbali ya kesi bila kumjali. Ilikuwa kama vile hakuna mtu mbele yake, na
kipindi cha muda kikapita bado wakiwa vile kimiya, mkuu akiwa na mafaili yake,
na mwanadada akiwa kakaa pale, huku akionyesha uso wa kukereka.
Baadaye yule mwanadada akainuka kwenye kiti, akipiga miayo,
halafu akajinyosha, na wakati anafanya hivyo yule mkuu wa polisi akainua uso na
kumwangalia kwa jicho la kujiiba, akatisa kichwa, huku akiwaza yake kichwani,
hakusema neno, ….
‘Hivi utaniweka hapa mpaka saa ngapi maana kila kitu
nimeshakuambia, unataka nini zaidi?’ akauliza yule wakili.
‘Nataka uniambie kila kitu,….tatizo lako unatufanya sisi
hatujui, sisi kila kitu tunajua,…wakati mwingine tunawezakukuuliza kitu kupata
ukweli wako, sisi tunajua sheria, na tunaifuta baada ya kufanya uchunguzi na tunajua
hata hicho ulichoficha kicwani mwako,…’akatulia na kumwangalia.
‘Unajua waakti mwingine nawaza sana, hebu nikuulize wewe
binti mzuri kwanini unataka kujiingiza kwenye matatizo , hili nilishakuambi ni
kazi ya polisi,lakini wewe unajifanya mjanja, sasa utakaa hapa mpaka tukamlishe
huo uchunguzi wetu. Nisingelipenda wewe ukalale gerezani eti unashikiliwa kwa
mauaji,….sipendi kabisa…’akatikisa kichwa huku akimkazia huyo mwanadada macho.
‘Mkuu, siwezi kufanya jamboo kama hakuna sababu, na ….ngoja
kwanza, nikuulize ni muda gani wakili kama mimi nastahili kushikiliwa na
polisi….?’ Akauliza.
‘Hata siku nzima, ilimradi zipo sababu za msingi za kukushikilia,
na usizani kuwa hatuna sababu, tunazo
taarifa kuwa siku ile ya tukio ulikuwepo, na ukiunganisha na mashitaka
yaliyokuja kuwa wewe huenda umehusika na kifo cha huyo mwanadada, tunasababu ya
kukushikilia ili utoe ushirikiano, huku tukiendelea na uchunguzi….’akasema huyo
mkuu
‘Kama hiyo ndiyo sababu muhimu ya kunishikilia,mbona
mumeshanishikilia na sikukataa kuja hapa licha ya kuitwa bila utaratibu, hakuna maelezo kwanini naitwa huku kituoni, nimechukuliwa kienyeji tu,.... nimeitikia wito wenu, nimekuja hapa, mumeniuliza
maswali nimewajibu, nimekaa muda muafaka, ….kitu gani zaidi mnahitaji kuhusu
mimi…..?’ akauliza.
‘Tunaendelea kukushikilia kwasababu tuna imani kuwa
hujatuambia kila kitu,….tumekuuliza maswali, lakini mengine umekataa kutujibu,
kuonyesha kuwa unatuficha ukweli,…sasa
kwa vile unatuficha ukweli, ngoja tufanye uchunguzi kwa kupitia njia nyingine,
huku tukiendelea kukuhoji, na tutaendelea kukuhoji mpaka turizike na majibu
yako,…’akatulia na kuangalia saa.
‘Haya endelea kunihoji,….maana nusu saa imepita, upo kimiya,ndio
kuhoji gani huko?’ akauliza huyo mwanadada.
‘Nasubiri majibu ya maswali niliyokuuliza mwanzono ambayo hujanijibu...’Akasema mkuu.
‘Maswali yapi ambayo sijakupa majibu, angalia kumbukumbu
zako vyema,kila swali nimeshakupa majibu yangu, sijui ulitaka majibu mengine yapi, labda unifahamishe vyema…’akasema wakili.
‘Kuna habari kuwa ulikuwepo wakati maujai hayo yanafanyika, na
uchunguzi ukikamilika, tunaweza kukushika kwasababu ya kushukiwa katika
mauaji,…isingelikuwa mimi nakufahamu vyema , ungelishashikwa kwa ajili hiyo,
lakini mimi nakufahamu vyema,huwezi
ukafanya jambo kama hilo. Na usichukulie hilo kama kigezo kuwa, kwasababu
nakufahamu kwa hivyo, ndio niache sheria isifanye kazi, yake, hapana, ….sheria
ipo pale pale….’akatuli na kuangalia jarida moja wapo alilolifungua.
