Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, November 11, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-48



Rose akiwa na haraka aliingia mle hotelini baada ya kuachana na Inspekta, alikumbuka alivyowasiliana na mkuu wa ulinzi wa ile hotelini, ambaye alimpigia muda mfupi tu alipowasili hapo hotelini, alimwambia akifika humo, aisharakishe kuingia ndani, kwanza apitie pale mapokezi, ambapo atapata maagizo ya nini la kufanya.

‘Inabidi tuchukua tahadhari zote, huwezi jua , labda kuna watu wanakufuatilia, na wanataka kujua wapi chumba chako kilipo, na mimi hili ndilo ninalojitahidi kulificha, …hata humu ndani wengi hawajui mpo chumba gani, kwahiyo hakikisha unafanya utakavyoeleekezwa….’akaambiwa.

‘Aaah, haya, ila mimi bado sijaelewa, hayo yote ya nini, kwanini na wanataka nini, sawa nitafanya hivyo, natumai huo mtu wangu hajambo.?’akasema Rose huku akiwa hana furaha.

‘Huyu hajambo, na nipo naye wakati nakupigia hii simu, …unataka kuongea naye kidogo ili uhakikishe kwua hajambo..?’akauliza mkuu wa ulinzi.

‘Aaah, hapana haina haja kwasababu nakuja huko tutaongea naye, hilo liisikutie shaka, ila naomba wasinikawishe hapo mapokezi…’ akasema Rose .

‘Hutakawizwa maana, kama nilivyokuambi nipo hapa na huyu mtu wako, sijui kwanini unamuita mtu wako badala ya mume wako….aaah, mara mtu wangu, mara ….Sweetie, ….mna vituko nyie, hata jina lake ni la kiajabu akabu, sijui mnaficha nini….aah, ndio ulisema ni kwasababu, ..ok,.naona kuna simu inaingia, tutaongea baadaye….’akasema yule mkuu wa ulinzi wa hapo hotelini na kukata simu.

Rose aliingia hotelini na kama ilivyo kawaida akapitia chumba cha ukaguzi, halafu akaingia mapokezi, alikuwa na haraka ya kufika chumbani kwake, na yale masharti aliyopewa kuwa akifika hapo mapokezi, atapata maagizo, aliyaona kama kumpotezea muda wake, lakini alikuwa hana jinsi, kwani hayo ni kwa ajili ya usalama wao, hakujali sana usalama wake, alijali sana usalama wa Sweetie wake.

‘Kama ingelikuwa mimi mwenyewe, nisingelijali sana, wanifanye wanavyotaka wao, sijali…, lakini huyu mtu wa watu, naoana kama dhamana kubwa kwangu…’akajisema moyoni, na baadaye akajiuliza `hivi nafanya hivyo kwasababu ya kuwa ni dhaman, au kuna jambo jingine,….mmh’ alaipowaza hivyo akacheka, na kusema kwa sauti; `ama kweli kupenda ni ugonjwa….ina maana nafanya hivyo kwasaababu ya kupenda, na..hivi kweli Sweetie ananipenda kama ninavyompenda yeye…sijui, sijui…’akaangali huku na kule wakati huo alikuwa keshatoak kile chumba cha ukaguzi, alijishuku huenda kuna mtu akamsikia akiongea peke yake.

Alipofika pale mapokezi, akafuata hao masharti, kwanza alijivunga vunga kupoteza na muda, na kujaribu kuangalia huku na kule kama kuna mtu anamfuatilia au kumtiza tizama, …cha ajau alikuta wengi walikuwa wakimtizam yeye, hata alishindwa kujua ni nanii ana shauku na yeye,…..`kwanini watu wengi wana niangalia mimi, na wengi wa wanaonitizama ni wanaume ….aah, hawa ni tamaa zao, niachane nao…’akasema kimoyomoyo.

