Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, November 14, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-49



Turejeeni kwa Maua , kwa kujikumbusha tuanze na kipande hiki kidogo, na mamo mazuri zaidi yanakuja....


*******************
Chumba maalumu ambacho Docta Toboa Toboa alikitumia, kilikuwa kimetulia kimiya, na Maua alikuwa keshapanda juu ya kile kitanda kidogo, akiwa bado hana wasiwasi, alijua ni jambo la dakika chache kama alivyoambiwa, na halafu mambo yatakuwa yamekwisha, atasahau kabia kuwa alikuwa na kitu tumboni. Maua akalaza kichwa chake akiangalia juu, na hapo wasiwasi ukaanza kumwingia, . Aliawaza mengi, kwanza yupo peke yake na huyo dakitari, na lolote linaweza kutokea, ndio anamuamini kama dakiatari, lakini hisia za kibinadamu zikamtanda kuwa anaweza akafanyia kitu kibaya.

‘Usiwe na wasiwasi kabisa ni jambo la muda mfupi tu, mambo yatakuwa yamekwisha, ….’akapewa matumaini na huyo dakitari ambaye alishavaliwa manguo yake na kuficha sura yake.
Wakati Maua keshalala, kwenye kitanda maalumu, docta aliingia chumba cha pembeni yake ili kuchukua baadhi ya vifaa vingine na kuchanganya dawa, nakumuacha Maua akiwa kalala huku kaangalia juu, …hapo mawazo makali yakamtinga…ghfala kitu kama kijiusingizi kikamtanda usoni na mara kwa mbele yake akaona sura ikimjia, …ilikuwa sura ya aliyekwua mume wake, sura hiyo ingawaje ilionyesha kufifia, lakini aliweza kuiona dhahiri kuwa ilikuwa sura ya mume wake, …ooh, Mhuja, …mume wangu, …alianza kuweweseka, na cha ajabu alimuona akitoa machozi, …Maua akataka kuinuka lakini nguvu zilikuwa zimemuishia kabisa, hakuamini macho yake….

‘Hebu niambie unataka kufanya nini,…’Mume wake akamwambia huku akionyesha sura ya chuki, sura ya dharau, …akatikisa kichwa na kuendeela kusema `Unataka kumdanganya nani,. Kunidanganya mimi, au kumdanganya rafiki yangu kuwa wewe ni mtakatatifu…’ Ile sura ambayo ilionekana kichwa tu ikasema tena na machozi yalikuwa yakimbubujika.

‘Hapana, unajidanganay mwenyewe, unashindwa kujua kuwa aliyewezesha kuwepo kwa hicho kiumbe tumboni kwasababau ya uzaifu wako,hadanganyiki, hadanganyiki na hilo na wala hadanyiki na akili yako inavyokutuma, yeye anajua kila kitu kilichopo akilini mwako,….mungu mwenye ujuzi, mwenye akili, mwenye hekima, mwenye nguvu anajua kila kitu…’aiaksema ile sura na kuangalai juu. Halafu ikawa kama inamsogelea, na Maua akajaribu kuinuka ili kutka kukimbia.

‘Unataka kukimbilia wapi, wakati dhamira yako imeshakushitaki, kwanza umekuwa msalaiti wa ndoa, pili ukazini, na tati uanataka kuua, …kumbuka mungu ni muweza , sababu na akili yako unashindwa kujua kuwa huyo mweneyuwezo wa kukiweka hicho kiumbe tumboni mwako, ana uwezo wa kukifanya hicho kiumbe kikatoka na kila kitu kichopo huko ndani na usiweze na uwezo tena wa kupata ujauzito mwingine, na baada ya hapo utamlaumu nani….’ile sura ikaendeela kuongea, na sasa machozi yalishakauka, ikawa kama ina fifia, huku ikisema `Sawa kama umemaua hivyo tunakutakia mafanikio mema, lakini kumbuka majuto ni mjukuu huja baada ya kitendo…’ ile sauti ilikuw akama mwangwi fulani masikioni mwa Maua ghfla iakpotea na mbele yake akamuona yule dakiati akiwa kashika mikasi na vifaa vingine.

Alijshnaga jinsi nguvu zilivyomtoweka, na alishakataa kupigwa sindan ya kulala, kwania alimabiwa kuchagua, apigwe sindano ya kulala, na kila kitu kifanyike akiwa usingizini, aua afanyiwe akiwa anaona ila atapigwa sindani ya ganzi tu, akasema anataka sindani ya ganzi tu, na aendelee kuona kinachotendeka.

