Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, November 9, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-47




Rose akiwa kaka kwenye gari, huku akiwaza mbali sana mawazo yale yalirudi nyuma kidogo, akamkumbuka Adam, na wazo hilo lilipomjia akilini mwake akakunja uso, akasema kimoyomoyo, `Jinsi nilivyomuamini huyu mtu, kumbe ana mambo ya ajabu kabisa, nini anakitaka, kipindi kile nilikuwa anmzania anapata shida kwasababu ya mke wake, lakini kumbe alikuwa na mambo mengine yanamuumiza kichwa..hapana, kweli wanadamu wana mambo mengi kichwani mwao na ukiyafunguliwa yaonekane hadharani hutaamini…’

Akamkumbuka jinsi alivyokasirika pale alipokuja nyumbani kwake, na wakati huo Inspekta alikuwa kajificha nyuma ya mlango, na alishangaa jinsi Adam alivyogundua kuwa kuna mtu mwingine ndani, akawa ahataki kuingia ndani…

‘Rose upo na nani humu ndani…?’ akauliza Adam.

‘Kwani hiyo inakuhusu nini, hata nikiwa na mwanaume, ni maisha yangu…mbona unanifuata fuata kama vile tumeingia uchumba na wewe….’akasema Rose kwa hasira.


‘Sikiliza Rose, mimi sio mjinga kufanya haya ninayofanya , ungelijua jinsi gani ninavyopata taabu kwa ajili yako usingelitoa hiyo kauli…Rose, ncho yetu hii ina maadui wengi sana, na nyie mna bahati mnaishi huku mnalindwa bila kujijua, lakini hamna shukurani, …nakuuliza tena yupu nani humo ndani…?’akauliza Adam.

‘Yupo mshikaji wangu, nilikuwa napoteza naye mawazo, siku nyingi nilikuwa sijaonana naye…sawa umesikia naomba uondoke maana tuna maongezi naye kidogo….’akasema Rose kwa nyodo.
‘Nimekua nina maongezi na wewe nayo ni muhimu sana , kuliko hayo yako, ni kwa ajili ya maisha yako, ni kwa ajili ya usalama wako, nakuomba unipe muda kidogo, na kama inawezekana tuongelee kwenye gari langu…’akasema Adam.

‘Kwakweli sina muda kabisa, hata huyu jamaa yangu nimemuomba sana aondoke maana nachelewa kufika mjini, nimepewa mwisho saa kumi na mbili, je utanikodia ndege niwahi huko mjini…?’ akauliza Rose.

‘Kama ikibidi nitafanya hivyo, nipo tayari kwa lolote ulihitajilo, lakini kwa sasa cha muhimu ni usalama wako..na naomba tuongelee mbali maana …’akasema Adam na kujaribu kuchungulia kwa ndani kama atamuaona huyo mtu.

‘Tafadhali sana, Adam, nashukuru sana kwa kunijali, lakini sina muda huo, naomba tafadhali ondoka nijiandae, kama ni kuongea siku nyingine,…..samahani sana…’akasema Rose na kufunga mlango.

Adam aligeuka bila kusema jambo akaingia ndani ya gari lake kwa ahsira na kuliendesha kwa kasi kueleeka ufukweni, hakuamini kuwa Rose ndiye huyo , ndio yule mtu walieyekuwa wamependana, na kusaidiana wakati wote, alikumbuka jinsi alivyoweza kumtoa kwenye makucha ya ulevi, …hakuamini kuwa amemkosa huyo mwanamke, akaapa moyini kuwa atafanya kila hila mpaka atampata tu.

‘Lakini ni mwanaume gani yupo naye humo ndani…?’ wivu ulimjaa, akataka kugeuza gari arudi na kuingia ndani, lakini akaona sio jambo la busara, …alichofanya ni kutafuta sehemu ya kulihifadhi lile gari na kurudi kwa miguu, nia amuone huyo mwanaume ni nani…

Alipofika maeneo ambayoo anaweza kuona nyumbani kwa kina Rose, alikuta gari likiondoka, na hakuamini macho yake, alishikwa na kizunguzungu, mwili mzima ulimuishia nguvu, akatafuta sehemu akakaa kwanza na kutulia, hakuamini, …sasa mambo yameiva, kazi imeanza, kama ndio kajiunga huko, basi sina lawama nay eye…lakini hapana nitajitahidi kumtafuta kwa dawa na uvumba….akawa anajisemea mweneywe kama kichaa….

