Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, November 22, 2010

Asiye na bahati habahatishi-6

`Baba jamani baba, yaani ndio leo mumeamua kuja kunikoa baada ya miezi sijui mingapi, yaani wazazi wangu hamna Huruma hata kidogo na mimi….oh, …’ akamshika baba yake kwa nguvu ambaye aliduwaa na kukodoa macho yake ambayo hayakuamini kuwa anachokiona na kweli au ni miujiza au ni mzimu . Alijikuta akishikwa na kwiki na machozi yakamtoka kama maji…hakuamini kuwa kumbe dua na maombi hukubaliwa, na huu ni mfano wake.


Anakumbuka siku aliyopewa taarifa kuwa binti yake kapotea, jinsi alivyochanganyikiwa, akaapa kumtafuta kwa udi na uvumba. Alitumia ujuzi wake wote, akatafuta kikosi maalumu cha vijana anaowajua ili wasaidiane lakini hawakufanikiwa kitu. Akasema kama kweli katekwa hatakuwa na msamaha na hawo watu waliomteka!

Hakuna hata siku moja aliyokwenda kitandani bila kuomba, bila kumuomba mungu kuwa kama mtoto wake yupo hai anaomba arudi salama, na kama kafa basi wapate fununu au kuyaona maiti ya mtoto wake kipenzi. Kweli huyu binti alikuwa mwanae kipenzi na hata mke wake alikuwa akikasirika kwa kumuona jinsi gani aanvyompenda binti yake huyu kupita kiasi!

Anaikumbuka sana siku ile alipokuja mshenga kuleta mahari na taarifa ya lini ndoa ifungwe baba mtu huyu alishikwa na huzuni kubwa, kwani alijua kuwa sasa binti anayempenda ambaye kila siku alitaka awe karibu naye anaondoka, na huko aendako ni nchi za mbali, na kuonana nay eye huenda ikawa mara moja kwa mwaka, lakini alikuwa hana jinsi, kwani ndoa ni heri katika familia. Akakubali na kumpa Baraka zake…!

Ndoa hiyo ilipangwa ikafanyikie kijijini, kwa maombi ya wazazi wa mume, na baba yake, na familia yao hawakuwa na kipingamizi. Maandalizi yakafanywa huko kijijini na binti akapelekwa kijijini ambapo muoaji anatokea huko huko ni watu wa kabila moja, na familia yao inajulikna kwa kila jema. Mtoto wao mkwe wake mtarajiwa alibahatika kusoma nje na akajaliwa kupata mikataba maalumu ya kufanya kazi huko nje.

Kipindi hicho cha likizo alikuwa na lengo la kutafuta mchumba, aliyekuwa naye mwanzoni hawakuelewana, kwahiyo akaona atafute mtu wa kutoka maeneo ya kwao , ambaye kitabia, kimila wataelewana, siku moja katika matembezi yake akakutana na huyu binti wakatokea kupendana na hatimaye kufikia hatua ya kuoana.

Taratibu zikafuatwa na mahari ikalipwa, ikabakia siku ya kufunga ndoa…

Ikiwa imebakia siku tatu, binti akiwa kijijini, na kijijini kwao kama kawaida maji ni ya kwenye mito, au kisimani, basi siku hiyo binti huyu akiwa na wenzake walienda kuteka maji na kufua. Wakati wanarejea, binti wa huyu askari mstaafu akachepuka kidogo kujisaidia, na ndio ikawa mwisho wa kumuona huyo binti… hadi hii leo, ambapo baba yake na familia yao walishaaminikuwa keshafariki dunia!

Alimkumbatia binti yake na hakutaka aondoke kifuani kwake, kwani aliogopa aisije akapotea tena, akamwamchilia na kumwangalia usoni, machozi ya furaha yaliyochanganyika na huzuni yalimtoka kitu ambacho sio kawaida yake. Akamkagua kuhakikisha kuwa hajaumia mahala popote na kwambia dakitari wa kundi hilo ahakikishe hana tatizo. Na dakitari alipompima na kuhakikisha hana tatizo akamrudisha kwa baba yake. Baba yake akamwambia anataka kujua nini kilitokea haraka iwezekanavyo ili ajua hatua gani ya kuchukua, kwani waliofanya hivyo anataka washughulikiwe na iwe mwisho wa tabia hiyo.

