Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, September 26, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-30




NB: Ili twende sawa ni vyema ukarudi kuisoma sehemu ya 27, tulipoishia,….hapa ndio muendelezo wake! Ukumbuke ilibidi tumuingilie docta Adam kumuona undani wake, ili tumjue vyema, na ukumbuke alianza kumpenda hata wakati huo ana mke wake, kabla hata hawajaachana, lakini docta huyu alikuwa na msimamo, …kilichoharibu ni tabia za mke wake na matatizo aliyokuja kukutana nayo. Na ukumbuke ana tuhuma kuwa chanzo chote ni Rose, nay a kuwa kutokana na Rose ndio imefikia hata yeye kuachika, alikuwa anamtafuta sana, wakutane uso kwa uso na sehemu ambayo atamuonyesha makali yake, kwa minajili hiyo ndio maana tukakatisha sehemu hiyo na kumchimba Docta Adam.

Baada ya kuyaona maisha ya Adam na mkewe yalivyokuwa, tukagundua kuwa kumbe kuna tabia zinzjijenga au ni za kurithi , huenda ni kutokana na kuona wazazi wanavyoishi au hata za kujitakia, …lakini mwisho wa siku zinakuwa kikwazo katika ndoa, inabidi tujadiliane hili kwa wale wenye uzoefu, je hili ni kujitakia au kuna tabia ambazo zinajijenga kutokana na familia husikika au zinarithiwa toka kizazi hadi kizazi..? Kwa kisa chetu kilivyotokea, imeonekana wazi kuwa kuachika kwa mke wa Adamu sio kweli kuwa chanzo ni Rose, kama alivyodai mke wa Adamu, na kama tulivyoona, ….

Hata baada ya ukweli huo, lakini mke wa Adam amejenga uadui mkubwa kwa Rose, na alishaahidi kuwa siku akikutana naye ni vita kwa kwenda mbele. Na hili lilimuogopesha sana Rose, na pale alipoona ule mzozo, na hata kuona jinsi gani Adam anavyopigana na mke wake, akaogopa, hakuamini kuwa watu wanaweza kupendana na baadaye kuja kuchukiana kiasi kile, akaogopa…na pia alishangaa kuona mke yule alivyo, alikuwa akihadithiwa tu na Adam, lakini hakuwahi kuwa na karibu, kweli mke yule sio wa kawaida anapigana kama mwanaume, kama bondia…!

Yeye alipoona hivyo, hakuweza kuvumilia, kwani alijua kuwa wakiamuliwa na kuanza kuulizwa, nini chanzo, huyo mke akiulizwa nini chanzo, …kiuhakika atamnyoshea kidole Rose , kuwa Rose ndiye chanzo……kwa kulikwepa hilo Rose akaondoka pale harakaharaka kurudi kwake, licha ya kuwa alifika pale kwa jambo muhimu sana , alikuwa kahisi kuwa huenda Docta Adam, kamchukua Sweetie wake aua anajua wapi alipo Sweetie.

Alipotoka pale akiwa katahayari, na kujisikia vibaya kwa kuabishwa vile, ….hakuwa na hamu tena ya kuonana na Docta Adam, na ikibidi itajitahidi kujenga umbali kati yake na bosi wake huyo, uhusianao wao uwe wa kikazi tu, ….lakini kwa shinikizo la kutaka kujua kuwa kweli anajua wapi walipo Seetie akaahidi kuwa akifika nyumbani kwake atampigia simu Adam ili ajue nini kimeendelea,na amuulize wapi alipo Sweetie, au yeye kampeleka wapi lakini huyo mgonjwa wake. Lakini sivyo ilivyokuwa, kwani alipofika nyumbani tu… alimuona mtu…..ooh, yule sio Sweetie….oooh, kumbe ni Sweetie wake,… na ndipo safari ya mjini ikatayarishwa , safari ambayo ilizaa jambo…nisikupe hamasa sana, tuwemo kwenye sehemu inayofuta,….

