Nikiwa pale hosptalimoyo wangu ulikuwa ukidunda kwa haraka,
nikiwa na wasiwasi,…..na akili yangu ilikuwa bado haiamini kilichotokea, je ina
maana kweli nina hisia zinazoniongoza, au ni watu hao waitwao wahenga,…..hapana
hizo ni kudra za mungu, zilizoniongoza,..siwezi kabisa kuamini mambo hayo ya
mizimu, ….
‘Ahsante sana mungu, maana bila wewe yote haya
yasingeliwezekana…’nikasema na kuangalia juu, huku nikiwaza tukio nzima
lilivyokuwa na kabla sijafika mbali kimawazo mara docta akatokea, nikamsogela
na haraka nikamuulizia;
‘Vipi hali ya mgonjwa docta?’ nikauliza.
‘Mgonjwa hali yake sio mbaya, bado tunaendelea kumhudumia,
inaonyesha kuwa walimpiga sindano ya madawa ya kulevya, na tulichofanya ni
kuiondoa hiyo hali mwilini, na sasa keshazindukana,… na jereha la kichwani,
halikuleta athari kubwa …..na hata damu
haikupotea nyingi, usiwe na wasiwasi hali yake itakuwa njema tu….
‘Naweza kwenda kumuona…?’ nikauliza.
‘Mhhhh, Kwasasa hapana, …kwa vile bado hajazindukana vyema
na bado kuna huduma tunampa, wewe subiri kama saa moja hivi, akiwa tayari tutakuambia….wewe
ni mume wake,au…?’ akaniuliza docta.
‘Hapana mimi sio mume wake, ni rafiki yake….’nikasema.
‘Ok,haina shida ….mambo mengine tumeshayaweka sawa,…..tulishaongea
na watu wa usalama na wametueelekza kuwa huyo ni nani, na ….kwahiyo usijli sana…’akasema
huku akionyesha kuwa ana haraka ya kuondoka.
‘Sawa docta, niwashukuru sana kwa kazi yenu nzuri…’nikasema na
yeye akataabsamu na kusema..
‘Usijali hiyo ndio kazi yetu….’akasema na kuondoka.
Kiti kilikuwa hakikaliki,maana nilikuw ana hamu sana ya
kumuona huyo mgonjwa,..nikawa na kaa dakika chache mara nainuka, ilimradi hali
iliyokuwepo haikuniwezesha kutuliza kichwa, na baadaye nikawa nawaza jinsi
ilivyokuwa;
********
Siku hiyo nilipata kibarua kwa Mhindi mmoja, na baada ya
kupigika kitumwa, nikamwendea huyo Mhindi anipe mshiko wangu, akawa
ananizungusa zungusha, na hapo tukaanza kupandishiana, …kumbe ndio ilikuwa
tabia yake na wenzangu walipoona kuwa nampandidhia na wao wakajiunga pamoja na
mimi, wakaondoa uwoga waliokuwa nao mwanzoni, na hamaki ikachukua mkondo wake,
karibu ya kumpiga huyo Muhindi , ambaye baadaye alitoa hizo pesa huku
akitushutumu kuwa tumemharibia siku yake.
‘Kama ulikuwa huna hela ya kutosha kwanini ukatuajiri
wengi,….?’ Nikamuuliza.
‘Sio mingi nyie, ..tatizo mnadai pesa mingi….’akasema.
‘
Pesa mingi gani hizo, au ndio unatuzarau kuwa hatujui pesa,
mbona huyo ndugu yako msimamizi umemlipa pesa nyingi, pesa uliyomlipa yeye peke
yake ni sawa an jumla ya pesa yote uliyotulipa sisi wengi?’ nikamuuliza.
‘Yeye ni msimamizi, ..bosi wenu, lazima apate pesa mingi
mingi, kwanza yeye kasoma zaidi…..ni ‘expatriet’ ’akasema
‘Kwani yeye kanizidi nini mimi kielimu,,au kwa vile unaniona
nimekuja hapa kwako kuombakazi,mimi nimesoma hadi nje,lakini bahati yangu ni
mbaya tu…sijapata kazi, au kwa ajili ya ngozi yetu..?’nikasema
‘Kesho leta vyeti yako,mimi nitaajiri veye….kama iko soma,
naona waongea English nzuri veye..’akaniambi na mimi nikawa na imani kuwa sasa
nitapata ajira angalau ya kuvuta siku, sikuwa napenda kufanya akzi kwenye
kampuni yake, kwani nilivyomuona ni mbabaishaji, atanilipa mshahara mdogo
lakini ni heri kuliko kukaa nyumbani.