Binti akamkalia baba yake mapajani akaanza kuongea kwa furaha.

‘Siku ile tulienda kisimani na wenzangu, tulipomaliza kufua tukawa tunarudi nyumbani, mimi nikataka kujisaidia , nikachepuka pembeni, na wenzangu walikuwa wakinisubiri, mara, nikasikia kitu kikivunja majani, nikasisimkwa na nywele, nikataka nigeuke nyuma niangalie kuna nini, mara mkono wenye nguvu, ukaniziba mdomo na sijui alikuwa na dawa gani, kwani sikumbuki tena ilikuwaje. Nilijikuta nipo sehemu ngeni nilipozindukana.

`Ilikuwa nyumba ya nyasi imezungushwa miba inayochoma sana, kama boma la ng’ombe, na mimi nilikuwa nimalala kwenye majani. Nilijaribu kutafiti nipo wapi bila kuinua kichwa ili wasijue kuwa nimeamuka. Cha ajabu nikakuta watu wanapigana, yaani ile ya kutaka kuuana, na kwa vile naelewa kidogo lugha yao nikagundua kuwa walikuwa wakinigombea mimi, kila mmoja akidai kuwa anahaki ya kunimiliki. Kulikuwa na vurugu hadi watu wanatoana damu.

`Moyoni nikasema kama wao kwa wao wanadiriki kutoana damu, sembuse mimi ambaye sina udugu nawo, watakuwa na Huruma name kweli. Kwanza hadithi zao tunazozisikia ni za kutisha, ingawaje nyingine ni za kutunga, kwani nina marafiki wanaotoka huko, wanasema hayo ni mambo ya kale, lakini sasa nimeamini kuwa bado yapo…baba bado yapo, wapo watu wanatisha, nahisi kweli wanaweza wakawa wanakula watu…’ akaangalia pembeni kuhakikisha usalama wake, na baba yake akamtuliza na kumwambia asiogope, yupo kwenye usalama.

‘ Wale watu walikuwa wakipigana na kukimbia huku na kule, nakaona hapo inabidi nitumie akili ya kutoroka, na aple waliponiacha kidogo tu, nikatambaa taratibu kwenye yale majani, hadi nilipofika mbali na walipokuwepo, nikatafuta upenyo wa kutokea kwenye lile gome la miba, na uzuri ni kuwa mawazo yao yote yalikuwa katika kupigana walikuwa wamenisahau kwa muda ule. Nikawa naomba huku nikainuka taratibu na kuanza kukimbia.

‘ Baba unajua kukimbia, unajaua mimi nilishika namba ya kwanza shuleni kwa kukimbia, basi siku ile niliongeza mara mbili, nilikuwa kama mtu anayepaa. Nikakimbia huku naangalia nyuma, na sikujua kuwa nimefika kwenye korongo nilitahamaki napaa juu kwa juu, kuzama kwenye lie gema ni refu ajabu, hadi nilipodondokea kwenye majani mengi, ambapo ilikwa ni salama yangu, vinginevyo ningevunjika vunjika, aua kuumia vibaya sana. Lilikuwa korongo refu na huko chini kulikuwa na kitu kama chemuchemu na majani yalistawi vizuri. Panapendeza kweli kweli kuishi, lakini…mmmh, upweke baba, hakuna mtu, labda ndege, nyani…

‘Kwa kuchoka na woga nilijikuta nimelala, na kama ndoto nikasikia kelele za watu, nikafikiri nipo kwenye harusi yangu, lakini akili ipipotulia, nikakumbuka…oooh, nikaamusha kichwa taratibu, ili nyasi zisitingishike. Zilikuwa kelele za watu, kama wanaimba nyimbonyimbo, halafu vitu vinadondoka toka juu, karibu na pale nilipolala nilitizama juu na kuwaona watu wakirusha matunda, vyakula hata pesa, nikakumbuka kisa alichonihadithia rafiki yangu anayetokea maeneo ya huku, yeye alitoroka kwao siku nyingi akawa anasomeshwa na taasisi moja ya dini.