‘Wewe binti mrembo sana, unaoana watu wengi wanakutizama wewe kwa macho ya shauku, …macho ya tamaa, umeolewa wewe …?’ akajikutwa akiulizwa na yule mtu mmoa aliyekuwa pembeeni yake.
‘Nashukuru kwa sifa zenu za uwongo, maana nyie wanaume, kila mwanamke mnamtamani....ndio nimeolewa, na mume wangu nampenda sana,..ahsanet samahani naomba nipite, …’akasema Rose na kumpita huyo mtu kuelekea mapokezi.

Alipofika kwa yule mtu wa mapokezi, alimuuliza kuwa ana ujumbe wowote toka kwa mkuu wa ulinzi wa humo hotelini, yule jamaa akamwambia asubiri kidogo, …akachukua simu na kuwasiliana na huyo mkuu wa mapokezi, baadaye akaikata na kumsogelea Rose, akamwambia kwa kumnong’oneza kuwa asubiri kidogo, atapewa malekezo. Rose alijitahidi kufanya hivyo, lakini aliona wanamchelewesha, mpaka akahisi kuna jambo limetokea, …

‘Kwani kuna nini, mbona mnanikalisha muda mrefu hapa mapokezi, kuna nini kimetokea …’akalalamika Rose.

‘Bosi kasema usubiri kidogo, kuna mambo anayaweka sawa, usitie shaka mpendwa,…samahani sana kwa kufanya hivyo, …’akasema yule mtu wa mapokezi. Rose akasogea pembeni na kijaribi kuwatizama watu waliomo mle ndani, na macho yake yakatua kwa mtu mmoja aliyekuwa kashika gazeti, sura yake ilimtisha kidogo sijui kwanini…sio kwamba ana sura mbaya, lakini mwilini alihis hisia za kumuogopa tu, alihisi kuwa anamchungulia kwa siri, lakini hakujali kwani sio yeye aliyekuwa akifanya hivyo, ili huyu uangaliaji wake ulikuwa wa kimahesabu. Akawa isije ikawa ndio hawo watu alioambiwa wana nia mbaya. Kama ni wao shauri lao.

Rosi akawa anamuwaza Sweetie wake, kitu alichomuwazia zaidi ni kuhusu kama kumbukumbu zake zimerejea vyema, kama zimerejea vyema cha muhimu ni kuwa na uhakika hisia zake kwake, aikumbuka lile tukio la siku ile ambalo hakulitaraji, ingawaje kinamna moa alijuta kuwa hakuweza kuzizuia hisia zake, lakini kwa namna nyingine aliliona kama tendo liloinua hisia zake ambazo alikwisha kata tamaa nazo.Akaegemeza kichwa kwenye sofa na kuingia ndani ya mawazo huku akitabasamu kwa mbali..

‘Dada …’ Rose akasikia yule mtu wa mapokezi akiita, akamgeukia akijua ni yeye kaitwa `bosi kasema sasa unaweza kwenda ila usitumia lifti kunaznia hapa chini, panda kwanza kwa kutumia ngazi,halafu ukishafika rosheni ya pili, ndio utumie lifti ….karibu sana’akasema yule mtu wa mapokezi kwa kumnong’oneza.

‘Hamana tabu, nashukuru sana….’akasema na kuondoka hata bila kuangalia nyuma. Alizipanda zile ngazi za kuelekea juu kwa haraka na alipofika sehemu ya kufikia roseheni ya kwanza akasimama kidogo, kwani alihisi kuna watu wanakuja, nia yake ni kuwachunguza ni akina nani, watu hawo hawakuja juu haraka , walionekana kuongea kwa chini, na wakati anaangalia hivyo macho yake yakatua kwenye mtu mmoa aliyekuwa kama kajificha kwenye upenyo wa ngazi za kupandia juu, alichunguza, kwa makini, akaona labda ni mmoja wa wahudumu wa humo.

