Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, October 8, 2010

Usia wa mama waniweka njia panda-2

Kilikuwa kipndi cha wiki moja cha mateso, sio kwangu tu kwa mdogo wangu na mke pia walikuwa kama kuku walionyeshewa na mvua. Ile hali niliyowakuta nayo ilijieleza wazi, hawakuweza kupinga , na mdogo wangu akawa mkweli mbele yangu , alisema alishindwa kujizuia pale mke wangu alipokuja kumwambia kuwa kuna watu wanatembea nje, na wakati huo alikuwa akiangalia picha yenye matendo ya kikubwa ndani yake.


‘Shemeji alipokuja alishikwa na butwaa, akaniuliza naangalia nini muda wote huo wakati kuna watu wanatembea nje. Alipoona hiyo picha naye akavutika kuiangalia, ilifika mahali tukashindwa kuvumilia tukajikuta tunafanya dhambi…kaka nisamehe sana, mimi sijui ni nini kilinipata, kwani hata shemeji alilia baada ya kitendo kile hadi usingizi ukamshika, na kuzinduka wakati unapiga hodi.Nimejuta sitarudia kuziangalia picha za namna hii tena…’ akalia na kulia, lakini kwangu sikuona sababu ya kufanya walichofanya.

Nilipogonga mlango kwa nguvu walianza kuulizana kwa wasiwasi, kwani walijua kuwa nitakuja kesho yake, na hawakuwa na uhakika kuwa mimi. Nilisikia kishindo cha mke wangu akikimbilia chumbani kwetu na nikasikia mlango ukifungwa….

‘Nikuulize mdogo wangu, unampenda sana shemeji yako?’

‘Nitampendaje shemeji wakati ni mke wako, kaka nielewe kuwa sikukusudia kabisa na sijui …’ akalia sana.

Kila nikitaka kuinua mkono kufanya kitendo kibaya ikawa naiona sura ya mama yangu mbele, nikashindwa hata nifanyaje, nilitaka nitoe kipigo lakini naona ninayempiga ni mama. Nikaamua nitoke nje, nilipofika mlangoni nikamkuta mke wangu yupo nje naye analia, akisema

‘Atakuwa mgeni wa nani, ataenda wapi, amekosa nini kwa mungu, kwanini alifanya alichofanya…’ alilia kama mtu aliyefiwa

‘Sasa unalia nini wakati wewe ndiye uliyemfuata mdogo wangu chumbani kwake, ina maana ulikusudia au?’ nikajikuta nabwabwaja.

‘Mume wangu, siku ile nilipoahidi mbele yako kuwa ni wewe peke yako nikupendaye ilikuwa ni kweli tupu. Mimi nakiri kufanya kosa hilo, na sijui kitu gani kilinipeleka kwa mdogo wako, siijui kwanini nilivutika kuangalia ile picha, sijui kwanini nilishindwa kujizuia. Miezi mitatu yote nilikuwa siachi kukuwaza wewe, …naomba unisamehe na unipe adhabu yoyote ile ili moyo wako uridhike kuwa nakupenda…’ akasema huku analia.

‘Nakupenda…’ nikayarudia yale maneno na kuguna!

Nilimwangalia kwa Huruma nikamkumbuka mama yake na kauli yangu niliyoitoa kuwa sitamuacha, na hata kama nikimuacha atakwenda wapi, hana baba wala mama, hana ndugu yoyote, na hatima yake ni kuishia uchangu doa. Nikakusudia kwenda kuonana na mama ili nione kama atanishauri nini. Hili ni kosa kubwa nililofanya, kwani mama aliposikia hivyo shinikizo la damu likapanda na kulazwa hospitali.

Nilimuita mdogo wangu aje nyumbani haraka na alipofika alimuomba radhi mama na kumuomba aniombee msamaha kwani kosa alilofanya ni kubwa. Mama akatuita na kuniuliza je nini kusudio langu. Nilitafakari na kumwambia sina cha kufanya , sina kusudiio lolote baya, nimewasamehe. Na kwa vile tulishajenga kibanda tukaona mdogo wanguu aje akae na mama, ili amuuguze.

