Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, May 7, 2012

Hujafa hujaumbika-32Nikiwa pale hosptalimoyo wangu ulikuwa ukidunda kwa haraka, nikiwa na wasiwasi,…..na akili yangu ilikuwa bado haiamini kilichotokea, je ina maana kweli nina hisia zinazoniongoza, au ni watu hao waitwao wahenga,…..hapana hizo ni kudra za mungu, zilizoniongoza,..siwezi kabisa kuamini mambo hayo ya mizimu, ….
‘Ahsante sana mungu, maana bila wewe yote haya yasingeliwezekana…’nikasema na kuangalia juu, huku nikiwaza tukio nzima lilivyokuwa na kabla sijafika mbali kimawazo mara docta akatokea, nikamsogela na haraka nikamuulizia;

‘Vipi hali ya mgonjwa docta?’ nikauliza.

‘Mgonjwa hali yake sio mbaya, bado tunaendelea kumhudumia, inaonyesha kuwa walimpiga sindano ya madawa ya kulevya, na tulichofanya ni kuiondoa hiyo hali mwilini, na sasa keshazindukana,… na jereha la kichwani, halikuleta athari kubwa …..na hata damu haikupotea nyingi, usiwe na wasiwasi hali yake itakuwa njema tu….

‘Naweza kwenda kumuona…?’ nikauliza.

‘Mhhhh, Kwasasa hapana, …kwa vile bado hajazindukana vyema na bado kuna huduma tunampa, wewe subiri kama saa moja hivi, akiwa tayari tutakuambia….wewe ni mume wake,au…?’ akaniuliza docta.
‘Hapana mimi sio mume wake, ni rafiki yake….’nikasema.

‘Ok,haina shida ….mambo mengine tumeshayaweka sawa,…..tulishaongea na watu wa usalama na wametueelekza kuwa huyo ni nani, na ….kwahiyo usijli sana…’akasema huku akionyesha kuwa ana haraka ya kuondoka.

‘Sawa docta, niwashukuru sana kwa kazi yenu nzuri…’nikasema na yeye akataabsamu na kusema..
‘Usijali hiyo ndio kazi yetu….’akasema na kuondoka.

Kiti kilikuwa hakikaliki,maana nilikuw ana hamu sana ya kumuona huyo mgonjwa,..nikawa na kaa dakika chache mara nainuka, ilimradi hali iliyokuwepo haikuniwezesha kutuliza kichwa, na baadaye nikawa nawaza jinsi ilivyokuwa;
********
Siku hiyo nilipata kibarua kwa Mhindi mmoja, na baada ya kupigika kitumwa, nikamwendea huyo Mhindi anipe mshiko wangu, akawa ananizungusa zungusha, na hapo tukaanza kupandishiana, …kumbe ndio ilikuwa tabia yake na wenzangu walipoona kuwa nampandidhia na wao wakajiunga pamoja na mimi, wakaondoa uwoga waliokuwa nao mwanzoni, na hamaki ikachukua mkondo wake, karibu ya kumpiga huyo Muhindi , ambaye baadaye alitoa hizo pesa huku akitushutumu kuwa tumemharibia siku yake.

‘Kama ulikuwa huna hela ya kutosha kwanini ukatuajiri wengi,….?’ Nikamuuliza.

‘Sio mingi nyie, ..tatizo mnadai pesa mingi….’akasema.
Pesa mingi gani hizo, au ndio unatuzarau kuwa hatujui pesa, mbona huyo ndugu yako msimamizi umemlipa pesa nyingi, pesa uliyomlipa yeye peke yake ni sawa an jumla ya pesa yote uliyotulipa sisi wengi?’ nikamuuliza.

‘Yeye ni msimamizi, ..bosi wenu, lazima apate pesa mingi mingi, kwanza yeye kasoma zaidi…..ni ‘expatriet’ ’akasema

‘Kwani yeye kanizidi nini mimi kielimu,,au kwa vile unaniona nimekuja hapa kwako kuombakazi,mimi nimesoma hadi nje,lakini bahati yangu ni mbaya tu…sijapata kazi, au kwa ajili ya ngozi yetu..?’nikasema

‘Kesho leta vyeti yako,mimi nitaajiri veye….kama iko soma, naona waongea English nzuri veye..’akaniambi na mimi nikawa na imani kuwa sasa nitapata ajira angalau ya kuvuta siku, sikuwa napenda kufanya akzi kwenye kampuni yake, kwani nilivyomuona ni mbabaishaji, atanilipa mshahara mdogo lakini ni heri kuliko kukaa nyumbani.

