Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, September 20, 2010

tutaonana mungu akipenda-3

 Hapana haiwezekani, huyu anaweza asiwe ndiyo yeye…akili haikutaka kukubali ukweli, na isingekuwa mke wangu kuiona ile hali na kuja kunishika kwa nyuma, huenda ningeanguka, kwani kizunguzungu kilishaanza kuniingia machoni!


‘Vipi mume wangu, mbona hivi, hebu kaa hapa kidogo, umebadilika ghafla..’ akasema huku anamwangalia Yule mwanamke tuliyemuona , akiwa naye kaduwaa akiniangalia kwa mshangao.

Yule mwanamke aliduwaa, na machozi yalikuwa yakimtoka kwa wingi, na mwishowe akaikota ile hela na kuanza kuondoka. Nilitamani nimuite asiondoke lakini kinywa kilikuwa kikavu na sikuweza kupanua mdomo wangu. Mke wangu alipoona nimemtulia akamkimbilia Yule mwanamke na alipomfikia wakawa wanongea kwa sauti ambayo sikuweza kuisikia vyema. Na mara wakawa wanarudi wote pale nilipokaa.

‘Twendeni nyumba, naona unahitaji kupumzika, nimemuomba huyu mama twende naye, ili tuone jinsi gani tutakavyomsaidia kwani hata hivyo ninahisi unamjua, sidhani hii hali iliyokubadili ghafla baada ya kumuona ni hali ya kawaida tu…’ nilitamani kumwambia aachane naye lakini kauli ilikuwa imekataa kutoka.

Tuliingia ndani ya gari kimya kimya , nikawa naendesha gari huku nikizuia machozi yasitoke, sijui ni kwasaababu ya huzuni au ni hasira au ni kitu gani kilichoniingia mwilini, lakini hatimaye machozi yaakaanza kunitoka kama maji , na nashukuru mke wangu na Yule mama walikaa viti vya nyuma na wote walikuwa katika mawazo yao.

Tulipofika nyumbani nilipangusa uso wangu haraharaka na kujifanya hakuna kilichoniathiri, tukaingia ndani , mimi nikakimbilia chumbani na kujilaza kitandani, na usingizi ukaniingia ghafla.

Moto mkali ulikuwa ukiwaka, kuelekea nilipolala, na pembeni yangu kulikuwa na sura ambayo nahisi niliijua, na moto huo ulikuwa ukitujia pale tulipolala kwa kasi ya ajabu, na sio moto to hata wadudu kama nyoka, nge , na wadudu wengine, nawo walikuwa wakija kutuelekea pale tulipolala, kwani na wao walikuwa wakiuogopa ule moto. Mimi nilijitahid kujiinua kwa shida kuukimbia, lakini Yule mwanamke, aliyekuwa amalala karibu nami, hakuweza hata kujisogeza, akawa analia `nisaidie nisaidie…’

Nilijitahidi kumvuta lakini alikuwa mzito kupita uweo wangu, na moto ulishaanza kumuunguza, na hata nyoka na wadudu wengine walishamtanda wakimtumia yeye kama njia, au hifadhi… nikaogopa kwani mmoja wa nyoka mkubwa alikuwa akija kuelekea pale nilipomshika Yule mwanamke mkono, na kwa uwoga wa kuona nyoka ananijia nikauachia ule mkono, …na mara moto ukawa mkali na kumfunika Yule mwanamke, huku analia kwa sauti, nisaidie, nisaidie….’.Nami nikalia kwa sauti nikiita jina la mke wangu wa zamani, kuwa ajitahidi kukimbia asiiungue…!

‘Vipi mbona unapiga kelele hivi, unamwiita nani…’ ilikuwa sauti ya mke wangu ambaye alikuwa karibu yangu akinikanda kwa leso yenye maji ya uvuguvugu..

‘Naona una homa ngoja nikupe vidonge vya kutuliza maumivu’ akasema na kwenda kunichukulia vidonge na maji. Nilipokunywa nikawa na nafuu kidogo.

‘Hebu niambie, ukweli ulikuwa ukijua kuwa ‘huyu aliyekuwa mke wako ‘alisharudi hapa nchini?’ lilikuwa swali la kwanza la mke wangu, kumbe walishaongea na keshamjua kuwa ni nani. Nikamwambia hapana, tangu alipoondoka siku ile , sikuwahi kuwa na mawasiliano naye tena, hadi leo nilipomuona katika ile hali.

‘Basi mimi naomba mukaongee, na yaliyopita si ndwele, msamehe, kwani sote ni binadamu, tunapitia katika hali za makosa, ni mbora wa wote ni Yule anayekubali kumsamehe mwenzake akikosea….’ Alisema maneno ambayo sikuyapenda kuyasikia, ila ukweli uliniingia,..

‘Hapana, mtu kama Yule sidhani kama anastahili msamaha, ungelijua jinsi gani nilivyoteseka kwa ajili yake ,usingeyasema hayo, nilitamani nifanye kitu mbaya, lakini hkuwepo upeo wa macho yangu, lakini subira ilinisaidia. Yule nilimsaidia sana, yeye na familia yao, nilipomtoa kijijini kwao, yeye na wazazi wake walikuwa katika hali mbaya, nikawajengea nyumba, nikawasomeshea ndugu zake, kwasababu ya kumpenda yeye. Lakini nini alichonilipa?...’

‘Lakini huoni kuwa keshaadhibiwa vya kutosha, na kama hutamsamehe atateseka sana. Sio wewe tu uliyekumbwa na msukosuko kama huo, mimi kisa changu huenda kinauma zaidi ya kisa chako, lakini mimi mwisho wa siku nilimsamehe mwenzangu, kwasababu yote hutokea ilii iwe sababu, je tungekutana kama yasingelitokea haya. Ngoja sasa nikusimuliea nini kilichonitokea hadi uliponikuta siku ile nikilia…

****************
Jamana samhanini, sikujua kuwa tumeshaingia ukurasa wa tatu, tutaendeela na kisa chetu baadaye kidogo!
Enhanced by Zemanta

6 comments :

Anonymous said...

Duuu, sijui ilikuwaje kwa huyo mke wako, lakini kwasababu umempata umpendaye ni kumsamehe tu mwenzako...ila kama inataka moyo

Nasibu said...

Hapa mimi nimekosa comment kabisa ,,swala hili ni gumu kwetu wanadamu nadhani Mungu atapitia kwa huyo mke wa pili kwa kurudiana huyu mke wakwanza na huyu bwana,,ila kwangu ni ngumu mno!!!!!!!!!!!

Anonymous said...

Kwanza anaumwa nini? inaonyesha huko alikotoka kaukwaa..kwahiyo kwa vyovyote itakavyokuwa `akapime kwanza'...
Wanasema usiache mbachao kwa mswala upitiao,lakinii kama `umechakaa utafanyaje?'
Akili kichwani mwako!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

...nani kwambia jehanamu ni mpaka ufe? Tafakari!

Simon Kitururu said...

Mmmh! Tunasubiri stori iendelee...

emuthree said...

Inakuja wakuu, ila mtandao na majukumu ya kuwatafutia watoto kitu cha kuwawezesha kwenda choo, yamenibana, lakini yote ipo kichwani kwasasa...mkae mkao wa kula