Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Friday, September 17, 2010
Fimbo na haki za watoto
Hakuna mzazi anayependa kuona mtoto wake anapotea, kwa minajili hiyo kila mmoja anajaribu kila awezalo kumuweka mtoto huyo katika njia anayoiona kuwa ni sawas. Kuna watoto wakielezwa mara moja wanaelekea, na kuna ambao hata upige gitaa inaingia sikio hili na kutokea sikio jingine, anaitikia sawa , lakini kesho au kesho kutwa anarudia kosa lilelile. Kwa wazazi waliokutan na haya mtaniunga mkono, au labda ni watoto wetu tu…!
Ni kweli mtoto hashindiki kwa mzazi, na samaki hukunjwa angali mbichi, je kama akiwa mbichi umemueleza na kutumia hekima zako zote, kwa mdomo hajasikia utafanyaje? Hilo ndilo swali muhimu kwa wadau , nimeulizw, nami naliuliza hapa kijiweni hasa kwa wale wanaopinga kabisa kiboko kisitumike!
Kuna usemi unaosema, `mke hupigwa na ukanda wa khanga, na mtoto huchapwa ` kwa uchelewa…’ una maana pana na sio kama unavyosomeka. Kuchapa au kupigwa hapa hakukulenga moja kwa moja `kuumiza’ bali ni busara katika kuwekeana sawa! Naomba tulielewe hivyo, hasa kwa akina mama, msije mkanidhania vibaya!
Labda niwaelezee kisa kimoja kilichonitokea nikiwa mdogo. Siku moja tulikuwa tukilinda mpunga wa babu tukiwa wadogo chini ya miaka saba hivi, na mara akatokea msichana mdogo wa umri wetu. Hatukumsemesha kwani tulikanywa na babu tusiwabughuzi watoto wa watu wanaokuja kuteka maji karibu na shamba letu la mpunga, ambako kulikuwa na kisima karibu yake. Yule binti akaturushia mawe, na jiwe moja likanipiga kichwani.
Hasira zikanipanda na kumwambia neno ambalo toka leo nashindwa kulitamka mdomoni, lakini kwa maandishi nitalisema, samahani lakini. ‘Wewe `msenzi’ nini..mbona unatupiga mawe…’ akacheka huku anateka maji na baadaye akaondoka, na mara kama nusu saa baadaye akarudi na baba yake, tukaitwa na Yule baba yake. Tulimpomkaribia tukakuta ana fimbo, tukajiuliza kulikoni.
‘Kwanini nyie mumemtukana mwanangu…’ akafoka yula baba
‘Yeye katuanza kwa kutupiga mawe, lakini hatu…kumtukana…’ mwenzangu alikuwa muongeaji sana akasema.
‘Yaani nyie mnamfanya huyu mwanangu kichaa, awazulie tu uwongo, ngoja nitaongea na babu yenu, kuwa badala ya kulinda mpunga mnawatukana wenzenu…’ akasema na kuondoka. Tulibaki tumeduwaa, na tulipomtizama Yule binti akiondoka na baba yake, alitugeukia na kubenua mdomo wa kutuonyeshea ishara kuwa tutaipata…siunajua ule mbenuo wa mdogo wa kukudhihaki.
Kwakeli tuliogopa, na tulichelewa hata kurudi nyumbani kwani tunamjua babu alivyo. Tulipofika nyumbani tukakuta Yule baba keshafika, na ….
‘Hebu niambieni kwanini mlimtukana mwenzenu’ akaanza kusema babu kwa upole, huwa ndio kawaida yake
‘Babu huyu alikuja kuteka maji, tulikuwa kimya, mara tukasikia mawe yakirushwa na moja likanipiga hapa kichwani, unaona hiki kinundu, mimi kwa hsira nika…mwambia …she-she..nzi..’
‘Nini, nanii aliwafundisha kutukana, …hebu rudia hilo neno tena, ulisemaje’ babu akapandisha hasira
‘Nilimwambia shenzi…tu sikusema tusi lolote..’
‘Na kwa ujinga wako unarejea kutamka hilo tusi sasa wewe utapata bakora ili iwe fundisho…’
Nilipata bokora tatu , na bokora tatu za babu sio mchezo, anakuchapa nyuma kwenye paja, na wakti huo tunavaa kaptura. Tukapewa mawaidha kuwa neno hilo ni tusi, tusirudie tena. Toka siku hiyo hadi leo, hilo neno naogopa kulitamka mdomoni.
