Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, September 28, 2010

Tajiri na mali yake, masikini na watoto wake!

`Hivi kweli mimi mnanionaje wenzangu?’ hili lilikuwa swali tata kutoka kwa rafiki yangu aliyenitembelea, nilishindwa nimjibuje, lakini kwa vile ni mtu wa heshima , tajiri na anayejulikana kila kona, ikabidi nimtupie sifa kedekede.


‘Hapana, mimi nimechoka na hizoo sifa na najua nyingii hazina ukweli, watu wananisifia na kuifanya wananipenda kwasababu tu labda wanavyoniona kuwa ni tajiri. Lakini nikuambie ukweli rafiki yangu, sina raha kabisa. Hutaamini nikisema hili, na watu wengi wanafikiri kuwa tajiri ni raha, hapana, …’ akasema huku anaiangalia saa yake ya dhahabu.

‘Kwanini unasema hivyo, kwani huamini kuwa sifa hizo ni zako, na ni ukweli mtupu…mimi kwa vile sipo kwenye kundi la utajiri nashindwa kukubaliana na usemi wako, labda unielezee ni nini kinawakwaza matajiri’ nikamuuliza huku nikitamani huo utajiri wake anaouona haumpi raha. Kwangu mimi nilihisi matajiri wengi wanapokuwa katika hali hiyo, wanataka wafanye kila kitu `kitajiri’ sasa hali hiyo ya ushindani inawapa shida.

‘Sasa hivi ni miaka ishirini tangu nimuoe mke wangu, na binti yetu sasa, karibu anafunga ndoa! Ina maana akiondoka kwenda kwa mume wake, tutabakia mimi na mke wangu na wafanyakazi wa ndani. Huoni kuwa hii kwangu ni huzuni kubwa. Sina mtoto mwingine zaidi ya huyu binti, huoni kuwa ninakosa kitu muhimu katika maisha, watoto…watoto …watoto…’ alirudia neno hili watoto mara nyingi kama vile mtu anayekariri hizo herufi mpaka nikaona nimkatishe.

‘Kwani mimi nilidhani kuwa mumependelea kuwa hivyo, kwani wengi hawataki kuwa na watoto wengi, hasa matajiri, kwani walisema wahenga, tajiri na mali yake , masikini na watoto wake…’nikasema lakini akanikatisha.

‘Asikudanganye mtu, hakuna tajiri asiyependa watoto, angalau watatu au wane, lakini hawapatikani. Na sio kuwa hawapatikani kwa kuwa matajiri hawa hawana uwezo wa kuzaa, hapana, wanauwezo kiafya lakini mimba hazitungi, hili ni tatizo kubwa kwangu…’ akatoboa siri.

‘mliwahi kwenda kwa wataalamu..’ nikamuuliza

‘Labda mtaalamu ambaye sijamuendea ni mganga wa kienyeji, na kama itabidi hivyo nitamuendea’ akasema kwa dhati.

Moyoni mwangu nikataka kumkanya kwa kukumbuka kisa cha tajiri mmoja aliyetaka watoto kama yeye, akamwendea mganga wa kienyeji, na mkewe. Walipofika huko, mume mtu akawa anaambiwa abakie nje wakati mke anafanyiwa dawa. Unajua ilikuwaje, Yule mganga akibakia na Yule mke anamnyeshwa dawa Fulani za kumpumbaza na kinachofanyika huko ni shughuli za mke na mume, hadi Yule mke akatunga mimba, na mimba si ya Yule tajiri bali yam ganga.

Alipozaliwa mtoto sura kama yam ganga, lakini Yule mganga alipojua haya alipotea kabisa, na huyu tajiri kwa vile hakuchukulia manani , yeye aliona ni dawa za mganga zimefanya kazi, na siku moja akaamua kwenda kumtembelea Yule mganga. Na lipofika, aligundua kuwa sura ya Yule mganga inafanana moja kwa moja na Yule mtoto wake. Alichofanya ni kibaya zaidi kwani baada ya siku kadhaa Yule mganga alikuwa ufukweni akiwa kauwawa, na wengi walihisi kuwa huyo tajiri ndiye aliyemuua, lakini hakuna ushahidi wowote uliowahi kupatikana.

Kisa hiki kikanifanya nimuonye rafiki yangu huyu kuwa kama kweli amepima hospitali na kuonekana hana tatizo yeye na mke wake, kinachotakiwa nikumuomba mungu ipo siku watapata mtoto, na mtoto halizimishwi kupatikana na kama watahitaji mganga wa kienyeji , inabidi wachukue tahadhari kubwa sana.

‘Mimi sio mtoto mdogo hayo yote nayajua, ikibidii kwenda huko, simpi nafasi huyu mganga kumchezea mke wangu, kama ni dawa anipe, nitampa mimi mke wangu…’ tukacheka, lakini usoni mwake kulionyesha huzuni kubwa, sana.

Ama kweli utajiri sio raha zote, mali nyingi bila watoto zina faida gani? Haya labda turejee huo usemi kuwa tajiri na mali yake na masikini na watoto wake…hiyo siri aijua muumba pekee!

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Hata mimi nashangaa sana, matajiri wengi hawazai watoto wengi, kumbe sio kuwa hawataki, bali...pesa mbele kuliko mambo mengine!
Lakini pia nafikiri ile tamaa ya mali inamfanya afikiri kuwa akiwa na watoto wengi watagombea mali yake, sasa akipiga mahesabu watoto wawili akiwagaia urithi, bado atabakiwa na mali kibao
Lakini yote tisa Muumba ndiye ajuaye yote