Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, September 27, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-31



‘Ina maana kweli Maua amekubali kuolewa…? ‘Akauliza mama mmoja
‘Kwanini asikubali kwani kuna ajabu gani ina maana yeye kawa mjane wa kudumu, …haiwezekani, kwanza bado mdogo, hata kuzaa bado, na kaomboleza miaka miwili …hakuna zaidi iliyobakia, naona kama akiendela hivyo atachnganyikiwa, kwahiyo nimeshukuru sana kuwa kampata mtu ambaye anaweza akachukua nafasi ya marehemu, ….’ Akasema shangazi yake Maua, huku akiangalia saa yake, alifika hapo kwa shoga yake kumpa kadi, lakini kabla hajafanya hivyo ukaanza umbea mdogomdogo, na aliona akiendela kukaa hapo atazidi kupoteza muda wake mwingi wakati anahitaji kuwapitia mashoga zake wote, kwani shughuli ni watu, na watu usipowaambia uso kwa uso inaishia kuwa lawama.

‘Hapana nilikuwa naulizia maana maneno hayo nimeyasikia juu kwa juu, nikasema ina maana shoga yangu ananificha, hata kadi hatupati , au itakuwa ndoa ya mkeka….’ Akasema yule mwanamama.
‘Ndoa ya mkeka..?’ akamaka shngazi mtu kwa jaziba na halafu akasema `Wewe vikaoni hufiki unataka uletewe kadi nyumbani, sawa kadi yako hii hapa, na kwa vile umeniomba mapema kabla sijakupa mwenyewe, natumai hata mchango utafanya hivyo hivyo, ujue shughuli ni watu, na shughuli ya harusi siku hizi ni ya kijamiii, nije lini kuchukua mchnago wako…?’ akasema shsngazi huku akiiandika jina la yule mama kwenye ile kadi.

‘Ina maana hii ni kadi ya mchango, nilidhani utatoa kadi ya mualikwa,hahaha…kweli siku hizi umeishiwa, enzi zako ulikuwa ukitamba, sitaki mchango wa mtu, naalika tu, sasa kiko wapi, umeshuka hadi tume kuwa sawa…hahaha...sawa nikipata nitakuja mwenye kutoa mchango wangu, kwa ujumla sio kwamba hatupendi aolewe,ila ameteseka sana binti yetu huyo, ….na wengi tulifikia kuwa hataolewa tena, imekuwa kama yeye kafiwa kwanza, …hayo ni mambo ya muumba, inatokea tu, lakini binti yako alizidi….sawa, sio nakusimanga, ila tu tunaongea….!’ Akasema yule mama akiminya jicho la umbea.

‘Sina la kusema shoga yangu, nakuua kama ninavyojua kiganja cha mkono wangu, na nikija kwako , nakuja tu kwasababu ujirani mwema, lakini huwa najiuliza mara mbili, tatu, na kama isingelikuwa ni swalal la ujirani mwema na kuwa ndoa ni ya kijamii, nisingelikuletea kadi hii, ningekuletea kadi ya mualiko, lakini nakujau kuwa hata kama ningelifanya hivyo, mwisho wa siku ungenilaumu, kwanini unanipa kadi ya mualiko, kwanini hukunipa kadi ya mchango, siji….huna jema shoga yangu wewe…sitaki mengi, kwaheri, na kama ulivyosema kuwa uataleta mwenyewe huo mchango, sitasumbuka kuja kwako tena…’ akasema shangazi mtu.

‘Uje usije , mchango nitauleta, na ulisema anaolewa na nani vile, ?’ akauliza huku anaifunua ile kadi kuiangalia, halafu alipoona jina akaguna na kusema. `Mungu wangu, yaaani anaolewa na kakak mtu, huyu sio ndugu yake anayemuoa, mbona mnafanya mambo ya ajabu, ….’ Akasema yule mama huku akiitupa ile kadi kwenye meza.

‘Marehemu anatoka huko milimani huyu anayetaka kumuoa ni mtoto wa pwani, udugu huo umetoka wapi, ….we mwanamke kwa umbea,…kama hutaki kuchanga sema, lakini hawo hawana udugu kabisa …ila walikuwa marafiki tu, hata hivyo nakupa kadi zingine, uwagawie wambea wenzzako, maana naweza nikawasahau…’ akasema shsngazi mtu.