Alifika kwenye roseni ya kwanza na alipoona hakuna mtu anayemtilia shana akaingi akwenye lifti na kwenda juu, ndani ya ile lifti walikuwemo watu wanne, na mmoja wa wale watu alimuona kama alishawahi kumuona mahali, alijaribu kukumbuka bil mafanikio, wakafika rosheni ya pili, akatoka kwenye lifti na kuanza kutembea kuelekea sehemu ya vyoo vya akina mama, alikaa kidogo halafu akatoka nje, na hapo nje alikuwa watu kadhaa, hakujali akaijifnya kama mtu wa humo ndani na kuelekea sehemu iliyoandikwa `onyo’ na maelezo mengine yakafuata chini yake kuwa sehemu hiyo ni kwa ajili ya wafanyakazi maalumu tu ofisini, hakuna mtu mwingine anayeruhusiwa kuingia huko. Rose akatoa ufunguo na kufungua mlango.

Mlango ulipofunguka akaangalia nyuma, na akaona kama kuna jamaa anakuja kuelekea pale usawa wake, na kwa nyuma ya yupo jamaa mwingine, aliyemkumbuka vyema, alikuwa yule aliyekuwa akshika gazeti kule chini…akahisi mwili mzima ukizizima, …akawa anajiuliza kwanini anamuogoa sana huyu mtu, hakuelewa kabisa, akajipa moyo.

Alipowaona hawo watu waaneleeka usawa ule alipo, akajua hawa wana nia mbaya na yeye, harakaharaka akaingia ndani na ule mlango ukajifunga, aliufunga harakahraka na ufungua, akaingia kwenye sehemu kama ukumbi, na hapo kuna vyumba viwili vinavyoangaliana akasogelea chumba ambacho ndipo alipo Sweetie wake, akagonga mlango, kimiya, akagonga tena kimiya, akaduwaa, kuna nini kimetokea,…akagonga tena kimiya, ndipo akaamua kumpigia simu mkuu wa ulinzi, na simu ilkawa inaita tu haipokelewi.

‘Mungu wangu sasa nifanyeje, …’akajiuliza huku akiendelea kuugonga ule mlango kwa nguvu, …aliogopa sana kutoka mle na kukutana na hawo watu wanaomfuata, ambao hawajui na hazanii kuwa ni walinzi wa humo ndani, na huko ndani hajui ni nini kimemkuta Sweetie wake, kwanini anagonga mlango haufunguliwi na aliambiwa kuwa Sweetie kaachiwa ufunguo, je yupo humo ndani au katoroka, au anaumwa, au…aliogopa hata kufikiria hivyo….

NB: Wapendwa najua wengi mnaona nipo taratibu sana, lakini ni hali halisi inyonizunguka, hutaamini kuwa naafika asubuhi saa moja na kuanza kuandika, ili ikifika saa mbili na nusu niwe nimeandika angalau kitu cha kutuma kabla weney kampuni hawajafika, ...sipati muda mwema wa kupitia, ninachofanya ni kuandiaka kwenye Microsoft words, halafu nikimaliaza na copy na kupaste kwenye blogs...Lakini yote hayo nayafanya kwa ajili yetu, wapendwa wangu. Ijumaa njema

Ni mimi: emu-three

6 comments :

mimi said...

Asante m3 nawe pia. tunashukuru kwa kidogo pia usijali. kazi njema

Anonymous said...

Asante, ubarikiwe, hiki kidogo unachoandika kinatosha nasi tunaelewa situation yako. Ijumaa njema kwako pia

Anonymous said...

mh mi sijui

Precious said...

Yaani siku nyingi sijacheck huku majukumu yamezidi..Pole kwa yote M3 tunajua uko katika wakati mgumu sana na unafanya katika mazingira magumu ila Mungu bado yupo nasi na tunazidi kukuombea....yaani Rose na Sweetie wake mpk wanatia imani kwa kweli maana hiyo misuko2 ni balaa. M3 na wapenz wote wa blog nawatakia ijumaa njema na w/end njema wapendwa.

EDNA said...

Nimepita kusalimia,nakutakia weekend njema kaka.

Simon Kitururu said...

Wikiendi njema Mkuu!Tuko Pamoja!