Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, August 24, 2010

Nilivyomtaka mke mwenza-2

‘Mimi naona nikutafutie mwenzako au unasemaje’ siku moja akasema hivyo kimzaha, nami nikamjibu kwa ukali. ‘Katafute, kwanza utanipunguzia usumbufu, nyie penzi ni tendo la ndoa basi tafuta atakaye kubali hilo tendo kila siku’ nikamwambia hivyo kwa hasira. Hutaamini kauli ilinipandisha hasira nikaamua kumwekea bifu, tukakata miezi mitatu hakuna tendo la ndoa. Ilifikia hatua nikajua hata yeye hana hamu na mimi tena.


Siku moja akanikalisha chini kuliongelea hili swala tena, akaongea mengi , akatoa ushauri, na mimi nikamsisitizi kuwa kama anataka kuoa mke mwingine , kama alivyosema awali na aoe tu sina tatizo.

‘mke wangu pale nilikuwa nakutania tu, mimi sina nia ya mke wa pili, ninachotaka ni kuondoa hili tatizo miongoni mwetu…’ akasema kwa unyonge

‘Kwani kuna tatizo hapa, nishakuambia tatizo labda ni wewe, kwani upendo hauji bila tendo la ndoa, nishasema nikijisikia tutafanya, wewe hilo ndilo wazo lako kila siku…’ nikasema na kuondoka zangu.

Mume wangu akavumilia mwishowe akaamua kweli kutafuta mke wa pili, siku aliponiambia kuwa keshatafuta mtu anayefaa kuwa mke mwenza, niliwaka, nilihamaki, kwani sikuwa na nia hiyo nilipomwambia awali kuwa atafute mke wa pili, yote niliyasema lakini sikuwa nimedhamiria hivyo. ‘Ukimleta huyo mke hapa, naondoka zangu, au labda umtafutie nyumba yake, simtaki humu ndani’ nikasema kwa hasira na tangu siku hiyo tukawa hatuongei, kumbe mwenzangu keshachumbia na iliyobaki ni ndoa tu.

Nikaipata hiyo fununu basi nikaona sasa nimelikalia kaa la moto, nikaanza kubadilika na kuanza kumhudumia mume wangu kama itakiwavyo, na hutaamini ile hali ikaisha na hata baridi nikawa sisikii tena, nikajiuliza kumbe tatizo lilikuwa mimi, nilikuwa sijitumi, nilikuwa nachukia kitu ambacho ni lazima kwa mume na mke na kumbe hakuna madhara bali huleta faraja, na wakati mwingine ukijisikia vibaya, kichwa kinauma mkikutana na mume wako yote yanaisha, nikasema moyoni sasa nitampa haki yake mpaka ajue kuwa mimi ni mke mzuri, lakini nilishachelewa.

‘Mke wangu wiki hiz mbili umebadilika kweli kiasi kwamba naona ni mke tofauti na ninaye mjua , umeamua nini kubadilika hivi, au kuna mtu kakupa shule?’ akaniuliza mume wangu ,nami nikamjibu kwa upole kuwa nimeamua tu, kwa vile nimejisikia, na nikaongezea `kwasababu nakupenda mume wangu na sitaki upate shida’.

‘Lakini mke wangu ujue nishachumbia na mahari nimeshatoa, kwasababu nilikuuliza mara nyingi ukanihakikishia kuwa kuoa mke wa pili kwako sio tatizo, sasa sina jinsi inabidi tu uwe na mke mwenzako’ akasema kwa Huruma. Niliumia kupita maelezo, kiasi kwamba nikaona niondoke niende kwetu kwa muda na mume wangu akakubali.

Nilipofika kwetu, nililia, nikajuta na mwishowe nikasema `yote nimeyataka mwenyewe. Mama akanishauri mengi na yakuwa kuwa na mke mwenza sio tatizo, kinachotakiwa nikuhakikisha unamuonyesha mume wako kuwa wewe ni zaidi.

‘Nitamuonyesha kweli kuwa mimi ni zaidi.

Alivyoletwa lile wiki la fungate, nikaanza kusoma vile vijarida, nikaanza kuangalia ile mikanda ya mafunzo ya mapenzi nikagundua kweli tatizo lilikuwa mimi, na nikajiandaa katika ushindani wa mapenzi, na nilishinda hilo, kwani kila mume wangu alipokuwa kwangu aliishia kunisifia na kusema sasa anakiri kuwa amefanya makosa kukimbilia kuoa mke wa pili, mimi nikamwambia `nab ado, ipo siku utamsahau huyo mke wako kabisa’.

Ni mengi yakuwaelezea, hasa mikasa yangu na mke mwenza lakini ngoja niishie hapa kwa maoni kwenu kuwa wakati mwingine sisi wanawake tunafikiria karibu tu, na hatutaki kujifunza dhana nzima ya ndoa na kudharau yale ya muhimu katika ndoa. Ndoa ina mambo yake makubwa mengi ambayo wengu tunayajua macheche tu, mimi nilikuja kugundua kuwa tendo la ndoa ni tiba ya akili, ni chachu ya mapenzi na muhimili wa ndoa. Nawaombeni msifanye makosa kama yangu kwani , kama sio mke mwenza basi mume wangu angeishia kwenye nyumba ndogo, na hasara ingekuwa kwa nani!

Mimi mama A

Enhanced by Zemanta

10 comments :

Anonymous said...