‘Na kweli bora umelikumbuka hilo, nitawapa mashoga wangu, maana nikikutana nawo nitakuwa na chakuongea, mimi siamini kuwa wale hawakuwa ndugu,….mmoja anaweza akazaliwa milimani na mwingine Pwani nab ado wakawa ndugu, nyie, ……siwamalizi, au kuna kitu…nahisi kuna kitu…’ akasema yule mama.

‘Kuna kitu gani, labda kitu hicho unakijua wewe , kwaheri….’ Akaondoka shangazi mtu huku akiwa kachoka, maana watu kama hawa ukikutana nao lazima waweke

**************

Maneno alikuwa kama kawehuka kwa raha aliyokuwa nayo, akawa kila mtu anayekutana naye hata kama hamjui anamsimamisha na kumwambia, kuwa anatarajia kuoa, halafu anauliza `unaajua ni nani nataka kumuoa, na hata kabla huyo mtu hajamjibu, humalizia kwa haraka akisema namuoa malikia wa dunia, ua lenye kupendeza dunia nzima, Maua….unamjua Maua wewe…hahaha, karibuni kwenye harusi yangu.
Siku alipokubaliwa na Maua kuwa yupo tayari aolewe, alitamani dunia isimame hata kwa sekunde moja…na hapo hapo akauimba ule wimbo wa mlimani park usemao; `

Uliponikubalia tuwe mke na mume
Nilitamani Dunia isimame hata kwa sekunde moja
Ili niione nuru ya mapenzi yako
Na roho yangu iwe radhi kuwa huru….

Akawa nauimba huo wimbo huku akicheza mpaka Maua akacheka, na ndilo alilokuwa akilitaka Maneno na baadaye akamsogelea na kutoa pete ya thamani, aliyoinunua siku nyingi sana, siku alipokuwa akivizia Maua na bahati mbaya hakuwahi kumpata, pete hiyo akaihifadhi sandukuni, na leo ikawa imefika kwa mlengwa, akamuomba Maua kidole chake, akaiona ile pete aliyokuwa kaivaa Maua awali, ya Mhuja, akamwangalia Maua machoni, hakusema kitu, akaitoa ile pete, na kuiweka pembeni, halafu akamvika ile pete yake…

‘Sasa Maua nakuhakikishai utakuwa na raha, rah azote za dunia nitakupa, ilimradi ziwe ndani ya uwezo wangu, nakuomba unipokee kwa mikono miwili, kwani nafanya haya kwa mapenzi, kwa mapenzi niliyokuwa nayo tangu siku ya kwanza kukuona, …nilikutafuta mashariki na mgharibi, sikukuona, …na siku niliyokuona ulikuwa kwenye himaya ya Mhuja, na kwa vile yule alikuwa rafiki yangu sikuweza kufanya lolote….sasa naona mungu kaunikubalia ombi langu umerudi kwangu…’ akasema Maneno, lakini Maua alikaa kimiya tu…

Maneno akiwa anawaza tukio hilo la aina yake katika misha alikumbuka jinsi alivyohangaika , alihangaika sana hasa pale alipokutana na shangaziye Maua na kumwambia kuwa ili asifungwe, ili aisjije akaaibika kwa alifanya kitendo kibaya kwa mtu asiyekuwa anajitambua, na ikimaanisha kuwa alibaka, basi ajitahidi sana kumshawishi Maua awe mke wake, na hilo alifanya haraka sana. Hakujau kwanini shangazi huyu alimshurutisha hivyo kuwa afanye haraka sana, lakini kwa uapnde wake, ilikuwa faraja kufanya hivyo.

Alichofanya Maneno ni kuhakikisha kuwa kila siku anapita kwa Maua, ambaye alikuwa yupo nyumbani kwa vile wale waajiri wake walisafiri, kwahiyo muda mwingi unaweza kumkuta nyumbani na wakati mwingine yupo kwenye biashara zake. Na hili lilizidi kumfanya Maneno azidi kufanya juhudi kwani alijua atampata mke mchakarikaji, ambaye watashirikiana huku na kule, …

Ilifanya hivyo kila siku anafika kwa Maua wanasalimiana na kila akianzisha hiyo hoja ya uchumba, wanakorofishana, na mwisho wake Maneno anaondoka, akiogopa kumuudhi zaidi Maua, mpaka ikafika mahali akakata tamaa, na siku moja shangazi akaja kumtembelea tena na kumuulizia wamefikia wapi
‘Shangazi, sijui kwanini Maua hataki kunielewa, sijui kuwa labda hanipendi, au sijui niseme nini, nimejitahisi kila njia, lakini ….’ Akasema Maneno.

