Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, November 18, 2010

Asiye na bahati habahatishi-4

  
   Binti mtoro wa ndoa akaanza kulia, na kumuomba mungu, alijuta kwanini kafanya kosa lile, kwanini alikataa kuolewa, kwanini, ikawa kwanini, lakini hakuweza kujua jinsi gani ataokoka na janga lile. Akaingalia ile nyama, hamu ya kuila ikamjia, kaoana ni heri ale asija akafa na njaa, na ili apate nguvu za kutoroka . Akaanza kipande kidogo, akaona tamu, akaongeza, kingina, na kingine, na kingine mapak shanai ikawa nyeupe, akajisikia kushiba, ….mara akasikia unywele ukimsimama. Alihisi woga, na woga ule ulimuashiria hatari. Akawaza, sasa ana nguvu, cha muhimu haina haja ya kuangalia nyuma,kinachotakiwa ni kuruka kitandani na kukurupuka mbio kama mwehu.


Akahesabu moja, mbili tatu….

Sasa endelea na sehemu inayofuata:

Aliruka pale kitandani akiwa kaandaa nguvu zote za kukimbia, alijikuta akipaa hewani, huku mguu mmoja umening’inia toka darini ukiwa umefungwa kamba, kichwa chini. Kumbe alikuwa kafungwa kamba ya mtego wa wanyama, na alipokuwa anataka kukimbia aliivuta kwa nguvu na kutegua mtego maalumu ambao ulimwamsha mwenyeji na kitu kama debe likagongwa mara mbili kwa nguvu ya ajabu.


Yule mwenyeji aliruka kwa wepesi na mara hiyo mkuki mrefu ulishakuwa mkononi ukiwa tayari kutupwa kwa adui, lakini alipoona kuwa hakuna adui bali ni mtu wake anataka kutoroka akaguna na kuurudisha ule mkuki mahala pake, halafu akasimama kumwangalia mwanadada anavyoning’inia kwenye kamba, huku gauni likiwa limevuka na kuacha sehemu ya chini ya kiwiliwili ikiwa wazi , huku limefunika kichwa chote, kwani alikuwa kama mtu aliyening’inizwa kichwa chini , miguu juu!

Alibakia vile kwa muda, huku mwenyeji wake akimtizama kwa jicho la tamaa, na alipoona anaumia akaanza kuomba msaada, na mwenyeji wake akapanda juu na kuifungua ile kamba . Na binti akadondoka chini kama gunia akitanguliza kichwa. Mwenyeji akamwinua na kumweka kitandani, halafu akaifunga ile kamaba tena.

Siku ya pili, mwenyeji aliondoka kwenda kwenye mawindo yake au kwenye kazi zake ambazo hakuna anayejua zaidi ya mwenyewe mwenyeji. Binti Yule alijitahidi mapakaakaifungua ile kamba. Alipofanikiwa akatoaka nje na kuanza kukimbia kuelekea kule alikojua ndipo njia ya nyumbani kwao. Alikimbia hadi kwenye lile ziwa, kazi ikawa jinsi gani ya kulivuka.Akakumbuka mamba, lakini akasema ni heri aliwe na hao mamba kul;iko kurudi kule kwa hawa watu ambao anasikia kazi yao ni kula watu.

Akaambaa ambaa na ule mto kutafuta wapi alipotokea siku ile, lakini alikuta kote kumejaa maji na mara nyingi aliponea kuzama kwenye mataope. Alipofika sehemu ambayo ina njia nyembamba ya kupita, ili utokee upande wa pili, akasikia mawimbi ya maji na ghafla kitu kama mvua ikamwagika toka juu, kumbe ni mamba aliruka akiwa na nia ya kumdaka, akamkosa na kuzama upande wa pili ambao ulikuwa na matope. Mungu wangu, ina maana Yule ni mamba…sasa hapana hapa ni mbio kwenda mbele.