Wakati anamsubiri huyo docta kufanya vitu vyake, akaribu kusema kitu , ili kumwambia Docta, kuwa kuna mtu nyuma yake, lakini hakuweza, na huku akili yake ikiwa inasononeka kwa huzuni kwa kufikiria jinsi gani kiumbe hicho kitakavyotolewa,…aliwaza na kuwazia huo unyama anaotaka kuufanya, akajaribu kukisia kiumbe hicho kitakavyotolewa bila hata ya kujitetea, ina maana anaua kiumbe kisicho na hatia, anaua bila hata ya kukipa muda wa kujitetea, hapana haiwezekani, huo sasa ni unyama, ina maana kweli keshafanya zambi ya kuzini, na baada ya kumsaliti mtu aliyempenda kwa moyo wake,wote, na baada ya kuzini, akamkubalia mtu ambaye lishamchukia kwa tendo hilo, na sasa ndio anataka kuua, ….hapana, …

Kuna hisia nyingina zikamjia na kusema ‘Lakini nisipofanay hivyo, ni nani ataniamini kuwa haikuwa dhamira yangu, na hata huyo aliyenilfanya hivi atakubalaiana na mimi kuwa huu ni ujauzito wake, …kwani muda ulikuwepo wa kumwambia, na alishawahi kuulizwa mara nyingi akakataa kabisa kuwa hana tatizo lolote….akamkumbuma Maneno kuwa kila mara wanasalimiama naye hajawahi kumwambia hili....leo kwasababu anataka kunioa ndio nimwambia kuwa nina ujauzito wake, …kweli ataniamini, ukweli….je mfano kama angeliamua kumwambia na mara akaamua kumkatilia angelikuwa mgeni wa anni…ooh, achia huyo Maneno je shangazi yangu akigundua hili atamuelewaje, …hapana lazima niitoe hii mimba kama nikuanza na huyo Maneno tuanze nikiwa sina kiumbe chochote…..’mara simu ikalia na kukatisha yale mawazo yake …

‘Nilikuambi ukiingia humu uzime simu yako, sasa unaona, hujui nani huyo kakupigia na usipoipokea itakutia mawazo , kiasi kwamba tutashindwa kuifanya kazi yetu vyema, haya ipokee kabla sijaanza kazi….’akasema Docta.

‘Hapana…nipe niizime, sitaki kupata mitihani mingine wewe anza kazi yako,….’akasema Maua.

‘Hpana ipokee kwanza hiyo simu, ni muhimu sana ukaondoa kila kitui moyoni mwakp…..’akamshauri Docta huku akimpa Maua ile simu aipokee. Na Maua akaichukua ile simu na kuinaglia ni nani aliyempigia aliona kuwa aliyempigia ni shangazi yake.

‘Maua unafanaya nini huko hospitalini…’Ilikuwa sauti ya shangazi yake ikionyesha kuwa na wasiwasi.

‘Nimekuja mara moja tu kuangalia afya yangu..’akasema Maua.

‘Maua tafadhali…. , nakuomba usije ukafanya jambo la kunitia aibu…., tafadhali sana, kama umeshapima na kugundua chochote , nakuomba usichukulie pupa,….tuliza akili yako….na nisubiri nakuja ….unasikia Maua ujue chochote utakachokifanya sasa, kinaweza kukuletea majuto makubwa sana. Unamkumbuka yule rafiki yako aliyeishia kujiua baada ya kutoa mimba, …aliitoa akijua kuwa keshamalaiza tatizo lakini kumbe alikuwa kaanzisha tatizo jingine, akawa kaharibi kizazi….tafadhali sana…Maua..’akasiki shangazi yake akiongea na ilionyesha kuwa yupo ndani ya gari.

‘Shangazi mbona unanongea hivyo, nani kakuambia kuwa nina mimba,,,,siajaja huku hospitalini kwasababu hiyo, nimekuja kungalia mambo mengine ya afya yangu….’Maua akajaribu kudanganya’
‘Maua mimi naju akila kitu, hali hiyo nilishaijua mapema sana, ..sasa kama umepima na kuambiwa lolote, usifanya chochote mpaka tuoanane, najua kila kitu Maua, najua kuwa una ujauzito na huo ujauzito ni wa Maneno, hilo nalijua mapema sana, ila sijamwambia Maneno, nitamwamambia baada yaw ewe kufunga ndoa….’akasema Shangazi na kumfanya Maua ashituke na kusimama ghafla.

‘Kumbe wanajua, kumba shangazi anajua ….hapana siwezi ….jamani …’akashuka pale kweney kitanda na kukimbilia chumba cha kubadili nguo.

‘Vipi mbona unakwenda wapi , unataka kufanya nini, mimi nimeshatayarisha dawa , na hizo dawa ukishazitayarisha huwezi…..,mbona nilishakupa muda wa kutosha wa kutafakari…kwa minajili hiyo gharama zako hautarudishiwa…’akasema Docta.

‘Unataka kusema nini…kwanini,….hujafanya lolote ni lazima utanirudishia sehemu ya gharama, ….’akasema Maua na kabla hajamaliza wakasikia docta akiitwa na nesi …na sauti nyingine ikawa ainaongea ….kwa mbali Maua alisikia sauti ya shangazi yake, na sauti nyingine ya mwanaume ambayo hakuitambaua vyema…Maua hakutaka kusikia zaidi ,….akamwambia docta amfungulie mlango wa nyuma, ….docta naye hakufanya ubishi akafungua huo mlango….Maua akatokea mlango wa nyuma, huku nyuma akasikia sauti ya shangazi yake akiuliza, Maua yupo wapi….

Na alipotizama mbele yake aliliona gari limesimama,.....gari la Maneno....mungu wangu.....


Ni mimi: emu-three

No comments :