Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, October 13, 2010

huu ni utumwa, wa kupinga asili yako!

‘Mimi nimezaliwa 1920, naijua nchi yangu vizuri, namshukuru mungu kwa hilo…’ sauti ya babu ilisikika akiwa kasimama ndani ya daladala, na watu wema walitaka kumpisha akae kwenye kiti, lakini yeye hakutaka kukaa, akasema bado anaweza kuhimili kusimama. Na kweli ukimwangalia bado anadai, ana afya yake kinyume na umri wake.


‘Babu hebu tuambie siri ya afya yako, kwani umri kama huo sidhani kuwa sisi tunaweza kufikia, na kama mtu akifikia hataweza kutembea, na kama akitembea sidhani kuwa akili zake zitakuwa sawa na wewe…’

‘Siri kubwa nii nyama ya ulimi, mimi nimeweza kuishi hadi leo kwanza kwa kudra za muumba, na hata hivyo mimi nachunga sana ulimi wangu ambao unaweza kuleta matatizo katika mwili, watu wakikupenda utaishi sana, kwani midomo yao haiishii kukuteta kwa wema, na kukumombea maisha marefu …lakini hata hivyo nyie siku hizi vyakula vyenu vimejaa sumu, mwataka kula vyakula toka Ulaya, vimesindikwa karibu miaka kumi iliyopita mnakula leo. Ili visioze lazima viwekwe madawa ambayo ni sumu kwa miili yetu.

Mzee huyu alikuwa akianza kuongea mtatamani gari lisifike upesi kwani kila alichoongea kilihitaji kuhifadhiwa . Alianza kuongelea majina ya mahali na kwanini yaliitwa hivyo, kwa mfano alisema Changombe inatokana na mhindi mmoja alikuwa akifuga ngombe, na ndipo jina la changombe lilipotokea. Akasema pia kuna sehemu inaitwa Toroli, na kwasababu kulikuwa kuna vitoroli nafikirii ni maeneo ya bandarini, wanatumia kuchukulia mizigo ya bandarini.

‘Mnaiua Keko nyie, keko ilisifika kwa uchawi, kulikuwa na mama mmoja toka Songea alikuwa akiitwa MAGURUMBASI, jina hilo liliogopewa, kwani mama huyu Mngoni, alikuwa maarufu kwa uchawi, alikuwa akitaka kujisaidia hajisaidii hapa Dar, anasafiri kwa uchawi wake hadi Songea , na akimaliza shughuli zake za kujisaidia anarejea hapa Dar, …’ watu wakacheka.

‘Nyinyi mtaona utani, lakini enzi zetu waliokuwepo watasadikisha haya.

‘Nawashangaa leo, majina ya asili zetu mumeyabadili, angalia barabara hii iliyokuwa ikiitwa `barabara ya Pugu, sasa sijui mnaiitaje, …mumekuwa watumwa, huku mwajifanya mnapinga utumwa. Kila kukicha maina yanabadilika, mara Livingston, Victoria, hawa waligundua nini, kwanini sisi hatukuwepo, huu ni utumwa wa kupinga sili yako? Nawauliza wanahistoria, wanafanya nini, mbona hawadai haki za historia yao, au ni wati wa mazingira tu, au watu wa wanyama tu, au watu wa watu wanaodai haki za Nyanja zao, hawa wa historia wanakula dona la bure….’ Akasema huku kaegemea kwenye kiti.

Mimi nilimuunga mkono nikasema wazee kama hawa walitakiwa wapewe hifadhi Fulani, na watu wawe wanakwenda kuhifadhi kumbukumbu na historia, lakini hutaamini, wengine wakiona wazee kama hawa wankimbilia kuwaita wanga…jamani kwanini tunajilaani wenyewe, kama wengekuwa wanga, wangewazaa nyie…

‘Nyie mnaijua KURASINI, zamani haikuitwa kurasini, ilikuwa inaitwa KURAZINI, wamekuja kubadili kutokana na matamshi , kwa Musa Hasani, sasa mnaita Msasani… sasa sisi wazee tunajua mengi, lakini nyie vijana wa leo mnatudharau…’ dereva nishushe nimefika. Akateremka na watu wakabaki kuzungumza kila mtu na lake, huku wengine wakiwa hawaamini kuwa Yule mzee ana miaka tisini!

