Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Friday, September 17, 2010
tutaonana mungu akipenda-2
Niliamua kwenda kijijini kwa wazazi wake kujua zaidi, lakini wao walijifanya kushangaa, na kusema kuwa wao wanachojua nipo na mtoto wao. Lakini mmoja wa ndugu zao akaniambia kuwa wao waliambiwa huo mpango na ulifanyika kwa siri, baada ya wazazi kushindwa kumshawishi binti yao.
Niliposikia hivyo nikawa sina jinsi, nikaamua kuishi kivyavyangu, sikutaka tena kusikia habari za mke. Wazazi wangu walinishawishi na kuniahidi kuwa watanitafutia mke mzuri zaidi ya Yule, lakini sikuwaelewa. Nikakaa hivihivi mwaka mzima, na hali ya kiafya ikawa inazorota, kwasabbu ya mawazo na upweke.
Siku moja nikiwa ndani ya daladala, alikuja binti mmoja akakaa karibu yangu, wakati basi linaondoka nikashangaa kumuona analia na kujificha uso wake na viganja vya mikono yake , huku akifjaribu kufuta macho yake na leso iliyokuwa imelowana machozi. Nilihisi kuwa labda amefiwa, nikaona kiubinadamu nimpe pole hata kumliwaza, kwani wote tunapitia majozi kama hayo.
‘Pole sana, dada yangu nahisi umefiwa na mtu unayempenda sana, usijali wote ndio njia yetu..pole sana..’
‘Nani kakuambia nimefiwa, nyie mnadhani uchungu nikufiwa tu, tafadhali kaka niache na yangu’ akasema Yule binti kwa upole, lakini Maneno yake yalikuwa machachu kama shubiri. Nilifyata mkia na kukaa kimya, nikijisemea moyoni, hawa ndio walewale wanawake na tabia zao, chuki , uwongo , na usaliti…sina muda nao tena!
Basi lilisimama kituo kimoja kabla ya kufika mwisho, na Yule binti akashuka kwa haraka, nilipoangalia pale alipokuwa amekaa nikaiona simu ya gharama sana, nikaichukua na kuchungulia dirishani nikiwa na maana ya kumuita kabla hajafika mbali. Nilimuona akikatisha barabara nikamuita kwa sauti kubwa , lakini hakujali na akawa kama vile anakimbia kitu na kueleka anapopajua mwenyewe.
Nikaona jambo jema ni kutafuta uwezekano wa kuwasiliana naye, nilpoikagua ile simu nikakuta sehemu alipoandika maelezo yake na kama simu ikipotea , muokotaji anatakiwa awasiliane na nani, yalitajwa majina matatu, halafu tahadhari kuwa hata ukiamua kuichukua hutaweza kuitumia kwa m uda mrefu kwani haki zake zimenakiliwa na kuhifadhiwa kwa watengenezaji. Wataisimamisha kutumika na wanaweza kumfuatulia mtumiaji mpya.
Sikuyajali sana maelezo yake nikawapigia wale waliotajawa kwenye ile simu na wao wakanielekeza wapi binti huyo anapoishi. Nikafunga safari hadi kwenye nyumba niliyoelekezwa. Ilikuwa nyumba nzuri , na imezungushiwa geti kubwa, nikaingia na kukutana na mlinzi ambaye alinieleza kuwa mwenye nyumba hiyo kaacha maagizo kuwa hataki usumbufu wowote. Nikamshawishi Yule mlinzi mpaka akakubali.
Ilikuwa kazi sana kwa yule binti kukubali kuongea na mimi, hata pale nilipomkabidhi simu yake, aliishia kunishukuru na kusema hajisikii kuongea na mtu yoyote, nikaondoka. Kesho yake akanipigia simu kuwa kama sitojali niende kwake. Sikupenda kabisa kuanzisha mahusiano na mwanamke yoyote, na kwa mualiko ule niliupokea kwa shingo upande, nikiwa na hamu ya kujua tu, ni nini kilichomkuta Yule binti.
Mualiko ule ukazaa mialiko mingine, hadi mwisho wa siku tukawa marafiki. Lakini hakutaka kabisa kunisimulia kilichomsibu. Alisema hataki kumsimulia mtu kwani akifanya hivyo atatonesha majeraha yaliyokwisha anza kupona.
Ila baadaye urafiki wetu ukakua na kuishia kuoana na tulikuja kujua kuwa kweli sisi ndio tuliositahili kuoana tangu mwanzo. Tulikaa naye tukajaliwa Watoto wawili.
Siku moja wakati tupo mitaani kariakoo, tukakutana na mama mmoja akiwa na hali mbaya sana. Unajua hali mbaya, basi huyu ilizidi unavyojua wewe. Nafikiri alikuwa akiumwa, kwani mwili wake uliisha na alikuwa na madonda, akatuomba msaada. Nikatoa hela kumpa, wakati namkabidhi…Mungu wangu, nilipatwa na mshituko wa ajabu na mwili ukaniisha nguvu, sikuamini macho yangu, niliyakodoa kuhakikisha kuwa kweli huyu ni binadamu, au ni...ile hela niliyoshika ikanidondoka mkononi, huku mwili mzima ukiisha nguvu...hapana..haiwezekani...!
Je jamaa aliona nini cha ajabu. Naona muda umekwisha hebu tuishie hapa, kwani hata mimi nina hamu ya kusikia nini alichokiona huyu jamaa, mapaka akaishiwa nguvu!
Tuonane baadaye kidogo!
3 comments :
Eeeh! umekatisha palikuwa patamu hapa naweza kuhisi ni nini aliona lakini nasubiri hiyo baadae kidogo.....
Mmmmmmm! Ni patamu kweli, haya tusubiri.......
Aaaaaah, wewe kwanini umekatisha...aah, palikuwa panakwenda kulekule nilipodhania...mmmh, aisee hongera, hivi wewe umewahi kutunga kitabu? au kutunga movie, mmmmh, aisee, i wish ungekuwa mtunzi wa movie, mbona zingetoka..anyway, naomba usikawie kumalizia, manake nina usongo, usongo...na huyu...
Post a Comment