Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Friday, September 30, 2011
Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-32
‘Ushahidi ni huo uliopo tumboni mwako,..…’ akajiuliza Maua ni ushahidi gani huo…akajiangali tena tumboni, lakini hakuona tofauti, yumbo lake lilikuwa la kawaida tofauti na jinsi alivyojiona kwenye ndoto…, na hapo akaanza kuingiwa na wasiwasi na hayo maneno, ingawaje mwanzoni aliyachukulia kama ni ndoto tu…lakini kila alivyozidi kutafakari alihisi kuwa huenda hiyo ndoto ina ujumbe maalumu.
Na kwanini kila mara anamuoma Mhuja kuwa yupo hai….na amekuwa mara nyingi anamuota katika mazingira tofauti tofauti, na akichunguza kwa makini kila alichokluwa akimwambia hutokea…na je ina maana ndoto hii inayoashiria kuwa ana ushahidi tumboni ina ukweli ndani yake.
Baadaye akaamua kuichukulia kama ndoto tu ya kawaida, kama zilivyokuwa ndoto nyingine, …na kilichomfanya aichukulie kama ndoto ni kuwa ndani ya hiyo ndoto alijiona ana tumbo kubwa, kitu ambacho sio kweli,…hana tumbo kubwa, tumbo hilo kubwa litokee wapi….’ akajaribu kuangalia kalenda na kuhesabau siku, aliona miezi miwili imekwisha pita…akahema kwa nguvu…na kusema mbona hii sio mara ya kwanza..
‘Miezi miwili kupita sio mara ya kwanza, imeshatokea mara nyingi, nimewahi kukaa hadi miezi mitatu, bila kuona siku zangu, na hata nilipoenda kupimwa hospitalini, sikuonekana na ujauzito….’ akajishika tumboni na kujaribu kujituliza kusikilizia kuwa atahisi kitu, lakini hakusikia dalili yoyote….akainuka pale alipokuwa amekaa na kukiendea kiyoo kikubwa kilichopo kwenye kabati la nguo, akajitizama kwa karibu…, hakuweza kuona tofauti, zaidi ya kujisikia vibaya na kuwa na usingizi wa mara kwa mara, lakini yote hayo aliyachukulia kama sehemu ya maisha yake ambayo amekuwa nayo hasa baada ya kufariki mumewe…,….
‘Ili kuondoa haya mawazo lazima niende kupima, na nitafanya hili kwa siri…maana akijua shangazi sijui kama kutakuwa na amani…hata hivyo kwanini niwe na wasi wasi wa mimba, nitakuwa nimeipata wapi, name simjui mume zaidi ya Mhuja, na tangu aondoke imeshapita miaka miwili…au…hapana haiwezekani, ina maana lile tendo alilonifanyia Maneno, haiwezkani, ….ina maana tendo lile alilonifanya Maneno linaweza kuwa limeasabaabisha haya, ….kama ni ujauzito….mugu wangu, ….ooh, mungu naomba uniepushie mbali…lakini kwanini itokee hivi, hapana, sikubali…hapana sina mimba sio mimba, sio mimba….’ akasema Maua huku akiruka ruka na mikono kaiweka kichwani.
Baadaye akaona asiwaze sana hayo mambo ambayo anayaona sio kweli, haiwezekani akawa na ujauzito….hilo alilikataa kabisa akilini, akili yake haikutaka kulikubali hilo….Na ili kutokuwaza sana hilo, akaamua kubadilisha mawazo kwa kufikiria kitu kingine na akaamua kuwaza jambo lililopo mbele yake. Kwa kuanzia akaanza kwa kumuwaza Maneno, alijijutia kwanini kaamua kuchukua uamuzi wa haraka haraka wa kumkubalia Maneno, aliona kuwa kama nikuolewa alihitaji kukaa kama miaka mitano hivi, ndipo afikirie maswala ya kuolewa, alitaka ahakikishe kuwa akilini keshamsahau Mhuja na ya kuwa kweli hayupo duniani, maana akilini mwake alikuwa bado ana imani kuwa bado yupo duniani….lakini miaka miwili, kama kweli yupo duniani kwanini asitoe taarifa…….
Maua aliendelea kujilaumu kwanini kamkubalia Maneno harakaharaka hivyo,lakini kilichomfanya amkubalie Maneno ni kwasababu ya shinikizo, na hasa shinikizo kutoka kwa shangazi yake ambaye alilivalia njuga hilo swala la kuolewa utafikiri yeye ndiye anayetaka kuolewa. Akilini akawa anamlaumu sana shangazi yake kwa kumshinikiza kuwa ni lazima aolewe, na akwa hana jinsi akakubaliana….sasa afanyeje, hana jinsi kilichobakia ni kujipanga vyema.