Nikachukua pesa yangu na kuelekea maskani….ambapo tunakutana na marafiki kubadilishana mawazo, imekuwa ndio tabia yangu sasa, kila nikihangaika mchana badala ya kwenda kulewa au kutumia pesa ovyo , nafikia hapo kijiweni , na hapo Napata kahawa, huku tukiingia kwenye mijdadala mbali mbaliya kimaisha,ndio maisha tutafanyaje….maisha bora kwa kila mtu.

‘Haya msomi umekuja,njoo hapa kuna ajenda ya leo,sijui wewe unasemaje,kuhusu ndoa, kwasababu wewe umesoma na unadai umewahi kuoa mara mbili au sio, sasa tuambie eti ukioa mke zaidi ya mmoja wote utawapenda sawasawa…utawezaje kuhakikisha uanwepnda sawasawa,au ndio kuvunga, kudanganya…?’ nikakaribishwa kijiweni kwa huo mjadala.

Na kabla sijakaa sawa, nikahisi kichwa kikiniuma, ….kilianza ghfla,….nikanunua maji na kunywa, lakini kikawa hakitulii, na mara nikaanza kujsikia vibaya, …hali ambayo sikuitarajia, na hali kama hiyo ikinitokea Napata shida sana, nikaona hapo kijiweni hakukalilki, naikaomba dharura kidogo…

‘Samahani kidogo naona hali haijakaa sawa,endeleeni nakuja….’nikasema huku nikiiondoka hapo kwa haraka, na kuelekea sehemu yenye choo.

‘Usikimbie nenda kajisaidie ,uje hapa maana wewe ndiye unajifanya kijogoo,eti unaweza ukawamiliki wanawake watatu kwa mpigo, unafanya mchezo nini….’akaniandama jamaa mmoja ambaye tumefahamiana hapo hapo kijiweni.

‘Endeleeni nakuja….’nikasemahuku nikiwa nakimbilia huko ndani ya choo…

Nilipofika sehemu ya kujisaidia mara nikahisi nipo na mtu,….lakini sikuweza kumuona huyo mtu, nikahisi joto likizidi mwilini,mapigo ya moyo yakaongezeka,…mwili ukawa kama unatikisika,…na mara nikasikia kitu kama sauti ikisema niende mitaa fulani,haraka…Hali kama hiyo ikitokea huwa huna jinsi unajikuta unakwenda tu kama kipofu aliyeshikwa mkono. ….

Nilitoka pale sehemu ya kujisaidia nikuwapita wenzangu waliopo kijiweni,bila hata kusema neon, nilikuwa siwaoni tena, naona hisia za kuniongoza tu,na haraka haraka nikawa nafuatilia hiyo mitaa niliyokuwa nikiambiwa na kutokea kwenye jengo moja….jengo hilo ni jpiya lipo kwenye ujenzi.

Nilipofika pale ile hali ya jotojoto ikaisha,..mapigo ya moyo yakarudi kweney hali yake, na hali yangu ikawa kama kawaida, nikahisi kuwa huenda hapo ndipo natakwia kufika, na hata kabla sijatulia vyemai,mara gari moka likafika ,nikajificha kwenye ukuta, na kuangalia nini kitatokea, . Na kwenye hilo gari wakateremeka watu wanne,….

‘Mtoeni haraka bosi anakuja,…’akasema mmojawapo.

‘Angalai watu wasituone…’akasema mtu mwingine.

Na mara gari jingine likafika na  kusimama pembeni ya hilo gari, akateremka dereva na kuja sehemu ya mlango mwingine akaufungua, ….na mara akatokea mama mmoja, alikuwa kavaa miwani mikubwa iliyofunika sehemu kubwa ya uso wake.

‘Mtoeni na mpelekeni hadi ghorofa ya nne….’akasema huyo mwanamke.

Nikaliangalia lile jengo ambalo halijaisha lilikuwa na ghorofa kama sita zilizokamilika, na bado linaendelea kujengwa,….na ina maana huyo mwanamke atakuwa analijua vyema hilo jingo, kwa jinsi alivyowaeleekza hawo wenzake. Na mara wakamtoa mtu akiwa kabebwa…alikuwa ni mwanamke….kafunikwa usoni. Nikaongiwa na hamasa ya kuwafuta….