*********
Safari ya mjini ikaanza, na wakati Rose anaondoka, hakufanya kama ilivyo kawaida yake, kuwa akiondoka, humuachia rafiki yake ufunguo, safari hii aliondoka na funguo zake zote, hii aliifanya kwasababu ya usalama, na ili mwisho wa siku ajue ni kwanini watu wanaweza kuingia kwake kirahisi wakati kafunga milango, na funguo. Hata hivyo wakati wanaondoka rafiki yake huyo hakuwepo, alikuwa kazini akiwajibika hospitalini…

Wakati wanaondoka hakujua kabisa aanzie wapi, kwani biashara hii ya madini imegubikwana utapeli wa kila hali, akawaza sana, lakini baadaye akumkumbuka mmoa wa jamaa zake ambaye alijikita kwenye biashara hiyo, lakini yeye ni kama wakala tu, akaona amtumie hiyo, kwahiyo alipofika mjini alimuendea jamaa yake huyo, na kweli mambo yakawa mazuri zaidi na alivyotegemea, jamaa yake huyo akamsaidia kupata sehemu yenye bei nzuri na hata huyo mnunuzi alishangaa wapi dhahabu nzuri namna hiyo zimepatikana, alisema dhahabu kama hizo zinapatikana Zaire na Congo. Rose hakujua awaambie vipi , maana hakuwa anaua wapi zilipopatikana.

Baada ya kuzikamata hizo pesa kiusalama Rose alikwenda moja kwa moja hadi benki kwenye akaunti yake na kuzihifadhi hizo pesa, akiwa na maana kuwa akirudi ataweza kuchukua kiasi kwenye kwenye tawi dogo la benki hiyo! Cha muhimu sana kilichokuwa mbele yake ni kulipia deni la huyo mgonjwa, na moyoni alisema sio huyo tu, hata wale aliowadhamini kama hela itatosha atawalipia …Walipofika benki aliweka hizo hela na kubakiwa na kiasii fulani ambacho kinahitajika kwa muda ule, baadaye wakajimwaga mjini kufanya `shopping’ ya nguvu ha kununua baadhi ya mahitaji yao na zawadi ….

Ilipofika jioni walitafuta hoteli nzuri ya kujipumzisha ili kesho yake warejee makwao, na walipopata hoteli inayofaa, Rose akamwambia Sweetie anataka waende makitaba ambayo pia ianauza vitabu, anaifahamu sana, huwa kila akienda mjini lazimia apitie, kama sio kununua vitabu anafika kusoma mambo mbali mbali yanayoendana na fani yake. Leo ana pesa za kutosha, kwahiyo alidhamiria kununua vitabu vingi kidogo, kwa ajili ajili ya kujiandaa kwamasomo yake ambayo ameshaweka nia kuwa lazimisha asome zaidi, hata kama sio kwa kwenda nje….alikuwa na hamu ya kuwa dakitari bingwa na ikiwezekana kufungua kituo chake mwenyewe cha matibabu. Wakaingia maktaba na hapo kila mmoja akawa na shauku ya kutafuta vitabu anavyovipenda , kwa mtindo huo wakawa wanapoteana kwa muda. Baadaye Rose akatoa ushauri , na kusema;

‘Naona hatutaweza kufuatana kila mahali, humu kuna vitabu vingi, na kila mmoja ana hamu na vitabu vyake, sasa tufany hivi, wewe tafuta vitabu vyako unavyopenda, ngoja mimi nielekee huku kwenye vitabu vya amsomo ya udakitari na sayansi kwa ujumla…’ akasema Rose.

‘Haya mimi huko nahisi kama sio sehemu yangu, ingawaje sikumbuki vyema kuwa nilikuwa katika nyanja gani kiutaalamu, …hata hivyo sidhani kuwa nimesomea mambo ya sayasi maana hata nikisoma hivyo vitabu naona haviingii akilini ….ngoja nielekee huko kwenye vitabu vya masomo ya biashara, uhasibu na….yah…naona haya yaninifaa….’ Akasema Sweetie huku akikagua vitabu mbalimbali.