‘Nijipange kwa harusi….’ Akasema kwa sauti kubwa, akawaza jinsi harusi hiyo itakavyokuwa, kwanza hakupenda harusi kubwa, harusi kubwa ya nini, nataka kumuonyesha nani, …..
Aliwaza jinsi walivyokubaliana na shangazi yake walipokuja na Maneno muda mfupi uliopita,kuwa harusi hiyo ifanyike haraka iwezekanavyo, na hili alilisisitizia sana shangazi yake, kama yeye alivyotaka, lakini kutaka kwake hakukuwa na sababu yoyote, lakini alivyoongea shangazi yake ilionyesha kuwa ana sababu. Kwanini iwe haraka hivyo, …ndio nimekubali kuolewa, lakini nataka muda wa kutafakari kwanza, lakini shangazi kasema harusi ifanyike haraka..haraka iwezekanavyo…., alijiuliza akilini kuwa kwanini shangazi shangazi keshanihisi vibaya kuwa nina….hapana, …
ninavyomjua shangazi kama angelikuwa kanihis hivyo, angeshanibwatukia…’ Akajishika tena tumboni
Baadaye shanagzi akampitia tena, kwani walitakiwa kukutana kama wanafamilia kujadili hilo swala la harusi na walipokutana ilikuwa mvuatano wengine walipinga kabisa swala la harusi hiyo kufanywa haraka haraka, lakini shngazi mtu alilivalia njuga hadi likapita, ikabadkia maandalizi ambayo wengi walidai hawatayaweza kwa muda mfupi uliotakiwa..`wapi tutapata hela kwa muda huu mfupi, kama mumeamua hivyo, basi itakuwa harusi fupi tu…’
‘Sawa hatutaki harusi kubwa, hata muolewaji mwenyewe hataki harusi kubwa…’ akasema Shangazi mtu
‘Kwani yeye hilo linamuhusu nini, yeye kama muolewaji keshalifikisha kwa wanafamilia kazi yake imekwisha, yeye hahusiki tena, kama angelikuwa anajimudu mwenyewe, asingelileta kwenye familia, kwahiyo maswala ya maandalizi na lini itanyika hiyo shughuli haimuhusu tena huyo binti, lazima aheshimu taratibu za familia hii, asituburuze,labda kama kuna sababu nyingine ya msingi, utueleze wewe uliyebeba jukumu la malezi yake…?’ akauliza mwenyekiti wa familia.
‘Kwasababu za kikazi na makubaliano kati ya binti yetu na mtarajiwa wake, wote wamekubaliana iwe hivyo, na wamekubali kuwa wapo tayari kwa vyovyote itakavyokuwa, wanachotaka wao ni kufunga ndoa tu, na kama itakuwepo sherehe fupi kwa wanafamilia watafurahi, lakini wanataka ndoa ifungwe mwezi huu, huu…’ akasema shangazi na kusimamia kwenye msimamo wake huo hata pale wajumbe wengi walipopinga hiyo hoja, na mwisho wa siku ikabidi wajumbe wakubali kwa shingo upande, na hapo hapo wangine wakaahidi kuotoa michango yao hapo hapo na wengine wakasema kwasababau ni ya haraka sana watatoa tu kile watakachojaliwa nacho…
************
Maua akiwa chumba cha dakitari, alichukuliwa damu na mkojo kwenda kupimwa, na baada ya kuchululiwa vipimo hivyo, akawa anasubiri chumba cha mapumziko, huku akiwa na mawazo mengi, aliwaza mengi kuhusiana na hali hiyo, lakini moyo wake haukumpa wasiwasi kwani sio mara ya kwanza kumtokea hivyo, kipindi akiwa na mume wake Mhuja, na kama itatokea kinyume chake safari hii, hana jinsi ila kukubaliana na hilo. Lakini akawa anajiluliza kiundani, kama ikiwa ana ujauzito, je jamii italichukuliaje hilo, …sio kwamba watamuona kuwa alikuwa akijifanya ana majonzi huku kwa siri wana mahusiano na shemeji yake….
Akakumbuka jinsi watu wengine ambao haliwapiti dogo, walishaanza kuvumisha kuwa Maua alikuwa na mahusiano na Maneno, na ndio maana walichukuana hadi Arusha. Maneno haya yalipingwa kwa hasira na aliyekuwa mpiga debe mkuu akaitwa kwenye kikao cha wazee, akaonywa vikali sana, na huyo jamaa baadaye alisema hata kama kaomba msamaha kwa wazee, ili kuondoa sintofahamu hiyo, lakini lisemwalo lipo kama halipo laja….na huyo jamaa kama itatokea kuwepo na ushahidi kama huo basi vumbi lake halitulii….
