Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, October 15, 2010

kakosa mwana na maji ya moto

       
Jana wakati nipo nyumbani baada ya matibabu, nilitembelewa na mtoto wa mbunge mtarajiwa. Nilifurahi sana, maana watu kama hawa wanaweza wakakuunganishia maisha bora kwa kila Mtanzania.

‘Vipi mtarajiwa umekuja kuniomba kura au kunisalimia’ nikaanza kwa utani.

‘Acha hayo bwana wewe hujui nini kimetokea au unanitania’ akasema kwa uchungu.

‘Kwani vipi, mbona unahuzuni.

‘Kama hujasikia baba yupo ndani na hapa tuna haha huku na kule kumtafutia dhamana, lakini imegonga mwamba, kwani mama hataki wala kusikia habari hizo, kama mama angekubali kushirikiana na sisi baba angeshadhaminiwa. Lakini…ngoja nikupe ilivyokuwa.

Siunajua tena wasee wetu hawa, hawatosheki, basi bwana, mzee katika kuusaka ubunge alichukuana na hawara yake na kushukia hoteli moja njiani akielekea Dodoma, na ilipofika saa tisa usiku alibanwa na mkojo, akatoka , na sijui alijisikiaje badala ya kurudi tena kitandani akaona atoke nje apate upepo kama saa moja akitazima maadhari ya usiku, baadaye akaamua kurejea chumbani kwake.

Anasema alipofika, alijaribu kumsemesha mwenzake akaona kimya, akawasha taa, na alipomshika mwenzake alimuona katulia tuli. Akamsukasuka , kama kazidiwa na ulevi lakini kimya, na kilichomshitua ni kuwa hawara huyo alikuwa kamkodolea macho tu, hayafumbi.

Basi ikabidi atulia na kutumia ujuzi wake wa kidakitari akaona kuwa huyu hawara keshakufa.

Sasa endela na kisa kilivyokuwa:-
                                                  ************
Mbunge mtarajiwa alihaha huku na kule, alirudi tena pale kitandani na huku mkono unatetemeka , alkalivuta shule polepole, akiomba kile alichokiona mwanzoni kiwe ni ndoto tu , lakini pale kichwa kilipoonekana , ilidhihiri wazi kuwa hiyo sio ndoto, kwani sura ya Yule mrembo ilimkodolea macho ambayo yalionekana hayana uwezo wa kufumba tena , bila ya msaada. Akapeleka kidole chake kwenye shingo na kusikiliza mapigo ya moyo, na kuurudisha mkono wake haraka kama mtu aliyeshika kaa la moto.

`She is dead…my Gog, imekuwaje masikini, hili sasa balaa, kama ukisikia kuumbuka, sasa nimeumbuka…’ akajisema mwenyewe kwa sauti, huku akitembea huku na kule kwenye chumba kile kilichojaa kila kitu cha kifahari. Hii ni hoteli aliyokuwa akiitumia na huyu binti kila anapokuwa na safari zake za kuelekea Dodoma.

Binti huyu alikuwa kati ya mabinti aliowawezesha hata kugombea urembo. Alikumbuka alipomtoa kijijini akamsomesha, na kumnunulia nyumba. Alimpenda sana, kwani pamoja na mengine, alikuwa mwenza katik biashara zake za chini kwa chini. Akamsogelea pale kitandani na kumwangalia kwa macho yaliyojaa huzuni. Akavuta shuka vizuri na kumfunika. Lakini imekuwaje afe hivihivi tu, au alikuwa anaumwa hakuniambia…

Sasa imetokea, nifanyeje, na kwanini majanga yote haya yanitokee mimi tu kipindi hiki cha kukaribia uchaguzi, lazima kuna mkono wa mtu..’ akasema kwa sauti huku akiwaza mlolongo wa matukio ambayo yalimfanya afunge safari ya ghafla kuja huku Dodoma, katika kikao cha kukamilisha uteuzi wa majina.

Kwanza kupitishwa jina lake katika orodha ya wanaogombea ilikuwa ni kazi kubwa, kwani wajumbe walishamtilia shaka kuwa hakubaliki, lakini alitembeza fitina, akahakikisha kil mjumbe kampitia na kumweka sawa, na hii ilimgharimu nyumba yake aliyoiweka rehani kwa wadosi wawili kama rehani.

