Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Friday, November 19, 2010
Asiye na bahati habahatishi-5
Je aliweza kutoroka, hebu tuone muendelezo wake:
*********
Wazee na wanakijiji wote walikata tama kabisa ya kumpata binti yao, na wengii walihisi kuwa huenda keshaingia mikononi mwa watu wa msituni, na huenda keshakuwa kitoweo cha hawo watu kama walivyoamini kuwa watu wa msituni hula nyama za watu. Wengine walisema huenda kama alikimbilia msituni kaliwa na wanyama wakali hasa Mamba.
Mama wa mtoto alilkuwa hali akiwa anamkumbuka mwanae, akawa mgonjwa kwa shinikizo la damu, na ikabidi akalazwe hospitali. Alilia sana na kujuta kwanini imetokea hivyo kwa mwanae, akasema kama watu wameshindwa kumtafuta yeye yupo radhi akaingie humo kwenye msitu akamtafute wmenyewe mwanae. Baba mtu akaamua kuomba masaada toka mjini, na kumwambia mkewe kuwa kwa vile kaka yake ni askari mstaafu wanaweza kumtumia kutafuta watu wanaojua hiyo kazi wakapata kibali toka serikalini na hatimaye wanaweza kumpata binti yao.
Mjomba wao huyu aliwahi kuwa katika jeshi la kivita na waliwahi kutumwa nchi mbalimbali zenye misitu ya kutisha. Na kabla ya kustaafu alikuwa mwalimu wa maaskari wa porini, na mkuu wa kulinda hifadhi za taifa, kwahiyo waliona kuwa uzoefu wake anaweza akapata watu anaowajua, wakaja kuchunguza na hata ikibidi kukomesha tabia ya watu wa porini, ya kuwateka wasichana wao,na kupotelea huko msituni.
Miezi miwili imepita hata serikali na uchunguzi wake haikuambulia kitu. Na taarifa hii ilipofika kwa mjombamtu kaja na kikosii maalumu cha kufanya uchunguzi wa mwisho, walikuwa na silaha na vyombo maalumu vya kutafiti, watu hawa wameshwahi kufanya kazi hiyo kwenye misitu ya Kongo, kwahiyo waliahidi kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kama kweli kachukuliwa na watu wa msituni
Kilikuwa kikosi cha watu saba, makomondoo wa vita, wakapata maelezo mazuri kuhusiana na msitu huo, na walivyotafiti kwa mara ya kwanza walisema kama kweli yupo ndani ya huo msitu kwao ni kazi rahisi kwasababu haujajifunga kama misitu ya kongo. Walichoomba ni kibali amabcho kitawaahalalishia hata kuua ikibidi. Wakaambiwa wajitahidi kama itawezekana wasifanye hivyo, ila tu wawafikishe mbele za sheria wahusika kama wapo.
Msafara ukaanza lwa landrover maalumu inayoweza kuhimili mbuga na matope, na wakafanikiwa kuingia ndani kabisa yam situ, hadi walipofika kwenye bwawa la Mamba. Hapo ikabidi waiache landover mahala kwa kuificha na kuanza kazi ya kutembea kwa miguu. Hii ndio ilikuwa dhamira yao kuchunguza bila gari, kwani gari hutoa sauti!
Walitembea kwa siku nzima bila kupata lolote, na siku moja wakati wamepumzika wakasikia sauti za ajabu zikitokea maeneo ya juu, na walipotazama na viona mbali wakaona kikosi cha watu waliovalia manyoya wakija upande wao, wakiwa na mikuki na mbwa. Kwa mtizamo ule uliashiria vita. Wakajipanga kukabiliana nao. Na haikichulkua muda wakaja mbwa watatu wakikimbia huku wanabweka. Jamaa wakawanyamazisha kwa risasi zisizotoa sauti.