Baadaye walikutana na kila mmoja akiwa na vitabu vyake alivyokuwa anavihitaji , wakapewa gahrama za hivyo vitabu na kuvilipia,wakawa sasa wanatoka mle kwenye makitaba, ….wakati wamefika sehemu ya maulizo , wanapopumzika watu wakisubiri kupatiwa huduma nyingine, kwa pembeni waliona magazeti ya siku nyingi yakiwa yamewekwa kwenye kabato la viyooo, macho ya Sweetie yakaona gazeto moja likiwa na picha iliyomvutia, kwenye lile gazeti, sijui kwanini alivutika nayo, akalichukua lile gazeti toka kweye lile kabati na kuanza kulisoma, na juu yake kulikuwa na kichwa cha habari…

‘Wahanga walionusurukia kwenye ajali ya MV Bukoba huko Tanzania waelezea jinsi ilivyokuwa…’ aliendelea kusoma habari ile kwenye gazeti na akaangalia picha ya ile meli na kujikuta akiwaza, alikuwa akiwaza kuhus ndoto aliyoiota siku kadhaa nyuma , kuwa alikuwa anazama …na picha kama ile ilikuwa imejionyesha kwenye hiyo ndoto.

‘Vipi Sweetie, mbona unaliangalia sana hilo gazeti…? Akauliza Rose
‘Sijui ni kwanini maana kinachoelezewa hapa kinaendana na ndoto niliyowahi kuiota, ….nakumbuka kama niliona kitu kama hiki….meli kuzama, lakini ilikuwa kama nimelala, halafu naona meli inazma mbele yangu, kama mtu anaangalia sinema hivi….na baadaye nikajikuta nimo humo, kama mhusika wa watu wanaozama, nikajitahidi kujiokoa lakini …nikazindukana, …ngoja nilichukue hili gazeti …’ akasema Sweetie,

‘Lichukue tu hilo gazeti, ukalisomee hotelini kama unalitaka, nitalilipia….’ Akasema Rose
Rose hakuwa na mawazo yoyote kuhusiana na lile gazeti au ile picha, na kwanini Sweetie kavutika nayo. Rose akili yake ilikuwa na hamasa ya kurudi nyumbani kwake akalipe hilo deni na kuwa huru na hawo watu waliotishia amani yake na alitaka kama itawzekana akujitolea kwa halina mali kuhakikisha kuwa hakuna kitu kitamdhuru tena Sweetie….kwake yeye Sweetie alimuona kama kaka yake, hakutaka kusema vinginevyo,….jinsi moyo wake unavyotamani, …..

‘Unajua Sweetie, hakuna jambo ninalolitamani sasa hivi kama kurejea nyumbani haraka, …’ akasema Rose

‘Kwanini unatamani iwe hivyo, …nakumbuka uliniambia kuwa umeaga kazini kwa ruhusa ta siku tatu za mapumziko…? Akauliza Sweetie.

‘Ndio siku tatu na moja imeshaisha, lakini natamani turudi haraka ili niwalipe hawo watu deni lao, ili wakome kunitishia amani, unajua kuna barua waliindika na msharti kibao, lakini cha ajabu siku waliponipa ile barua sikuwahi kuisoma, nikaiweka kwenye begi langu, na bahati mbaya siioni tena, ila Adam aliniambia kuwa hawo wadhili walianisha mashari mengi ambayo baadhi nimeyakiuka…na ya naweza kuniweka matatani, sasa sijui akatika hayo mashari kulikuwa na muda maalumu wa kulipa hilo deni au vipi, lakini kwa vyovvyote iwavyo, kilichotakiwa mwisho wa siku ni kulipa hilo deni na pesa tunazo, …’ akasema Rose, na alipotumia neno hilo tunazo Sweetie akatabasamu.