Nikachukua pesa yangu na kuelekea maskani….ambapo tunakutana
na marafiki kubadilishana mawazo, imekuwa ndio tabia yangu sasa, kila
nikihangaika mchana badala ya kwenda kulewa au kutumia pesa ovyo , nafikia hapo
kijiweni , na hapo Napata kahawa, huku tukiingia kwenye mijdadala mbali mbaliya
kimaisha,ndio maisha tutafanyaje….maisha bora kwa kila mtu.
‘Haya msomi umekuja,njoo hapa kuna ajenda ya leo,sijui wewe
unasemaje,kuhusu ndoa, kwasababu wewe umesoma na unadai umewahi kuoa mara mbili
au sio, sasa tuambie eti ukioa mke zaidi ya mmoja wote utawapenda sawasawa…utawezaje
kuhakikisha uanwepnda sawasawa,au ndio kuvunga, kudanganya…?’ nikakaribishwa
kijiweni kwa huo mjadala.
Na kabla sijakaa sawa, nikahisi kichwa kikiniuma, ….kilianza
ghfla,….nikanunua maji na kunywa, lakini kikawa hakitulii, na mara nikaanza
kujsikia vibaya, …hali ambayo sikuitarajia, na hali kama hiyo ikinitokea Napata
shida sana, nikaona hapo kijiweni hakukalilki, naikaomba dharura kidogo…
‘Samahani kidogo naona hali haijakaa sawa,endeleeni nakuja….’nikasema
huku nikiiondoka hapo kwa haraka, na kuelekea sehemu yenye choo.
‘Usikimbie nenda kajisaidie ,uje hapa maana wewe ndiye
unajifanya kijogoo,eti unaweza ukawamiliki wanawake watatu kwa mpigo, unafanya
mchezo nini….’akaniandama jamaa mmoja ambaye tumefahamiana hapo hapo kijiweni.
‘Endeleeni nakuja….’nikasemahuku nikiwa nakimbilia huko
ndani ya choo…
Nilipofika sehemu ya kujisaidia mara nikahisi nipo na
mtu,….lakini sikuweza kumuona huyo mtu, nikahisi joto likizidi mwilini,mapigo
ya moyo yakaongezeka,…mwili ukawa kama unatikisika,…na mara nikasikia kitu kama
sauti ikisema niende mitaa fulani,haraka…Hali kama hiyo ikitokea huwa huna
jinsi unajikuta unakwenda tu kama kipofu aliyeshikwa mkono. ….
Nilitoka pale sehemu ya kujisaidia nikuwapita wenzangu
waliopo kijiweni,bila hata kusema neon, nilikuwa siwaoni tena, naona hisia za
kuniongoza tu,na haraka haraka nikawa nafuatilia hiyo mitaa niliyokuwa
nikiambiwa na kutokea kwenye jengo moja….jengo hilo ni jpiya lipo kwenye ujenzi.
Nilipofika pale ile hali ya jotojoto ikaisha,..mapigo ya
moyo yakarudi kweney hali yake, na hali yangu ikawa kama kawaida, nikahisi kuwa
huenda hapo ndipo natakwia kufika, na hata kabla sijatulia vyemai,mara gari
moka likafika ,nikajificha kwenye ukuta, na kuangalia nini kitatokea, . Na kwenye
hilo gari wakateremeka watu wanne,….
‘Mtoeni haraka bosi anakuja,…’akasema mmojawapo.
‘Angalai watu wasituone…’akasema mtu mwingine.
Na mara gari jingine likafika na kusimama pembeni ya hilo gari, akateremka
dereva na kuja sehemu ya mlango mwingine akaufungua, ….na mara akatokea mama
mmoja, alikuwa kavaa miwani mikubwa iliyofunika sehemu kubwa ya uso wake.
‘Mtoeni na mpelekeni hadi ghorofa ya nne….’akasema huyo
mwanamke.
Nikaliangalia lile jengo ambalo halijaisha lilikuwa na
ghorofa kama sita zilizokamilika, na bado linaendelea kujengwa,….na ina maana
huyo mwanamke atakuwa analijua vyema hilo jingo, kwa jinsi alivyowaeleekza hawo
wenzake. Na mara wakamtoa mtu akiwa kabebwa…alikuwa ni mwanamke….kafunikwa
usoni. Nikaongiwa na hamasa ya kuwafuta….