‘Haiwezekani kama kuna ujauzito, hautapokelewa najua wabaya wangu watanianika uchi, …kama upo ujauzito ni bora ukatolewa mbali, kwanza ni miezi miwili tu, kwahiyo Maua alihisi kuwa itakuwa ni rahisi kutolewa …nitauweka wapi uso wangu, hasa kwa huyo mbeya wa mitaani, siwezi kukubali kufedheheka kiasi hicho, kwanza hata Maneno mwenyewe hajui, ….itakuwaje tukioana halafu ndio nije kumwambia kuwa nina uajzito wake,anaweza ajaniruka…Na je akiniuliza kuwa nimeupatapataje nitasema nini…?’ akawa ana waza na kuwazua, na mwisho wa siku akaamua kuwa njia bora ni kuutoa huo ujauzito kama kweli upo.
‘Maua ingia ndani….’ Akaitwa na dakitari
Aliinuka pale kwenye kiti akiwa anajisikia vibaya , kizunguzungu na kichefuchefu, akajikaza hivyo hivyo na kuingia kwa dakitari. Alimkuta dakitari akisoma maelezo ya vipimo vyake, na baadaye akamwangalia usoni.
‘Naomba nikuulize mwenzako yupo wapi…?’ akauliza yule dakitari akimtizama kwenye mkono uliovaa pete
‘Mwenzangu yupi, mbona nimekuja peke yangu….’ Akasema Maua
‘Sawa, lakini vipimo hivi vilihitaji muwe wawili, …unajua mnafanya makosa sana , sijui kwanini, …mara nyingi tunashauri kuwa mnapo-oana, ni vyema mkija kupima maswala kama haya mnakuwa wawili, ili nyote msikie, ni kwa ajili ya manufaa yenu. Kwasababu licha ya kuwa wewe ndiwe umebeba huo mzigo, lkini majukumu muhimu ni juu yenu wote, mkishauriwa na dakitari kila mmoja atajua nini mwezake anahitajiwa….na ..’ akawa anaongea dakitari lakini Maua alikuwa mbali kabisa, alikuwa kama yupo kimwili tu, lakini akili yake ilishakwenda mbali, alikuwa akiwaza jinsi gani ya kumshawishi huyo dakitari kuwa kama ni mimba haitaki, anataka kuitoa.
‘Docta naomba unipe hayo majibu, mengine yatafuata….’akasema Maua.
‘Sawa majibu yako ni haya, na nitangulize kukupa hongera….’ Akasema Docta
‘Nini, una maana gani…’ akashituka Maua
‘Kwani vipi, hukutarajia kuwa hivyo, una ujauzito, na sijui tokalini ulipokoma kuziona siku zako….? Akauliza docta.
‘Lakini mara nyingi inatokea hivyo, huwa naweza kukaa hata miezi mitatu bila kuziona siku zangu, naona docta umefanya makosa kwenye vipimo vyenu, haiwezekani…..hapana, ..nina mimba hapana…’ akawa analalamika Maua;
‘Vipimo vipo sahihi kabisa, na dalili zote unazo….huwa inatokea hivyo, kwa watu wengi, na baadaye mimba hushika, sio jambo la ajabu, na kama nilivyokuambia awali kama angelikuwepo mwenzako hapa ningewapa maeleekzo pamoja, lakini sio mbaya, kinachotakiwa sasa hivi ni kufuata masharti yote ambayo nitakayokuelekeza…’ yule docta akawa anamuelezea hayo masharti na jinsi gani afanye ili asije kupata matatizo, lakini kwa Maua hakuwa anayasikiliza ilikuwa kama vile hayupo.
‘Docta kwani mtu akitoa mimba ya miezi miwili inaleta madhara…nina maana kuwa nikiitoa hii mimba itanileta matatizo…?’ ghafla akauliza Maua.
‘Kwanini uitoe,…kwani…?’ Docta akaingiwa na mshangao, ingawaje ndio moja ya kazi zake, lakini hakutarajia mrembo kama yule na ana pete ya kuonyesha kuwa ana mwenzake akimbilie kutoa mimba, akamwangalia kidoleni ambapo pete ilikuwa iking’ara.