‘Hilo ni jukumu lako, na kama umeshindwa, kwanza utaumbuka, pili kuna mtu anamtaka Maua kwa udi na uvumba, yeye …akaongea tu na Maua sidhani kama itachukua siku nzima, …lakini kwa vile wewe ulishaanzana naye na umefikia hatua ya kumzalilisha, nikamsimamaisha huyo mtu kuwa huyo shangazi yangu ana mtu tayari, sasa, nakupa siku tatu, baaada ya hapo hutanisikia tena,….’ Akasema shsngazi na kuondoka.

Siku hiyo Maneno hakulala, wivu ukamjaa, ina maana kuna mtu anamwinda Maua, ndio wapo wengi, lakini huyu mpaka akaamua kumwendea shangazi mtu, …atakuwa kakusudia kweli, na labda keshaongea na Mua ndio maana Maua hanitaki, oooh, mungu wangu nisaidie nimpate Maua…ooh, mungu. Alikesha akiomba, na kesho yake akadamkia kwa Maua, na kumkuta akiwa mnyonge sana kama anaumwa.
‘Maua vipi unaumwa mbona mnyonge kiasi hicho….? Akauliza Maneno

‘Aheri ningelimuwa nikajua moja, nashindwa hata kuelewa, kwanini shangazi…’ akakatisha kuongea na Maneno akamsogeela na kumfuta machozi ambayo yalishaanza kumtoka…., Maneno akwa anajiuliza afanyeej maana kamkuta mtu yupo katika hili hiyo na akianza kuongea kuhusu swala la uchumba, ndio atazidisha , na hakupenda iwe hivyo.

‘Basi Maua mimi naondoka, lakini kwa hali hiyo , naona haupo sawa, nahisi kama unaumwa, kwanini tusiende hospitalini…’ akasema Meneno.
‘Nimesema siumwi……’ akasema Maua kwa mkato.

‘Maua labda mimi nakusumbua sana, lakini nafanya hivyo kwa nia njema.nakupenda sana Maua, na kama ungeliingia moyoni mwangu, uakatambua nini kilichopo moyoni mwangu ungelinihurumia na kunikubalia ombi langu, lakini kwa hali kama hii, naona tusubiri tu mpaka ukiwa tayari, …’ akasema Maneno akitaka kuondoka.

‘Ombi lako limekubaliwa…’ akasema Maua

‘Eti nini…..oooh, Maua umesema, ….sijasikia mungu wangu…’ Maneno akapiga magoti mbele ya Maua na kumwangalia usoni, `sema tena Maua umenikubalia ombo langu, kuwa uwe mchumba wangu…’ akasema Maneno na safari hii machozi yakawa yanamlenga lenga kwa furaha.

‘Ndio nimekukulia, kuwa niwe mchumba wako, na naomba tusikawie kufunga ndoa, kama kweli unanipenda…ndoa ifungwe haraka iszidi mwezi huu…’ akasema Maua.

‘Hata kama ungetaka leo, mimi ningelifanya hivyo, sasa…..oooh , sijui nifanyeje, sijui nikupe nini…ngoja naondoka nyumbani nikirudi tutaongea…’akasema Maneno na kuondoka.
*********

Maua libakia akitafakari kwa makini, akikumbuka maneno ya shsngazi yake ambaya alikuja na kumkaripia kweli, alimgombeza kama mtoto mdogo na alimwambia kuwa achague watu wawili Maneno na jirani yao mmoja ambaye naye amekuwa akiwa anakuja kumshawishi shawishi kama alivyo Maneno, lakini huyo jirani yao licha ya kuwa ni mzuri, lakini alikuwa hapendi tabia yake, anapendwa sana na wasichana na tabia yake sio tabia ianyoendana na yake, ….kwahiyo aliona ni bora ya Maneno, ambaye wamezoeana…