‘Mkuu hujaniuliza swali hapo, hayo ni maelezo, naomba
uendelee kuniuliza maswali, kama yamekwisha muniambia….’akasema mwanadada. Mkuu
hakusema kitu akawa katulia akiandika kitu kwenye yale mafaili aliyo nayo pale
mbele, na yume mwanadada akasema;
‘Sikiliza nikuambie kitu mkuu, ngoja niondoke, maana
kunishikilia hapa tunapoteza muda na kuna mambo yanasimama, mambo ambayo
yangelitusaidia kukiangamiza hiki kikundi, mimi nina njia yangu, na nyie mna
njia yenu, habu niachieni nifanye nionavyo mimi, muone nini kitatokea….mtafurahi
wenyewe…’akasema.
'Unafanya hiyo kazi kwa nani, hujatuambia mteja wako ni nani,...pili nimekupa huo muda umeshindwa kuutumia….’akasema huyo mkuu.
‘Muda gani ulionipa mkuu….?’ Akauliza.
‘Hapa nimekupa muda wa kutosha ili uniambie ukweli,…hujataka
kufanya hivyo, hutaki kuniambia huo ukweli, hii ina-niweka katika mahali ambapo
sitaweza kukuamini….na kama utaendela hivi, usishngae nikikubadilikia, maana
mimi nafuta sheria na taratibu za kikazi yangu, kujuana isiwe ni kikwazo kwenye
taratibu za kazi yangu…’akasema
‘Muda wa kukuambia ukweli ukifika nitakuambia mkuu, ujue
mimi ni wakili, sitaweza kusema kitu mpaka niwe na ushahidi wa kutosha,….ndio
maana naomba kibali chako,… kunishikilia hapa hakutasaidia kitu, wewe
unanifahamu vyema, sio mtu wa kuongea ovyo bila ushahidi uliojitosheleza….na
mkiendelea kunishikilia hapa ushahidi wote niliotarajia kuupata utapotea,…na hata
huyo muuaji anaweza akapotea pia na matokeoa yake mtashikilia watu wasio na
hatia….’akasema .
‘Haya tusaidiene , niambie ukweli siku ile ya tukio la
mauaji ya huyu binti anayeitwa Kimwana, ulikuwa wapi, ukinijibu hilo swali
tunaweza tukaenda sambamba….?’ akauliza.
‘Nimeshakuambia kuwa nitalijibu hilo swali nikisha kusanya ushahidi wangu wa kutosha,…
tunarudi kule kule kwenye maswali yenu, uliyoniuliza awali,, na amjibu
nimeshawapa….na kama mna mashaka na mimi kuwa nimehusika katika hayo mauaji,
basi nishikeni kwa uhalifu huo, …lakini fuatenu utaratibu wa kisheria...’akasema
wakili.
‘Haya kama hutaki kunijibu hilo swali utaendelea kukaa hapa
mpaka hapo vijana wangu watakapofanya uchunguzi wa kutosha….na ole wako
ikigundulika kuwa ulikuwepo au unajua nini kilichotokea na wewe unaamua
kutokushirikiana na polisi….na kuficha ushahidi’akasema huyo mkuu wa polisi na
Mwanadada wakili akangalia saa yake, na alipoona muda wa yeye kushikiliwa pale
umekwisha akachukua mkoba wake na kuinuka.
Aliposimama, akasita pale alipoona anajiona kwenye kiyoo che meza, ya hiyo ofisi, akatabasamu na kusema;
'Nyie mnajitahidi sana mkuu, meza ya kiyoo....haya tuyaache haya ...hebu niambie, ushahidi gani ninaouficha...?'akasema na huku akiwa kashikilia ile meza huku akijiandaa kuondoka.
'Tatizo lenu mnawachukulia kuwa ofisi za maaskari hazitakiwi kuwa za kuvutia wateja,...nyie ni wateja wetu mnahitaji pia mjisikie vizuri mkiwa kwenye ofisi zetu, au sio....unaionaje hiyo meza.....?' akauliza na alipoona wakili hajibu kitu, kamkazia macho akisubiri jibu la swali alilouliza akasema;.
‘Kuna kitu alikuwa nacho marehemu, simu na saa, kama ujuavyo kuwa hivyo wamekuwa wakivitumia kama alama zaoza kujilinda na kujitambusliha wapi walipo,...na pia hivyo vifaa vinanaswa kwenye mitambao yao , na kama tungelivipata, vingelitusaidia kuona tukio nzima lilivyokuwa,.....tunao wataalamu wakuweza kuvitumia na kugundua nini kilitokea, ...hivyo vifaa tunauhakika, alikuwa navyo marehemu, na ni ushidi muhimu kwetu,…’akasema huyo mkuu.
