Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Monday, September 27, 2010
tutaonana mungu akipenda-5
Mchumba wangu alinipenda sana, hilo sikuwa na mashaka nalo, kwani siku aliponitamkia kuwa anataka mimi niwe mchumba wake, alinipa Zawadi ya nyumba, hati na kila kitu kiliandikwa jina langu, na siku ya kunitamkia kuwa tufunge ndoa alinipa Zawadi ya gari, kila kitu kwa jina langu. Huo ni upendo wa thamani, naweza kusema ni kwa vile ukoo wao ni matajiri, lakini tabia yake na mienendo yake ilikuwa haina ubaya wowote, kwani uchunguzi wa kina ulifanywa na familia yetu ikagundua kuwa hana tabia mbaya, na alikuwa akinipenda kweli na kwa dhati.
Mimi nilikuwa na Bahati ya kuchumbiwa na watu wengi na wote walikuwa Watoto wa matajiri, niliwakatalia na wengine niliwapenda kiasi kwamba nilishindwa kuamua, lakini mwisho wa siku nikaamua anioe huyu.
‘Nakuahidi hutajuta kwa kunikubalia mimi, nitakupenda na kukuenzi hadi mwisho wa uhai wangu’ hii ndio ahadi yake aliyonipa siku akinikabidhi ufungo wa gari kama Zawadi. Alikuwa kila saa akinipigia simu , kama hakuwahi kuja nyumbani kwetu, kwahiyo hakukuwa na dalili yoyote ya unafiki.
Mimi nilimwambia mama twende hadi kwa bwana harusi, mama akasema hayo sasa yamevuka mpaka, tukaenda hadi nyumbani kwao ilishafika usiku wa saa mbili, tulipofika, wazazi na jamaa ambao walikuwa wamekutana na maandalizi ya harusi yalikuwa hayajafungwa wakatukaribisha na wao wakasema hawana taarifa yoyote na wamejaribu kila wawezalo hawajui wapi mtoto wao alipokwenda.
Basi tukaamua tuondoke, wakati tunatoka maeneo ya familia ile, akaja jamaa mmoja akasema anahisi wapi tunaweza kwenda kumuona huyu jamaa. Akasema jamaa huyu ana nyumba moja aliinunua siku za karibuni, akiwa na nia ya kunipa mimi kama Zawadi nyingine, lakini alisema ataifanya kama siri hadi tutakapomaliza sherehe za harusi. Mimi nikamuambia mama lazima twende huko. Mama alishachoka , lakini hakutaka kuniacha peke yangu.
Tulifika maeneo hayo saa nne za usiku, na tulipofika kwenye hiyo nymba tukakuta taa zinawaka na mziki wa taratibu unalia toka ndani. Hapo mama akanishauri turudi kwani alihisi nitakuta yatakayoniumiza zaidi. Nikamwambia, mimi nimejiandaa kwa lolote, ninachotaka nikuhakikisha kwa macho yangu kuwa je mwenzangu kaamua kunisaiti.
Tukafika getini na mlizi alishikwa na butwaa akshindwa hata kutuzuia, tukaelekea kwenye mlango na kukuta haujafungwa. Maja kwa moja, tukaingia ndani, na barazani tulkuta meza imeandaliwa lakini vyakula vililiwa kidogo tu. Mama akasimama, akaogopa kuendelea zaidi, nikamwambia anisubiri pale, mimi nikaelekea juu, ambako nilihisi ndipo kwenye chumba, na ndip mlio wa mziki ulikuwa unatoka.
Nilianza kutetemeka kwa woga, lakini nikajipa moyo! Hata hivyo maswali mengi yalinijia kichwani na kujiuliza, je kama nitamkuta ni mume wangu yupo na mtu nifanyeje? Na kama yupo na rafiki yangu ambaye tuna udugu fulani nichukue hatua gani, hapana, awe yeye au nani, mimi nitapambana naye nakuwaonyesha kuwa mimi nami ni mwanamke mwenye uchungu, potelea...nikavuta hatua hadi kwenye ule mlango wa chumba….
