Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, May 9, 2011

Dawa ya moto ni moto-7



 Maua alifunua macho yake kwa shida, hayakuweza kufunuka, akajaribu tena mara ya pili huku akiinua mkono kushika kichwa,akili ilikuwa haifanyi kazi kabisa, anachojua ni maumivu ya kichwa. Alikaa hivyo kwa muda, na akili ikaanza kurejea kidogokidogo na hapo akaanza kujiuliza kumetokea nini mapaka kichwa kiume hivyo, na mume wake yupo wapi…akajaribu kufumbua macho, …mume wangu yupo wapi akajiuliza tena. Na kuna nini mbona kuna sauti ambazo hajawahi kuzisikia …na mbona kichwa kinamuuma hivyo, mwili wote ulikuwa umelegea na kushindwa hata kuinua mkono. Maumivu ya kichwa yalikuwa hayapungui na ndipo akaona afumbe macho alale tu,… lakini haikusaidia kitu.
Mara akasikia sauti kama maji yanatiririka mithili ya bomba,…akashangaa, kwani maji ya bomba ya chooni, huwezi kuyasikia ukiwa hapo chumbani, ….akaanza kuhis mabadiliko ya hali ya hewa, na hata mazingira, hali kama hiyo haipo kwake…akatikisa kichwa….lololo…akawa kakichokoza , kikawa kinagonga kama nyundo…. mara kwa upande mwingina akasikia sauti zikisema, `imetoka vyema eeh, safi kabisa, twende zetu…hii sasa dili’ sauti hiyo kama ya kike!
Akainua kichwa tena kwa haraka kutizama nani huyo anaongea, na …Na mara kwa mbele yake akaona taswira ya mtu akija,kwani macho yake yalikuwa kama yana ukungu, akayafumba haraka na kuyafumbua, akajaribu kuinua mkono ili apikiche macho, lakini mkono ulikuwa hauna nguvu. Hali hii ilizidi kumpa mawazo, kwanini mwili ulegee namna hiyo, anaumwa?
Huenda anaumwa, au …akainua kichwa kukiweka vizuri kwenye mto ili awezekumtizama vyema mume wake, lakini kila tendo lakukitikisa kichwa ilikuwa ni kosa, akajituliza, huku kitamani kulia, na hali hii ikamfanya akiligeze kichwa na kulala upande upande na mara akahisi hata shuka za kitandani ni tofauti, akaanza kuingiwa na wasiwasi.
Aliinua kichwa tena na kumtizama mume wake akijua katoka bafuni, lakini aliona kama anaumbo kubwa isivyo kawaida yake, na kafunga taulo….mume wake kwa kawaida harudi chumbani na taulo, ana aibu sana…akaona mabadiliko mengine, akafumbua macho kwa kulazimisha kumtizama mume wake, aliomba asogee karibu amshike kichwa huenda kingepona, lakini aliona hasogei kasimama, na anatizama dirishani. Akawaza hivi mbona hata mpangilio wa chumba ni tofauti!
‘Mpenzi kichwa kinaniuma…nipe dawa…kwanini kichwa kinaniuma hivi ,,,’akasema kwa shida
‘Leo nashukuru mungu kuwa umeniita mpenzi, ….oh Maua mpenzi, sikiliza , hata mimi kichwa hapa hakinipa nafasi, na sio kawaida yangu, nakunywa sana pombe, lakini za jana ilikuwa kama kufuruu…yote hii ni kwasababu nakupenda..’ akasikia sauti ambayo ilimfanya asiamini anachokisikia.
 Alikurupuka haraka na kutoka kitandani, akajikuta uchi wa mnyama, akachukua shuka na kuifunga, akili zilikuwa zimemrejea na alitamani apige kelele, alitamani alie, alitamani dunia ipasuke imzike mzima mzima, lakini ilikuwa kama maji yameshamwagika hayazoleki, akaanza kulia kwa kwikwi….
 Na wakatii huo ndipo akili zikaanza kumrejjea na kukumbuka nini kilitokea jana, alikumbuka kuwa alialikwa na bosi wake, kupata naye chakula cha jioni, kama alivyoambiwa, na kulikuwa na kazi za ambazo alitakuwa kuziwakilisha kwa bosi, bosi akamwambia kwa kuwa kazi hizo nyingi zinahitaji maelezo, basi watazifanya jioni, cha muhimu ni kumfahamisha mume wake kuwa anakazi maalumu ambazo ni kwa ajili ya wakaguzi wa mahesabu!