‘Kwahiyo mnanishikilia kuwa ninavyo hivyo vitu au sio, au
mnanishilia kuwa nimehusika kwa hayo mauaji, ….niembeni wazi, ili nijue vipi nitajitetea…?’
akauliza huyo mwanadada.
‘Tumekuita hapa kwa kukuhoji, kutaka kujua ukweli, wewe kama
wakili tuna imani kuwa utatuambia ukweli, ili na sisi tuweze kufanya kazi yetu
vyema…’akasema mkuu.
‘Kama mnataka kunsihikilia kwa makosa hayo, ya kuwepo huko,
ya kuchukua ushahidi, naomba mfuate taratibu,…., lakini muda wangu wa kukaa
hapa umekwisha na naona huna maswali mengina ya kuniuliza, kwahiyo sina budi
niondoke…’akasema huyo mwanadada na kuanza kuondoka.
‘Unakwenda wapi…?’ akauliza mkuu wa kituo huku akimwangalia
kwa hasira.
‘Muda ambao mimi kama wakili wa kushikiliwa hapa umekwisha
kama unataka kunichukulia hatua chukua, na mniambie ni kwanini mnanichukulia
hizo hatua kwa kosa gani, ….lakini tafadhali, naombeni mfuate taratibu za
kisheria, na tutakutana mahakamani….’akasema yule mwanadada huku akiwa
hamuangalii huyo mkuu usoni, akiwa na wasi wasi na hiyo hatua anayoichukua…..
Yule mkuu wa polisi akamtizama kwa muda yule
mwanadada,…alikuwa keshafiki hatua ya kumuachia, lakini kitendo cha yule
mwanadada kuamua kujiondokea,
hakikumfurahisha, akiona kama vile kazarauliwa. Na hapo hasira
zikampanda huku akiwaza achukue hatua gani ili huyo mwanadada amuheshimu,
akasogeza mkono wake pale ilipo simu ya mezani, kutaka kuwapigia vijana wake,
waje wamkamate huyo mwanadada na kumweka ndani.
Na kabla hajafanya hivyo,mara simu ya yule wakili ikalia
kuashiria ujumbe mfupi wa maneno, akasimama , na kuusoma kwa haraka huo ujumbe,
na baada ya kumaliza kuusoma ule ujumbe, akageuka na kumtizama mkuu ambaye
alishainua simu ya mezani, kutaka kupiga namba, ila alisita pale aliposikia
mlio wa huo ujumbe toka kwenye simu ya huyo mwanadada, wakataizamana machoni.
‘Haya niambie, maana nataka kuchukua hizo hatua za kisheria unazozidai,
kwa mamlaka niliyopewa na jamuhuri,…sema kuna nini kimetokea maana wewe
unajifanya polisi, ….badala ya kufanya kazi yako ya uwakili unaingilia kazi
zisizo kuhusu,…niambie, huo ujumbe unasemaje, maana unavyoniangalia inaashiria
jambo…?’ akauliza.
‘Umesema kuwa unanihitaji mimi nishirikiane na nyie, kuhusiana
na mauaji ya Kimwana,, sasa soma huu ujumbe halafu uniambie unataka nini
zaidi….’akasema na kumpa yule mkuu ule ujumbe wa maneno, ujumbe ulitoka kwenye
namba isiyo na jina ulisema;
‘Yule muuaji yupo kituo cha Ubungo, anakimbilia Morogoro, ….fika haraka
hapa kituoni, kanipa lifti, lakini kuna foleni, gari aina ya landcruiser T908
CSA…..’
‘Huu ujumbe umetoka kwanani?’ akauliza yule mkuu huku
akiuangalia ule ujumbe na kumtizama huyo wakili na kuutizama ule ujumbe tena.
‘Hilo sio swali la msingi kwa sasa, cha muhimu ni wewe
kufanya akzi yako, au twende huko ukapambane na huyo muuaji mwenyewe,…..’akasema
huyo wakili huku akiangalia saa yake, na alipoona huyo mkuu hasemi kitu,
akasema;
‘Kama bado unataka kuendelea kunishikilia hapa , naona muda
wangu wa kuwasubiri umepita, sina budi niondoke, na kama mna lolote juu yangu,
fuateni taratibu za kisheria, kwaheri….’akasema yule wakili akianza kuondoka,
na kabla hayatembea hatua mbili yule mkuu wa kituo akainuka na kusema.