Mwezi ukapita na mke wangu akaanza kuumwaumwa. Akapimwa malaria akaonekana hana, tukahangaika karibu wiki, na siku moja tukiwa kwa dakitari akaniambia unajua kuwa mkeo ni mja mzito na inavyoonyesha ana mimba ya miezi miwili. Nikashituka kidogo, kwani kama ni miezi miwili basi hiyo mimba sio yangu. Nikaamua kumpeleka kwenye hospitali nyingine na wao wakathibitishs hilo.

Hatua hii ilinifanya niamue jambo kubwa la kumuacha mke wangu. Siku nilipomuita kumuelezea hili, akawa anaumwa sana, na ikabidi alazwe hospitali. Akiwa huko, aliniomba sana nisimuache kwani adhabu aliyoipata inatosha. Nikamuuliza anauhakika kuwa hiyo mimba ni ya kwangu. Alisema hajui , yeye anajua kuwa ni ya kwangu. Alisema kitendo walichotenda wao siku ile moja haiwezi ikaleta mimba. Nilijua kuwa ni ufahamu wake mdogo wa hilo.

Wanajamii, mimi nikasema basi, nitamezea na kujifanya hiyo mimba ni yangu, ili kuwaridhisha mama zangu hawa. Je hatua hiyo ni udhaifu au mnanishauri nini?

*****
Kisa hiki nimekileta ili kuona hatari ya kuwa na mikanda ya `ngono' au jamii ya naman hiyo na kuiacha mahali ambapo watoto, ndugu zako wanaweza kuiona! Inawezekana uliichukua kwa nia njema, kwani mingine inatoa mafunzo kwa wanandoa, lakini ikiingia mikononi mwa wasiositahilini hatari kubwa sana!
Nimewakilisha kwenu
 mimi: emu-three

5 comments :

Yasinta Ngonyani said...

Narudia tena kama kwenye kipande cha kwanza! kweli kabisa kikulacho kinguoni mwako. Wakati mwingine, ndugu/rafiki yako aweza kuwa ndiye msaliti wako mkuu, abiria chunga mzigo wako. Paka kutoka Panya kutawala. Duh!

Simon Kitururu said...

Stori hii imenikumbusha story ya kaka zake Michael Jackson Randy Jackson na Jermine ambao wote wamezaa na mwanamke mmoja Alejandra Genevieve Oaziaza Randy mtoto mmoja na Jermine watoto wawili. Huwa najiuliza hivi wakikutana kwenye shughuli ya kifamilia huwa Wanafikiria nini hawa wote watatu ,Randy, Jermaine na Alejandra.

Tukiachana na hilo:

Mimi naamini ndoa ya huyo jamaa imeshakufa kwakuwa si amini katika mapenzi ya hofu. Ingawa husemwa muda huponya maumivu ya moyo lakini kumbuka muda pia hugeuza majivu yenye joto kuwa baridi kabisa pia na wala haugeuzi majivu kurudi kuwa mkaa wa moto.:-(

Kuhusu mikanda ya kiburudisho murua: Katika hilo tusiruke kuwa U-SENSITIVU wa watu ni tofauti katika hamu za kukuna kipele ndio maana kwenye Daladala mtu utesekako kuna wapandao Daladala angalau kugusana na mtu kinguonguo na hilo huwa tosha katika kuzalisha kibaruti.

Kwa hiyo tukumbuke kuwa kuna watiwao majaribuni kwa kuangalia ISIDINGO idhaniwayo sio simulizi za NGONO PASE, kwa hiyo usishangae kugundua tatizo kwa wengi wala halihitaji watu waone mikanda ya ngono wakati tu mdada mtaani na viguo vyake vifupi inaweza kuwa kashapangisha mtu mori na kihitajiwacho ni mazingira tu na gazeti la udaku kufanya Mtu na Mke wa mtu kupandwa na jazba ya kukuna kipele kwa kuibia kitu ambacho inasemekana kinautamu wake tofauti kwa kuwa kwanza- MNAIBIA.

SAmahani nimeandika harakaharaka na samahani kama mtiririko wa hoja na nachoitaka kusema kina udhaifu katika kueleweka!

mumyhery said...

mtihani huu ni mgumu sana, radhi ya mama, radhi ya mkwe!!!

Mzee wa Changamoto said...

Mmhhhhhhh!!!
Nasikia aibu kusema nasom hii darasani. Sasa ntarejea kutoa maoni sasa.
Ndio naanza na ndio wa hapa mie.
PamoJAH

emuthree said...

Nimelikumbuka hili tukio,naona limetokea tena kwa jamaa mmoja