Wakawa wameingia ndani na mimi nikawafuatilia nyuma nyuma,kwa
kujificha,…hadi tukafika huko kwenye gorofa ya nne, ….na wakaingia kwenye
chumba kimojawapo, …kilikuwa wazi hakijajengwa chote, kwahiyo ilikuwa rahisi
kwangu kuona nini kinafanyika humo ndani. Sehemu niliyokaa ni rahis kuonekana
lakii cha ajabu hawakuwa wakijali kuangalia upande ule nilipokuwa….
‘Ajenda iliyopo ni kuwa huyu anatakiwa aonekane
kajiua….mwekeni pembeni kabsa ya ule ukuta pale, halafu akizundukana tu, atajinyosha
na moja kwa moja atadondokea huko nje,…haponi huyo, akipona basi siku zake
bado…’akasema huyo mwanadada.
Kweli akidonoka pale anaangukia kwenye makorokoro,vyuma, ….hawezi
kabisa kupona, nikaanza kuogopa, ….nikaomba mungu waondoeke haraka ili
nikamuokoe,inagwaje sijui ni nani….
Kwa muda ule yule mwanamke alikuwa kimiya, sijui walikuwa
wamempa kitu gani, maana alikuwa kaa mfu. …
‘Lakini kapoteza damu nyingi,asije akawa keshakufa….’akasema
mmoja wao.
‘Hajafa huyo….’akasema huyo mwanamke.
‘Kwanini tusimumalizie kabisa?’ akasema mwingine.
’Sitaki ubishi, fuateni ninayowaambia…..’akasema huyo
mwanamama aliyevaa miwani mikubwa meusi.
‘Mimi nilikuwa anona tumalize kazi, kwasabbu mimi
alishaniona, ana nijua na kwa vile ni
wakili…jambo hili litatupeleka pabaya’akasema huyo jamaa, na aliposema ‘wakili,’
nikashituka,…
‘Ndio maana sitaki tufanye kosa ,kama ni kufa afe mwenyewe,
sio kwa mikono yetu, nasikitikia huyo aliyemgonga kichwani,…..sikutaka kabisa
iwe hivi,hamuoni kuwa kapoteza damu nyingi,na yule mwanamke akisikia kuwa
mlimuumiza hatatusamehe, mkumbuke keshaonja jela…’akasema huyo mwanamke.
Hapo nikavutika zaidi, huyo aliyeonja jela ni nani, sio yule
mwanamke aliyekimbia jela..atakuwa ni yeye,na
kwa mtizamo huo huyo hapo atakuwa yule wakili mwanadada…..nikachukua
simu yangu nikatuma meseji kwa mtu wa usalama ninayemjua.
Kundi lile lilipoweka mambo yao sawa, likawa linaondoka, na
mara nikasikia ving’ora vya polisi vikisikika huko chini barabarani,…nikajua
huenda ujumbe wangu umefanyiwa kazi haraka. Na kweli hivyo ving’ora vilipofika
hapo kwenye hilo jingo vikatulia na askari wakatoka na kuanza kupanda hilo
jingo. Sikujali kuwaangalia nilichofanya ni kwenda pale alipolazwa huyo mwanamke,
na nilipomfikia ndio nay eye alitaka kuzindukana, na kweli kama nisiengelimuwahi
angelidondoka,….
Nikamwahi na kumvutia ndani,halafu nikamlaza vizuri,na kuondoa kile kitambaa
usoni….ooh, kweli alikuwa yule wakili mwanadada,licha ya kulowana damu sehemu
kubwa ya kichwa na usoni, lakini nilimtambua mara moja, na muda huo huo watu wa
usalama walishafika, akiwemo yule jamaa ninayemfahamu.
‘Huduma ya kwanza, na awahishwe matibabu inaonekana kapoteza
damu nyingi….’nikasema na wao kumbe walikuja wakiwa wamekamilika, walimfanyia
huduma ya kwanza, na baadaye wakamwingiza kwenye machela ya wagonjwa na
kumchukua kwenda hospitalini.
Mimi niliingia kwenye
gari la watu wa usalama na yule jamaa
ninayemfahamu akawa ananihoji ilikuwaje, na na maelezo yangu yaliwasaidia,
lakini lile kundi lilikuwa limeshaondoka…hawakuwhi kumkamata mtu, walisema
walipofika hapo waliona watu wakishughulika na ujenzi, hawakuwajali.
