Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, October 6, 2010

tutaonana mungu akipenda-hitimisho

  
Soma sehemu iliyopita kwa kubofya hapa: sehemu ya nane
Polisi wa kimataifa walikuja kuhusishwa baadaye na kadhia hii baada ya ile barua pepe kufichua mambo mengi zaidi. Na walipofuatilia wakagundua kuwa marehemu aliyekuwa mke wangu alikuwa mteja mzuri wa madawa hayo, na alisha-athirika, sio kwa madawa tu bali pia na ugonjwa wa ukimwi.


Na katika orodha kubwa ya wahanga wa kisasi cha Yule mwanamke ndugu wa mke wangu, waligundulika wengi ni wanachama wa kuuza madawa ya kulevya. Na ukaanza msako wa nyumba kwa nyumba, hadi alipogundulika kiongozi mmojawapo ambaye aliwakilisha wenzake hapa nchini.

Wakati kesi inaendelea Yule mjomba, wa uongo akakamatwa, na polisi walipofanyiwa vitu vyao akafichua siri yote, kuwa alipewa siku kadhaa awe amemuua aliyekuwa mke wake vinginevyo angeuwawa yeye. Alipoambiwa hivyo alichanganyikiwa, na mwanzoni alifikiri wanamtania, lakini walipomkamata siku moja na kumtesa ndipo alipokiri kuwa sasa ama zake au za mkewe. Alijua hata akimuua mkewe lakini yeye atafuatia baadaye, kwanii walishamtoa kwenye imani yao.

 Kwahiyo alichofanya ni kumpa taarifa huyu mkewe , na kwa pamoja watafute njia ya kuokoka. Akafanya juu chini kumlinda mkewe asiuwawe, ingawaje walishagombana na kutengana, kwani alikiri kuwa bado alikuwa anampenda licha ya yote yaliyotokea. Alikuja kuwadanganya kuwa keshamuua, na alipotakiwa kuonyesha ushahidi akashindwa. Akapewa muda wa mwezi mmoja awe amemaliza kazi na alete ushahidi kamili kwa mmoja wa wahusika.

 Alijaribu kila njia akashindwa, kwani kazi ya kuua haikuwa fani yake.Hilo kundi lilipogundua kuwa anamficha huyo mwanamke wakaamua kumtafuta wenyewe. Na kilichosaidia ni huyu mwanamke kujibadili kama ombaomba na kichaa, na kuhama huku na kule kwahiyo ilichukua muda sana kwa wao kumgundua wapi alipojificha. Wakamtuma mtaalamu wao ambaye pia anajulikana kama `mtoa roho’ katika kundi hilo!

Alipofika akafanya uchunguzi wake na akamgundua na kufuatilia nyendo za marehemu, na alipoingia ndani ya nyumba yangu, alikuja na kujificha akitafuta upenyo wa kumaliza kazi yake. Alipoona kuwa marehemu kabakia mwenyewe, akaingia kwa kutumia funguo zao zinazofungua mlango wowote. Na akakiona kile kisu kikiwa juu ya kabati, na akaamua kukitumia badala ya silaha aliyokuja nayo.

Wapelelezi wa kimataifa walikuja kumnasa huyu muuajii akiwa anavuka mpaka kuingia Kenya, na hakukubali kirahisi kukamatwa, ikabidi polisi watumie nguvu za ziada na katika majibazano ya risasi yakasababisha kifo chake.

Ushahidi uliokusanywa ukaweza kugundua kila kitu na siku ya kesi yetu, watu walijaa sana, na hatimaye tukaachiwa huru, hatukuamini macho yetu.

Na huu ndio mwisho wa kisa, hiki , tumeamua kukifupisha ili tusiwachoshe sana, yapo mengi tumeyaacha ili kuweza kufikia hatima ya kisa hiki chenye mafunzo ndani yake, kuwa hatima ya uovu ni mbaya, na mnaposalitiana ndani ya ndoa kuna kitu kamaa `laana'. Laana hii inaweza ikamsumbua mtu bila kujijua . Swalii ni kwanini uamue kusaliti, kwanini msiambiane ukweli kabla? Sijui, lakini yote hutokea ili iwe sababu kwetu kujifunza.

Tunawashukuruni sana, na kama kuna maoni au chochote msisite kutuandikia kwa e-mail yetu ; miram3.com@gmail.com.

Ni mimi: emu-three

14 comments :

Anonymous said...

Hatimaye umekimalizia kisa, mmmmh, ngoja nikisome kwa undani sasa halafu niseme yakusema. Kwa kifupii wewe upo juu, umtunzi mzuri...!

Pamela said...

poleni sana nimeumia na machozi kunitoka lkn pia nimefurahi mliachiwa huru cjui mlikaa rumande kwa muda gani??

emuthree said...