‘Tunazo au unazo Rose, usinitie kwenye majaribu…..na kwanza wewe siumekataa kuwa wewe sio mke wangu…’akasema Sweetie.

‘Sweetie, siwezi kukudanganya kwa hilo, …..kama unahisi kuwa ulikuwa na mke, basi atakuwepo mahali anakusubiri, lakini ukumbuke sasa ni miaka miwili, je huyo mke atakuwaje, na je mliachana naye kwa vipi, ….lakini cha muhimu ni wewe upone, ili ukakutane naye, atakuwa na hamu sana ya kukuona…na ooh, ukipona ina maana mimi na wewe tunaachana….mmmh,unakwenda kukutana na mkeo au sio….?’ Akasema Rose kwa unyonge, hadi Sweetie akageuka kumwangalia kwa makini, alitamani kumuulizia lile swali alilowahi kumuulizia mwanzoni kuwa kwanini mrembo kama yeye hana mume, kama kweli yeye sio mume wake, lakini akaumbuka siku ile alivyomuulizia na kumfanya aingiwe na machungu na hata kufikia kutoa machozi....

‘Rose, unajua mimi sijaamini kuwa wewe sio mke wangu,….sijui kwanini, yaani kila niotavyo sura ninayoonyeshwa kuwa huyo ni mke wangu, ni wewe , inafanana na wewe, naiona sura yako kabisa…kwanini kama kuna mke mwingine nisiione sura yake nyingine tofautii na wewe…?’ akasema Sweetie kama anauliza.

‘Hiyo ni kwasababu ya kumbukumbu hazipo, kwahiyo akili yako inakumbuka kile kitu unachokiona wakati ule na akili bado haijafunua taswira zilizopita….itachukua muda, labda itokee mktane naye tena, au litokee tukio la kuweza kuushitua ubongo wako, lakini hali kama hiyo haihitaji haraka, ukilazimisha sana unaweza ukapata madhara, kwahiyo wewe fanya subira tu, ipo siku utakumbuka, na ipo siku utakutana na Sweetie wako, maana siku zile ulikuwa hauishi kumtaja, ….Sweetie wako..’ akasema Rose.

‘Natamani Sweetie wangu awe ni wewe….’ Akasema Sweetie

‘Umeshaanza maneno yako…nitawahi kuwa Sweetie wako, yupo anayestahili kuitwa hivyo …najua atakuwa mahali anakusubiri…mmmh, usikonde mgonjwa wako utakutana naye na mimi utanisahau kabisa…’akasema Rose kwa unyonge tena, hali hii ilikuwa ikimpa shida sana Sweetie, kuwa ni lazima kuna jambo linamuumiza sana Rose anapozungumzia maswala hayo...!
‘Rose siku ile nilikuuliza swali ukajifanya hulikumbuki na bahati mbaya hatukuweza kuliendeleza lile swali, na hata mazungumzo yetu yalikatishwa, ….au hukutaka kunijibu hilo swali , naomba sasa unjibu hilo swali langu kutoka ndani ya moyo wako….’ Akasema Sweetie

‘Swaali gani hilo Sweetie, maana tumewahi kuongea mengi, na siwezi kujipa uhakika kuwa swali hilo ni kadhaa, mpaka unikumbushe, au hata hilo swali umelisahau, unahitaji nikukumbushe, siwezi kuwa na uhakika kuwa ni lipi, unalikumbuka mpendwa…?’ akasema Rose kama anauliza, huku anamwangilaia kwa jichoo la kujiiba!

‘Umeshaniona mt u wa kusahahu sahau kila kitu….nilikuuliza kuwa kama sina mke na hivi sasa akili yangu na mapenzi yangu yapo kwako, utakuwa tayari kuwa mke wangu….?’ Akauliza Sweetie.