Wakawa wameingia ndani na mimi nikawafuatilia nyuma nyuma,kwa kujificha,…hadi tukafika huko kwenye gorofa ya nne, ….na wakaingia kwenye chumba kimojawapo, …kilikuwa wazi hakijajengwa chote, kwahiyo ilikuwa rahisi kwangu kuona nini kinafanyika humo ndani. Sehemu niliyokaa ni rahis kuonekana lakii cha ajabu hawakuwa wakijali kuangalia upande ule nilipokuwa….

‘Ajenda iliyopo ni kuwa huyu anatakiwa aonekane kajiua….mwekeni pembeni kabsa ya ule ukuta pale, halafu akizundukana tu, atajinyosha na moja kwa moja atadondokea huko nje,…haponi huyo, akipona basi siku zake bado…’akasema huyo mwanadada.

Kweli akidonoka pale anaangukia kwenye makorokoro,vyuma, ….hawezi kabisa kupona, nikaanza kuogopa, ….nikaomba mungu waondoeke haraka ili nikamuokoe,inagwaje sijui ni nani….
Kwa muda ule yule mwanamke alikuwa kimiya, sijui walikuwa wamempa kitu gani, maana alikuwa kaa mfu. …
‘Lakini kapoteza damu nyingi,asije akawa keshakufa….’akasema mmoja wao.

‘Hajafa huyo….’akasema huyo mwanamke.

‘Kwanini tusimumalizie kabisa?’ akasema mwingine.

’Sitaki ubishi, fuateni ninayowaambia…..’akasema huyo mwanamama aliyevaa miwani mikubwa meusi.

‘Mimi nilikuwa anona tumalize kazi, kwasabbu mimi alishaniona, ana nijua na kwa vile  ni wakili…jambo hili litatupeleka pabaya’akasema huyo jamaa, na aliposema ‘wakili,’ nikashituka,…

‘Ndio maana sitaki tufanye kosa ,kama ni kufa afe mwenyewe, sio kwa mikono yetu, nasikitikia huyo aliyemgonga kichwani,…..sikutaka kabisa iwe hivi,hamuoni kuwa kapoteza damu nyingi,na yule mwanamke akisikia kuwa mlimuumiza hatatusamehe, mkumbuke keshaonja jela…’akasema huyo mwanamke.

Hapo nikavutika zaidi, huyo aliyeonja jela ni nani, sio yule mwanamke aliyekimbia jela..atakuwa ni yeye,na  kwa mtizamo huo huyo hapo atakuwa yule wakili mwanadada…..nikachukua simu yangu nikatuma meseji kwa mtu wa usalama ninayemjua.

Kundi lile lilipoweka mambo yao sawa, likawa linaondoka, na mara nikasikia ving’ora vya polisi vikisikika huko chini barabarani,…nikajua huenda ujumbe wangu umefanyiwa kazi haraka. Na kweli hivyo ving’ora vilipofika hapo kwenye hilo jingo vikatulia na askari wakatoka na kuanza kupanda hilo jingo. Sikujali kuwaangalia nilichofanya ni kwenda pale alipolazwa huyo mwanamke, na nilipomfikia ndio nay eye alitaka kuzindukana, na kweli kama nisiengelimuwahi angelidondoka,….

Nikamwahi na kumvutia ndani,halafu  nikamlaza vizuri,na kuondoa kile kitambaa usoni….ooh, kweli alikuwa yule wakili mwanadada,licha ya kulowana damu sehemu kubwa ya kichwa na usoni, lakini nilimtambua mara moja, na muda huo huo watu wa usalama walishafika, akiwemo yule jamaa ninayemfahamu.

‘Huduma ya kwanza, na awahishwe matibabu inaonekana kapoteza damu nyingi….’nikasema na wao kumbe walikuja wakiwa wamekamilika, walimfanyia huduma ya kwanza, na baadaye wakamwingiza kwenye machela ya wagonjwa na kumchukua kwenda hospitalini.

 Mimi niliingia kwenye gari la watu wa usalama  na yule jamaa ninayemfahamu akawa ananihoji ilikuwaje, na na maelezo yangu yaliwasaidia, lakini lile kundi lilikuwa limeshaondoka…hawakuwhi kumkamata mtu, walisema walipofika hapo waliona watu wakishughulika na ujenzi, hawakuwajali.