Rafiki yangu huyo anasema kwao bado wanaimani za kale, hawajui dini nyingine, wao wanaamini mila za mababu zao, mizimu na mazingara yao. Anasema wao wana ibada zao na sehemu takatifu ambazo ni za asili. Aliniambia kwao kuna korongo moja kubwa ambapo ni sehemu ya ibada zao za kimila. Humo wanasema ni sehemu takatifu, kwani muanzilishi wa kabila lao aliishi hapo, na Baraka zote zinapatikana hapo.Humpo kila siku mtu anakwenda kutoa sadaka ya sehemu ya kile alichojaliwa nacho. Kama kavuna mazao anatoa sehemu Fulani ya mavuno yake, na kama ana mifugo, anachinja na kutupa sehemu ya nyama kwenye eneo hilo kwa ajili ya mizimu yao.

‘Nikashukuru mungu , kwani tatizo la nini nitakula lilikuwa limetatuliwa, walipoondoka tu nikaenda pale waliporushia vyakula, nikachagua vile vya hamu na kula kwa shibe yangu na baadaye nikashushia na maji ya chemuchemu, nikalala. Ikawa kila siku naafanya hivyo. Usiku nakumbuka nyumbani, ninalia mpaka usingizi unanichukua, nalala naota npo nyumbani na wazazi wangu.

Baadaye akili ikaniia kuwa nifanye uchunguzi huenda nikagundua njia ya kutoka mle korongoni, nikajaribu kutafuta sehemu ya kupanda juu, mara ya kwanza nilishindwa kabisa, lakini baadaye nikafanikiwa kwa shida na kutoka mle ndani. Nikawa najaribu kutoka na kurudi tena mle ndani kwani pale nilitaka kupafanya kama nyumbani kwangu. Kutoka ni kugumu, kushuka kuingia mle ni rahisi, kwani uanaserereka tu hadi chini, lakini nilijitahidi nisiache alama za kuwaonyesha watu kuwa kuna mtu anaishi humo.

‘ Baadaye nikaanza kutafuta mwanya wa kutoroka nirudi kwetu, lakini kila nilipojaribu kuelekea njia Fulani nilikutana na vikwazo vingi, na baadaye narudi eneo langu la kujifichia. Ujue eneo hilo wanaliheshimu sana, kwahiyo wao hawaingii mle korongoni ovyo, labda wazee wa kimila wakiwa na jambo muhimu sana, hapo wanasema ni sehemu mizimu yao inapumzika, kwahiyo haitaki kusumbuliwa. Ila nilichogundua ni kuwa Yule jamaa aliyeniteka toka kijijini kwetu alikuwa akifika kila siku kutafutatafuta kuwa huenda kuna sehemu nimejificha. Siku zikawa zinaenda, na mimi nikawa naanza kukata tamaa, na kupazoea pale kama nyumbani kwangu.

‘Niliwakumbuka sana wazazi wangu, nikamkumbuka sana mchumba wangu ambaye kwa najua kwa muda huu atakuwa keshaondoka kurudi huko anakofanyia kazi zake, na huenda kakata tamaa na mimi tena, kwani kutoweka kwangu hakukuwa na taarifa yoyote kwake. Nililia sana, nikafikia hatua hata ya kuwalaumu wazazi wangu kuwa ina maana hawawezi kuja kugundua huku nilipo, wakanikoa, ina maana hakuna polisi ina maana hata wanakijiji hawajui kuwa kuna sehemu kama hii? Wakati mwingine nililia sana hadi usingizi unanichukua na hata katika ndoto nikawa naota hivyohivyo!

‘Masiku yakawa yanakwenda na hata mwezi kuisha, na baadaye nikawa sihesabu tena kuwa imepita muda gani, nikawa nashukuru mungu kila kukicha salama. Lakini hata hivyo sikukata tamaa kabisa, nikawa naendelea na uchunguzi wangu tu nikiwa na tumaini ipo siku nitaokoka tu. Na siku moja katika uchunguzi wangu, nikawa nimefika kwenye bwawa la mamba, wakati natafuta upenyo, mara nikasikia sauti ya mtu akipiga mayowe, nakafuatilia yale mayowe, na nikaona msichana kabebwa na hawa watu wa huku porini, nikajua ni mhanga mwenzangu. Nilimfuatilia hadi alipoingizwa kwenye kibanda kilichojificha karibu na ule mlima pale juu….’ Akaonyeshea kwa kidole maeneo ya juu kwenye majabali makubwa!