****
Inspekta alimwambia Rose kuwa sasa ni muda muafaka wakushirikiana na vyombo vya usalama, akamwambia `kama kweli unajali maisha yako na ya mwenzako, inabidi unisikilize mimi nitakachokuambia, …..lakini hilo nitakuja kukuelekeza baadaye…’aligeuka na kumtizama Rose, hata hivyo Rose hakumjibu, kwani ilionekana anawaza mbali sana, na kimawazo hakuwemo pale kabisa.
Baadaye Inspekta alipewa taarifa kuwa hatua zimeshachukuliwa kwahiyo wasijali, wanaweza kuingia maeneo ya hotelini bila wasi wasi, akampa ishara dereva wake aongeze mwendo, na wakaingia hotelini kwenye saa moja usiku.

Hoteli ile kwasababu ni ya watalii, wengi walioonekana pale walikuwa ni wazungu, hata hivyo, Insepkta hakutaka kujulikana, kwahiyo alichofanya ni kumwambia dereva wake apite nyuma nyuma ya gari lililokuwa mbele yao. Na walipofika getini, mtu wao akafika na kuwaruhusu wapite, na wakati wanapita pale getini mawazo yake yalikuwa yakijaribu kutafakari mchakato huo, akilini alijaribu kutafakari wazo la kumtumia Rose kama chambo, lakini bila hata yeye mwenyewe kujua, ingawaje alijua kabisa kwa kufanya hivyo wanaweza kumtumbukiza Rose katika hatari kubwa sana.

Aliongea na mtu wake na huyo jamaa yake alimpa uhakika kuwa wameshaweka watu wao waaminifu kuhakikisha kuwa usalama huo upo na huyo jamaa yake akamhakikishia kuwa hata yeye mwenyewe yupo mstari wa mbele kuhakikisha kuwa mtego huo unafanikiwa…..

‘Safi kabisa basi tumeshawasili , kwahiyo mimi nitakuwa namfuatilia chambo chetu, mengine tutawasilianana baadaye..’akasema Inspekta na kukakata simu.

‘Akaanza kuwaza jinsi gani ya kuhakikihsa kuwa Rose hatazurika. Kiujumla anavyolijua hilo kundi na jinsi alivyosikia Adam akiongea na Rose, ilionekana wazi kuwa hawo watu wasingeliweza kumzuru Rose, na kama ni kufnya haivyo hawataweza kufanya akiwa humo ndani, …ila ni muhimu kuchukua tahadhari zote. Kitu cha kuangalia ni huyo jamaa yake Rose, inaonekana nia yao ni kumuua, lakini hata wasingeliweza kumuua humohumo ndani labda watumie silaha ya kiona mbali, kwani hakuna mtu angeliweza kuingia kwenye hiyo hoteli na silaha…

Kazi ilikuwa jinsii gani yeye angeliweza kuingia na silha humo ndani, na asipate bugudha yotote, lakini kwa hilo alishaongea na jamaa yake aliweke sawa, walichofanya nikuomba kibali cha hiyo hoteli, ilibidi waombe hivyo kwa siri, ingawaje kwa utendaji wao waliruhusiwa kufanya hivyo, …lakini hawakutaka kusimamishwa simamishwa kuulizwa maswali, kwani wengi wao walikuwa wamevalia kiraia, na kwa mtindo huo walijua kuwa hawo watu watakuwa na watu wao pia,na ambao wangelitumia mwanya huo na kuingia na silaha, inagwaje ni kazi kubwa sana kufanya hivyo kwenye hoteli ambayo ilikuwa na ulinzi mkali , na vyombo vya kisasa vya kugundua kitu chochote kisichoruhusiwa…

Wakati wanaingia chumba maalumu ambacho mtu hupita na kama una kitu kisichoruhusiwa alama maalumu ya hatari huonekana, akatoa ile kofia yake ili yule mlinzi na mtu wao alieykuwemo naye amgundue na apite bila kupata bugudha yoyote….lakini lionekana kuwa yule mlinzi mle ndani hakuwa anajua hilo, akamsimamisha Inspekta, na alimpomkaribia akamgundua , akainama kwa heshima kumuacha apite.

