Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, August 20, 2010

Nilivyomtaka mke mwenza

Naomba emu-three niwekee hii kwako ili niwape fundisho wenzangu;


Sasa hivi mimi nina mke mwenzangu, na chanzo cha kuletwa mke mwenzangu nimechangia mimi mwenyewe.

Niliolewa miaka mitano iliyopita, mume wangu alinichukua nikiwa bado mbichi, na nakiri matatizo yote yalianzia mwanzoni mwa maisha yetu ,hasa ile siku ya kwanza ya kukutana na mume wangu. Siwezi kuyasimulia maumivu niliyoyapata siku ile kwani ilikuwa balaa tupu, wiki ilipopita nilitamani kama inawezekana mume wangu afie huko huko asirejee nyumbani, kwani kila tukikutana naye ni matatizo.

Niligundua baadaye kuwa mimi nilikuwa mchangiaji mkubwa wa hata kupata hayo maumivu, kwasababu sijui ni kwanini nilikuwa hivyo, sijui ni kwasababu ya malezi au vipi, kwani kila mume wangu aliponitaka nilikuwa mgumu kupita kiasi, sijui ni kwasababu ya yale maumivu ya mwanzoni au ni hali niliyojijengea mwenyewe mwilini.

Katika miaka hiyo mitano tukabahatika kupata watoto wawili, baada ya kujifungua mtoto wa kwanza sikuwahi kupata yale maumivu tena, naweza kusema maumivu hayo yalitoweka baada ya miezi kadhaa, nilikuwa kama kawaida, lakini ile hali ilinikaa akilini. Sio kwamba mume wangu hajui kuniweka sawa, anajitahidi lakini nilikuwa mgumu kukubali kila alichonielekeza. Kwanza mume wangu ni dakitari kwahiyo anajua nini kifanyike vipi lakini mimi nilikuwa kichwa ngumu.

Baadaye nikawa sitamani kabisa tendo la ndoa, nikawa najariibu kila mbinu kumkwepa mume wangu, na ikipita siku bila kukutana naye najipongeza. Wakati mwingine nilimuonea Huruma, anavyohangaika, anajaribu kila mbinu, kunibembeleza, kunionyesha hiki na kile chenye kunivuta katika hisia lakini wapi. Ikabidi aninunulie kanda za mafunzo ya mapenzi lakini wapi, akawa ananiletea vijarida lakini wapi, kila siku nikawa namwambia `hivi nyie wanaume mnafikiri mapenzi ni tendo la ndoa tu, kwanini tusikae hivihivi tu…’

Iliweza hata kupita miezi miwili bila kukutana na mume wangu, kiasi kwamba jamaa akawa sasa anakasirika , `kwanini unakuwa mgumu hivi, hebu nieleze mke wangu, tatizo lipo wapi’ akawa mara kwa mara ananiulia. `Mimii sina tatizo, labda tatizo lipo kwako’ nikawa namjibu kimkato. ‘sasa niambie mimi nina tatizo gani ili tujaribu kulirekebisha’ ananiuliza. ‘Kwani we shida yako nini’ ninamuuliza kwa ukali.

‘Unajua mke wangu ndoa hujengwa na mengi na mojawapo kubwa ni kukidhiana haja ya tendo la ndoa, sasa naona kwako ni shida, ndio maana nataka tutafute ufumbuzi wa hili’ mume wangu alisema mara nyingi usemi huu.

‘Hivi nyie wanaume, mbona tendo la ndoa mnaliona la maana sana kuliko mengine, mimi sina hamu ya hilo tendo, nikijisikia tutafanya, kwasababu hilo huja tu bila kuniambia’ nikasema kwa kunyenyekea kidogo, huku moyoni nikiumua kuwa kweli namtesa mtoto wa watu. Kuna siku tuliyojaribu , lakini mwisho wa siku napatwa na baridi kali, nilishangaa badala ya maumivu sasa inabadilika kuwa baridi, na naishia kutetemeka kabisa kwa baridi, nikajisema hii ni raha gani.

‘Hili tatizo sasa naona limekuwa kubwa sana, mbona huniambii nini kinakutesa, mimi ni dakitari ukiniambia hata kama sitakupa jibu leo nitalitafuta tu na utakuwaa huna matatizo, nimbie nini kinaenda kombo.

‘Nilishakuambia hakuna tatizo, nini shida yako’ nikamjibu hivyo.

‘Mimi naona nikutafutie mwenzako au unasemaje’ siku moja akasema hivyo kimzaha,
 
Je huu mzaha mzaha ulitumbua usaha au waliweza kusuluhisha hilitatizo. Ngoja nikatize hii habari ili tuweze kutafakarii na kupeana mawazo, na tukijaliwa tutaileta sehemu ya pili yake.
 
Kutoka kwa mama A.

11 comments :

Anonymous said...

Huyu mwanamke hakufundwa kwao, nafikiri hata Kitchen Party hakupitia. Lakini hili sio atizo lake pekee, wapo wengi wanateseka hivi, ni tatizo la kutokuwaandaa maharusi na kuchukulia ndoa kijuu-juu tu.
Umelilia wembe sasa umeupata, pole sana. Hata hivyo imekusaidia kujifunza mengi, kila jambo hutokea ili iwe sababu , nimeupenda huu ujumbe wako emu-three

malkiory said...

Huyu mama kwanza kabisa naweza kusema alijiingiza kwenye ndoa bila kuelewa maana halisi ya ndoa. Ndiyo maana alilichukulia tendo la ndoa kwa mzaha,dharau,ukatili na hata unyanyasaji kwa mumewe, nadhani hii si dhana sahihi.