‘Mbona mimi sikuona watu wakijenga, wakati ninapanda…’nikasema,na huyo mtu wa usalama akawaamrisha watu wake wawakamte hwo wanaojenga,lakini hawakukuta mtu, walishaondoak zamani.

‘Huyo mwanamama anaweza akawa ni nani?’ akauliza askari usalama.

‘Kwakeli siwezi kumjua, maana alikuwa kajifunika uso wake ni miwani mikubwa…’nikasema.
Kun akundi tunalihisi ….inabidi nifike huko nikaonane na mmammoja, huyo tumeshamuhisi siku nyingi kuwa ana mambo yasiyoeleweka,…’akasema huyo mtu wa usalama. Nkaomba tufutane naye.

Kwa muda ulesikujali kwenda kumuona huyo mgonjwa, nilijua hata kama ningelifutana nao, wasingeliniruhusu kumuona, lengo langu nikumuona huyo mwanamama, kama ni yeye aliyekuwa pale itakuwa rahisi kwangu kumtambua,..

‘Sawa twende maana kamani yeye utaweza kumtambua….’akasema huyo mtu wa usalama,tukaondoka nayehadi eneo analolijua yeye, ilikuwa ni hoteli na nje ya hiyo hoteli kuna duka kubwa. Yeye hakuingia ndani ya hoteli moja kwa moja akafikia kweney hilo duka.

‘Vipi yulemtu wetu bado yupo?’ akamuuliza

‘Yupi huyo afande?’ akauliza yule mfanya biashara kwa wasiwasi.

’ Yule mwanamama bwana, wewe siku ili nimekupa kazi gani…’akamwambia huku akicheka.

‘Aaah,hizi kazi zenu bwana, kwani utanilipa shilingi ngapi, kazi ya ukuwadi mimi siijui ….’akasema huyo jamaa.

‘Utalipwa na jamuhuri kama raia mwema…tatizo lako wewe unafikiria namataka huyo mwanamama kimapenzi…nipo kazini ’akasema huyo mtu wa usalama.

‘Yule mwanamama aliadimika mwezi mmoja ,na juzi alikuja , …..tukajau kuwa huenda kesharudi,nasiki alilipa bili yake na kusema anaondoka….’akasema huyo mfanya biashara.

‘Hebu nikuulize huyo mwanamama yupoje?’nikadadisi.

‘Sijawahi kumuona akiwa uso wazi, ….na kichwani huwa anakuwa kama anavaa nywele za bandia, na kwasababu anazibadili mara kwa mara, kwahiyo  hana sura kamili…sijawahi hata siku moja kumuona uso wake ukiwa wazi kwahiyo siwezi kusema ana sura gani,…’akasema huyo jamaa.

‘Anaongeaje,lafudhi yake?’ nikauliza kama vile mimi ni mtu wa usalama.

‘Ajabu ndio hiyo , hana lafudhi moja, leo anaweza akaongea kama  mtu wa pwani,kesho kama mzungu mzungu, siku nyingine anaongea lafudhi tofauti….kwakeli huwezi kusema anatokea wapi….ni kama mtu tofauti tofauti, lakini ni yule yule…’akasemahuyo jamaa.

‘Kazi kweli kweli…lakini atapatikana tu….’aaksema huyo mtu wa usalama, nay eye wala hakutaka kuuliza maswali mengi, inaonekana hayo niliyouliza yote alikuwa akiyajua.

*********

‘Sasa unaweza kwenda kumuona, ….’akaniambia docta, nami kwa haraka nikaingia kwenye chumba alicholazwa huyo mwadada wakili, nilipoingia alionekana kulala, lakini mara akafunua macho na a aliponiona tu akatabasamu na hata kabla sijasema kitu yeye ndio akaanza kuongea;

‘Nashukuru sana , nasikia ni wewe uliyewahi kuja kuniokoa, je ulijuaje kuwa wamenikamata hawa wahuni…..?’akauliza

‘Yaani ni mambo yale yale niliyokuhadithia, kuwa kuna vitu vinanitokea na kuniekeleza ….na ndivyo ilivyotokea …..Vipi unajisikiaje…?’ nikamuuliza.