Alipofika mbali katikakati ya maji, kwani kinjia hicho ni kama kisiwa ndani ya hilo bwawa ambalo limundwa na miti miwili inayotokea milimani. Akasikia maji yakirushwa huku na kule, kuonyesha kuwa kuna Mamba anakuja. Akasema sas basi tena, nimekoswa na mtu mla watu, naliwa na mnyama! Wakatii anawaza hilo, mbele yake uso kwa uso na mdomo wa mamba, ambaye alipana lidomo lake, tayari kumvuta majini.

Akafumba macho, huku anamumomba mungu wake, angalau yale meno yasimpe maumivu makali. Ni heri nife tu kabla sijasikia nikitafunwa na yale mane, ambayo yalionyesha uchafu, kwani harufu aliyoisikia wakati lile mamba linapanua mdomo wake ilikuwa haivumiliki. Akajisikia anapaishwa, na hakutaka kufumbua macho yake tena…

Wakati anafumbua macho alijikuta yupo kwenye majani , na alipoangalia mbele yake akakuta maji yanakuja na kurudi, lakini yalikuwa mbali sana na yeye. Akawaza ina maana Yule mamba kaamua kumtema ncho kavu ili aje amle baadaye, au miujiza gani imetokea tena. Kabla hajapata jibu, akasikia sauti nyuma yake , akagwaya na kusema, sasa kitoweo kinahitajika kwa mwenyewe.

Akageuka taratibu kumwangalia huyo Mamba aliyemtema nchi kavu, na moyo wake ukapasuka kwa woga. Mhhh, mwenyeji wake, mtu mla watu alikuwa akimwangalai kwa hasira…akamjia na kumshika mkono. Akamwangalia usoni kwa macho yaliyojaa hasira, halafu akabebwa kama mtoto mdogo, nafikiri ndio safari ya kurudishwa nyumbani. Kumbe yeye ndiye aliyemuokoa mdomoni mwa Mamba, akashukuru, ingawaje sasa anaingia kwa Mamba mtu!

Alipofikishwa nyumbani akabwaga kitandani, na baadaye jamaa akasogea upande wa pili, na aliporudi kitandanii alikuwa uchi wa mnyama! Binti wa watu akatizama pembeni hakujua kuwa kashtua hisa za mnyama aliyekuwa kaficha makucha yake. Mungu kinafuata nini, kuliwa au kuba…hapana, mmmh, mungu niue haraka jamani….akalia kwa kugugumia huku akijikunyata, bila mafanikio!

Kilichofuata ilikuwa kama mtoto anayeogoshwa, na mara maumivu makali kama msumari wa mato uliozamishwa mwilini ulimshitua binti wa watu na kuanza kupiga kelele, na kwa ajili ya maumivu makali akapoteza fahamu. Alipoamuka alijikuta kabeba mzigi mzito uliozidi uwezo wake kifuani, huku akisikia maumivu makali katika sehemu zilizofichika. Akajaribu kuinua ule mzigo, auweke pembeni bila mafanikio, kwa ajili ya maumivu na kuumia kwa kulaliwa muda mrefu akaona dawa na kumuuma meno huyo jamaa ili apate kupumua…

Kumbe kwa kufanya vile akawa ndio kaishitua tena ila hamasa iliyojificha ndani ya jamaa yake ambaye sasa ni mume wake, adhabu ya mwanzo ilikuwa afadhali, safari hii ilikuwa kama kidonda kibichi kiwe kinapitishwa kaa la moto. Alilia, akaugulia na baadaye vinyota vikatanda usoni na kupoteza fahamu tena. Alipozinduka alijikuta kawamba huku na kule na maji ya moto pamoja na majani yalikuwa yakitumika kumkanda, hapo alijisikia nafuu kubwa sana. Lakini alivyowekwa alihisi sasa yeye ni kitoweo kinachoyatayarishwa , kwani hakujiona tofauti ya Yule mbuzi aliyewambwa kwenye moto.