‘Subiri….tunakwenda wote, maana hutaweza kupita kwenye
foleni mimi nina uwezo wa kufanya hivyo…najua jinsi gani ya kufanya….’Akasema
na kupiga simu kituo cha ubungo na kuamrisha kuwa gari aina hiyo ya Landcruser,
T908 zSA…..lishikiliwe, lakini kwa mbinu ya kuchelewesha foleni, na kama huyo
muendesha hilo gari atataka kutoroka wahakikishe wanamkamata.
*******
Jangiri, akiwa kashikilia simu sikioni, alisikiliza ile simu
ikiita na kila mlio wa kuita ulivyokuwa ukisikika masikioni mwake ndivyo
alivyozidi kupandwa na hasira, akatizama mbele yake na kuona msururu wa magari
kuonyesha kuwa foleni ni ndefu ajabu, na nyuma yake halikadhalika,huku akiwa
kashikilia hiyo simu sikioni,
Foleni kwa muda ule haikumtia wasiwasi sana, alijua muda wowote magari yataruhusiwa ataondoka, lakini kilichokuwa kikimuuma na kumtia wasiwasi ni jinsi gani ataweza kuishi huko ugenini, anahitaji pesa, na alishaahidiwa kuwa atazipata. Sasa hizo pesa hazijapatikana na kwa ujumla hana pesa kabisa, huwa yeye akipata pesa ni za matumzi kwa kwenda mbele, hana hata akiba….
Mara siku ikapokelewa na sauti ya mtu ikihema, kuonyesha
kuwa hayupo katika hli njema ya kuipokea, ila kaipokea tu , kwa vile hakuna
jinsi. Na huyo mpokeaji akasema kwa sauti nzito ya kike;
‘Niambie,…’
‘Bosi,Pesa zangu , vipi, ….unajua mimi hapa sina pesa, na
hizo ndizo nategemea kunisaidia huko ninapokwenda,unakumbuka ulivyoniambia,
…hapa penyewe sina uhakika wa petrol kuwa inaweza kunifikisha huko
ninapokwenda…foleni imebana `uwese’ unateketea,’akasema na huyo mtu sehemu ya
pili akawa katulia kimiya hamjibu kitu, na baadaye huyo mtu sehemu ya pili
akasema.
‘Umemaliza….?’
‘Ulitaka niongee nini zaidi Bosi,….mimi naona nimemaliza….nakusikiliza
wewe bosi,’alitaka kupayuka, lakini akagundua kuwa anaongea na nani ,akatulia
kusikiliza.
‘Hivi wewe umenisahau, ushajiona mtu wa maana sana, ...kwanza
umeharibu, pili unadai pesa kama zako, wakati huna ulichokifanya,….nini
makubaliano yetu, fanya kazi upate pesa, ukiharibu hupati
kitu,…umeharibu,…nakuuliza hujaahribu?’ akaulizwa.
‘Lakini Bosi….’akaanza kujitetea.
‘Jibu swahli, umeharibu au hujaharibu, mimi nimeamua kukupa tu hizo pesa…. tu,kwa vile
wewe ni mtu wangu wa siku nyingi, vinginevyo nisingekupa hata senti moja,
kwanza hustahili hata kupata hiyo nafasi yakuongea na mimi, ilitakiwa sasa hivi umeshabadilika
jina na kuitwa marehemu….umenisikitisha sana,…hujui tu, ….unajua thamani ya
huyo mtu uliyemuondoa duniani bila hatia…’akasema huyo mtu na kutulia.
‘Bosi nilishakuambia ni bahati mbaya…na tupo kweny simu,
hayo tuyaache,….unajua bosi hata mimi imeniumiza sana wewe hujui tu,
..nashindwa hata kulala, kuona kuwa mkono wangu umemuondoa mtu niliyekuwa
nikimpenda sana….sijui nifanyeje,lakini sina jinsi maji yameshamwagika, lakini
naahidi kuwa nitalipiza kisasai chake tu….’akasema.
‘Utalipiza kisasa chake kwa nani , wakati wewe ndiye
uliyemuua, ni nani aliyekuambia umuue..basi jiue mwenyewe ndio tuseme umelipiza
kisasi chake….na inabidi iwe hivyo, sioni umuhimu wako tena kwangu…’akasema.