‘Sijambo, kwa ujumla nasubiri tu docta aniambie niondoke, sina tatizo jingine, tatizo langu tu,ni jinsi nitakavyowasaidia hawa walionifanyia hivi,najua wanahitaji msaada wa kimawazo, kuliko kuwakamata tu na kuwakweka ndani….’akasemahuyo mwanadada,nakunifanya nimshangae.

‘Yaani watu walitaka kuku-ua halafu wasamehewe hivi hivi, huoni kwa kufanya hivyo tutakuwa tunafuga wahalifu…’nikasema.

‘Tatizo hapa sio uhalifu, tatizo ni kwanini wakajiingiza kwenye mambo kama hayo, ni vyema yakajulikana, ili iwe rahisi kutoa ushauri,…usipoyajua na kuwashauru, kuwapa nasaha,hata ukiwafunga miaka mingi, haitasaidia kitu, utakuwa unambebesha mtu mzigo juu ya mzigo, na mwisho  wake ni kumharibia kabisa maisha ya huyo mtu, ndio maana nilitaka nionane nao kwanza, nijue tatizo ni nini,ili hata kama watakamatwa, mwisho wa siku wajirudi…’akasema,

‘Kama ingekuwa hivyo, basi wahalafu wengelikuwa wana raha,….ni kweli ingelitakiwa iwe hivyo, jele iwe sehemu ya mfunzo, watu wakifungwa wawe wanafundisha na kuelemishwa ubaya wa hayo waliyoyafanya , kuwe na watu maalumu wa kumpitia kila mfungwa na kumtathmini, kumpa ushauri nasaha, na sio kuwafunga na kuatesa tu….sijui kama hili linawezekana?’nikasema huku najiuliza mwenywe.

‘Inawezekana,….hakuna lisilo wezekana kama kweli tuna nia ya kueleimisha,…kama kweli tunajali hisi za watu,….’akasemahuyo mwanadada.

‘Lakini je ni rahisi kiasi hicho, maana ukishaitwa mhalifu, hunahaki tena…na isitishe kuna wachache ambao wameingizwa huko hata bila kosa, ….mimi nimekutana nao, na wameshakakata tamaa kwasababu hawa njia ya kudhihirisha kuwawao hawana makosa….sijui wanaotetea haki wapo wapi…?’ nikasemahuku nikiangalia huku na kule.

‘Wanaotetea haki,ni mimi na wewe…ndiowapo watu wengine wanajulikana hivyo…’akatulia kidogo kamaanawazajambo fulani, mimi nikasemakwaharaka;

‘Unajua hata mimi nawashangaa hawo watu wanatetea haki za binadamu ambao wanafikia kusema mtu akiua nay eye asipewe adhabu ya kifo, lakini hawalioni hilo….wanakimbilia kuondoa adhanu hata zile alizozihalalisha mungu..lakini hawajali hisa za watu, je huyu mtu kwanini aliua, kwanini aliiba, kwanini..hilo hawalizungumzii, kwanini wafungwe wasiwe na wshauri nasaha, wakiwa jela,….ili wajirudi…’nikamwangalia mwanadada ambaye naye alionekana kazama kwenye mawazo.

‘Ndio maana nakumabia mtetezi wa haki ni wewe na mimi,kila mmoja anawajibika kwa hilo,ili mwisho wa siku hiyo haki iwe imeseimamiwa na kila mmoja, na ikipitishwa kama sheria inakuwa na nguvu…makundi hayo machache yanayotetea haki za bindamu, yameundwa na watu,…na wao wanaweza wakawaan udhaifu wao,….je utajuaje, kama mimi na wewe hatutajutolea,…..’akasemana kutulia.

‘Mimi naona labda hawo watetezi wa haki za binadamu wanaogopa kuwa na wao wakiua watauliwa….maana kama wanamjali huyo aliyeua na kumsahau huyo aliyeuliwa na watu wake….haki hiyo naiona itakuwa ni ya upendeleo na itawavuta wengine kutokuogopa ku-ua, huoni kuwa sio haki kwa wote,…ina uoendeelo. Nafikiri hawow atuu wa haki zabindamu, wanaona kuwa mtu ikishakufa keshakufa, hana haki tena hapa dunia,….’nikasema.