Wakati wanatafakari wachukue hatua gani , mara mshale ukamkosakosa jamaa yao mmoja na kumchana sikio, na hapo wakajiandaa kwa vita. Silaha zenye darubini zikawekwa tayari, na kwa mbali kikosi chenye mikuki kilikuwa kikiwakaribia. Jamaa wakaona wakisubiri watawahiwa na mishale yenye sumu, basi wakaona watupe bomu dogo kueleke kwa hicho kikosi. Lilipotua karibu na pale walipo, likalipuka, na pata shika ile ikawasambaratisha kabisa askari wale wa mikuki. Walikimbia na kupotea misutuni.
Makomandoo hawa wakaanza kazi maalumu ya kusaka kila kona, baadaye wakagundua kuwa kuna mapango ya ndani kwa ndani, wakafikiria kuingia lakini wakaona sio wakati muafaka kwa ni hatari kwao, kwani huwezi jua humo ndani ya mapango kumeandaliwa nini. Walichofanya kila pango walilolipita ni kujaribu kupiga bomu la machozi, na baadhi ya mapango walifanikiwa ila waliotoka ni wazee na wanawake, ambao kimawasiliano ilikuwa vigumu.
Ilibidi atafutwe mkalimani mtu anayejua lugha yao, na hapo waliokamatwa wakawasiliana na wenzao na hatimaye kukutana na mkuu wao wa koo mbalimbali. Baada ya mazungumzo ya muda, wakakubali kusaidia kuongea na vijana wao ili kujulikana nani aliyemchukua huyo binti, na ikiwezekana kama wapo wengine warudishwe kwa familia husika. Vijana wa hawo watu wa misituni wakakataa katakata kwa kuwa wao wanadai wamewaokota hawo wanawali na kimila zao hawo ni wake zao halali.
Siku moja wakati wanasubiri usuluhishi wakiwa kando ya huo mto wakaibuka mamba wawili, wa ajabu, na kuaanza kuwashambulia. Ilibidi watumie silaha kubwa kubwa kuwakalipua hawo mamba lakini mwisho wa siku askari wao wane walikuwa katika hali mbaya baada kuumizwa sana na hawo mamba. Ikabidi msaada uombwe toka mjini. Na gari likawarudisha hao majeruhi mjini kwa matibabu. Wakabakia makomandoo watatu!
Wakiwa wamebakia askari watatu, na wakisubiri msaada toka kijijini, usiku wakasikia mchakato kwenye hema lao, kumbe kwa muda huo askari wa doria alikuwa keshapigwa mshale, na hawa wawili waliobakia walikuwa ndani wakiwa wamechoka, na mara wakavamiwa na vijana waliovalia mavazi ya chui. Kwa hali waliyokuwa nayo ya kuumizwa na uchomvu wa siku nzima wakawa hawana jinsi bali kujisalimisha kwa hawo vijana wenye mishale ya sumu, na kupelekwa kwa mkuu wa vijana.
Walifungwa kamba, na kuninginizwa kwenye mto wa mamba, kichwa chini miguu juu. Chini yam to huo walijaa mamba wenye njaa, wakijaribu kuruka ili wawanyakue hawa askari ambao walikuwa wamechoka sana. Na hapo ikageuka kama onyesho kwao, kwani Yule aliyeshika kamba akisubiri amri ya kuwaachia wadondokee ndani ya huo mto alikuwa akiwachezea kwa kuwashusha kidogo na mamba anapowarukia huipandisha ile kamba juu.
Ulikuwa mchezo wa kutisha kwa hawa mateka! Wale askari walikuwa wakihaha kwa woga, wakijua ndio mwisho wao. Na wakati wakifanya maonyesho haya, mkuu wa koo za watu hawa akaja mbele yao na kuwasihi vijana hawo wawaachie kwani hawo askari, kwani hawo ni watu watu wa serikali, lakini vijana wakikaidi, wakasema hawaitambui hiyo, wao ndio wamechokozwa ndani ya eneoo lao!