Nataka kuwaonyesha mfano tu, kuwa wazee wetu walikuwa na busara, kuwa kuna wakati kiboko hutumika kidogo ili kukuwekea kumbukumbu ya kutokutenda tendo Fulani, hasa wanapokukanya mara mbili bila kusikia, na wengi tuliopitia huoo umrii tuna visa vingi ambavyoo vilitokea na kupata viboko ,na kutokana na viboko hivyo tulijifunza na hatukuweza kurudia tena kosa kama hilo.
Sasa tunaakwenda na wakati, viboko niukiukwaji wa haki za watoto, sawa, je kipi jema, mtoto kuendelea na kosa ambalo huenda umemkanya mara nyingi bila kusikia au kumchapa ili aliache, na je ukimwacha na kukua na ujeuri huo hatujakiuka haki za kumlea? Ndio wazo langu la leo wadau, tuchangie!
Ni mimi: emu-three
7 comments :
Mimi napinga moja kwa moja kutumika viboko, kwani ni uzalilishai wa mtoto. Nasema hivi kwasababu wewe mtu mzima ukikosa, ili uhukumiwe inabidi ipite kesi kwahiyo unaweza kufungwa au kuchapwa viboko. Sasa huyu mtoto kapitia mahaka ganii mpaka umuchape.
Chukulia mfano wako ulioutoa hapo, mbona ulichapwa hata bila kosa..kwasababu haki haikutendeka, hakuna mahaka hapo...
Wewe kama mzazi unaweza ukatumia hasira bila kutafakari, ili haki itendeke kuwa na mahakama za watoto..
Napinga viboko moja kwa moja...nilichapwa sana na sikuona manufaa yake zaidi ya `kuwa na adabu ya kuogopa'
Hata mimi napinga kabisa viboko kwani ni kweli kabisa mtoto anakuwa tu mwoga na ahakuna anachojifunza kwa kweli. Kuna njia nyingi za kumsaidia mtoto .Je wewe ulipotukana hilo tusi ilikuwa mara ya kwanza au?
Mkuu, pongezi kwa mada nzuri na yenye kujenga. Kwa kweli huu utandawazi umeshatuharibu kifikra. Mimi binafsi wanangu wakiboronga lazima wale kichapo angalau kidogo.
Binafsi kama siyo kichapo nilichokuwa nikipewa na mama wakati nikifanya madadu, nadhani leo hii ningekuwa katika ulimwengu tofauti na ninaoishi sasa.
Sio kwamba napinga, ila nami ningependa kutoa mchango wangu, kwa mdau wa kwanza aliyeona kuwa ni vyema pia kabla ya kumuadhibu mtoto angepelekwa mahakamani ili haki itendeke, kwani huenda mtoto huyo akaadhibiwa hata kama kosa hana.
Nionavyo mimi mtoto kama mtoto bado yupo kwenye milki ya wazazi, mahakama yake ipi kwenye malezi ya mzazi wake, kwani bado akili yake haijakomaa `kiutu uzima’ na kutambua jema na baya. Mara nyingi kuna usemi unaosema mtoto anazaliwa akiwa na `tabia njema’ kinachomuharibu ni kwanza wazazi wake pili mazingira anayokulia. Kama mzazi huwezi kukwepa jukumu la ulezi, kwani mtoto upendo na usikivu wake unamjali sana mzazi wake.
Mimi wakati nikiwa mdogo mama yangu(sasa ni marehemu, mwenyemungu amlaze mahali pema peponi) alitufundisha , na hakutuambia kwa maneno, ilikuwa viendo tu, kwa mfano tunapokwenda kuwatemble ndugu, tukikaribishwa chakula, akituminyia jicho Fulani, tunajua kuwa haturuhusiwi kula, tutasema `tumeshiba’ hata kama tutabembelezwa vipi hatuwezi kula. Pia kulikuwa na ishara ya kufinywa, akikuoana hujamtizama, atakufinya, na ile ishara kuwa kwanza hutakiwi ule, pili utafute upenyo wa kuondoka hapo!