‘Mbona mimi sikuona watu wakijenga, wakati ninapanda…’nikasema,na
huyo mtu wa usalama akawaamrisha watu wake wawakamte hwo wanaojenga,lakini
hawakukuta mtu, walishaondoak zamani.
‘Huyo mwanamama anaweza akawa ni nani?’ akauliza askari
usalama.
‘Kwakeli siwezi kumjua, maana alikuwa kajifunika uso wake ni
miwani mikubwa…’nikasema.
Kun akundi tunalihisi ….inabidi nifike huko nikaonane na
mmammoja, huyo tumeshamuhisi siku nyingi kuwa ana mambo yasiyoeleweka,…’akasema
huyo mtu wa usalama. Nkaomba tufutane naye.
Kwa muda ulesikujali kwenda kumuona huyo mgonjwa, nilijua
hata kama ningelifutana nao, wasingeliniruhusu kumuona, lengo langu nikumuona
huyo mwanamama, kama ni yeye aliyekuwa pale itakuwa rahisi kwangu kumtambua,..
‘Sawa twende maana kamani yeye utaweza kumtambua….’akasema
huyo mtu wa usalama,tukaondoka nayehadi eneo analolijua yeye, ilikuwa ni hoteli
na nje ya hiyo hoteli kuna duka kubwa. Yeye hakuingia ndani ya hoteli moja kwa
moja akafikia kweney hilo duka.
‘Vipi yulemtu wetu bado yupo?’ akamuuliza
‘Yupi huyo afande?’ akauliza yule mfanya biashara kwa
wasiwasi.
’ Yule mwanamama bwana, wewe siku ili nimekupa kazi gani…’akamwambia
huku akicheka.
‘Aaah,hizi kazi zenu bwana, kwani utanilipa shilingi ngapi,
kazi ya ukuwadi mimi siijui ….’akasema huyo jamaa.
‘Utalipwa na jamuhuri kama raia mwema…tatizo lako wewe
unafikiria namataka huyo mwanamama kimapenzi…nipo kazini ’akasema huyo mtu wa
usalama.
‘Yule mwanamama aliadimika mwezi mmoja ,na juzi alikuja , …..tukajau
kuwa huenda kesharudi,nasiki alilipa bili yake na kusema anaondoka….’akasema
huyo mfanya biashara.
‘Hebu nikuulize huyo mwanamama yupoje?’nikadadisi.
‘Sijawahi kumuona akiwa uso wazi, ….na kichwani huwa anakuwa
kama anavaa nywele za bandia, na kwasababu anazibadili mara kwa mara,
kwahiyo hana sura kamili…sijawahi hata
siku moja kumuona uso wake ukiwa wazi kwahiyo siwezi kusema ana sura
gani,…’akasema huyo jamaa.
‘Anaongeaje,lafudhi yake?’ nikauliza kama vile mimi ni mtu
wa usalama.
‘Ajabu ndio hiyo , hana lafudhi moja, leo anaweza akaongea
kama mtu wa pwani,kesho kama mzungu
mzungu, siku nyingine anaongea lafudhi tofauti….kwakeli huwezi kusema anatokea
wapi….ni kama mtu tofauti tofauti, lakini ni yule yule…’akasemahuyo jamaa.
‘Kazi kweli kweli…lakini atapatikana tu….’aaksema huyo mtu
wa usalama, nay eye wala hakutaka kuuliza maswali mengi, inaonekana hayo
niliyouliza yote alikuwa akiyajua.
*********
‘Sasa unaweza kwenda kumuona, ….’akaniambia docta, nami kwa
haraka nikaingia kwenye chumba alicholazwa huyo mwadada wakili, nilipoingia
alionekana kulala, lakini mara akafunua macho na a aliponiona tu akatabasamu na
hata kabla sijasema kitu yeye ndio akaanza kuongea;
‘Nashukuru sana , nasikia ni wewe uliyewahi kuja kuniokoa,
je ulijuaje kuwa wamenikamata hawa wahuni…..?’akauliza
‘Yaani ni mambo yale yale niliyokuhadithia, kuwa kuna vitu
vinanitokea na kuniekeleza ….na ndivyo ilivyotokea …..Vipi unajisikiaje…?’
nikamuuliza.