Pili inaelekea pia hakuwa na upendo wa dhati kwa mumewo huyo zaidi yakuwa alimkubali kwasaba tu ya hadhi yake kama daktari.

PASSION4FASHION.TZ said...

Pole mwaya ngoja tusubiri kiendeleacho.

Anonymous said...

hUYO LABDA ANA MAPEPO, INAHITAJI KUOMBEWA, SI BURE, KWELI HICHO KITU UNAKIONA KIBAYA, MWENZETU UMENYIMWA RAHA, LAKINI UTAJUA TU, NGOJA TUONE ILIVYOISHIA

nyahbingi worrior. said...

Duh!!

Yasinta Ngonyani said...

kaazi kwelikweli!!

Anonymous said...

Kwa uoni wangu mdogo, kuna tatizo la kujiamini kwa huyo binti, na hii huwapata mabinti wengi wanapoolewa, kazi kubwa ni kuwajenga kifikira kuwa hayo maumivu sio endelevu, lakini ili kumsaidia mtu kama huyo inabidi na yeye awe tayari kusaidiwa.
Inavyoonyesha huyo binti hakuwa tayari, labda hiyo ndoa haikuwa ya hiari, au ndio wale mabinti wanaoolewa kwasababu ya pesa tu, lakini hana upendo kwa huyo anayemuoa, na hii ni mbaya sana.
Tukumbuke kuwa tendo la ndoa ni haki ya kila mmojawapo, akilihitaji, labda kuwa na dharura zinazojulikana, kinyume chake huleta mabaya katika ndoa yenu, kama magonjwa au kutokuelewana kusiko na sababu, utamuona bwana ka kasirika, kumbe amedaihaki yake kanyimwa. Wengine ndio hao wanakimbilia kuoa mke wa pili, au anatafuta nyumba ndogo, kumbe suluhisho lilikuwa dogo tu.
Akina mama, akina dada, mimi nawapa siri moja, mume ujana wake wote ukitaka kumpatia na `tendo la ndoa' kama mtaliwezea na kumpawagisha mume wako, hilo ndio limbwata la asili, halihitaji dawa.
Samahani kama nitakuwa nimekiuka maadili

Mzee wa maadili na hekima

EDNA said...

Heeee pole mwaego.

Anonymous said...

CJUI NISEMEJE. LABDA ANGETOA SHORT STORY YAKE NJISI WALIVYOKUWA NA MAUSIANO KABLA YA NDOA YAO. AU NI MCHUMBA ALIYECHANGULIWA NA WAZAZI YEYE HAKUMPENDA. NA JINSI ALIVYOELEZA KWA JINSI NILIVYOMUELEWA MIMI KAMA NDIYE ALIYEKUWA MTU WAKE WA KWANZA KUMUINGILIA KTK TENDO LA NDOA. SASA ASIPOANGALIA ITAKULA KWAKE. NA HUYO MME WAKE INAVYOONEKANA NI WALE WANAUME WA NEVER MISS HILO TENDO LA NDOA.

AU 2SEME LABDA ANA PEPO AMBALO HALITAKI ASHIRIKIANE KIMWILI NA HUYO MME WAKE. LABDA 2MUULIZE, JE HUWA ANAOTA ANAFANYA TENDO LA NDOA?

AU ALIKUWA ANALETA MAPONZI TU KWA KUONA KUWA HUYO MME WAKE KAFIKA KWAKE NA HAWEZI FANYA LOLOTE LILE?

SASA ITAKULA KWAKE.

HUYO MUMEO ANAONYESHA ANA MAPENZI YA DHATI KWAKO. NDIO MAANA AME2MIA MBINU ZOTE KUKUWEKA SAWA LAKIN WAPI.

emuthree said...

Nashukuru kwa maoni mbalimbali yaliyotumwa hapa kijiweni kuhusiana na kadhia hii, nilijaribu kuwasiliana na mlengwa kwa e-mail, sijapata jibu lolote, ili kujua zaidi kutokana na maswali yaliyojitokeza humu.
Naona tuendelee na sehemu iliyobaki, kwani huenda ikajibu baadhiya maswali hayo na kutusaidia kutoa maoni zaidi.
Tukumbuke kuwa mlengwa alituma hili ili watu wengine(hasa wanandoa) wakumbuke wajibu wao. Wengi wakishaolewa wanona basi wamefika na kusahau kuwa kila kitu kinahitaji `utunzaji', kujifunza zaidi na maboresho.
Ndoa nyingi zimekuwa zikiingia katika mitihani mikubwa na utakuta chanzo ni wanandoa wenyewe, kwa kutoiangalia ndoa na misingi yake.
Labda swali litabakia kichwani, hivi hii misingi ya ndoa inatofautiana kati ya mtu na mtu, mila na desturi moja na nyingine, imani za kidini nk. Na kama ni hivyo basi huenda wanapokutana wanandoa wanaotofautiana ndipo kunapotokea sintofahamu fulani!
Lakini vyovyote iwavyo misingi mikubwa ya ndoa inajulikana, na kuivunja hiyo tunajisababishia matatizo wenyewe.
Nawaombeni tujumuike tena kwenye sehemu iliyobakia na hapo kila mtu atakuwa na uwanja mpana wa kushauri , kuuliza na kuelewa nini kusudi la mlengwa kututumia hili tukio lake.
Nawe kama unalo kama hili au jingine tutumie ili tuelimike sote

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mmmmh!