Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Wednesday, August 25, 2010
wivu sina, ila roho ina uma
Niliinama chini na kujikuta ninalia, na ujue mwanaume kama mimi akilia yamenifika shongoni, nikawaza wakumwendea kumkopa nikamkosa, wote nilishawakopa na kila ninayeenda kwake kumpigia hodi nakuta taarifa `mwambie sipo’ nikakata tamaa ya maisha. Lakini hili nililo nalo sasa linahitaji zaidi ya rafiki, je nitampata wapi.
‘Mume wangu sasa tufanyeje na hali ndio kama hiyo, hatuna hela, unaumwa na hospitali za serikali tumeenda tumechoka, huponi na ….hata mimi sasa nachoka’ hiyo ilikuwa sauti ya mke wangu, ambaye amejitahidi sana kunivumilia kipindi hiki cha shida na mara nyingine alikuwa akinisadia kuuza baadhi ya vitu ndani ili tupate kuishi.
‘Mke wangu, hii inaonyesha wazi kuwa muda wangu wa kuishi umekwisha, kama naumwa , halafu hatuna hela, hospitali hawaoni kitu unafikiri imebakia nini, wewe jitahidi na maisha yako, mimi najua si muda mchache mtanisahau na utapata mwingine…’nilisema huku moyoni nikiomba atokee msamaria mwema ili aliokoe hili jahazi.
Mke wangu alitoka kidogo na mara akaja na rafiki yangu. Rafiki yangu huyu kidogo tunajuana toka mbali kwasababu ya shughuli za hapa na pale, alikuja na basikeli, na nia yao wanipeleke kwenye hospitali moja ya binafsi eti wamesikia kuna dakitari bingwa wa matatizo yangu. Niliwauliza mnanipeleka hospitali ya mtu binafsi mtapata wapi hela za matibabu.
‘Wewe ngoja tufike kwanza huko, mengine yatafuta baadaye, hujasikia watu wanaotuma maombi ya kusaidiwa baada ya kupata vyeti vya dakitari, utaombaje misaada wakati huna ushahidi wa unachokiombea’ akasema Yule rafiki yangu.
Tulifika hapo hospitalini na rafiki yangu akalipa pesa za kumuona dakitari, baadaye vipimo vikaanza, na hatimaye dakitari akashauri nilazwe…nilazwe, gharama atalipa nani, nikajiuliza moyoni, sidhani rafiki yangu atakuwa na uwezo huo zaidi. Kipindi hicho mke wangu alishaondoka , nafikiri kutafuta chochote.
‘Rafiki yangu, mimi nakushauri kitu, wewe fuata utakachoambiwa na wanaokusaidia, cha muhimu hapa ni afya yako, mengine tuachie sisi..’akasema Yule rafiki yangu nami nikamkubalia, kwani namuamini sana, huenda ataitisha harambee kijiweni nitapata chochote. Na kweli kesho yake alikuja na pesa za malazi ya hapo na baadhi ya dawa, lakini hazikutosha kitu.
Baadaye dakitari alikuja na vipimo, akanikuta mimi na mke wangu, aliongea moja kwa moja na kusema ‘jamani ugonjwa huu unahitaji upasuaji wa haraka, na mngechelewa kidogo tungesema mengine, na tumegundua kuwa mgonjwa ana upungufu wa damu, kwahiyo kabla ya hiyo operesheni anahitajika kuongezwa damu, nahii mtaifanya wenyewe au mtoe pesa ili ipatatikane damu ya haraka. Na kingine kabla ya huu upasuaji tunahitaji shilingi laki tano kama kianzio kwani gharama ya upasuaji ni shilingi laki nane na hamsini….’
Mengine yaliyofuata wala sikuyasikia, sijui kilitokea nini nikapoteza fahamu. Nilipozindukana nikajikuta chumba cha wagonjwa mahututi, na ninasubiriwa nizinduke ili wakanifanyie huo upasuaji. Nikasema hivi hizo pesa wanafikiri tutazipatia wapi, manake kwa mahesabu ya haraka nahitajiwa zaidi ya milioni moja, pesa ambazo zijawahi kusishika mikononi. Mara nikaingizwa chumba cha upasuaji kumbe damu nilishaongezwa sina habari.
Baada ya siku tatu, nikawa naendelea vyema, na mara akaja rafiki yangu kuniangalia hali , nikiwashukuru kwa misaada yao. Rafiki yangu akasema, sisi misaada yetu ilikuwa midogo sana, zaidi nafikiri wa kumshukuru ni mkeo, sisi tulikusaidia shilingi laki moja tu, mambo mengine anajua mama watoto wako inabidi umpe shukurani hizo. Wakati tunaongea hivyo, mara mke wangu akaingia na mwanaume mmoja, nilimkumbuka haraka, alikuwa mshikaji wa mke wangu kabla sijamuoa.