‘Mlima upi, hebu tuonyeshe, kwasababu binamu yako naye alitoroshwa kama wewe, ndio tunahangaika kumtafuta’ akasema baba mtu.

‘Binamu yupi huyo?’ akauliza kwa mshangao

‘Binamu yako Tausi,…’

‘Mungu wangu, na kule kusahau sahau kwake, au alipotendea njia, au alikamatwa kama mimi…au..’ akawa anajaribu kutafakari, kuwa Yule msichana aliyeona akiwa kabebwa anaweza akawa mtu anayemfahamu. Hapana hakumbuki kabisa kumuona sura yake.

‘Tunaomba utupeleke hapo alipopelekwa, ili kama yupo tukamuokoe..’ akasema askari mmmoja

‘Mimi..hapana, kama nimeweza kuokoka na hili janga, sitaki kabisa kurudi mikononi mwa hawa watu hivi mnawajua hawa watu vyema…hapana, nyie fuateni njia hii hadi kwenye lile jiwe kubwa, chini yake mtaona kitu kama kimsitu, mle ndani kuna kibanda, hamtapotea…’ akasema huku anawasiwasi akiangalia huku na kule wasije wakatokea hawo watu tena.

‘Sawa mkuu ngoja tufuatilie, akasema kamanda mmoja na wakati wanajiandaa kuondoka mara ghafla……

***********
 Naona tuendelee baadaye maana hata mimi naogopa nini kimetokea tena, tuwepo na nguvu mpya ya kusubiria hilo tisho au sijui kitu gani kimetokea...
Ni mimi: emu-three

8 comments :

Anonymous said...

Hili ni zinga la movie, yaani kama litapata mtaalamu basi hapa ni kitu na boksi. Kwasababu gani linagusa hali halisi ya kibongo, pili lina kisa chenye mvuto wa hadhira!
Tatizo bongo wapenda dezo ni wengi, hapa watakiona hicho kisa, watakigeuza geuza, mwisho wa siku wanatunga kinamna yao, kama wao ndio wamebuni...kwanini tusiwe wema na wapenzi wa mungu, tukubali huyu katunga, na tumpe haki yake, tukae naye pamoja tumpe haki yake...
Lakini...we utaona tu...nashangaa watu mnalalamika mafisadi mafisadi kumbe wapo wanaoipenda kuiba kazi za wenzio kwa manufaa yao, na hawa ...na hawa...narudi tena na hawa HAWATAFANIKIWA ABADANI...kwasababu wanakula jasho la wengine...
Usikate tamaa wangu...we tupe vitu sisi, kazi yetu kusoma na kuishia kukusifia tu...tutakupa nini...mungu ndiye atakulipa!

elisa said...

mmh kweli sisi kazi yetu kusoma tu na kukusifia , mengine Mungu atakuongezea.

Yasinta Ngonyani said...

Duh! inasisimua na kuogopesha! nasubiri kwa hamu kujua nini kilitokea hata kama naogopa:-)

Anonymous said...

MUNGU YUPO NAWE, IPO SIKU YAKO ATAKUINUA TU. Kama alivyosema huyo Anony. No.1 na elisa,

Hayaaaaaaa!!!!!!!!

BN

mumyhery said...

mhu sijui nini kitatokea!!!

Anonymous said...

Jamani mbona inatisha???? Mmmmh! kuna wakati nasitisha ili nisije ota usiku maana inatisha. Babu kubwa M3

Pamela said...

jamani kikweli japo nasoma nikiwa na woga fulani natamani niujue mwisho nawe M3 unapenda kutuacha kwenye suspence loooh!
anyway kazi nzuri kama move ya kutisha napata amani nikifikiria kuwa Tausi ataokolewa....

Faith S Hilary said...

Kama mdau wa kwanza hapo juu alivyosema, hii inaweza kuwa bonge la movie ila kama nchini tungekuwa na production ya hali ya juu na casting then ingeweza hata kwenda kwenye Oscars International movies because the story line is AMAZING...but I am dreaming too much hehehe...can't wait for the next part!!