‘Sio hivyo Docta, ni kitu ambacho kimetokea bila kujiandaa, na kama upo uwezekani huo naomba unisaidia maana sitopenda watu wajue kuwa nina mimba, unanielewa…?’ akasema Maua
‘Sikiliza mpendwa, wewe kwanza kaongee na mwenzako mkubaliane, huenda mwenzako hana maneno na hiyo mimba,…na mkikubaliana na hilo tutaangalia,…lakini nakushauri kuwa sio vyema kutoa toa mimba, kuna madhara yake, hata kama mtu atachukua tahadhari zote, huwezi jua …Mimi ni mtaalamu ndio nakubali, lakini lazima nikushauri hivyo…’ akasem Docta.
‘Docta unaweza kuitoa hii mimba au huwezi…ndio maana nimekuja hapa kwako, na je nikiitoa itachukua siku ngapi kuwa katika hali ya kawaida maana baada ya wiki mbili hivi ninatakiwa kufunga ndoa, je nitaweza kuhimili kasha kasha za ndoa, na je…hata hivyo nimesikia sifa zako, sasa je inawezekana au ahaiwezekani, …?’ akauliza Maua kwa jaziba.
‘Hiyo mimba bado ni ndogo, kuitoa ni kazi ndogo tu, ni pesa yako tu,na baada ya kuitoa na baada ya wiki moja unakuwa katika hali yako ya kawaida …. ila kama dakitari lazima nikupe ushauri, isije iakatokea matatizo ukaja kunilaumu baadaye, lazima tuiwekane sawa, na mimba kama hiyo haina mambo mengi, ni dakika chache kitu kimetoka, …..’ akasema Docta.
‘Basi naomba tuitoe, …’ akasema Maua.
‘Sawa kama umedhamiria kweli, na una uhakika kuwa mwenzako hatakuletea shida wewe lipia hii ghrama hapa, na jiandae twende chumba hicho cha pili…’ akasema Docta, na badaye wakatoka pale na Maua akaingia chumba cha kubadili nguo na kuvaa nguo zao za hospitalini. Na wakati yupo mle ndanai anabadili akawa anawaza sana, je atapata madhara, akawa anajipa moyo kuwa hiyo ni mimba ndogo tu , hakutakuwepo na madhara, na kwa vile hakuna anayejua ,mambo yatakwenda shwari kabisa, akavua nguo zake na kuvaa nguo za pale hospitalini….
NB. Kila nikipata mwanya nitakuwa najitahidi kutoa angalau kidogo, mungu yupo nashukuruni sana kwa kuwa nami, na mungu atatusaidia tu, ipo siku...!
Kuna watu wameniulizia kuwa ninafanya kazi gani, ili kama ikipatikana nafasi wanitonye, mimi ni mhasibu, mwenye ADCA, Maelezo mengine tunaweza kuwasilina kwa e-mail, kama....
Ni mimi: emu-three
4 comments :
Jamani story inazidi kunoga, mmmmh! Maua usitoe mimba mpenzi maana naongea hivyo kwa uzoefu kama mwanamke. Usijali maneno ukimwambia ataelewa na atafurahi.
m3 jamani mauwa wenziwe tunawatafuta hatuna hata wa kulea
m3 vp upo salama kazini mungu yu pamoja nawe riziki mtoaji mungu kwa binadamu inapita tu
Ndio wapendwa bado nasubiria,ingawaje nafika kazini .kinachosubiriwa na huyo atakayekuja kuchukua nafasi yangu aje nimkabizi. Ingelikuwa heri kama mambo yangeendweshwa kistaarabu lakini inakua kama ule usemi usemao ukitaka kumuua mbwa kwanza umuite majina mabaya. Lakini mungu yupo. Nitaweka kidogokidogo na kama mlivyoona tunaelekea karibu na hitimisho,rejea mwanzoni mwa kisa hiki utagundua hili. Na ili twende tutarudi tena kwa Sweetie huko kuna tukio zito limetokea.
Ex wangu alinisababishia maumivu mengi na nimevunjika moyo na kuharibiwa tangu wakati huo. Nimewasiliana na wachawi wengi na wananinyang'anya pesa bila matokeo yoyote. Nilituma barua pepe nyingi sana nikitafuta uchawi wa kweli hadi nikaelekezwa na mwanamke wa miaka 45 ambaye Dk DAWN aliwahi kusaidia hapo awali, bila kujua niliwasiliana na Dk DAWN ingawa sikuamini, lakini baada ya kufanya kile alichoelezea, nilifuata maagizo yangu. ex alirudi kwangu akiniambia nimsamehe na nikamsamehe na leo nina furaha na ndoa yangu. Unaweza kuwasiliana na Dk DAWN kupitia barua pepe kwa ( dawnacuna314@gmail.com ) au kupitia WhatsApp kwa (+2349046229159) na jaribio litakushawishi.
Post a Comment