Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Thursday, September 16, 2010
Kilio cha mtoto
Ilikuwa saa mbili na nusu usiku , anga na taswira za usiku zilishatanda , na mara sauti kali ikasikika na kuvunja utulivu uliokuwepo, utulivu huu ulisababushwa na kukatika kwa umeme. Sauti kali ile ilikuwa kilio cha mtoto;
‘Jamani majirani njooni mnisaidie mama ananiua ,jamani nakufaaaaa, nisamehe mama sitarudia tena…’ wakati kilio hiki kikiendelea tulisikia sauti ya fimbo ikitua kwenye kiwiliwili cha huyo mtoto, huku mama mwenyewe akisema kwasauti, `kufa…nitazaa mwingine, huna adabu we, kila siku naongea, kila siku nakuchapa lakini hubadiliki na wala hunisikii…’ maneno, viboko na kilio cha mtoto, vilitufanya sote tuingiwe na Huruma.
Karibu kila siku huyu mama humchapa mtoto wake, kiasi kwamba tunajua kuwa karejea kwenye shughuli zake za biashara tunaposikia kilio cha huyu mtoto. Majirani tumejaribu kuingilia kati lakini haijasaidia. Na leo mimi na mama watoto wangu tuaksema hii imevuka mpaka, kwasababu mara nyingi mtoto Yule hucheza na watoto wetu. Mtoo Yule ni mkimya ajabu, msafi na hapendii utukutu. Nafikiri kutokana na kipigo cha mama yake au vipi, lakini mara nyingi alionekana mnyonge sana.
‘Hodi mama nani-hii, hebu tfungulie kwanza, acha kumpiga huyo mtoto..’ mama nanihii wangu akaita. Na kwa vile huyu mama anatuheshimu sana, akatuliza kipigo na kutufungulia. Hasira zilinipanda kuona kile kiboko alichoshika, utafikiri cha kuulia nyoka.
‘Hivi wewe huyu sio mtoto wako wa kumzaa..?’ nikajikuta namuuliza kwa hasira.
‘Jamani majirani najua ninawauzi sana, najua mnfikiri mimi napenda kumchapa huyu mtoto, mnafikiri mimi sina ubinadamu…’ akaanza kulia. Mimi sikuelewa kwanini analia, nikamwangalia mwenzangu ambaye naye aliishia kushangaa.
‘Mimii jamani nimeteseka sana na mtoto huyu, nimemzaa kwa taabu na aliponea tundu la sindano. Naogopa sana asije akarithi tabia ya baba yake…’ alipoanza kusema hivyo, nikaona nifungulie kinasa sauti change cha asili, ubongo, kwani kuna kisa kinakuja.
‘Baba yake huyu tulioana kijiini na maisha yetu mwanzaoni yalikuwa mazuri tu, mara ikatokea kupunguzwa kazi, baba wa huyu mtoto akawa kijiweni, mimi ndio nimetokea kijijini ni mama wa nyumbani, kula na kila kitu nilikuwa namtegemea yeye. Hali ile ya kukaa bila kazi na kutafuta kazi kwa muda mrefu ikaanza kumtesa mume wangu, na matokeo yake akaanza kulewa.
Ilikuwa kidogokidogo, na baadaye akawa mlevi wa kutupwa. Nisingejali sana ulevi wake, lakini alianza tabia ya kunipiga, kila akirudi toka huko alikotoka, anakuja kwa wimbo wa sauti kubwa, `wewe Malaya humo, ndani nifungulie mlango, la sivyo nitaingia nawo, na nikiingia nawo ujue ni kifi chako…basi ataanza kuimba hapo nje anacheza utafikiri mwehu. Wapangaji tuliokuwa nawo wakahama wote…
Tatizo nikimfungulia na kujaribu kumbembeleza, nitapigwa kama mtoto mdogo, na mara nyingi nilikuwa nikiishia hospitali kwa majeraha, na nikiulizwa nadanganya kuwa nimanguka au nasema lolote ilimradi nimlinde mume wangu.
Kipindi hicho alichozidi sana kulewa nilikuwa na ujauzito wa huyu mtoto, na mara mbili niliponea chuchupu kuipoteza mimba ya huyu mtoto. Na mara ya mwisho alinipiga bila kuali kuwa nakaribia kuzaa, na kunivunja mguu. Ndio maana mpaka leo siwezi kutembea vizuri.
