Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, September 24, 2010

Onyo, tahadhari kabla ya hatari


‘Ndugu yangu jirani, nimejiwa na wageni, na kama ujuavyo nina vyumba viwili tu, sasa mimi naomba kama inawezekana unisaidie watoto wangu hawa wawili waje walale kwako?’ Ilikuwa sauti ya Huruma ya jirani yangu.


‘Mhhh, nashindwa nikuambiaje, lakini sina budi wewe walete halafu nitaangalia watakavyolala na wenzao humu kwangu, lakini wote si mabinti?’ nikamuuliza kwa wasiwasi.

‘Ndio siunajua tena mimi nina mabinti watupu, huyu mdogo ni mvulana tutalala naye hakuna tabu’ akasema jirani yangu huyu , huku akipumua kwa kukubaliwa ombi lake hilo.

Mimi nilibaki nikiwaza, jinsi gani nitakavyowachanganya na watoto wangu, kwani kwa vyovyote iwavyo, ni vyema wageni wakirimiwe vyema. Nilikumbuka jana kwenye runinga, walipotagaza jambo lililonitia wasiwasi wa kukirimu wageni.

Habari hiyo ilisema kuwa `mjomba mtu kamnajisi mtoto wa miaka minane’. Ilikuwa habari ya kusikitisha sana, kwani mtoto huyo wa miaka minane aliamua kwenda mwenyewe kumuona mkuu wa polisi wa mkoa na kutoa shitaka lake. Alisema kuwa aliogopa kuwaambia wazazi wake kwani wangeliweza kulimaliza kindugu na haki isingelitendeka.

Mtoto huyo wa miaka minane alikuwa akilala na momba wake huyu(mdogo wa mama yake). Usiku mjomba mtu alikuwa na kazi ya kumuingilia mtoto huyo wa kiume na kumharibu sana sehemu zake za nyuma. Imeeleza kuwa mtindo huo uliendelea karibu siku kadhaa, na mwisho wa siku Yule mtoto akamsimulia rafiki yake.

Rafiki yake akamshauri aende kushitaki, na kumwambia ni bora akamuone mkuu wa polisi kwani huko haki itakuwa imetendeka! Mtoto huyo alifanya hivyo, na tunaimani kuwa hki itatendeka. Na tungewaomba watu wa huko, Moshi kama sikosei , mlifuatiliye hilo swala na kuhakikisha huyu kijana aliyemharibu mtoto wa dada yake anapata adhabu inayostahili!

Nia ya kulileta hili swla hapa ni kutoa onyo na tahdahari kuwa sasa hivi dunia imekwisha. Ule udugu, ule upendo wa kuhurumiana umeingia doa. Kama atakujia ndugu, jirani au rafiki mpe kitanda chake na kama unauwezo mpe chumba chake. Usifanye makosa kumlaza ndugu yako, jirani yako, au yoyote Yule na watoto wako. Huwezi jua nini kinafanyika usiku? Wewe umalala kumbe mtoto wako anapata shida. Ni dhambi kubwa sana.

Ile enzi tuliyosimuliwa kwenye vitabu vitakatifu, enzi ya Sodoma na Gomara, ipo machoni mwetu. Ni visa vingapi vimetokea ambavyo vinadhihirisha haya! Hatuoni wanaume waliojiweka kama wanawake(mashoga) wakizidi mitaani! Je hujasikia ndoa za watu wajisia moja zikitangazwa na bila aibu, na watu wanaongeaa na kucheka kwa dhihaka! Jamani hivi tunakwenda wapi! Je ile gharika iliyoongelewa hatuikumbuki, au tunaona ni visa vya pauka pakawa?

Onyo na tahadhari, usilogwe kufanya kosa hilo sasa, kwani `utandawazi na ibilisi wameiweka dunia katika mahala ambapo tusipoangalia kizazi chetu kitatulaumu! EWE MZAZI, chukua tahadhari, ni bora ulaumiwe kuliko kukiangamiza kizazi chako!

Hilo ndio wazo langu la leoo Ijumaa


Ni mimi: emu-three

5 comments :

Anonymous said...

NDIOhata mimi nimeisikia, kumbe wachaga nao wamo...mmh, jamani sasa utamwamini nani, manake yule alikuwa mjomba mtu, mdogo wake mama...fikiria mama, ndio huko tunasema wana uchungu na familia, kwasababu yeye ni sawa na mama, ila yeye kazaliwa dume...
Jamani hata ukiwadadisi hawa walioharibikiwa watakuambia kuwa waliosababisha hivyo ni ndugu tu wa karibu...
Mtoto akishabaleghe, usimchanganye na wengine, hilo walilijua tangu enzi za mababu, kwetu huwa wanajengewa vibanda vyao pembeni !

Simon Kitururu said...

Dunia inapokwenda yangu macho!:-(

EDNA said...

hivi wajomba huwa wanakuwa na matatizo gani? mara nyingi wao ndio wanatuhumiwa kubaka watoto wa dada zao.Hii dunia imekwisha Eee Mungu na utuepushe na haya mabalaa.

mumyhery said...

hali inatisha jamani!!!

Yasinta Ngonyani said...

Dunia sasa imekwisha kwa kweli hakuna uaminifu kabisa. Niliwahi kusikia kuwa dada na kaka iliwahi kutokea walifanya jambo kama hilo. Sijui mwisho wake ni nini kama sio ndo mwisho wa dunia. Mtoto wa dada yako kwa kweli inasikitisha sana na ni unyama kabisa. Sijui wanaume ni watu wa aina gani???