Maua alijua kuwa hiyo ni moja ya kazi za kiofisi na hakuna kitu kilikuwa kikimugopesha kama wakaguzi wa mahesabu, huwa anajua kazi yake kafanya vyema, lakini kutokana na uzoefu wa kampuni hiyo ya wakaguzi, wanakuwa hawakosi cha kulaumu, yeye aliona ni kupotezeana muda, …basi bosi wake akasema atawaweka sawa, na hili watajidaili katika mkutano wa jioni na iliandaliwa na chakula pia.
Maua alimfahamisha mume wake kuwa kuna mkutano muhimu kwa ajili ya wakaguzi wa mahesabu na kwahiyo huenda ukaenda hadi usiku. Mume wake akamwambia hakuna shida kwani ni majukumu, ila kama atarudi usiku , ni bora yeye aje masubiri mahala, ili warudi wote. Maua akamwambia hiyo isimpe shida, kwani usafiri upo, kama kutakuwa na zaidi atamfahamisha yeye abakie nyumbani tu, kwani na nyumba nayo inahitaji usalama wake.
Basi chakula cha usiku kiliandaliwa, pamoja na wafanyakazi baadhiiwa idara hiyo, chakula na vinywaji vya kujipongeza kiliandaliwa baada ya mkutano, kwani ilikuwa kazi kubwa sana ya kuweka mahesabu sawa, na ilimalizika saa mbili na nusu. Wakala na kuanza kunywa, na rafiki yake alikuwepo, alikuwa akimshauri sana kuwa leoo ndio muda muafaka wakumjua bosi wake.
‘Rafiki yangu, bosi unaye leo, …’ akamwambia, halafu rafiki yake alimwambia kuwa anadharura anaondoka, na baaadhi ya wafanyakazi wakaondoka, yeye alibakia kwasababu alitakuwa kuhakikisha kuwa vitu vyote vimerejea ofisini, na kulipa madeni na hapo hotelini. Alifanya haya kwa haraka na ikafika muda wa kumwaaga bosi kuwa anaondoka.
‘Maua nina maongezi nawe, usiondoke kwanza..’ akasema bosi wake, Maua akataka kusema neno lakini ikashindikana kwani bosi alikuwa akiwasiliana na wakaguzi wa mahesabu kwenye simu. Alipomaliza, akamshika Maua mkono akimwongoza ndani kabisa ya Hoteli, alishikwa na butwaa.
‘Vipi bosi unajua sasa ni usiku, na mume wangu atakuwa na wasiwasi sana..’ akasema Maua
‘Nilikuwambia umwambia kuwa haya amhesabu sio mchezo, lakini haitachukua muda ni maongezi machache, na kujuana tu, sina zaidi..’ akasema bosi.
 Basi mara vinywaji vingine vikaletwa na nyama choma, Maua akataka kukataa kula chochote, lakini akaona sio vyema mbele ya bosi wake. Akanywa juisi na kula nyama, …
‘Maua ina maana wewe hujawahi kabisa kunywa pombe…hii inasaidia sana kuondoa mawazo ya kimahesabu, kunywa kidogo tu…utaona ladha yake..’ akasema bosi. Alikataa kata kata, lakini msisistizo ulizidi mpaka akaona aonje kidogo, kwanini asionje kidpogo aoane ni nini kinaitwa pombe, akaonja, akaona chungu, akaambia ajaribu tena,…kila mara alikunywa kidogo, kidogo na mwishowe akamaliza gilasi aliyopewa…akaanza kuchangamka.
 Baada ya hapo kumbukumbu zilianza kumtoka, ilikuwaje baadaye, anakumbuka waliondoka hapo wakelekea maeneo ya chumba…akiwa hajitambui, akiwa …alipofika hapo akashikwa na kichefuchefu na kukimbilia chooni, huko alitapaika sana, mapaka kataka uzimia, halafua akajimwagia maji , na kuingia bafuni, alioga huku analia, akiwaza nini kilitokea baadaye, lakini akili ilikuwa haikumbuki kitu. Akawaza hadi kufika hatua ya kumkumbuka mama yake.
