Jana nilikutana na rafiki wa siku nyingi, nilipomuona nilishangaa mabadiliko ya kimwili, mwanzoni alikuwa mwembamba , na hakuwa na dalili ya wale watu wa kunenepa, hata mwenyewe alikuwa akisagia watu wanene kupita kiasi, leo ana kitambi nan i pandikizi la mtu, nikasema moyoni ama kweli hakuna mtu mwembamba duniani;
‘Vipi Mate, mbona umekiuka miiko, nakumbuka miiko yako ni kutokuwa na kitambi…vipi kulikoni?’ nikamuuliza
‘Bwanawe, acha tu, nimegundua kuwa vitu hivi vinakuja vyenyewe, hata mimi sikutegemea hivi…’ akasema, na kuniacha hoi
Aliniambia hali ile ilikuwa baada ya kupata cheo ofisini, akawa mtu wa kupata kila akitakacho, basi hata muda wa mazoezi ukamtoka, akitoka kazini, jioni anaelekea sehemu za viti virefu, siku za mchana anakuwa na mikutano na watu wazito, napo huko ni kinywaji baridi na nyoma choma, na alipo-oa, baada ya kushinikizwa na wazazi na ndugu ndio ikawa balaa..
‘Kwanini iwe balaa, na kwanini uoe kwa kushinikizwa?’ nikamuulizia
‘Kwasababu sikuwa na mawazo ya kuoa, kwani nilikuwa najirusha na wasichana mbalimbali, pesa si-ipo, yoyote nimtakaye nampata, na niliogopa kuoa kwasababu nitakwaza, sitakuwa na uhuru…basi nikaona nioe, mtoto mzuri lakini mshamba…’ akasema
Nilipomdadisi sana akasema kuwa msicha aliyemuoa hapendi pombe, hapendi kujivinjari kwenye baa na kumbi za starehe, yeye anapenda kuwa mama wa nyumbani, sasa anashindwa afanyeje, na ilihali kazi yake na tabia yake, sio kushinda nyumbani.
Na baya zaidi tabia yake ilivyo na huyo mwanamke haviendani, eti kwasababu hajui kumpa kile anachokitaka, raha za mapenzi na mihamaniko ile anayoitaka..
‘msichana hata kubusiana nhataki, siunajua tena nimezoea zile za kizungu…’ akasema, nikasihia kucheka.
Basi wakati natafakari hili nikapata e-mail kutoka kwa dada mmoja aitwaye Aika;
Hello dada dinnah, mimi nimeolewa nina uimri wa miaka 28 na nina miaka mitatu kwenye ndoa yangu, tatizo langu mume Wangu amekuwa anakunya sana pombe tangu tumeoana na nimejaribu kumsihi sana aache lakini haachi na kila akisha kunywa ana omba msamaha nimechoka na misamaha yake ya uongo kila siku kwani anarudia kila siku na hata nimejaribu kuongea na wazazi wake ila mama yake anasemma nimuache anywe, mimi hilo jambo limenichosha sana kwani linasababisha ugomvi kila siku nyumbani nyumba imekuwa haina amani.naomba ushari wenu nifanyaje ili aache kabisa kwani pombe ina mambo mengi mabaya na mimi sipendi hadi imefikia hatua nataka niachane naye kwani imekuwa kero kwangu sana.
Naomba ushauri
-Email hii imetumwa kwangu kama `nakala’ nahisi mtumaji alinitaka nifike kwenye blog ya dada Dinah nitoe ushauri huko, lakini nikaona hata hapa inafaa.Naomba tusaidieni kwa hili, kwasababu wengi wetu tuna desturi ambazo haziendani na mwenzako, kwa mfano kunywa pombe, kuvuta sigara , nk, wanandoa wengi wanasigishana kwa hili, mmoja anakuwanya au anavuta sigara mwingine hapendi kitu kama hicho, je watu hawa wataishije?
Kwa ushauri wangu mimi, ukichunguza sana watu wanolewa, kama sio tabia aliyoianza awali, basin i mabadiliko yaliyomtokea baadaye ndiyo yanayoweza kumsababishia akawa `mlevi’ au mvuta sigara, kwa mfano hali asiyoridhishwa nayo ya nyumbani. Kama kuna `sintofahamu’ ya wanandoa , mmoja kwa akili zake akaona sehemu ya kuondoa mawazo ni sigara, au kunywa pombe!
Cha muhimu kama sio tabia ya asili, basi jaribu kumdadisi mwenza wako ana kitu gani ambacho kinamkwaza, hata atake `kuondoa mawazo kwa njia hiyo’ …huenda tatizo lipo humohumo ndani. Wewe kama mke una jukumu kubwa sana la kumrudisha huyo mume kwenye msimamo. Kwa ujumla wanawake wana-mitego au wamebarikiwa kipaji cha namna hiyo, cha kumliwaza mume, cha kumfanya mume ajisikie hakuna kingine zaidi ya mke wake. Hilo lipo dhahiri kwenye kwenye maandiko imeandikwa kuwa `wake ni mapambo..’ wake ni tulizo la roho..’ nk, wanadini wanalijua hilo zaidi.
Niwaachie wengine walichangie hili, ili tuweze kuiokoa ndoa ya mwenzetu huyu.
Hili ni wazo la Ijumaa, kuwa hivi kweli `TABIA HAINA DAWA
Ni mimi: emu-three
2 comments :
Tabia ina dawa, huu msemo ni wakuendekeza tu tabia za kijinga jinga. Na kama kweli tabia ingekuwa haina dawa basi tusingekuwa tunawadisplini watoto wetu majumbani ili waache tabia mbaya, tungeliwaacha tu kama walivyo na kusema kuwa tabia zao ndivyo zilivyo hazina dawa.
Tukirudi kwenye ishu ya huyo jamaa mlevi, hata kama mkewe akifanya nini kama yeye mwenyewe huyo mlevi hajaamua kuacha haitasaidia kitu. Inatakiwa mwenyewe aamue kuwa sasa pombe basi, kitu gani kitamfanya aamue sasa pombe basi hapo ndipo mbinu za mke zinaweza kuingia. Hasa akiwa mtu mwenyewe ni alcoholic haswa, na sio wale wa moja moto moja baridi. Akishaona madhara ya pombe basi atatafuta msaada wa wataalamu ili aache hizo pombe maana alcoholism sio tatizo dogo yeye peke yake hawezi kuacha!
Ushauri wangu ni kwamba kama unaona maisha yenu ya ndoa hayaendani ni afadhali kupeana nafasi. Hili ni wazo langu... ngoja tuona wengine wanasemaje...
Post a Comment