Jina likapita, na kivumbi ilikuwa kwenye uchaguzi, mwenzake akampita kwa kura kadhaa, na hapo akawarudia wadosi wake, akaongezewa pesa na kutembeza fitina, hadi matokeo yakapanguliwa kinamna yeye akaonekana ndiye mshindi. Siku lilipotangazwa jina lake watu wakaandamana, na wengine kumwingilia nyumbani kwake. Hali hiyo ilinyamazishwa kinamna.

Sasa kikao kikuu cha kupitisha washindi kimekaa huko makao makuu, na fununu ni kuwa jina lake linataka kuondolewa kuwa imebainika kuwa kacheza rafu. Jamaa anayempigia debe akamtonya kuwa afike makao na wingi wa fitina. Jamaa sasa sio nyumba tu aliyoweka rehani bali na gari lake la thamani kubwa. Alifanya hivyo akijua, vyote hivyo atavirudisha pindi akishinda, sio mara yake ya kwanza.

‘Mke wangu vita hii ni kubwa, natakiwa niende makap na si chini ya milioni themanini, sasa wadosi wetu watatupatia nunsu yake, na yule jamaa mwingine kakubali kwa rehani ya gari letu wewe unaonaje?’

‘Sawa, lakini uwe mwangalifu, kwani nyie wanaume mkishika hela zinzwawasha, usije ukapitia mahala uksema upoteze mzwazo kidogo…’ mke wake akamuonya.

‘Acha hayo mke wangu ina maana huniamini tena, mimi wazo langu ni moja tu sasa kuupata huu ubunge kwa njia yoyote, ili tuweke mambo yetu sawa, kwani baada ya hapa, tunaachana na mambo ya siasa…’ akasema huku kamshika mkewe begani.

Mawazo yalikatishwa na mtu anayepita nje ya mlango , akaruka kama chura na kuhakikisha kuwa kafunga mlango. Akaanza kutafakari nini cha kufanya.

Akafikiria kuwa cha muhimu ni kumpa kitu kidogo mwenye hoteli ile, ile ule mwili wa binti ambaye sasa marehemu uhamishwe kwenye chumba kingine, na isijulikane kabisa kuwa alikuwa naye. Lakini…akakumbuka kuwa jana wakati wanastarehe na vinywaji alikuja kiongozi mmoja wa polisi ambaye naye alikuwa katika msafara wa kwenda Dodoma, na kaitka kujinadi, akajitambulisha kwake na mrembo wake, kuwa ni mmoja wa wapiga debe wake . Sasa hapa ipo kazi, lakini kwani si mpiga debe tu, yeye alikuwa na chumba chake na mimi change...

‘Ukiwa na pesa bwana kila kitu kinakwenda safi..’ Akajisema na kuelekea mlangoni , na wakati anatoka na kuhakikisha kuwa amekifunga ule mlango wa chumba, akakumbuka kuwa hajaangalia vyema pale alipoweka `briefcase’ yake iliyojaa mabulungutu ya pesa. Akarudi haraka, akaikuta palepale alipoiweka. Kwa kuhakikisha, akaichukua na kubonyeza namba zake za siri. Alishikwa na butwaa, ambayo hajawahi kuipata maishani mwake. Aliangalia ndani ya kabati kuhakkisha kuwa Ndiyo yenyewe au kuna nyingine. Briefcase ilikuwa nyeupe bila hata senti moja. Akapiga kelele kama mtoto mdogo. Aliirusha ile briefcase chini na kurukia kitandani akiwa kasahau kuwa anayemwendea ni marehemu, na alipomshika mwili ukamsisimuka na kurudi nyuma kama mtu aliyepagawa

‘Mungu wangu..’ kwa mara ya kwanza tangu aupate ulaji akamkumbuka muumba wake.

*********
Je kumkumbuka muumba kwake kutamsaidia, tuonane katika sehemu ya pili!

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Yasinta Ngonyani said...

natumaini wanaume wengi watajifunza. Sisemi ,mengi nangoje Sshemu ya pili maana kuna utamu hapa.......