Nilijua tu itaishia hivi, vinginevyo jamaa angetafuta nyumba ndogo awe anapunguzia matatizo huko, wengine huishia vilabuni au kwenye mabaa. Nawaambieni msione wanaume wengi wakirudi kazini wanaamua kupitia kwenye mabaa kwasababu gani, ni kama hivi, unajua ukirudi nyumbani hakuna `tulizo a roho' unaenda kupata kinywaji na kutamani wanawake wengine, huku akili inachora mengi
'Kama ningempata kama yule, mambo ynagekuwa shwari, kumbe unaye nyumbani lakini hajui wajibu wake!

Anonymous said...

Mimi nilikuwa na tatizo kama hilo la maumivu na nilichukia sana tendo la ndoa hadi nilipojifungua mtoto wa kwanza baada ya hapo mambo yakawa kama kawaida.
Kwa ushauri wangu, ulitakiwa usimfanyie mume wako hivyo, ilibidi umueleze kiundani nini kinakutesa moyoni, humpendi au hulipendi hilo tendo kinamana anavyofanya yeye au vipi sijui, ungekuwa karibu naye katika ushauri, kwanza yeye ni dakitari kwahiyo kama angeshindwa yeye angetafuta madakitari bingwa marafiki zake akajua kiini ni nini.
Hata hivyo hatima ya siku uligundua mwenyewe.
Mwili wa binadamu ni wa ajabu, utakavyouendekeza unakupeleka hukohuko!

Yasinta Ngonyani said...

Unajua sio wanawake tu hata wanaume inakuwa hivyo yaani mpaka mtu utumie aina ya kitisho na hapo anakubaliana tu nawe kuwa fanya tu akiwa na hakika ya kuwa ni utani tu huwezi kuniacha mimi/kuoa mke mwingine. Na wengine wanadiriki kabisa kusema nani atakupenda tena wewe. Kwa hiyo hapa huyu mama alikuwa anamjaribu mume wake ana mwisho ikawa kweli. Kitu ambacho hakufikiri kinaweza kuwa kweli. Nadhani hapo kama bwana akaishia kwenye nyumba ndogo basi ingekuwa hasara kwa wote. Nakubaliana kuwa ndoa iliistawi tendo la ndoa linachangia lakini je ni kweli lazima kufanya hilo tendo kila siku? Nimewaza tu kwa sauti.

Anonymous said...

'kila siku' hapana, kiafya sio nzuri, lakini kwa huyu mwenzetu alizidi, yeye kakiri kuwa aiweza kukaa zaidi ya mwezi bila kutimiza wajibu huo.
Kwa mizani eti ni nani zaidi wanawafanyia wenzao hivyo, yaani kutokutimiza hilo jukumu, kwa mtizamo wangu wanawake wanaweza kuongoza, kwasababu kwanza kutokana na majukumu yao, pili kuna wale waliokeketwa wanakuwa na taaabu sana, na hisia zao zinatoka ndani ...nk.
Swali kubwa ni jinsi gani ya kusaidiana kwa hili kwani unaweza ukamkuta mume ana hisia kubwa kuliko mke au mke ana hisia kubwa kulko mume, je mtawezaji kukidhiana bila kuumizana

mzee wa busara na hekima

Anonymous said...

Heey! Hebu 2fanye mwanaume ndio anamfanyia hivyo huyo mkewe hivyo vituko vyote. Cjui 2tasemaje, hampendi au ...?
Kwani kuna kisa kama hicho lakini ni mwanamme anamfanyia mke wake. Yaani hana mpango naye kabisa katika tendo la ndoa. Yaani anaweza wakakaa hata miezi miwili bila kukutana na kama wakikutana kwy hilo tendo ni mara moja tu kwa hiyo miezi miwili au mitatu. Ilikuwa inamuuma sana mke m2 lakini hakuwa na la kufanya. Akimuuliza anasema nimechoka na kazi. Ucniguse. Mpaka mme aliama chumbani eti mkewe anamsumbua. sasa hiyo utasemaje wadau nae mme ajui wajibu wa mke na mme? Au mapenzi yameisha? Mpaka mkewe ameamua kumuacha hivyo hivyo tu. Ilimpa taabu sana kuzoea hiyo hali lakini sasa hana budi kuishi maisha hayo. Sasa hilo nalo wadau mtasemaje?
Nae huyo utasemaje??? Wadau naomba michango yenu.

chib said...

Penzi ni kitendawili. Na wala hakina njia iliyo nyooka

emuthree said...

Anonymous said WA August 24, 2010 4:10 PM.
Hoja yako ni muhimu sana, e ingekuwa upande wa pili kuwa mwanaume ndiye kafanyiwa hivyo ingekuwaje?
Labda tumalizane kwanza kwa upande wa huyu mume aliyetendewa na tukimalizana naye hapo tuingie upande wa mke katendewa.
Unaonaje ukitupa hicho kisa kwa kirefu kidogo ili tukiweke hapa hewani , na ili wanaume wajue kuwa sio wao tu wanaoweza kufanyiwa hivyo hata wao wanawafanyia wanawake zao hivyo, je kama ingekuwa kwao ingekuwaje.
Ni ka ushauri kadogo tu kwa wadau na any. wa hapo juu

Anonymous said...

Lakini mwanume gani atakayetakiwa na mkewe atoe nje? Unajua mimi sielewi, mwanume alivyo mroho wa hicho kitu aambiwe `na-ku-ta-ka mume wangu halafu aseme `nimechoka' basi hilo sio dume rijali....
Samahani kwa lugha hiyo

NAJUA WAJUA said...

Hii habari nzito, kuna anayependa tendo la ndoa na siyependa tendo la ndoa, sasa watu hawa tofauti wakikutana kazi ipo!!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mchuma janga hula na wa kwaooo....lol!

Alivuna alichoanda :-(