‘Inawzekana mama alianza hivi hivi kwa kuhadaiwa, …mpaka akazoea, hapana, mimi siwezi kuwa hivyo, hapana…’ akasema na kuanza kuwaza zaidi, akamkumbuka mama yake siku za mwisho wake. Alikumbuka ile siku mama yake alipokunywa na ikawa mwisho wa uhai wake. Alikumbuka lile tukio ambalo lilikaa sana ubongoni mwake.
Alikumbuka siku ile, pale baba yake alipomwambia akapige simu kumuita dakitari, akajaribu kupiga simu lakini kila namba aliyojaribu ikawa haipatikani, na aliamua kurudi kule walipokuwa wazazi wake, alipofika pale alikuta chumba kitupu, watu hawapo, akili ikazidiwa na giza likatanda usoni, akadondoka na kupoteza fahamu, alipozindukana , alijikuta kazungukwa na kaka zake na baba yake, wote wakiwa na suti nyeusi, na suti hizi mara nyingi zinavaliwa kipindi cha msiba.
‘Kuna msiba wa nani..?’ akauliza haraka
‘Maua lala, tulia bado unahitaji kulala, usiwe na wasiwsi..’ aksema baba yake.
‘Hapana niambenai nani kafa…’ akauliza huku anainuka, nia kwenda chumbani kwa mama yake kumtizama. Akawaona wanatizamana na halafu kaka yake kipenzi akafunua mdomo na kuongea maneno ambayo hatayasahau milele.
‘Maua, mama tulimpenda sana, …lakini mungu kampenda zaidi..’ haya yalikuwa maneno ya mwisho ya kaka yake. Yeye hakuamini akainuka na kukimbilia chumba cha mama yake akakikuta kitupu, akarudi na kuwakuta watu wameshaazna kujaa, akamwendea baba yake pale aliposimama, na kumkwida suti yake kwa hasira akaanza kulia kwa sauti huku anasema;
‘Baba mama hajafa, mama yangu yupo wapi, mlete mama umempleleka wapi mama…’ akalia na baadaye lipogundua kuwa kweli mama hayupo duniani , akamfuta tena baba yake na kuanda kumpiga ngumi huku akisema kwa sauti;
‘Baba wewe ndiwe umeemua mama yangu, wewe ndiye chanzo cha kufa kwa mama…baba sikupendi …sikupendi wewe ni muuaji..’ akawa yeye na baba yake, mapaka kaka zake wakaja kummshika na kumweka pembeni na kuanza kumpa ushaurui nasaha. Ilichukua mud asana kukubaliana na tukio hilo, hadi anzikwa mama yake, mapaka zikapita arubaini mwaka, akawa haongei kabisa na baba yake.
 Baadaye akasahau na kuanza kujichanganya na kumalizia masomo yake na kupata kazi, lakini kila mara alikuwa akikumbuka msiba wa mama yake anajenga chuki kwa baba yake, hadi baba yake akaamua kumpa ushauri ambao uliaanza kumsaidia na kuwa karibu naye tena, lakini sio kama zamani.
‘Mwanangu, maisha ndivyo yalivyo, sisi wanadamu tunapenda kuishi, tunapenda kuishi tupendavyo, lakini wakati mwingine tunageuka kuwa chanzo cha kuumaliza uhai wetu wenyewe…utashangaa kabisa. Lakini hata hivyo lazima mtu afe, huwezi kabisa kuishi milele , kufa kupo, na lazima itafutwe sababau ya kufa kwa mtu...tutajiuliza, tutatafutana uchawi, lakinindivyo ilitakiwa iwe hivyo….mwanangu, mama yako kifo chake kilitakiwa kiwe hivyo…kama unakumbuka vyema tulijitahidi sana kumsaidia aondokane na ulevi wake lakini ilishindikana…na hili wakati mwingine ni fundisho katika maisha yetu…’ baba alipofika hapo alitizama juu kama anaangalia kitu halafu akamwangalia binti yake