Insepkta aliangalia nyuma yake kuwa kuna mtu anayeweza kumshuku kwa kitendo kile, maana katika kupita kwenye chumba hicho huwa wanapita watu watano watano, …lakini hakuweza kugundua lolote kati ya wale watu…ingawaje kitnendo kile cha kuvua kofia na kuivaa alikifanya haraka, ili kama kuna mtu alikuwa anamchunguza asiweze kumtambua. Hata hivyo Inspekta alishikwa na mshaka kuwa watu hawo ni waozofu, na kama kuna wao katika lile kundi atakuwa keshamgundua, kwa kitendo kile kilishamuweka Inspekta katik uwazi zaidi, na hivyo ilibidi awe mwangalifu, hakujali hilo kwa muda ule, alichojali nii maisha ya Rose.

Akaingia ndani ya ukumbi wa mapokezi, na hapo akapitisha macho yake kwa haraka kuangalia usalama na katika kunagalia huko aligundua sura za watu wawili ambao aliswashuku, mmojawapo ni yule aliyemuona akimfuatilia Rose toka nje, na huyu akamuweka katika kundi la hatari, na mwenzake alikuwa anajifnya anasoma gazeti, na alikaa kwenye sofa, akijifanya kumsubiri mtu,lakini macho yake kila mara yalikuwa yakimtiuzama Rose, na pia alionekana kuwasilina na sehemu nyingine kwa chombo alichokuwa kakivaa sikioni na mdomoni.

Rose alikuwa bado kasimama anaongea na mmojawapo wa watu wa mapokezi, na pale alionekana hana haraka kulekea chumbani kwake kinyume na alivyokuwa akionyesha wakati yupo na Inspekta ndani ya gari, …huenda alifanya hivyo, kwa maagizo ya mkuu wa ulinzi, kuwa akija asielekee chumbani kwake mara moja had atakapopewa ishara ya kuelkea juu kama alivyoahidiana na mkuu wa walinzi kuwa akija hapo asielekee moja kwa moja chumbani kwake, kwani huenda watakuwawamefichwa, kwenye chumba maalumu ingawaje hilo hawakuliweka wazi mbele ya Inspekta.

Alimwangalia yule jamaa alinayejifanya anasoma gazeti, na huku anamchunguza Rose, hali hii ilimpa wasiwasi sana Inspekta na kuiuliza imekuwaje, wakati huyu mkuu wa ulinzi alishasema kuwa hpo hotelini haparuhusiwi watu wenye vyombo kama hivyo , labda awe mtu wa usalama aliyejitambusliha na kuonyesha kitambuslisho, na huyu mtu hakuwa akbisa mtu wa usalama, …

‘Huyu mkuu wa ulinzi aliniambia watu kama hawa hawapewei muda wa kuingi humu ndani , mbona huyu mtu hajachukuliwa hatua, huenda jamaa hayupo ofisini kwake, na hii ni hatari, nilimshauri atafute msaidizi , haweze kufanya mambo yote peke yake…’akawa anajisemea mwenyewe huku anasogea taratibu kuzifata zile ngazi za kupandisha juu, alijifanya kama mmoja wa wateja walio na vyumba humo ndani, na ili kufanikiwa hilo alijifanya kuwa anaoongea na mmoja wa wapangaji wa humo, na huku anamfuatiia nyuma huyo mpangaji na kupanda naye juu.

Alipofika kwenye zile ngazi akachepuka haraka hadi sehemu anayoweza kuangalia chini, akaitoa bastola yake …lakini baadaye akairudisha, …sio muda wake huo.Akawa anamsubiri Rose apandishe na hapo kama kuna mtu anayemfuata kwa nyuma atakabaliana naye, aliona ni heri kumzuia mapema kabla hawajafanya jambo lolote la hatari, akashika pale lipoiweka bostola yake na kuitayarisha kuitoa, hakuhitaji haraka kufanya hivyo akasubiri na mara akasikia mtu akipanda kuja juu, akachungulia na kumuona ni Rose.

Rose alimpita Inspekta bila kumguindua, kwani sehemu ile liyojibanza sio rahisi mtu kugundua labda uwe makini , kilikuwa kama kiupenyo kilichojengwa kama chumba, lakini sio chumba, Inspekta akasubiri na kama alivyokuwa kakisia kuwa wale jamaa wanamfuatilia Rose, alimuona mmojawapo akija toka chini kwa haraka, akiwa anajitahidi asimkose Rose, na haikupita muda ma yule mwingine akaonekana akipanda hizo ngazi na walipofika pale alipojificha Insepkta wakaanza kunong’onezana.