‘Huo ni mjadala mwingine,…labda wanaharakati wanaweza wakauona na kuufanyia kazi, mimi sasa nipo kwenye tafiti yangu ambayo inaweza ikaligusia na hilo,nikitoka hapa nataka nikaonane na huyo mwanamama aliyekusudia kunimaliza, najua ana lengo lake, au kuna jambo ambalo limemshinikiza hadi kufikia maamuzi makubwakamahayo, sio bure, nataka kujua ni kwanini, ili kama ikiwezekana tumsaidie….’akasema na kutulia.

‘Ina maana unamfahamu?’ nikamuuliza.

‘Nahisi nitakuwa nimeshamfahamu, lakini nataka uhakika…siwezi kusema kwasasa ni nani….subira huvuta heri,…kila kitu kitakuwa shwari…lakini kwanza nionane nao…au naye…’akasema.

‘Huoni sasa utakuwa katika hatari zaidi maanane lengo lao hawo watu lilikuwa ni kukuua,….na lengo lao halikukamilika, ….najua kwa sasa watakuwa wakitafuta kila njia ya kukumaliza, nakushangaa nikisikia kuwa bado unataka kuwafuatilia….?’ Nikamuuliza.

‘Unapotaka kusaidia wenzako, usiogope kufa…kwasababu kufa kupo, na ujue kabisa kila mtu atakufa, …tofauti ya vifo ni sababu tu na muda, …’akasema huku akiwa kama anatafakari jambo, halafu akasema huku akiwa kama yupo ndani ya mawazo mazito;

‘Hivi unaonaje ukifa huku unatetea haki za watu, huoni kuwa utakuwa umefanya jambo jema, kuliko kufa ukiwa unafanya maasi…mimi nilipomshuhuidia mama yangu akifa kwa mateso akinitetea mimi mwanae, ….huku anaficha machungu makali aliyokuwa akiyapata,ili niweze kuishi,…ili nisije nikavunjika moyo wa kuishi, nimeona kuwa, kuishi kwa raha huku watu wanateseka ni dhambi…..ole wao wale waanoishi kwa raha, na utajiri, huku wanaona wengine wanateseka na kufa kwa njaa, maradhi na shida mbalimbali….

‘Kweli wewe ni mtu wa ajabu….sasa nimeanza kukuelewa, na kweli unabeba hulka ya mwanamke, huruma na upndo ….’nikasema na kumwangalia kwa macho ya kumtafakari, nay eye akaniangalia huku akionyesha uso wa fikara.

‘Kwa mtaji huo, natamani tuwe pamoja, ili kukamilisha hiyo dhamira yako y akweli, …na hata hivyo nimeingiwa na hamasa ya kukutana na huyo mwanamama au mwanadada au wanamama au wanadada waliojiingiza kwenye mambo hayo, ili na mimi nijue ni kwanini, na kwanini watake kumuangamiza mtu muhimu kama wewe,…. na sijui adhabu gali ichukuliwe juu yao…wanastahili kunyongwa…..’nikasema kwa ahsira.

‘Ukitaka jambo,…lifanikiwe, usilichukulie kwa hasira au kwa njia ya kulipiza kisasi, unachotakiwa ni kulichukulie kwa hekima na malengo mema,….kwahiyo kama unataka kuwa na mimi ni vyema ukatuliza akili yako na kujua kuwa hayo yote yanayotendeka, hutendwa na binadamu, ambaye ni kama wewe, ilakutokana na udhaifu,ulijengeka kwasababu maalumu ndio maana kafikia hapo, msaidie kwanza, na ondoa dhana ya kulipiza kisasi,kwani haina mwisho mwema….’

NB: Haya hata kama ni kwa shida tutajitahidi hivyo hivyo...sijui kama kisa kinaeleweka,....toeni maoni, 

WAZO LA LEO: Usiogope kutetea haki, hata kama kwa kufanya hivyo, utasababisha kuchukiwa na hata kuhatarisha pengine kuharisha maisha yako,...kumbuka ukitetea haki upo pamoja na mungu,na ni yeye pekee atayakayekulinda.


Ni mimi: emu-three

3 comments :

EDNA said...

Jirani natumaini umuzima wa afya njema.

emu-three said...

Jirani tupo maana majirani siku hizi kila mmoja kajizungushia ukuta. Hakuna kutembeleana. Nashukuru kwa kunikumbuka. Ubarikiwe sana

Yasinta Ngonyani said...

mmhh..nipo nyuma kidogo usiona ukimya ..hapa kazi ipo Tupo pamoja.