‘Sijambo, kwa ujumla nasubiri tu docta aniambie niondoke,
sina tatizo jingine, tatizo langu tu,ni jinsi nitakavyowasaidia hawa
walionifanyia hivi,najua wanahitaji msaada wa kimawazo, kuliko kuwakamata tu na
kuwakweka ndani….’akasemahuyo mwanadada,nakunifanya nimshangae.
‘Yaani watu walitaka kuku-ua halafu wasamehewe hivi hivi,
huoni kwa kufanya hivyo tutakuwa tunafuga wahalifu…’nikasema.
‘Tatizo hapa sio uhalifu, tatizo ni kwanini wakajiingiza
kwenye mambo kama hayo, ni vyema yakajulikana, ili iwe rahisi kutoa ushauri,…usipoyajua
na kuwashauru, kuwapa nasaha,hata ukiwafunga miaka mingi, haitasaidia kitu,
utakuwa unambebesha mtu mzigo juu ya mzigo, na mwisho wake ni kumharibia kabisa maisha ya huyo mtu,
ndio maana nilitaka nionane nao kwanza, nijue tatizo ni nini,ili hata kama
watakamatwa, mwisho wa siku wajirudi…’akasema,
‘Kama ingekuwa hivyo, basi wahalafu wengelikuwa wana
raha,….ni kweli ingelitakiwa iwe hivyo, jele iwe sehemu ya mfunzo, watu
wakifungwa wawe wanafundisha na kuelemishwa ubaya wa hayo waliyoyafanya , kuwe
na watu maalumu wa kumpitia kila mfungwa na kumtathmini, kumpa ushauri nasaha,
na sio kuwafunga na kuatesa tu….sijui kama hili linawezekana?’nikasema huku najiuliza
mwenywe.
‘Inawezekana,….hakuna lisilo wezekana kama kweli tuna nia ya
kueleimisha,…kama kweli tunajali hisi za watu,….’akasemahuyo mwanadada.
‘Lakini je ni rahisi kiasi hicho, maana ukishaitwa mhalifu,
hunahaki tena…na isitishe kuna wachache ambao wameingizwa huko hata bila kosa, ….mimi
nimekutana nao, na wameshakakata tamaa kwasababu hawa njia ya kudhihirisha
kuwawao hawana makosa….sijui wanaotetea haki wapo wapi…?’ nikasemahuku
nikiangalia huku na kule.
‘Wanaotetea haki,ni mimi na wewe…ndiowapo watu wengine
wanajulikana hivyo…’akatulia kidogo kamaanawazajambo fulani, mimi
nikasemakwaharaka;
‘Unajua hata mimi nawashangaa hawo watu wanatetea haki za
binadamu ambao wanafikia kusema mtu akiua nay eye asipewe adhabu ya kifo,
lakini hawalioni hilo….wanakimbilia kuondoa adhanu hata zile alizozihalalisha
mungu..lakini hawajali hisa za watu, je huyu mtu kwanini aliua, kwanini aliiba,
kwanini..hilo hawalizungumzii, kwanini wafungwe wasiwe na wshauri nasaha,
wakiwa jela,….ili wajirudi…’nikamwangalia mwanadada ambaye naye alionekana kazama
kwenye mawazo.
‘Ndio maana nakumabia mtetezi wa haki ni wewe na mimi,kila
mmoja anawajibika kwa hilo,ili mwisho wa siku hiyo haki iwe imeseimamiwa na
kila mmoja, na ikipitishwa kama sheria inakuwa na nguvu…makundi hayo machache
yanayotetea haki za bindamu, yameundwa na watu,…na wao wanaweza wakawaan
udhaifu wao,….je utajuaje, kama mimi na wewe hatutajutolea,…..’akasemana
kutulia.
‘Mimi naona labda hawo watetezi wa haki za binadamu
wanaogopa kuwa na wao wakiua watauliwa….maana kama wanamjali huyo aliyeua na kumsahau
huyo aliyeuliwa na watu wake….haki hiyo naiona itakuwa ni ya upendeleo na
itawavuta wengine kutokuogopa ku-ua, huoni kuwa sio haki kwa wote,…ina
uoendeelo. Nafikiri hawow atuu wa haki zabindamu, wanaona kuwa mtu ikishakufa keshakufa,
hana haki tena hapa dunia,….’nikasema.