Majirani walikuja wakaniokoa na kunikimbiza hospitali, huko madakitari wakachanganyikwa, kwani mguu upo katika hali mbaya, na mimba inaweza kuharibika, na sio kuharibika tu, bali hata mimi ningeweza kupoteza maisha. Nashukuru sana juhudi za madakitari, kwani waliniokoa mimi na mtoto akatoka salama, na mguu uliokolewa kwa kufungwa mhogo(POP)! Jaribu kufikiri mwenyewe hayo mateso niliyopata.
Mume wangu alikamatwa na ikatokea vurugu akamuumiza askari na alihukumiwa mwaka jela, na huko jela akagundulika kuwa ana kifua kikuu, ambacho kilisababisha umauti wake huko huko jela.
Sasa jamani ninapomchapa huyu mtoto, nashindwa kuvumilia, kila kosa linanikumbusha mbali, ile taswira ya mateso , vipigo na …kuchanganyikiwa , inanijia kila ninapomkuta huyu mtoto kakosea, naogopa sana asije akawa kama baba yake. Inaniuma sana ninapomchapa na kila mara nikimchapa, naishia kulia na kujuta kwanini nakuwa hivi…samhanini sana majirani, nampenda sana mtoto wangu sivyo kama mnavyodhania….
Alipofika hapa alianza kulia, na kilio kile kilimpelekea mwanae ainuke na kumfuata pale alipokaa na wote walikumbatiana na kuanza kuangusha kilio…
‘Mama samahani najua nakutesa, naahidi sitarudia tena, naomba mama usilie, mama, tafadhali usilie…mama yangu nakupenda mama...usilie’ waliendelea katika hali hii ikatufanya hata sisi wenye machozi ya karibu yatutoke…..
Ni mimi: emu-three
6 comments :
Mhh, mnanifanya na mimi nilie...mmmh, naomba basi umalizie kile kisa cha `tutaonana mungu akipenda...' please, tafadhali kwa msisitizo
Kumuadhibu mtoto kupita kiasi ni kumuharibu kisaikolojia
Nitamalizia kisa chetu, ila hili tukio lilinigusa ndio maana nikaona nilitoe kwanza halafu kisa chetu kije kuendelea.
Na kweli swala la kuchapwa watoto kupita kiasi ni kuvunja haki za watoto. Kumfunza adabu sio kumuumiza...unaweza kumchapa lakini sio kama unaua nyoka! Yeye ni binadamu na anaumia kimwili na kia-akili pia!
Watu wengi wamekuwa wakipinga adhabu ya viboko! Je ni vyema ikaondolewa, na kama mtoto akishindikana kuonywa kwa mdomo utampa adhabu gani?
Hiki kisa kwa kweli hata kama huna machozi ya karibu utalia tu. Yaani tangu nilipoanza kusoma mpaka nimemaliza nimelia. Ila namwonea huruma huyu mama kwani anamchapa mtoto wake kwa kulipa kisasi hii sio kweli kwani hapo sasa anamfunza mtoto wake pia akiwa baba achape watotowake na mwisho wake hii tabia ya kuchapa haitaisha. Ni furaha gani kumchapa mtu? Na kwanza kumchapa mtoto ni kumfanya awe sugu zaidi.
Emu -3 hakuna mtoto anayeshindikana kuonywa, kwani mtoto mkunje angali mbichi. Ukianza kumwonya mtoto wako yaani akikosea unamwita mnakaa china kwa saizi moja yaani ile ya usawa wake na mnaongea kistarabu sio MAVIBOKO...
hapo kama inaonekana kuna sababu ya huyo mama kumchaopa mwanaye kama sijaelewa vizuri kwani huwezi kulipiza kisasi cha mume kwa mwana uliyemzaa
Dada Dina, huyu mama kwa maelezo yake ni kuwa anapoanza kumchapa mtoto wake, kwa kosa ndio, lakini wakati anamuadhibu, kuna kitu kinamwingia kichwani na akawa kama vile hampigi mwanae, ila hiyo taswira inayomjia...sasa kwakweli hii ni hatari!
Tulimsihi sana, kuwa kama inawezekana atafute ushauri wa wataalamu wa akili na vitu kama hivyo,...lakini tangu tukio lile litokee na watu kujaa kwake tumeona mabadiliko makubwa!
Post a Comment