Nashukuru sana Pamela kwa kuwa nasi, tungefurahi kama ungejisajili na kuwa mpenzi wa blog hii kwa kufungua gmail account na hatimaye kujiandikisha kama marafiki .
Kama unavyojua kesi za mauaji zinachukua muda mrefu, hawa jamaa walisota rumande miezi miwili...lakini hatimaye ndio kama ulivyoona, wamechangia kuvunja moja ya genge la madawa ya kulevya, na kugundulika kwa siri ya mtu aliyekuwa akiambukiza watu ukimwi kwa makusudi kwa kisa cha kulipiza kisasi.
FUNZO na ONYO, je wangapi wapo katika mnyororo huo wa watu mia waliotambulikana...tuwe macho sana, kwani ugonjwa huu tiba yake kubwa ni kuachana na zinaa..na mkipatana na kuoana kapimeni kwanza kabla hamaingia kwenye tendo!

malkiory said...

Nakupa pongezi zangu kwa uandishi wako uliotukuka. Japo mimi si mtaalamu katika fani hii, lakini hata mpangilio wa kazi unatosha kumvutia msomaji bila kuingia kwenye content.

Pamela said...

Asante M3 nitafanya hivyo asante kwa ufafanuzi samahani na yule mume wa marehemu aliishia wapi kwani nae alikuwa ni mshiriki wa madawa ya kulevya

emuthree said...

Bila samahani Pamela, napenda sana watu waulize maswali, watoe maoni nk, kwa kufanya hivyo nitajua kweli watu wamesoma na hata kama hawakuipenda lakini kuna kitu kitakuwa kimewagusa.
Huyo mume wa marehemu kama utakumbuka sehemu ya kwanza ndiye yule mjomba wa uongo, aliyekuja akamtorosha `mke wa msimuliaji wa kisa hiki'. Huyu ndiye baadaye alikamatwa na alipoteswa akasema siri yote anayoijua, kwake yeye alijua hana cha kupoteza, ni heri polisi walisambaratishe hilo kundi ili na yeye apate salama yake.
Unajua vikundi kama hivi, ukiwasaliti ujue watakuua tu, kwao wanachojali ni mali,sio ubinadamu!

emuthree said...

Nashukuru sana Mkuu Malkiory kwa kutoa sifa hizo, na nia yetu pamoja na kutoa hivyo visa ni kutaka kujua je ujumbe umefika.
Na pia kama kuna mapungufu tunaomba tujulishwe ili nasi tujifunze. Wapo wataalamu wa visa, wataalmu wa utunzi nk, wao wanaweza wakatushauri kuwa hivyo sivyo tufanye hivi na vile. Kama yule mmoja aliyetupa ushauri mzuri wa kutumia majina badala ya `mwanamke' au `mwanaume' nk
Karibuni kwa maoni, maswali na kuchangia chochote

Yasinta Ngonyani said...

Hatimaye kisa kimaisha kwa kweli umefanya kazi nzuri sana, Labda niseme shukrani kwa wote alikusimulia hiki kisa na wewe mwandishi. Kimekuwa ni kisa cha kusisimua, kuogopesha, kufundisha pia na ningefurahi kama wanandoa wangi wangepata muda wa kusoma. Ahsante sana najua wengi wamepita na wamesoma hata kama hawajaweka chochote. Ama kweli katika ndoa inabidi kuaminiana sana ila naona usaliti umezidi zaidi.

Simon Kitururu said...

Ujumbe umefika Mkuu!Tatizo je tuliosoma baada ya kupata ujumbe kuna chochote tumejifunza?:-(

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

The law of cause and effects! Ama mtenda hutendwa imefanya kazi yake vema kabsaaa hapa!

Pamela said...

m3 'mjomba'alitoa siri genge likasambaratishwa je alihukumiwa kifungo au aliachiwa huru?? ndo ninachotaka kujua..

emuthree said...

Ahsante Pamela kwa swali hilo.
Tunapoongea saizi mjomba `ananyea pipa', alihukumiwa kama wahalifu wengine, licha ya kuomba kuwa asamehewa kwakuwa amejitolea sana kulisambaratisha hilo genge na hata hivyo yeye ni mgonjwa, kwenda kwake huko kutachangia sana kuwaambukiza wengine.
Hukumu ikatoka na walivyosema kapata punguzo la miaka, sikumbuki mingapi. Lakini yupo na hali yake kiafya sio nzuri!

Anonymous said...

Mimi nimesoma hicho kisa,hebu nijulishe ni kisa cha kweli au ni hadithi ki ukweli niko njia panda

emuthree said...

Hiki kisa kimemtokea mtu ambaye namfahamu, na kwa kukumbusha zaidi kama wewe umfuatiliaji wa habari, unakumbuka kuna binti mmoja alitangazwa kuwa kaambukiza watu kwa makusudi na akaandika majina yake. Habari hizi zilitolewa Kenya na huyu binti alitokea TZ...
Hili ni tukio lenye fundisho kuwa wapo watu wengi wameambukizwa na wenzao kwa makusudi, fikiria mwenyewe hawo mia wazidishe kwa mara ngapi katika hao mia katembea na wangapi, utaona mwenyewe jinsi gani hatari ya huu ugonjwa ulivyo!
Oa kama hujaoa, na kabla ya kuoa pimeni kwanza!