Kumbe jamaa yake pamoja na unyama wake wote alikuwa mtu wa Huruma, alipogundua kuwa kamuumiza mgeni wake , ikabidi akatafute majani ya kutibu majeraha, na akachemsha maji ya moto, akafanya utibabu anaoujua yeye, na kweli ulileta nafuu kubwa. Kwa binti wa watu alijiona kama kudhalilishwa, lakini angefanya nini!

Aliayapata matibabu haya kwa siku kadhaa, hakuwa na jinsi alikubali kudhalilika kwa matibabu hayo, na siku zilivyokwenda akawa anamuzoea mwenyeji wake na kugundua kuwa ni mtu mwema, na inaonekana alikuwa anajuta kwa kitendo alichomfanyia. Akawa anamwangalia kwa jicho la Huruma, na kila akimwandalia chakula akawa anakaa karibu yake kuhakikisha amekula, na akiona hali analishwa.

Baadaye siku moja akaja mbele yake akampigia magoti, akamuonyeshea kivitendo kuwa kakosa, anaomba masamaha! Binti akainamisha kichwa kuonyesha kuwa kakumbali kumsamehe. Halafu akamuonyeshea vitendo vingine ambavyo hakuvielewa, Yule binti akainamisha kichwa kukubali, lakini hakujua anakubali kitu gani. Jamaa akafurahi na kuruka huku na kule …akamletea nyama, supu na matunda, na siku hiyo akamfungulia kamba!

Siku moja wakaja watu wengine wawili, inaonekana ni jamaa za huyo mwenyeji wake, walikuwa wamebeba vibuyu na maziwa na ndizi na vitu vingine, waliongea lugha yao na baadaye wakaja kwake na kumfungua ile kamba ya mguuni, wakamkalisha kwenye ngozi ya chui, na Yule mwenyeji wake akaja wakakaa naye. Baadaye akaja mzee wa makamo akawa anazungumza maneno huku anamwaga kitu kama unga, huku na kule, baadaye akawamwagia maji, na ikaletwa kamba ya ngozi ndefu akafungwa binti na mwenyeji wake…kwa mtizamo ilikuwa ni ndoa, kwani baada ya hapo watu wakacheza na kuimba kwa furaha.

Binti wa watu akawa hana hili wala lile, kumbe ndio keshakuwa mke wa mwenyeji wake, na watu walipotawanyika, akabakia na mwenyeji wake ambaye alionekana kuwa na furaha sana, akatoka kidogo akarudi na gauni la ngozi nyororo akamkabidhi kuonyesha kuwa ni zawadi. Akamvalisha, na kamba ikafunguliwa, kuonyesha sasa yupo huru kama mke wa mtu! Sasa yeye ni mke wa watu wala watu…haiwezekani, lazima nitoroke, akasema kwa kimoyomoyo, lakini kwa njia gani?

Je ni nini kitafuatia. Tuendee kuwepo!


Ni mimi: emu-three

6 comments :

Unknown said...

burudani safi!! Nasubiri mwisho wake!! Ahsante mkuu..

Faith S Hilary said...

wow! I could see this in a movie...lakini sio kwa waigizaji wetu wa TZ - sio chuki, nasema ukweli

Simon Kitururu said...

Tunaendelea kuwepo Mkuu!

elisa said...

kweli hii ni burudani safi..

Anonymous said...

Hapo nimezidikukubali wewe mkali, pole kwa seke seke la foleni ulilokutana nao huko ardhi ndo utafutaji wa mkate huo mkuu yabidi 2 tuwe wavumilivu kama twataka kula mbivu. Mmmmh! i can't imagen hiyo ndo na huyo jamaa sasa sijui atatokaje. any way ngoja tusubili na tuone mwisho wake.

Upepo Mwanana said...

Nahisi nitakuwa addicted kwa kusoma stori za hapa