‘Hilo jibu lake lipo wazi, kwanza kwa mtizamo huo utakuwa na mke, hilo nimeshaliona, maana huachi kuwaza kuhusu mkeo na ndio maana ukawa unamuota, pilie unapowekwa nafasi ya pili unakuwa huna uhakika, na kibanadamu unakuwa huna hamasa tena,…..kwahiyo ngoja muda uongee, na utaongea tu siku hali yako ikitengemaa, usijitie katika hali kama hiyo na ikatokea vinginevyo na madhara yake yanaweza kuwa makubwa, ukaumia kisebeu sebu , na muumiai atakuwa mimi zaidi na nisingelipenda kabisa kuumia tena, ni bora ieleweke hivyo hivyo kuwa….wewe una mkeo , mimi sitaku tena mambo hayo ya kuolewa, nilishakata tamaa…..’ akasema Rose.

Sweetie akamsogelea na kuwa kama kamkumbatia, lakini kwa bega kwa bega sio kifuani, akasema kwa udhabiti…’kama kweli sina mke, basi wewe unanifaa, na nakuhakikishia kuwa nitafanya kila iwavyo wewe uwe mke wangu…hilo naahidi, lakini kama yupo,… sijui,… maana ni muda mrefu, huenda keshakata tamaa na mimi, hakijaharibika kitu…..sijui …., lakini moyo wangu upo kwako, je Rose unanipenda?’

‘Sweetie maswali gani tena haya jamani, usinitie kwenye majonzi…tafadhali nakuomba, wewe twende hotelini nafikirii unahitaji kupumzika….’ Akasema Rose.

‘Kweli nahitajii kupumzika, lakini akili yangu inahaha sana, sijui kwanini nahisi kama kuna kiti nakihitaji, akili hatulii, kuna hisia za ajabu zinajijenga akilini za kutaka kujua jambo, kuna hamasa, ya…..aaah, nashindwa hata jinsi ya kukuelezea Sweetie, ooh Rose, sidhani kama nitapata usingizi,….’akasema Swetie

‘Usijali Sweetie, nitakubembeleza hadi uupate huo usingizi, umeshahau kuwa mimi ni dakitari wako, naua hali kama hiyo itatokea, na huo ni mwanzo wa kuanza kurejewa na fahamu zako za kumbukumbu, na hapo unatakiwa utulie , nakuomba usijilazimishe kuwaza sana, kwani kuwaza sana kunaleta madhara, unaweza ukpatwa na mshituko wa moyo, na matokeao yake yanaweza kuwa mabaya, …kwanza kabisa tulia , na yapeleke mambo kama kawaida, ….’ Akasema Rose na kumshika mkono Sweetie wake huku wakielekea hotelini.

Rose mawazo yake yakahama toka kwenye kuwaza matumizi ya pesa na kurejea kwa mgonjwa wake, aliwaza hatima ya huyo mgonjwa, kwani dalili zote za kupona zimeshaanza kujionyesha, licha ya kuwa wataalamu walishauri kuwa kuna haja ya kufanyiwa upasuaji ambao ni kwa hapo nchini hakuna utaalamu huo ni mpaka nchi za nchi hasa India...

Pesa zilizopo kama zitalipa madeni zitakazo bakia zinaweza zikafanya jambo hilo, na hata kujisomesha hilo halina shaka, lakini wataalamuhawo walishauri kuwa ni vyema kusubiri fahamu za kumbukumbu zirejee kwanza, na je zikirejea huyumgonjwa atakubali kubakia hapo na kukubali kwenda naye huko India kwa upasuaji, ….na je ni nani, kwani huenda fahamu hizo zikirejea zinaweza zikabadili kila kitu….yote hayo yanategemea ufahamu huo wa kumbukumbu, haian haja ya kusumbua kichwa kwa muda huu, ila kama ana mke ina maana takuwa basi tena….basi tena maana itabidi arejee kwa mke wake, na haijulikani ni wapi ataeleekea….alipofika hapo akamwangilia Sweetie ambaya naye alionekana kuzama kwenye mawazo yake.