Alimuonea huruma sana Maneno jinsi gani amekuwa na juhudi ya kuja mara kwa mara na amekuwa naye wakato wote wa shida na raha, na nini anakihitaji kwa mume kama sio hicho, mtu aliyeonyesha upendo wa dhati kwake, akawa aanmuwaza Maneno kiundani, lakini kila akimuwaza, ile ndoto ya mara kwa mara ya Mhuja humjia akilini . Ndoto hiyo inamsema kuwa amekuwa msaliti wa ndoa, hakumbuki ahadi yao…

‘Ahadi gani na mfu, mimi najua mtu akifa basi ndoa haipo tena, je mimi nitakaa hivi hivi mpaka lini? Siku hiyo akauliza kwenye ndoto.

‘Nani kakuambia nimekufa, ….kama ningekufa tungeliongea hapa mimi na wewe , au unaniona kuwa mimi ni mzuka, au shetani, …hata hivyo unasubiri nini kukubali, wakati siku ile kule mbugani ulishamkubalia kivitendo….haina haja ya kumtesa rafiki yangu….’ Akasema Mhuja kwenye ndoto. Ndoto kama hizo zimekuwa zikijifululiza kila mara, mpaka akawa kama anachanagnyikiwa, na ikabidi awe anafanya ibada kwa nguvu, kumuomba mungu amuepushie na hayao marue rue ambayo aliyaona kama mashetani.

Na alipokuja shangazi yake kumsema, kuwa anajidekeza, na kama asipofnaya juhudi mwisho wa siku ataachwa mwenyewe na akipta tatizo hatapata mtu wa kumwendea;

‘Hivi wewe unafikiri ni wewe peke yako uliyefiwa, watu wanafiwa na baadaye wanasahau wnasonga mbele, lakini wewe utafikiri una mashetani maana, hutakii kukubali ukweli, hebu fikiri amika mwilii upo hivyo hivyo, utaomboleza mapaka lini, na kama huyo mtu angelikwua haii na kama kweli anakupenda, angelishawasiliana na wewe…nakuomba uchague moja, yupi unataka akuoe, huyo Maneno au jirani yangu, lakini ningelishauri uolewe na Maneno maana huko mbugani mlikokwenda…hakukufanyia mema, ….’ Akasema Shangazi mtu.

Na Maua alipokumbuka ya huko mbuga za wanyama walikwenda, akashituka, na hasa huo usemi kuwa hakufanyiwa mema,…na baada ya kwuaza sana, akaona hana jinsi ni kumkubalia Maneno tu, maana akikataa basi tena inabidi aolewe na huyo sharubaru, ambaye kila msischana anamtaka,alimuita sharubaru maana anajipenda kupita kiasi.

Wakati Meneno kaondoka, akawa anatafakari jinsi ndoa yao anavyotaka iwe, alitaka ndoa fupi tu isiyo na watu wengi, lakini anamvyomjua shangazi yake, lazima atataka ndoa kubwa, kitu ambacho hakukipenda, akachukua simu na kumpigia shngazi yake , wakaongea , kidogo , halafu aakmwambia kuwa amekubali Maneno amuoa, ….na simu ikakatika, dola ilikuwa imeisha..na wakati anasubiri kuwa shangazi yake atampigia akapitiwa na usingizi, na ilikuwa sio usingizi wa kufumba macho, lakini mara akaiona sura ya mhuja ikiwa imesimama mbele yake.

‘Hongera binti….’ Alishangaa sasa hivi anatumia neno binti,mara zote anasema mke wangu au Sweetie, lao katumia binti…akaseikiliza huku moyo ukimwenda mbio. `Najua huna la kusubiri, kwani ulishakuli toka awali, na uamuzi uliochukua ni wa kutimiza malengo tu, na sijui lini utamwambia rafiki yangu kuwa una tiketi yake tayari , tiketi ambayo haihitaji kusubiri, usijidanganye kuwa hukukubali, maana ushahidi upo wazi…’ akasema Mhuja.

‘Ushahidi gani huo, ….mbona …halafu wewe umeshakufa kwanini unanisakama kiasi hicho….’ Akasema Maua kwa shida.

‘Ushahidi ni huo uliopo tumboni mwako…’ akasema Mhuja.
‘Tumboni mwangu, ….’ Akashangaa Maua na kuinama kujiangalia tumboni, alijiona tumbo limekwua kubwa, kama mja mzito, na alipotizama mbele, akamuona kasimama Maneno na shangazi mtu.