‘Bosi tupo kwenye simu bosi,…..na eti nini, ina maana mimi sasa
huoni umuhimu wangu tena, siamini masikio yangu….’akasema huku hasira zikimpanda,
na akawa anawaza jinsi gani ya kufanya kutokana na kauli ile,….hasira za siku
nyingi kuhus huyo bosi zikamrejea, alishaapa kuwa akimpatia nafasi atamfanyoa
kitu mbaya aishilie pasipojulikana, lakini ndiye aliyemfanya aishi hapa
mjini,….akanywea.
‘Hebu niambie, hivi sasa una umuhimu gani, wakati unatafutwa
kila kona, na wewe ukishikwa unaweza ukapanua hilo domo lako, nakuhakikishia
kuwa kama utapanua hilo domo lako, hutakatiza masaa, …nitahakikisha mwenyewe
unalia kama mtoto mdogo kabla hujaenda kuwa chakula cha mchwa….unasikia ?’
akasema.
‘Bosi…bosi, ina maana huniamini..mimi sio mtu wa kuongea
ovyo,…watanifanya nini mpaka niongee….bosi , tafadhali naomba sana, kuhusu hizo
pesa , mimi nitalipiza kisasi kwa huyo aliyesababisha hayo, maana kama isingelikuwa
huyo wakili, natumai mambo yangelikuwa safi…sasa huyo wakili ndio kaharibu,
nitakula naye sahani moja, wewe utaona tu,…..ngoja nikatulie huko mafichoni kwa
muda….’akasema.
‘Hayo unajua wewe, …ila kama ulivyosema, sitaki nkuone hapa
mjini,na nikikuona hapa jijini sitaongea mara mbili, mimi mwenyewe nitahakikisha
risasi imepenya kwenye ubongo wako kama ulivyofanya kwa huyo binti
yangu,…..natamani kama ungelikuw akaribu nikafanya hivyo, ….pesa nimeshatuma
kwenye mtandao, nenda kibandani kachukue….’sauti ikasema.
‘Nimekwenda kibandani hakuna kitu, hapa kwenye salio la simu
inaonyesha kabisa hakuna pesa iliyoingia, …nimeangalia sasa hivi kabla
sijakupigia simu hii ni mara ya tatu naangalia, hakuna pesa
iliyoingia….’akasema kwa sauti.
‘Unajua unaongea nani, na kamwe usiniongelee kwa sauti ya
ukali,…. kwasababu hunidai, unasikia mimi natoa pesa kukusaidia tu…na pesa hiyo
nimeshaingiza kwenye namba ya simu yako, labda ni tatizo la mitandao,
usinisumbue, …’akatulia na kabla Jangiri hajasema kitu, akasikia sauti ya ukali ikisema;
‘Unasikia na ukinipigia simu tena na kuniongelea kwa hasira
kama vile mimi ni mkeo,…ukirudia tena, nitahakikisha simu yako haitoi sauti,na
masikio yako nayaziba…unasikia, usione upo mbali ya upeo wa macho
yangu,ukazania ziwezi kukufanya kitu, ….angalaia salio hata mara kumi,ni juu
yako ….unasikia …akili yako ndogo isiyo na maana….’simu ikakatika.
‘Na wewe akili yako kubwa lakini chafu, haina maana pia….’akasema lakini alipohakikisha
kuwa simu haipo hewani, na akawa mawazoni akijuliza kwanini huyo mwanamke
anamchezea, hajui kwake kumaliza uhaii wa mtu ni mara moja,…alipofikia hapo
akaanza kujuta, alijuta kwa vile mkono wake umemuua mtu aliyempenda, akaivuta
sura ya huyo binti na kumuwaza na kukubuka siku ile ya tukio livyokuwa.
*******
‘Huyo mwanadada wakili yupo, anaonekana katika mitambo yetu,
ingawaje imekatika, hatuna uhakika na usalama wa mtu wetu, hakikisha unammaliza
huyo wakili,….hakikisha hakuna ushahidi….’simu ikamwambia.
Harakaharaka akaichukua bastola yake na kuivalisha kiwambo
ya kuzuia sauti, akasogea hadi kwenye dirisha, dirisha hilolipo ndani ya chumba
kinachoangalina nachumba kingine,…lakini pazia ikawa kizuizi, asingeliweza
kulisogeza hilo pazia, kwasababu lipo upande wa pili ….
Akatafuta upendo na bahati akamuona bosi wake yupo kwa ndani
na kweli akamuona huyo aliyeambiwa ni wakili, akiwa kasimama, ulikuwa usawa
wake, na hapo ilikuwa nafasi nzuri kabisa, alijua kabisa hapo anaweza
kuitumbikiza risasi kwenye kichwa cha huyo wakili, bila ya kumzurubosi wake.