‘Pombe ni mbaya, sikukatazi mwanangu kunywa, ila..narudia tena neno hilo ila, hakikisha kuwa pombe haikutawali…ni kinywaji, hakina akili, hakina nguvu ya kukulazimisha, kwanini kiutawale ubongo wako, na ikibidi usinywe kabisa, kwani usipokunywa utapungukiwa na nini…pombe inaweza kuwa kishawishi kibaya …na mwanangu epuka sana kashifa zinazoletwa na pombe, unaweza ukaingia kubaya…ikawa shida kutoka, ukiuliza unasema kwasababu nilikuwa nimelewa, sikujua…., nina uzoefu mkubwa wa hilo…nakuomba mwanangu usije ukaingia kwenye mitego ya kibinadamu…kwani wao ndio vishawishi wakubwa, na wengi hutumia njia hiyo, ….ya kukulewesha…’ akatikisa kichwa huku akiangalia saa yake, kwani baba yake ni mtu muda, kila jambo hulifanya kwa muda maalumu.
Alipoyakumbuka maneno haya ya baba yake, akainuka haraka kama vile kazinduliwa toka usingizini na bila kujali kuwa yupo uchi, alitoka bafuni na kuingia chumba alichomuacha bosi wake, na kuanza kutafuta nguo zake ,hakuziona mle ndani, akajiuliza ina maana hata nguo wamemfichia, na ilikuwaje mapaka alale bila nguo, ina maana kuna kitu kimefanyika…akawaza, akakumbuka kweli alipoamuka alijihisi hali sio ya kawaida, kuna tendo lilitendeka…
Mungu wangu ilikuwaje mapaka nikafikia hatua hiyo, akajiuliza bila jibu, bile kumwangalia yule mtu ambaye naye alikuwa akivaa, akafungua mlango na kutokea chumba kidogo, ina maana vyumba hivyo ni maalumu , vina kila kitu, sehemu ya kupikia, choo, sehemu ya kupumzikia, na chumba cha kulala! Alizikuta nguo zake sakafuni, moja kule nyingine kule. Akakuta chupi iko kivywake, gauni,na…inaonekana alikuwa akizivua na kuzitupatupa huku na kule….je ni yeye mwenyewe alifanya hivi, au…hapana haiwezekani, akazivaa haraka haraka na kutoka mle huku akimwacha Bosi ambaye alikuwa keshavaa, huku akimtizama Maua, kwa uso kwa kutahayari…alikuwa naye akiwaza yake.
‘Maua usinielewe vibaya, kiukweli hata mimi sielewi kwanini ilitokea vile, ninalewa,lakini sio kama jana, kuna kitu kisicho cha kawaida…sidhani kama ni ulevi tu…, na tukio zima linanipa mashaka…nakuomba sana uniewle kuwa sikuwahi kupanga kitu kama hicho kiwe kama hivyo, mpangilio wangu ulikuwa kunywa kidogo na kuongea na wewe ili nikueleze lile la moyoni, lakini …sijui kulitokea nini…’ akasema huku anaangalia chini.
‘Maua …sielewi kwani hata mimi wakati mwingine nilikuwa nikikushangaa, ulibadilika kabisa, na mimi nikawa kaka …zezeta kufanya kile unachotaka, ulikuwa wakati mwingine wewe ndiye unanilazimisha kufanya lile nililokuwa naliogopa kukumbia, ingawaje nilitamani sana liwe hivyo….’ Maua aliposikia hivyo alizidi kuchanganyikiwa ina maana yeye ndiye …hapana, hawezi kabisa kuanya kitu kama hicho, huo ni uongo, hakutaka kabisa kumsikiliza zaidi …
 Akatoka nje ya maeneo ya vyumba daraja la kwanza, na ksuhukua chini ya hiyo hoteli, alipofika sehemu ya mapokezi moyo ukaanza kumuenda mbio, na hii ni dalili ya kuona kitu cha kumtia wasiwasi, kashituka, karibu adondoke kwa uwoga, akarudi nyuma kidogo na kujificha, hakuamini macho yake, …mungu wangu, nimesahau, ...kasema kimoyomoyo, kwani kwa mbele alimuona ....oh,....aliyemuona kwenye hoteli ile si mwingine ni baba yake akiongea na baadhi ya watu…akakumbuka kuwa hii ni moja ya hoteli ambayo baba yake hufanyia vikao vyake vya kibishara, akarudi haraka na kujificha, hadi alipoona baba yake kasogea ndani , akatoka mle huku akingalia kwa mshaka, na kukimbilia nje, alipofika haraka akaita taxi, na wakati taxi imefika, anataka kuingia ndani mara akagutuisha na sauti ikimuita toka nyuma…karibu adondoke pale aliposimama…
 Ngoja tuishie hapa, tukitafakari zaidi