Mara ndege ya jeshi ikapita na baadaye ikarudi na kutua karibu kabisa na wao, na haikuchukua dakika mbili , askari walivalia mavazi ya kivita walivamia ule msitu na kutupa mabomu ya machozi na hatimaye kuwaokoa wale mateka, na baadhi ya vijana wa porini wakakamatwa. Walipolazimishwa kusema wapi walipomficha binti anayetafutwa wakakataa kabisa,na kusema hawatasema hata wakiuliwa.
Ilikuwa usiku mwingine na mara kilio cha mwanamke kilisikika kwa mbali kwenye nyumba iliyojificha vichakani, na mara wakaona mwanamke mmoja akija mbio kuelekea pale walipo, na nyuma yao akatokea jamaa akiwa na mshale na mbwa mkali. Hakuwajli wale maaskari akawa anamkimbiza Yule mwanamke, na Yule mwanamke akaja hadi ndani ya kambi ya maaskari. Na Yule jamaa alikuja moja kwa moja hadi kambini hapo na kutaka kumkamata Yule mwanamke, lakini askari wakamshika, ikawa vuta ni kuvute, Yule jamaa akatoa kisu na kuanza kupamaba na wale maaskari.
Aliwajeruhi maaskari na wao wakona hawana jinsi ila kumnyamazisha kwa sailaha ya moto. Walimpiga risasi ya mkononi na kumuumiza vibaya sana, na akawa hajiwezi. Yule mwanamke alipoona hivyo, kuwa jamaa aliyekuwa akimkimbiza kaumizwa na ana hali mbaya, Huruma ikamia na kumwendea pale chini akaanza kulia, kuwa kwanini wamemuua mume wake. Na kipindi hicho mjomba wa Yule binti aliyepotea alikuwa keshafika na kikosi kingine maalumu!
Aliamurisha Yule jamaa aliyeumizwa na risasi akamtwe apelekwe hospitali ili baaadaye aisaidie polisi. Mjomba ambaye alikituma hicho kikosi akamsogelea Yule binti, ili kujua zaidi na huenda akawasaidia, na huenda akawa ni mmoja wa mabinti waliopotea, na alipomsogelea akashikwa na mshngao …alikuwa akishangaa nini, mavazi ya Yule binti, au aliona nini cha ajabu huyu binti.
Nawaomba tuwemo karibuni kwa sehemu inayofuatia!
Ni mimi: emu-three
6 comments :
haya tena..hii nayo ni ya ukweli au ?..maana mmh
Elisa unawafahamu Watindiga, ni kabila moja lipo maeneo ya Singida na Arusha. Kama wewe ni mfuatiliaji habari hukumbuki taarifa za machafuko ambayo yalitokana na hili kabila?
Kuna visa vilijificha ambavyo tunasema ni visa vya mtu mmojammoja kama hiki!
Ndio huenda nimeongezea chumvi, lakini nia ni kukupa raha...au unasemaje?
Usijali tuwepo karibu kwani kuna sehemu inakuja itakupa kile wewe wataka!
yap nakumbuka..mimi naishi arusha huwa tunasikia mengi tu kuhusu mambo ya hayo makabila...
Ila kuna wakati tunaona kama ni simulizi zisizo na ukweli ..japo kwa upande mwingine wa dunia ni vitu halisi kabisa vinatokea
Mmmmmh!! nini tena m3??!! mjomba amegundua nini? ni mjamzito mpwa wake au?
Any way tusubiri huo uhondo. Hongera sana.
BN
mhu!!!
Jamani jamani Kweli Tanzania tuna makabila mengi, binti wa watu kishamzoea huyo mme feki ndo maana kalia baada ya kuona mmewe kaumizwa. Mjomba kamgundua mpwa wake ndo maana kashangaa. Tupe mambo M3, japo siku hizi tunakumiss miss, sijui ndo boss anabana kiasi hicho. Eee mwenyezi mungu mmbariki M3 yeye pamoja wanaomzunguka ili asiwe na stress na azidi kutupa mambo maana twajifunza mengi kutoka kwenye visa vyake. Amen
Post a Comment