‘Akasogeza na kulenga shabaha, na wakati keshabonyeza kitufe
cha kufayatulia risasi, bosi wake akasogea ni kuwa sambamba na wakili, na
wakati huohuo wakili alishainama, ….ooh, kilichotokea hakuamini…
.
‘Lakini nakumbuka kama vile risasi niliyoipiga hakulenga,
…maana yule mwanadada aliinama...na bosi hakuwa katika lengolangu, alikuwa kasimama tenge,....ilikuwaje pale.....hapo sina uhakika,....na mimi mjinga kweli, kwanini sikuutafuta huo uhakika, ….maana alivyokuwa
kasimama yule wakili na akainama,risasi isingeliweza kumlenga yule bosi wangu,
.isingeliwezekana….pazia lile lilificha ukweli,…sijui, lakini nani mwingine
angeliweza kufanya vile, …maana tulikuwa peke yetu, nina uhakika huo…ooh, nimemuua Kimwana tulizo la roho yangu ,
hapo sina cha kujitetea….’akasema kwa sauti ndogo.
Alipofikia hapo akahisi machozi yakimlengalenga, ingawaje hana hisia za kulia, `Ina maana mimi
kweli nimemua mtu ambaye moyo wangu ulishampenda,na nakumbuka siku moja nilishamuambia kuwa ninampenda kuliko kitu ingine, na nilikuwa tayari kumpa chochote ili anikizie
matakwa, yangu, akanitolea nje, lakini nilijua ipo siku atanikubalia tu, sasa keshaondoka imebakia hadithi….,
Kumbukumbu zile zilipoyeyua kichwani, akaangalia salio kwenye simu yake, kwenye mtandao, akakuta pesa
hakuna, akairusha simu kwa hasira kwenye kiti, mpaka ikafunguka na vifaa vyake
vikasambaratika kila kitu kivyake, na wakati anataka kuviokota vifaa hivyo vya simu
alipogundua kuwa kafanya ujinga, mara akaona mtu kasimama pembeni ya gari akimwangalia,
na yeye akjikuta nashikwa na hamasa ya kumuangalia.
‘Huyu mtu nilimuona wapi….’akajiuliza na kusahau kuokota
vile vifaa vya simu, na cha kushangaza akaona huyo mtu akisogea karibu na gari
lake, akasema kimoyoni, asije akawa askari kanzu katumwa kumkamata, kama ni
askari kanzu hatakubali kukamatwa kirahisi hivyo, lakini alipomuangalia yule
mtu kwa makini akagundua kuwa hana sura ya uaskari kanzu.
‘Rafiki, unaelekea Morogoro….’mara akasikia huyo mtu
akiuliza, na akashusha kiyoo na kumwangalia kwa makini,nankumuuliza huku akiwa
kakunja uso kwa hasira.
‘Kwani wewe ni nani mpaka unaniulzia swali kama hilo..?’
akasema kwa hasira, na baadaye akaona ajilainishe maana asije akaleta vurumai
na polisi wakaingilia kati.
‘Mimi ni msamaria mwema tu, nimekwama na nahitaji kufika
Morogoro haraka, hapa jijini hakukaliki tena….’akasikia huyo mtu akiongea, na
maneno hayo yakampa faraja, na alipomuon ana begi la safari, akaona atapata mtu
wa kusadiana naye akikwama njiani, na mawazoni akasema kumbe na wewe una mawazo
kama ya kwangu.
‘Ingia, najua utachangia mafuta, hakuna cha bure
hapa….’akasema na huyo jama akafungua mlango na kukaa pembeni kama abiria.
‘Sura yako sio ngeni kwangu, nilikuona wapi vile?’
akamuuliza.
‘Kwakweli sikumbuki,tatizo mimi huwa sikumbuki sura za watu,
…kwanza nizikumbuke za nini..zitanisaidia nini mimi,labda kama ni suta za pesa,
njua nitapata pesa,….’akasema huyo jamaa.
‘Ina maana sura yangu sio ya pesa…?’akauliza Jangiri.
‘Siwezi kujua, …..cha muhimu ni kuzitoa sio kuonekana, …na hizi
foleni bwana , mbona leo hizi foleni zimezidi, watu tunataka tuongelee ndani ya
mji wa Moro…’akasema huyo jamaa.