Ni mimi: emu-three

6 comments :

Anonymous said...

tatizo unatuacha muda mrefu bila mwendelezo!lakini ni story nzuri kila la heri jitaidi kutuletea mwendelezo wake kazi njema

Anonymous said...

Mmmmmmmmmh!

emuthree said...

Hata mimi kwa ujumla sipendi kubakia na kisa kimoja kwa muda mrefu kichwani, kwani napata visa vingi na nia yangu ni kuweka visa vingi iwezekanavyo, lakini tukumbuke kuwa wakati mwingi inabidi nitumie muda na vifaa vya ofisi za watu kwa kujiiba, au internet cafe!
Kuna mpendwa mmoja alinishauri niandike kwenye kitabu kama `diary' ili niwe kama nanikili tu, lakini kwanguu mimi nikiandika kitu, nikija kuandika tena nitaandika kisa kwa vingine, nakuwa na mbadala mwingine kichwani!
Nitajitahidi iwezekanyo, ...
Naombeni sana ushauri, mawazo na kama nimesahau muendelezo fulani nikumbusheni ili twende pamoja!
TUPO PAMOJA

Goodman Manyanya Phiri said...

Wake za watu wakifanya kazi za usiku kwenye kampuni ni jambo la kawaida; lakini kama kampuni hazilipi hela maalum kuwapa ESCORT mpaka nyumbani kwao itakuwa kosa.


Yule bosi fisi kabisa mwenye kuvaa vyakondoo! Mabosi kama hao wasiende Uarabuni, hasa kwenye nchi zenye kutawaliwa na Taliban: watakuja kukatwa viungo fulani haraka kama umeme!

samira said...

m3 ni sawa sawa ulivyoandika imenoga sana yaani imenipa hamu ya kuisoma vizuri sana sijaona mahala uliposahau
tupo pamoja

Yasinta Ngonyani said...

Nimechelewa kiduchu kusema langu hapa ... Basi ngoja niseme kazi nzuri sana na inaleta utamu kusoma na iishapo unabaki duh imeisha....haya ngoja niendelee na muendelezo sasa...