Je nini kitatokea!
NB.Kabla ya kuendelea mbele na kisa hiki, hebu niwaulize wadau na wapenzi wa blog hii, kuna yeyote aliyewahi kukutana na tukio kama hili, au kushuhudia ndugu yake akifanyiwa hivyo. Nauliza hivi kwasababu uchungu, na taabuu anazozipata mtu aliyeachwa kwenye mataa wakati anamsubiri mwenzake aje afunge naye ndoa, na asitokee, sio rahisi kuuelezea kwa maneno.
Ni mimi: emu-three
10 comments :
Duu! m3, hii ni kali kuliko, usiombe yakukute wewe.
Tunaomba utumalizie kisa hizi usiishie hewani.
Kwa kweli kinasisimua sana.
miram3, eti leo inafikisha mwaka? Tujulishe wadau. Nimeinyaka kwa michuzi. Lakini atubainia haifunguki. Mwambie michuzi aache kubana bwana.
HAPPY BIRTHDAY miram3 Kwa kufikisha mwaka.
Mungu azidi kuinua ijulikane duniani kote na wadau waongezeke.
UMEBARIKIWEA MIRAM3.
Miye namjua aliyewahi kumuacha mtu ki hivyo na kwa bahati mbaya ni ndugu yangu!:-(
Ningependa kweli kusikia upande wa pili wa stori. Kwa kuwa daima kumbuka kwenye wawili kuna pande mbili za ZE STORI na hapa tunasikiliza upande mmoja .:-(
malizia story plz mana unaniacha kila mara nachungulia blog yako i wish ingekuwa part one and two na cyo mwendelezo cjui itafika mpaka ngapi
Jamani hizi stiri zinatoke kweli?mbona inatia oga sana!kwasababu hapa mtu anaweza hata kupoteza maisha.Duh!!
Kiasa hiki kwa kweli kinasisimua na kusema kweli sijawahi kushuhudia. Nilipoanza kusoma na kusoma na kusikia katika masikio yangu kuwa msichana alipewa zawadi nyingine baada ya nyingine hapa nikaanza kugundua kuna kitu kinatokea maana mtu ukimpenda mtu basi unampenda mtu kwa dhati sio kumpa hiki na kila huo si upendo wa dhati.....ngoja niache nisubiri muendelezo....
Ndio maana nikasema `uchungu wa matesoo haya sio rahisi mtu mwingine kuujua, mpaka umtokee, au auone kwa macho.
Stori hii ni ya ukweli na aliyenihadithia ndiye aliyepambana na dhahama hii! Na wapo wengi yaliwakuta, labda kama wapo hewani wanaweza kutuhadithia kama hawatajali!
Leta kipande cha pili. lah!
Jamani haya mambo yapo katika jamii yetu kwa kweli. Kama anavyosema m3, si rahisi mtu kuadithia wengi wao.
Hata mimi yalishamtokea ndugu yangu yamemtokea, lakini sijui kisa chenyewe kabisa. Si unajua hizi ndoa za kiisilam. Watu wameandaa vyakula, madufu na kaswida wana vyuoni wanapiga madufu, vigelegele na shamrashamra za harusi na Bi harusi amepambwa amewekwa ndani anamsubiri Bwana harusi lakini hakutokea mpaka kabisa.
Hebu fikiria aibu gani amekukuta, na watu ndio wamekuja kusherehekea harusi yako.
Kwa hivyo jamani hayo matukio yapo. na yanamkuta binadamu, sio wanyama na wala sio stori tu. Ni 'TRUE STORY' USIOMBE YAKUKUTE HAYO UTATAMANI KUFA. NA KAMA UNA ROHO NYEPESI UNAWEZA UKAJIUA
Nashukuru P, kwa kutupa ushahidi , ngoja niendeleze sehemu inayofuata, nawaomba msichoke kwani ni kisa kirefu kidogo, na, najaribu kufupisha kadri ninavyoweza, ili nisiharibu ujumbe wake!
Karibunituendelee sehemu inayofuta!
Post a Comment