Sasa ishara hiyo ya kufinywa kuna mzazi aliijaribu kwa mwanae kwenye zama hizi za utandawazi , mtoto alilia na kusema `mama mbona unanifinya’ kwa sauti, mzazi alitahayari aisijue la kufanya. Hii ni kuonyesha kuwa kama mzazi unaweza ukajitahidi sana kulea, lakini bado kuna mazingira yanayokuzunguka, haya yanakuwa kikwazo kikubwa kwa malezi unayoyataka.
Mtoto atakutana na watoto wengine wenye malezi tofauti, kwenye madaladala , na kama ujuavyo makondakita wetu matusi ni nje-nje , wanagombana wao wanamtukama mzazi wa kike…sasa hebu jenga hii picha uone jinsi mtoto huyu anavyokulia katika maisha ya utata, je afuate ya mitaani au afuate ya wazazi, na je mbona watoto wengine wanafanya hivyo yeye kwanini azuiwe, je….anakuwa na maswali mengi yasiyo na majibu rahisi. Ndio maana wewe kama mzazi unatakiwa utafute njia ya ziada ya kumfundisha ili `aelewe’ ubaya wa tabia Fulani, ikibidi `umfinye’ ikishindikana , mchape kidogo…
Dada Yasinta, kosa lile kwangu, sina uhakika kwasababu mtoto, ila sikuwa na tabia ya ugomvi au matusi, na neno lile lilinitoka tu, kwasababu nilisikia watu wakilitumia, na sikuwa na wazo kuwa ni neno baya, hadi nilipoadhibiwa….
Hii ni mada nzuri sana kuijadili kwa kina. Tusije tukadanganyika na hii utandawazi,suala la kumkea mtoto ni muhimu pale atendapo kosa. Lakini pia hii haimanishi ukatili uliokithiri wa mzazi kumcharaza mtoto bakora kupita kiasi, hata pengine bila kujali ni sehemu gani ya mwili inaadhibiwa. Kwa mfano ni hatari kumpiga mtoto au mtu yeyote sehemu za usogoni, kifuani karibu na moyo n.k
Waswahili walisema hasi ni hasara, kwahiyo wazazi wanapaswa kuwa waangalifu na adhabu watoazo kwa watoto wao.
Mwisho naupinga kwa nguvu zote kitendo cha mtoto kupiga simu polisi eti amekemewa na baba au mama. Hapa Ulaya huu ndiyo mtindo.
Nashukuru sana Mkuu Malkiory kutupa live za Ulaya, na hii itatusaidia kuona faida na hasara za ulezi wa Ulaya na huku.
Je tukiendelea na ulezi wetu tuliozoea, wa kukemea na kuchapa kidogo kuna faida au hasara ukilinganisha na Ulaya ambako hawachapi na mtoto? Tunaomba live zaidi kutoka huko...hukoooo!
Ndugu Emu-three,unajua watu tumetofautina katika hili, kwanini? kuna kundi hili ambalo limekwisha tekwa na utandawazazi, hawa hata upige mayowe namna gani watakupinga tu kuwa kutoa adhabu kwa mtoto ni ukiukwaji sheria na haki ya mtoto.
Sasa nikuambie kidogo kuhusu mimi mwenyewe. Nilipokuwa mdogo, nilikuwa mtukutu sana na nilikuwa na hasira ya ajabu. Huwa nikikasirika nilikuwa sijui cha shangazi au mjomba au binamu,nilikuwa hodari na mwepesi wa kurusha mawe.
Yote haya yalifikia kikomo kwasababu ya mama yangu mzazi, ambaye alikuwa akinitandika na kamba miguuni bila msaada wa mtu yeyote kujitokeza kuniokoa.
Lakini nilichompendea yule mama ni kwamba hapigi sehemu yeyote mbaya, yeye ilikuwa miguuni tu na baada ya kumaliza adhabu yake, anakanda ile miguu kwa maji ya vuguvugu na chumvi.
Kwa ujumla ninachotaka kusema ni kwamba tabia yangu niliyonayo leo hii ni matokeo ya kazi nzuri ya mama.
Mtindo huu wa Ulaya mimi sikubaliani nao mkuu, mtoto umzae wewe halafu yeye ndiyo kwanza akufundishi dunia. Haya mambo ya Ulaya yabaki huku huku lakini hayatufai sisi na hasa mazingira ya makuzi ya mtoto wa kiafrika.
Post a Comment