‘Kuwa makini lazima kuna vyombo vya kuchunguza watu, wanaoingiza humu, angalia kwenye kona ile pale, kile ni chombo cha kuangalia watu wanavoingia ndani, jifanye unaelekea kwenye chumba chochote, lakini hakikisha unafahamu wapi huyo binti anaelekea, na miminakua kwa nyuma…’akasema yule jamaa na mwenzake bila kusema neno akakimbilia juu.

Inspekta akasubiri hadi yule jamaa mwingine naye alipoondoka kuelekea juu akamfuta kwa nyuma, na walipofika eneo la varanda ya rosheni ya pili, alimuona yule jamaa wa kwanza akiwa karibu na Rose, huku akijifanya kama anatafuta chumba, na mwenzake akapitiliza kuelekea juu, nafikiri alishaotea kuwa Rose anavunga tu haishi kwenye rosehni hiyo ya pili.

Rose bila kujua akasubiri lifti na kuingia kuelekea juu, na Inpsekta akamfuatilia yule jamaa aliyeamua kutumia ngazi, na alimkuta akiwa anasubiri kenye lifti, ambapo Rose na yule jamaa mwingine walitoka pamoja, na bila kusemeshana wakawa wanatembea mwendo wa taratibu , huku wakijiiba kumwangalia Rose ataelekea wapi. Ilionekana kabisa kuwa Rose hana wasiwasi kuwa anafuatwa nyuma, akatembea mwendo wa haraka hadi sehemu yenye maandishi ya kuonya kuwa eneo hilo ni la wafanyakazi pekee wa hiyo hoteli hakuna mwingine anyeruhusiwa kuingia eneo hilo.

Rose alitizama nyuma kwa tahadhari, halafu kwa kujiamini akatoa ufungua na kufungua mlango , na ulipofunguka tu akaingia kwa haraka, …na mlango ukafunga. Wale jamaa wakabonyezana na kuondoka pale kuelekea juu zaidi. Insepkta alisimama kwa muda akitafakari, … akaona awafuate wale jamaa huko juu walipoelekea na alipofika eneo la rosheni ya juu alimuona mmojawapo akiwasilina na kile chombo cha simu alichokuwa kakivaa sikioni. Insepka akawa kasogea karibu na kuweza kuyasikia yale maneno aliyokuwa akiwasiliana….huyo mtu alisema kuwa wamesha gundua wapi mtu wao alipo lakini hawajawa na uhakika kamili,…

Inspekta alimpita yule mtu na kuhangaika kumtafuta yule mtu mwingine, hakuweza kumuona na hili likampa shaka zaidi kuwa huenda wamechukua chumba humo ndani ili kukamilisha dhamira yao, au kuna mahali kajificha, au ….au au zikawa nyingi, na zilihitaji uchunguzi kabla ya kufikia hitimisho. Mara alipogeuka nyuma, akamuona yule jamaa aliyekuwa akiwasilina na simu akimjia , ilionyesha dhahiri, alikuwa akimjia Inspekta, na hapo inspekta akahisi hatari, akasogeza mkono wake kushika bastola yake..

‘Wala usijaribu kufanya hivyo…’ upo chini ya ulinzi mkuu…’ sauti ya kikakamavu ikasikika nyumba yake, na wakati huo huo yule jamaa aliyekuwa akimfuata alisimama kwa ghafla alipoona kile kitendo, labda alikuwa kamgundua Inspekta au huyo jamaa aliyemkamata Insepkta hajuani naye…yote hayo hayakuwa na umuhimu kwa wakati ule, muda ndicho kilikuwa kikitakiwa, Inspekta akatulia kama alivyoagizwa, huku akimtizama yule jamaa aliyekuwa akimfuta,…kwani wakati huo huyo jamaa alikuwa akielekea upande mwingine akijifanya kama vile kasahau kitu na anarudi kikiufuata kule alipotoka.

‘Hebu tuambie wewe ni nani kwani unawafuatilia nyuma hawo jamaa wawili…?’akauliza yule na mara akatokea jamaa mwingina akamnong’oneza sikioni.

‘Mimi ni mmojawapo wa watu wa usalama, namimi nawauliza nyie ni nani….?’akauliza Inspekta.