Sweetie alikuwa akiwaza mengi,na sasa alikuwa akiwaza ile picha kwenye gazeti na hata alipofika hotelini, alikaa kwenye sofa lililopo mapumzikoni na kuanza kulisoma lile gazeti kwa undani, na humo ilionyesha kuwa kuna meli ilizama miaka miwili iliyopita huko Tanzania, na watu wengi walipoteza maisha,….ikaelezea chanzo chake na jinsi serikali hiyo ilivyofanya juhudi za kuwaokoa watu, …..alipofika hapo kichwa kikaanza kumuuma,

‘Kichwa…..ooh, kwanini kichwa kinaniuma….’ akawa analalamika, na Rose ambaye alikuwa akiongea na wahudumu aligeuka mara moja na kumuona Sweetie akihangaika, …harakaharaka akamwendea na kukaa karibu naye..

‘Vipi Sweetie , upo safi kweli…’ akauliza Rose

‘Kichwa …..kinaniuma kama nini sijui, mpaka naona giza….ooh, Sweetie, Rose…..hali sio nzuri….sioni kabisa, kichwa……’ akawa anahangaika sana. Rose akamsaidia na kuwmambia watoke waelekea hospitalini, …..kawanza akampa dawa ya kutuliza kichwa, na baadaye kidogo kikatulia, na wakaingia kwenye vyumba vyao, chumba kikubwa chenya vyumba viwili, ni hili kwa Rose aliliona ni muhimu sana kuwa hivyo kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa mgonjwa wake…
‘Unajisikiaje sasa Sweetie, ….’ Akauliza Rose

‘Sasa nahisi vyema kidogo, ila inakuwa kama mtu aliyezibuliwa kichwa na kuondolewa kila kitu ……oooh, nahisi kulala tu, lakini naogopa, naogoa hiyo hali iliyopita isirejee tena, maana nilijiona kama nakufa…’ akasema Sweetie na kulala, na Rose akaona mgonjwa katulia kwahiyo aondoke, lakini mara, mgonjwa akaanza kutingishwa, akawa anatetemeshwa , utafikiri kitu gani….
‘Sweetie vipi, ….’ Akauliza Rose akiwa anashangaa na mabadiliko hayo, akamshikilia kwa muda na baaaye ilre hali ikatulia, na mara Sweetie akafungua macho, akasema, `Oh, Sweetie , mpenzi bado upo, pole sana….’

‘Oooh ni kawaida Sweeti, ni vyema kweli ukalala, na usiwe na wasi wasi nipo pamoja nawe, ukipata usingizi nitakuacha kidogo ili nami nipumzike halafu nitarejea kuhalkikisha kuwa umeamuka au la….waonaje kwa hilo…?’ akauliza Rose

Sweetie hakutoa jibu mara moja, ilikuwa kama vile kalala , halafi baadaye akafungua macho na kusema ‘Hapana usiondoke Sweetie , naogopa sana Sweetie…mke wangu, Sweetie, usiniache…hali kama ile, ikitokea tena natamani kuikimbia…naogopa kitu fulani…sijui ni kitu gani,… inakuwa kama nipo ndani ya kitu kinanipa shida kupumua, nakuwa kama nimezamishwa…sijui niseme nipo ndani ya maji natafuta jinsi ya kutoka nje ya maji …oh, Sweetie, naku---ku--fa, na….. Usiniache mke wangu, natamani nikimbie niikimbie hiyo hali…’ akawa analalamika Sweetie, kama mtu aliyepagawa, huku anashika kichwa, kuonyesha kuwa kichwa kinampa shida, au kuna vitu vinamsumbua kichwani.

