Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Thursday, October 7, 2010
Usia wa mama waniweka njia panda
Mumba baada ya maisha ya kuhangaika baadaye alipata kazi nzuri, na hili lilimpa faraja kuwa ataweza kumsomesha mdogo wake pekee na kumlea mama yao ambaye ugonjwa wa vidonda vya tumbo na shinikizo la damu vilikuwa vikimla polepole na kuonekana kuchoka sana.
‘Mwanangu nashukuru kuwa sasa utaikomboa familia yetu baada ya mateso ya miaka nenda rudi. Baba yako alipokuwa hai alitabiri hili, ingawaje yeye hakubahatika kuikuta hii hali lakini naona utabiri wake umetimia. Ninachokuasa mwanangu ni huyu mdogo wako. Kama ujuavyo huyu ni kipenzi changu, sina maana kuwa na wewe sikupendi, ila imetokea kumuonea huruma sana mdogo wako, kwani ukuaji wake ulikuwa wa shida, kuumwaumwa na hii imenifanya niwe karibu sana na yeye…’ akamgeukia mdogo wangu ambaye alikuwa kainamia kitabu alichokuwa akisoma.
‘Chochote utakachojaliwa nacho muendeleze mdogo wako, mshiriane na yeye, na hata ukijaliwa kuoa, angalia sana mkeo asije akamnyanyasa mwanangu. Yeye akiumia kokote atakapokuwa nitajisikia maumivu. Hili limedhihiri mara nyingi kiasi kwamba nahisi akipata matatizo nitakuwa naumia sana..’ akaendelea kuongea.
‘Mama hilo lisikutie shaka, kwani sioni nani wa kumnyanyasa, hata nikioa, mke wangu atampenda sana kama shemeji yake. Naomba mama usiwe na mawazo juu yake, cha muhimu nikumsomesha ili afikie sehemu nzuri ya kuanza maisha…’ Nikampa mama matumaini.
Mazungumzo haya yalifanyika miaka mitano iliyopita, Miaka miwili baadaye nilioa, na wakati naoa, nilkuwa nikiishi na ndugu yangu na mama alibakia huko kijijini . Nilikuwa nimepanga nyumba yenye vyumba viwili na sebule. Tuliishi kwa raha hadi pale nilipopata uhamisho wa muda. Niliambiwa niende mikoani kwa muda wa miezi mitatu. Niliipanga familia yangu vyema, nakumwambia mke wangu ahakikishe anaishi na shemji yake vyema kwani yeye ni tulizo la mama mkwe wake.
***
Mke wangu alikuwa mwema, mpole na mwenye upendo, kwa kipindi chote tulichoishi naye hakuonyesha dalili ya ubaguzi. Nili wahi kumpeleka kuishi na mama yangu kijijini, na mama aliridhika kuwa kweli nimepata mke mwema. Naye alitokea katika familia ya kimasikini kama mimi , na alikuwa binti pekee katika familia yao.Yeye alikuwa akiishi na mama yake baada ya baba yao kufariki akiwa na miaka mitano. Akalelewa na mama yake kwa shida sana.
Mama yake aliishi maisha ya dhiki, ya kuombaomba kwa majirani, mpaka watu wakamchoka, na kwa hali ile ilimfanya azoofike sana uzeeni. Hali yao hiyo niliifananisha na ya mama yangu, ingawaje kulikuwa na utofauti kidogo. Tabia zao zilifanana kwani na huyu mama mkwe alimfanya binti yake huyu kipenzi chake kikubwa. Nakumbuka siku namuoa mke wangu huyu, mama yake aliniita pembeni akaniasa kuwa huyo binti yake ndiye uhai wake, kwahiyo nihakikishe kuwa namtunza vyema.
Baada ya miezi kadhaa mama wa huyu binti akaumwa sana, ikabidi twende na mke wangu kumuuguza, na haikuchukua muda akafariki. Siku hiyo kabla ya umauti haujamshika alituita wawili akawa anatupa Maneno ambayo yameniweka rehani. Mama huyu alinitaka nisimuache mwanae kwa vyovyote vile kwani yeye kanikabidhi mimi kama mama, kama baba na hakuna jamaa yao yoyote aliyebakia , kwahiyo nimtunze kama mboni.
‘Mama mimi naahidi kuwa sitamuacha kwa vyovyote vile, usiwe na wasiwasi wewe angalia afya yako…’ nlliongea mengi, kumbe wakati naongea huyo mama alishakata roho.ilikuwa pigo kubwa sana kwa mke wangu na mimi! Lakini ndio siku ilishafika hatuna jinsi.
***
Huko mikoani nilikuwa nikiwasiliana na familia yangu hiyo kwa simu. Na baada ya miezi mitatu nikarejea tena kuishi na familia yangu. Siku hiyo nilirejea usiku, sababu ya shida ya usafiri, kwahiyo nilifika kiasi cha saa sita za usiku. Nilipofika hapo tulipopanga nikagonga mlango, kimya, nikagonga tena, na mara nikasikia sauti ikitokea chumbani kwa mdogo wangu’
‘Wewe amuka nasikia kuna mtu anagonga nje..’ hiyo ilikuwa sauti ya mdogo wangu, sijui alikuwa akimwamsha nani liyelala naye! chumbani kwake, nikajisemea, kama mdogo wangu kaanzisha tabia ya kuwaingiza wasichana ndani itabidi nimseme, asije akaanzahaya maswala mapema.
‘Wewe nenda kamsikilize ni nani, mimi nimechoka nina usingizi....’ Hii sio sauti ya mke wangu, nikaingiwa na wasiwasi wa ajabu. Sidhani kuwa nimefanya makosa, hiyo ni sauti ya mke ...nilitamani nivunje mlangi niingie haraka nihakikishe kwa macho yangu, mbona wote wanaongelea chumbani kwa mdogo wangu, ina maana gani…
Oh, jamani muda umekwisha tutaonana kesho tukijaliwa!
Ni mimi: emu-three
7 comments :
Aaaah bwana we muda ganihuo umekwisha...oh, another episode ehe..
Kwanza nahisi `fumanizi' pili talaka, tatu udugu kuisha. Kama ni mimi yote yangefanyika bila `hestate' sivumilii wazinzi kwasababu mimi sio mzinzi, na ukificha ficha haya mwisho wa siku utalea watoto ambao sio wako!
Kisa kingine,lete M3 Unajua wengine hatujui kutunga ila twapenda kusoma visa. Mungu atakulipa kwa kutupa visa kama hivi vyenye mafunzo. Sijui na wewe unaneemeka lolote, kwani wengine wanalipwa na wanaoweka matangazo.
Aaaah Stori ilianza kunoga m3. Kesho basi Mkuu kamaulivyotonya -Tukijaliwa !
Mkuu Simon, nitajitahidi kesho, kwani kimeshatua kichwani, kilichobaki nikukiweka kwenye maandishi tu. Kuna mswali ya hapa na pale nilitaka kumdadisi mlengwa lakini hayana tija sana. Tuonane kesho hapa kijiweni! Insha-Allah
Duuuh story inanoga,ngoja nikawajibike nikirudi nitasoma sehemu ya pili...M3 unazitoaga wapi hizi story maana ni babu kubwa.
Kweli kabisa, kukulacho kinguoni mwako....
MMMMMMMM! M3 WEWE NI MKALI SANA. VISA VYAKO NI VYA KUSISIMUA MNO.
MUNGU AKUBARIKI
Post a Comment