‘Sisi ni watu wa usalama wa humu ndani, tunaomba kitambulisho chako…’akasema huyo mtu.

‘Nikiwa kazini mara nyingi sihitai kuwa na kitambuslisho kama hamuamini twendeni kwa bosi wenu…’akasema inspekta.

‘Hebu mwachie huyu hujui huyu ni nani wewe, utajitakia matatizo bure…., muda unakwenda twende zetu…’akasema yule jamaa mwingine na wote wawili wakaondoka, na hapo hapo naye akatoka na kuelekea kule anapohis yule jamaa aliyekuwa akimfuatilia kaelekea. Alitizama kila kona lakini hakuona dalili yake au dalilii ya yule mtu mwingine, akaamua kushuka chini na kuelekea pale alipoingia Rose, na aliposhika mlango kutaka kuufungua, mara mlango ukafunguliwa na Inspekta akashikwa na butwaa, hakuamini macho yake…..


Ni mimi: emu-three

6 comments :

Anonymous said...

Asante kwa masimulizi M-3, nakuombea Mungu afanye wepesi katika masuala yako.
Nimekuwa nikifuatilia kisa hiki tangia mwanzo, ila kwa sasa naona kama hakiendi mbele yani kinazungukia tu hapo hapo, nahisi kinapoteza hamu ya kusoma, ila mwanzoni kilienda vizuri sana. jaribu kuliangalia hili. Hope utachukulia kama positive critism ni kwa nia njema tu.

Mimi said...

AISEE KAZI! KILA LA KHERI M3 BADO TWAKUOMBEA

emuthree said...

Nashukuru mimi kwa kuendelea kuwa na mimi kivitendo.
Nashukuru sana mchangiaji wa pili ,hilo ndilo nikuwa nataka kusikia. Nashukuru sana kwa maoni yako na tutaifanyia kazi.
Nilikua natamani sana kusikia maoni kama haya,je unaonaje,je ulitaka iweje,au vipi ilitakiwa iwe! Ni vema nami nikachangia sababu za 'kuzunguka hapohapo ' ili tuone inafaa au haifai.
1. Hiki kisa ni cha kweli na mhusika licha ya hayo alikumbwa na majanga mengi alipokua huko. Hapo tu nimefupisha. Je tuachane na ukweli tuangalie kitamithilia?
2.diary kama ilivyo ni mchakato wa matukio.je tuache uhalihisia tuangalie kitamlisia?

Anonymous said...

Nashukuru kwa majibu yako, mie mdau wa kwanza hapo juu. Ni kweli usemayo ni kisa cha kweli lakini pia ni kama burudani kwa sie wasomaji, wewe ni muandishi mzuri bkz msomaji anazama ndani ya kisa as if ni part ya hayo yanayoendelea for this big up. I cant say much ila hivyo ndio mimi nilivyoona no foward movement, may be kumix part (I mean part ya Rose kidogo na part ya Maua)ingesaidia kuondoa hii kitu. ni maoni tu, ila tunashukuru kwa kujitahidi kuandika pamoja na matatizo

emuthree said...

Ndio mdau wangu, maoni yako ni mazuri sana nami nilishaliona hilo, lakini kwa sababu ya mazingira niliyonayo, huwa nikifika asubuhi, najikuta nimeshaandika huku kwa Rose, na muda wa kusema niandike tena kwa Maua unakuwa hakuna, ila tuvumilie kidogo tu, tutamuona Maua, na huko huenda ikawa ndio hitimisho....nashukuru sana, na kusema kweli wewe umefanya kile nilichokuwa nataka, kupata mawazo kutoka kwa wengine, wanaonaje, wanasaurije, ili nami nijue wenzangu wanafikiriaje...shukurani sana

Anonymous said...

Nashukuru sana for appreciation, you sound to be a very positive person. Ni sawa kuhusu kuchanganya part kwa vile una mpango wa kuja kutoa kitabu then you will have time ya kurekebisha. kwa kweli unajitahidi sana, na kipaji unacho kikubwa, I enjoy reading every part of what you write, niliijua blog yako toka kisa kile kilichoisha kilipokuwa katikati, basi nilirudi back na kusoma tangu mwanzo, since then sijaacha kufungua hii blog, so tupo pamoja na Mungu wa yote akufungulie njia ya pale palipofunga. Cheers