Rose akamsogelea, akasema ‘Usijali nipo pamoja nawe, kama ni hivyoo basi nitapumzika hapa pembeni yako….haya lala mgonjwa wangu…’akasema Rose, na huku anambembeleza kama mama amfanyiavyo mwane,….na hapo Sweetie naye akadeka kama mtoto, akajisogeza karibu yake, na hali hii iliendelea na kuna wakati Sweetie alianza kuumwa kichwa tena , na muda huo ulikuwa usiku mzito,…hata hivyo ilibidi Rose ainuka pale kitandani na kwenda kuchukua maji na dawa, ….mgonjwa akanywa ile dawa, na kipindi hicho, Sweetie alikuwa anatetemeka baridi, akabidi Rose afanye juhudi za kidakitari na baadaye ile hali ikatulia na wakati huo Rose amemkumbatia mgonjwa wake ili kumpa ujotoujoto…

Hali ya usiku ule ilikwenda mbali zaidi ya dakitari na mgonjwa wake, kwani Sweetie alihamasika zaidi kuna kitu kilimvuta akawa naye anamshkilia Rose, akamshikilia kw nguvu , na wakati huo Rose alikuwa kachoka na usingizi ulikuwa umembana kweli kweli, lakini hamasa za mwili zikawa zinamvuta, na hisia zikawa kali zaidi…akawa anafuta vile mgonjwa wake anavyotaka, …jambo moja likazaa mengine, kilichoendela hapo baadaye, ilikuwa ni kama baharini mawimbi yanapanda yanashuka….

‘Oooh Sweetie nakupenda sana…sijui ukiondoka itakuwaje…’ akasema Rose akiwa anazama kwenye usingizi.

‘Hata mimi nakupenda sana sidhani kama nitaondoka nikuache, wewe naona ndio mke wangu…sijui kama yupo mwingine zaidi yako…sijui?’akasema Sweetie naye akizingwa na usingizi.

Ilikuwa asubuhi sana , Rose alipoamuka na kujikuta yupo peke yake, ….akaamuka haraka haraka kitandani na alishangaa , kwanza hakuamini,alihisi kama ilikuwa ni ndoto….lakini kumbukumbu za usiku zilipomrejea vyema akakumbuka, …ooh ama kweli ni siku nyingi, …sijawahi kuipata ile starehe…oh sijui nitaweza kuipata tena hiyo starehe au ndio ilikuwa muagano, ooh Sweetie upo wapi asubihi hii..’ akajikuta akisema kimoyomoyo huku akinyosha, halafu akatoka pale chumbani na kuingia chooni, akakuta hakuna mtu, akatoka hapo na kuingia bafuni, moyo ukamlipuka alipoangalia pale sakafuni…ilionyesha dhahiri….oh, balaa,…. Sweetie alikuwa kalala pale sakafuni, na alipomsika shingoni, oooh…

NB, Muda, vitu vya watu , wenyewe hawo wanaingia…tuwepo kwenye sehemu ijayo, na huenda tukasafiri hadi kwetu kwa akina Maua na Maneno….



Ni mimi: emu-three

4 comments :

Anonymous said...

jamani umekatisha patamu!!!111 tupe uhondo m3 pls

samira said...

waw ni nzuri dear jamani wajuwa m3 mke wa docta adam inaonyesha alikosa malezi kwa wazazi wake pia limechangia hakuna kitu kama malezi ama family yake wako ivo
pili elimu hana pia inachangia
ki mtazamo hakumpenda au hajarizika na docta adam yaani mumewe tangu first day
just nachangia mawazo tu m3 na wadau wote msije kunihisi vibaya

emuthree said...

Wahenga hunena lisemwalo lipo kama halipo laja! Kama nilivyowaarifu awali kuwa kuna sintofahamu inayoniweka katik a mazingira magumu. Na sasa nimegundua kuwa kweli akufukuzaye hakuambii toka. Nimesikia kuwa mkataba wa ajira umefika mwisho na kama ni hivo nitakuwa na wakati mgumu wa kuwa hewani mara kwa mara...!

Yasinta Ngonyani said...

Mwenyezi Mungu yupo pamoja naye. Pia tupo pamoja halafu la msingi ni kwamba zingatia kwanza maisha ya famalia sisi hapa kijiweni tupo tunakusubiri upatapo nafasi basi turushie. Pole kwa yote.