‘Huo ni mjadala mwingine,…labda wanaharakati wanaweza
wakauona na kuufanyia kazi, mimi sasa nipo kwenye tafiti yangu ambayo inaweza
ikaligusia na hilo,nikitoka hapa nataka nikaonane na huyo mwanamama
aliyekusudia kunimaliza, najua ana lengo lake, au kuna jambo ambalo limemshinikiza
hadi kufikia maamuzi makubwakamahayo, sio bure, nataka kujua ni kwanini, ili
kama ikiwezekana tumsaidie….’akasema na kutulia.
‘Ina maana unamfahamu?’ nikamuuliza.
‘Nahisi nitakuwa nimeshamfahamu, lakini nataka uhakika…siwezi
kusema kwasasa ni nani….subira huvuta heri,…kila kitu kitakuwa shwari…lakini
kwanza nionane nao…au naye…’akasema.
‘Huoni sasa utakuwa katika hatari zaidi maanane lengo lao hawo
watu lilikuwa ni kukuua,….na lengo lao halikukamilika, ….najua kwa sasa watakuwa
wakitafuta kila njia ya kukumaliza, nakushangaa nikisikia kuwa bado unataka
kuwafuatilia….?’ Nikamuuliza.
‘Unapotaka kusaidia wenzako, usiogope kufa…kwasababu kufa
kupo, na ujue kabisa kila mtu atakufa, …tofauti ya vifo ni sababu tu na muda, …’akasema
huku akiwa kama anatafakari jambo, halafu akasema huku akiwa kama yupo ndani ya
mawazo mazito;
‘Hivi unaonaje ukifa huku unatetea haki za watu, huoni kuwa
utakuwa umefanya jambo jema, kuliko kufa ukiwa unafanya maasi…mimi
nilipomshuhuidia mama yangu akifa kwa mateso akinitetea mimi mwanae, ….huku
anaficha machungu makali aliyokuwa akiyapata,ili niweze kuishi,…ili nisije
nikavunjika moyo wa kuishi, nimeona kuwa, kuishi kwa raha huku watu wanateseka
ni dhambi…..ole wao wale waanoishi kwa raha, na utajiri, huku wanaona wengine
wanateseka na kufa kwa njaa, maradhi na shida mbalimbali….
‘Kweli wewe ni mtu wa ajabu….sasa nimeanza kukuelewa, na
kweli unabeba hulka ya mwanamke, huruma na upndo ….’nikasema na kumwangalia kwa
macho ya kumtafakari, nay eye akaniangalia huku akionyesha uso wa fikara.
‘Kwa mtaji huo, natamani tuwe pamoja, ili kukamilisha hiyo
dhamira yako y akweli, …na hata hivyo nimeingiwa na hamasa ya kukutana na huyo
mwanamama au mwanadada au wanamama au wanadada waliojiingiza kwenye mambo hayo,
ili na mimi nijue ni kwanini, na kwanini watake kumuangamiza mtu muhimu kama
wewe,…. na sijui adhabu gali ichukuliwe juu yao…wanastahili kunyongwa…..’nikasema
kwa ahsira.
‘Ukitaka jambo,…lifanikiwe, usilichukulie kwa hasira au kwa
njia ya kulipiza kisasi, unachotakiwa ni kulichukulie kwa hekima na malengo
mema,….kwahiyo kama unataka kuwa na mimi ni vyema ukatuliza akili yako na kujua
kuwa hayo yote yanayotendeka, hutendwa na binadamu, ambaye ni kama wewe,
ilakutokana na udhaifu,ulijengeka kwasababu maalumu ndio maana kafikia hapo,
msaidie kwanza, na ondoa dhana ya kulipiza kisasi,kwani haina mwisho mwema….’
NB: Haya hata kama ni kwa shida tutajitahidi hivyo hivyo...sijui kama kisa kinaeleweka,....toeni maoni,
WAZO LA LEO: Usiogope kutetea haki, hata kama kwa kufanya hivyo, utasababisha kuchukiwa na hata kuhatarisha pengine kuharisha maisha yako,...kumbuka ukitetea haki upo pamoja na mungu,na ni yeye pekee atayakayekulinda.
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Jirani natumaini umuzima wa afya njema.
Jirani tupo maana majirani siku hizi kila mmoja kajizungushia ukuta. Hakuna kutembeleana. Nashukuru kwa kunikumbuka. Ubarikiwe sana
mmhh..nipo nyuma kidogo usiona ukimya ..hapa kazi ipo Tupo pamoja.
Post a Comment