Hebu jamani ujumbe huo kwa watu wa historia, kuwa tuwe tunahifadhi kumbukumbu zetu za asili, yake majina ya asili yasibadilishwe, na kupachika majina ya kigeni, eti ili yafanane nay a kizungu. Majina kama ya `kwa rafaeli’ , Kwa msongolo, geza ulole, Mbwa kachoka, nk, yameitwa mahali Fulani kutokana na tukio Fulani, labda aliishi mtu Fulani mwenye sifa Fulani, tunahitaji kuzijua hisi sifa baadaye, na vizazi vyetu vijifunze, kwanini tubadili na kuita mitaa yetu kwa majina ya kigeni kama vile `London street, au Bombay street…nk’ huu ni utumwa , hii ni kuvunja haki za historia. Wana historia mna haja ya kudai haki hizo. Sioni mantiki ya kuziita majina barabara zetu majina ya wakuu, ili iweje, na wakati barabara hizo zilikuwa na majina ya asili. Wakuu hawa walishapata sifa zao tayari, kuwa alikuwa raisi, alikuwa nani…je huyu mliyemnyima haki yake ambayo alipewa na watu tutamkumbukaje?

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Simon Kitururu said...

Tatizo linajitokeza kwanza kwa swala zima la ASILI ni nini.

Kwa mfano tukitumia mfano wa Kwa Musa Hassan ambako panajulikana kama Msasani . Jina tu Hassan linatonya kuwa labda kabla ya akina Hassan kuna ambao walipaita mahali hapo hapo jina jingine.

CHa kujiuliza :
Si watoto waliozaliwa enzi za Tanzania Bara wanaweza zani Tanzania Bara ni jina la asili wakati wazee wao walio zaliwa enzi za Tanganyika kwao jina la asili ni Tanganyika?


Tukiachana na Uasilia Wa CHEKERENi ilikuwa kiasili inaitwa CHECK TRAIN, sanyingine mie nasita kukubali kila kitu cha OLD is GOLD hata katika misosi kwa kuwa ukifuatilia kilishe utakuta mpaka si muda mrefu data zinaonyesha kuwa Makabila mengi walikuwa hawali BALANCED DIET: Mfano Mmasai aliweza kuwa hagusi majani wala matunda na samaki kwake matusi .

Na ukicheki umri bado utakuta kuwa si kweli kila jamii ya zamani kwa kufuata ya zamani walikuwa hawafi chini ya miaka 40 . Ingawa kutokana na kuwa walioa mapema , mtu wa miaka Arobaini alishakuwa na wajukuu wa kutosha na sura ngangari.


Nawaza tu kwa sauti!:-(

emuthree said...

Hiyo mkuu Simon ni changamoto! Lakini ujue hiyo imeandikwa na ipo kwenye vitabu vya historia kuwa Tanzania ilitokana na Tanganyika, je nikuulize kabla ya Tanganyika ilikuwepo nini, na mlolongo wake kwenda nyuma.
Itakuwa vigumu kugundua hilo kama halijawekwa kwenye kumbukumbu za kihistoria!
Sasa chukulia majina kama hayo ya mitaa na maeneo, mengi hayana kumbukumbu za kihistoria, kwahiyo mabadiliko yakitokea ndio umesahau kabisa nini jina la mwanzo lilikuwa! Ili kumbukumbu hizo ziwekwe ndio mimi nikaona kuwa ni vyema lilie jina la `asili' lililotambulika, huenda kulikuwa na jingine nyuma likafutika na hatjui lilikuwa nini, basi hili ambalo tunalijua na kwanini liliitwa hivyo tulienzi....kama tutabadili tuweke `marejeo' ya kumbukumbu...
Ni nyongeza mkuu, na wadau wengine je mwaonaje kwa hilo!