‘Hata mimi zinanichosha,….lakini hakuna jinsi, hapa huwezi
kupenya popote, kwa hali ilivyo, inabidi kusubiri tu, tukipata upenyo, gari
litapaa , maana spidi ya kuondoka nayo, inabidi ufunge mkanda,…au unaogopa
kufa, mimi nikiwa kweney gari siogopi kufa,….naendesha kama sina roho….shauri
lako,kama umwoga bora ushuke kabisa….’akasema Jangiri.
‘Wewe usijali, ….ilimradi tufike tu, ……mbona naona vifaa vya
simu,….hii betrii ya simu, aah, hiki kifuniko,…na ile pale simu yenyewe,,,, ni
simu yako nini…?’ akauliza huyo abiria alipoona anakanyaga baadhi ya vifaa vya
simu.
‘Aaah, ….ndio ndio, wewe unafika kwenye nyumba unauliza
vyombo vilivyopo ndani ni vya nani,….unajua kuna mtu ninamdai, kanipandisha
hasira, na …’
‘Hasira unaimalizia kwenye simu, huoni kuwa utakuwa umepata
hasara mara mbili…’akasema huyo abiria.
Jangiri akainama kuokoteza vifaa vyake vya simu, na hapo
jamaa akapata muda wa kuandika ujumbe wa maneno kwa haraka na kuituma kabla
Jangiri hajainuka. Alipoinuka akaifunga simu yake vyema, na baadaye akajaribu
kupiga, lakini huko alikopiga ikawa simu haipatikani, akajaribu kuangalia
salia, akakuta hakuna pesa iliyoingia, akasonya na kushkilai usukani wa gari
kwa hasira,….
‘Sasa itakuwaje,maana sina pesa, na ninapokwenda natakiwa
gharama,hoteli na ……na kwamtaji huo itabidi nifanye jambo ambalo sikutaka
kulifanya,…sasa utaishije na halikama hii,..ndio maisha yetu…’akasema akiwa
kasaahu kuwa kuna abiria pembeni yake.
‘Jambo gani la kuingiza pesa maana hata mimi ni mtafutaji….nipo
tayari nikupe mkono, …..hata kama ni kubeba mizigo, au kuwa otingo wako nipo
tayari….’akasema huyo abiria na kumshitua dereva wake,ambaye alishasahau kuwa
ana abiria, kutokana na hasira alizokuwa nazo, akamgeukia na kusema.
‘Hebu niambie tulikutana wapi,maana nina uhakika kuwa
nimekuona mahali, sura yako naikumbuka, lakini sijaweza kukumbuka ni wapi…..na
kwa vile leo akili yangu haijatulia vyema, nashindwa kufikiria nilikuona wapi,….kwani
unafanyia wapi shughuli zako..?’
akauliza.
‘Nimeshakuambia kuwa mimi huwa sikumbuki sana sura za watu,
mimi ni mbangaizaji tu hapa na pale, leo tunafuuzwa na city hapa. Tunakimbilia
kule, leo nimepata kibaru hapa, ilimradi siku zinakwenda, kwa ufupi mimi ni mtu
wa kufanya vibarua hapa na pale, ….nimejikuta maisha hayaendi vyema, nikaona
sasa ni bora nirudi kijijini nikatambike kidogo,….na wewe una kazi gani?’
abiria akauliza.
‘Misheni town….mimi ni mtu wa dili za hapa na pale,….’akasema
dereva, akijaribu kuangalia salio tena kwenye simu yake….na kabla hajaweza
kufikia sehemu ya kuonyesha salio, mara simu yake ikaita, na akabonyeza sehemu
ya kupokea bila kuangalia nani mpigaji, na aliposikia sauti ya mpigaji akataka
kuanza kualalamika, lakini sauti aliyosikia iliashiria vinginevyo, akatulia kusikiliza
kwa muda,na sura ikabadilika, ….simu ikanyamza na hapo hapo akatizama huku na
kule, na baadaye akasema;
‘Sikubali,….hapa lazima nitafute njia ya kuondoka,’ akasema
kimoyomoyo,… akaangalia nyuma, hakuna nafasi , mbele hakuna nafasi , akaangalia
pembeni kuna mtaro,gari haliwezi kupita…kwingine halikadhalika mtaro, akaguna, akashika
mlango kutaka kuufungua, lakini kwanza akageuka kumwangalia abiria wake, na
kusema;
‘Unasikia…, wewe kaa humo kwenye gari,nakwenda hapo dukani
kununua vocha, …’akasem Jangiri huku akiangaza macho huku na kule.