NB: Jamani sehemu hii nimeiandika haraka isivyo maelezo itakuwa na makosa mengi, mnisamehe sana, nakimbizana na muda, nikisubiri baru yangu, nataka hadi hapo nikiambiwa byebye, tuwe tumefika mahala pazuri...nafanya hivi kwa kuwapenda wapenzi wa blog na visa hivi, tuombeane mungu, labda nitapata kijiwe kingine cha kujiegemeza. Yote ni mapenzi ya Mola na riziki hailazimishwi, au sio, nawapenda sana wapendwa wangu!

Ni mimi: emu-three

10 comments :

samira said...

jamani m3 imekuwaje hapo kazini nitakutafuta nikitulia
ila usijali kila kitu kinasababu yake mungu ndo anojuwa haya yote ni mapenzi ya mungu utapata tu kazi nyengine mimi kama mpenzi wa blog hii nipo pamoja na wewe kwa shida na raha ulitujali sana naomba mungu akusaidie

Anonymous said...

Hii habari ya kazi ni kweli M3 ama ni part ya kutuchangamsha? Kama ni kweli pole sana kaka yangu - Mungu atakufungulia mlango mwingine wenye neema zaidi. Ubarikiwe sana mimi ni mmoja wa wafuatiliaji wako wazuri sana ingawaje huwa napita kimya kimya ila leo umenigusa na issue ya kazi. Umesomea nyanja gani kuna nafasi ya kazi Rwanda inataka mtu wa issue za tabia nchi - if interested please let me know hapa hapa jukwaani kwako. Wish you all the best.

Anonymous said...

Helloo,
Hata mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa Blog hii,Usihofu Mwenyezi Mungu atafungua riziki sehemu nyingine wala usiwe mnyonge kwani mlango mmoja ukifungwa mwingine utafunguliwa.

Rachel Siwa said...

emu-tree, Ndugu yangu pole sana, lakini Mungu yu pamoja nawe sikuzote na safari moja huanzisha nyingine, natumaini huo si mwisho ndiyo mwanzo Mungu ameshafungua mlango wako,Usifadhaike ndugu yangu,Pamoja sana Ndugu.

nyahbingi worrior. said...

Habari za siku.
Kama mwanablogu kutoka Tanzania,nakuomba kushiriki kuchangia Mchakato wa KUFUFUA JUMUWATA(Jumuiya ya Wanablogu Tanzania).

Tafadhali naomba ufungue hii kurasa ya
http://blogutanzania.blogspot.com/
kisha upendekeze jinsi ya kufufua JUMUWATA.
Ahsante.
Luiham Ringo.

Anonymous said...

Eeeee mwenyezi mungu wewe uliyetujua hata kabla hatujaja hapa dunia, Naomba kati ya utakaowakumbuka katika mwezi huu basi ukamkumbuke na M3 katika hitaji lake la Kazi na iwe kazi ya kudumu isiwe ya kibarua katika jina la yesu naomba nikiamini. Mmmmh! kwenye hii story mpaka nabaki speechles maana Mhuja huko aliko nae hayuko sawa na maua vilele mambo si shwari. Kila la kheli wala usijali mungu atafungua mlango mwingine mama yeye huwa hashindwi na lolote. Jane

Anonymous said...

pole sana Mira, Mungu ndie muweza wa yote tunakuombea akutie nguvu na kukufanikisha ktk kipindi hiki cha mpito. kila la heri

Yasinta Ngonyani said...

Mwenyezi Mungu yupo nawe ..Upo katika sala zetu..

Precious said...

Nilipotea siku nyingi kidogo majukumu yalinibana M3 khs kazi ni serious au unatania if its real pole sana kila kitu kinatokea kwa sababu nina imani kuna mahali pengine pazuri Mungu kakuandalia. Uko kwenye sala zetu.

emuthree said...

Precious ni kweli hicho sio kisa, hapa nilipo ni kama mkimbizi, namsubiria huyo mhasibu mpya aje nikambidhi ofisi...Ni kweli hizo nami ndio dua zangu...na nashukuru sana kuwa kuwa nami nakunijali, mungu yupo, ipo siku nitapata sehemu ya kutulia....