‘Vocha si hizo hapo pembeni muite huyo jamaa akuletee,
foleni inaweza ikatembea na wewe haupo, na mimi hapa sina leseni…nani
ataendesha hili gari lako’akasema abiria,na mara sauti ya ving’ora vya magari
ikasikika kwa mbali, ikiashiria kuwa huenda
kuna msafara unapita …
‘Kumbe kulikuwa na msafara , ndio maana wanatugandisha hapa…hawa
watu bwana ina maana muda wote huo tunasubiri wakubwa wapite,hawajui kuwa kuna
watu wana safari zao za muhimukuliko hawo wakubwa zao…’akasema huyo abiria.
‘Ngoja tuone kama kweli ni msafara, au kuna jingine….hapa
nimechanganganyikiwa , kila dakika inanuka hatari,….na huyu,
keshanichanganaykabisa….sijui…’akasema Jangiri na kuangalia huko mlio wa
king’ora unapotokea.
‘Ni msafara huo, huoni kule….’akasema yule abiria, na
Jangiri akawa anaangalia huko sauti inapotoka kwa makini,lakini moyo wake
ulikuwa ukienda mbio, hakuwa na amani kabisa, alishahidi kuwa hakuna usalama, a
lengo lake lilikuwa kutoka pale kwenye gari na kukaa kwa mbali hadi atakapoona
kuwa magari yameruhusiwa ndipo aingie kwenye gari lake, hakutaka kabisa
kukamatwa kirahisi rahisi, akakumbuka bastola yake alioificha ndani ya gari,
lakini haikuwa an haja kwa muda.
Ni wakati sasa keshafungua mlango anajiandaa kutoka, kumbe
kwa nyuma kuna watu waliokuwa wakimchunguza kwa makini,na walipoona kuwa
anatakakushukakwenye gari, mmoja wapo akamsogelea na, na kusimama karibu yake,
lakini Jangiri alijua ni kati ya watu wanaopita barabarani, akamwambia abiria
wake.
‘Hapa siwezi kukaa, wewe bakia humo kwenye gari……na….’kabla
hajamaliza kusema akashitukia mtu akija pale mlangoni ,ambapo alishaufungua
tayari kushuka, na mtu huyo akatoa bastola na kumuonyeshea na kusema.
‘Mimi ni mwana usalama upo chini ya ulinzi…’ sauti kali
ikatoka na watu wengine wawili wakatokea kwa nyuma ya gari wakiwa nao
wameshikilia bastola tayari tayari. Jangiri kwa hasira akageuka kumwangalia
abiria wake ambaye alikuwa kaduwaa akishangaa, na alitaka kusema neno, lakini
alipomuona abiria wake akiwa akuduwaa, akanyamaza na kuwasikiliza wake maaskari
watasema nini, mara yule abiria kwa woga akasema;
‘Mimi simo,… niliomba lifti tu…..’yule abiria akajaribu
kufungua mlango akitoka kutoka, lakini akajikuta akionyeshewa bastola na kuambiwa
atulia kimiya.
‘Wewe unataka kwenda wapi, wote mpo chini ya ulinzi….’amri
ikatolewa.
NB: Haya jamaa haitaki jela, lakini alivy na bahati mbaya, kila
jambo analijiingiza anajikuta jela ikimnyemelea ni nini kitatokea, tuwepo ….je hakuna
maoni, je hii kazi mnaionaje…. ?
WAZO LA LEO:
Unapohangaika katika maisha yako,kamwe usisahau ulipotoka, tusiwasahau wazazi
wetu, na pia tusiwasahau wale tuliohangaika nao, hadi kufikia hatua tuliyo nayo
sasa, mshukuru mungu huku ukikumbuka kuwa inawezekana kabisa ukaporomoka…yote
ni mjaliwa ya mtoa riziki,…, kama wahenga walivyosema kuwa mpanda ngazi
hushuka, na huwezi jua, kwani
hujafa hujaumbika.
Ni mimi:
emu-three
4 comments :
Ahsante kwa Wazo za Leo ndugu wa mimi,pia nafurahi kuona kazi inasonga mbele,daima Pamoja ndugu yangu
Rachel, Wewe kweli ndugu wa mimi kwa shida na raha, mungu akubariki sana,Tupo pamoja
kazi nzuri m3 da yaani jamaa ana bahati mbaya kila anapopita lazma itokee ishuu
jela inanukia nasubiri nione itakuwaje
big up me upo juuuuuu
Amina ndugu wa mimi, Atubariki sote Ndugu yangu Pamoja daima!
Post a Comment