‘Naona mgonjwa wako anaendelea vyema ..’ akasema huku anamwangalia mke wangu kwa sura nisiyoipenda. Akanigeukia na kutoa tabasamu la uwongo. ‘pole sana mgonjwa, halafu akatoa bulungutu la hela akampa mke wangu nakusema hiyo hela itamalizia deni na mambo mengine, msijali sana..’ halafu akaondoka.
Nilimdadisi mke wangu akakubali kuwa gharama zote alikubali kulipa huyo mpenzi wake wa zamani, `sikuwa na jinsi mume wangu, na hakuna mtu angekubali kukulipia gharama hizo , lakini nilivyomuelezea huyu jamaa akanikubalia, nashukuru sasa umepona’ akasema akinijia kunipapasa kichwani. Nilitamani kumwambia aondoe mkono wake lakini nikashindwa. Nakumbuka rafiki yake mmoja alishaniambia kuwa mke wangu bado ana mahusioni ya kificho na huyu jamaa, lakini sikumjali kabisa, nikidhani ni fitina tu za wapita njia. Sasa ndiyo huyu kabeba gharama zote za matibabu, kwa malipo gani, ni kwa deni au ni kwa vipi?
Nilimuulizia mke wangu kuhusu hizo gharama akasema hayo hayanihusu kwa sasa chamuhimu ni afya yangu. Aliongezea kuwa hatudaiwi chochote kisiniumize kichwa. Nikajiuliza, nishukuru au niumie kimoyomoyo jamani , wivu sina lakini moyo unaniuma! Ingekuwa wewe ungefanyaje? Kupona nimepona lakini mke wangu kafanyaje mpaka akapewa hela zote hizo? Na kama nikigundua baadaye kuwa kuna mahusiano yaliyasababisha kupatikana kwa hizo hela nifanyeje… kwakweli wivu sina ila moyo unaumia sana!
Mimi bwana mawazo
7 comments :
Pole sana bwana mawazo la kwanza sahau kabisa yaliyopita, ujifanye kama huyajui na ugange yajayo, kwani afya yako ni muhimu kuliko chochote.
Chamuhimu ni kukaa na mkewe umuulize je upo tayari kuishi na mimi, kama akisema yupo tayari basi wekeaneni mazingira ya kuhakikisha hakuna kusalitiana.
Mimi sioni chakufanya hapo, kwani asingekuwa mkeo kujitolea mhanga ungekuwa wapi!
Nyie wanaume bwana, kila kitu wanawake, wanawake, ina maana wanaume hawakosei?
Na muone jinsi gani wanawake tulivyo na roho ya huruma, tupo tayari kuuza utu wetu kwa ajili ya afya zenu, bado tu wanawake, wanawake, kama ningekuma mimi ningelimuachilia mbali afe, halafu tuone kama sitapeta na mshikaji mwingine!
Tukubali kwamba kuna mahala inabidi ufumbe macho, hasa panapohitaji uhai wa mtu, hiyo ni dharura bwana, kwani hata hivyo , si bado ni wako hajamchukua jumla, eti...wivu utakuua bwana we, kwanza umeishiwa, pili mgonjwa , tatu una wivu...
Sasa naamini kuwa wanaume ni wagumu kuelewa. Hata kama wao bado wanapendana, lakini haoni kama kweli ni nani anapendwa kwa dhati. Yaani hapo hata helewi kuwa amependwa kwa kupendwa sio amependwa kwa pesa. Kwa sababu kama huyo mwanamke angependa pesa na sio penzi nadhani hangeishi na yeye. Ndo panakuja pale watu wanasema wanaume ni kama watoto lakini sio wote. Wewe mpaka roho ikuume kisa nini badala ya kusema AHSANTE. Mmmmh naacha!!!!
Wivu huua! shukrani ya punda ni teke. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
Yasinta umesema kweli kabisa. Hapo anayependwa ni mume yule mwingine anapendewa pesa.
huruma! hisia, mapenzi, kifo!
YULE BWANA HATA KAMA ALIKUWA MPENZI WAKE WA ZAMANI NI ZAMANI TU. NA HAKUWA ANAMPENDA KAMA WEWE MME WAKE. NDIO MAANA ALIJITAHIDI KWA KWA KILA NJIA ILI AOKOE UHAI WAKO KWA VILE BADO ANAKUHITAJI SAANAA. LA SIVYO ANGEKUACHA UFE ILI ATESE NA HUYO MSHIKAJI.
JE, WEWE UONI KAMA ANAKUPENDA KWA DHATI HUYO MKE WAKO? HAYO YOTE NI MAPITO TU. USI2DANGANYE KUWA WIVU HUNA, KAMA WIVU HUNA ROHO ITAKUUMAJE? WIVU UPO PALEPALE NA KWA SABABU YA MAPENZI KWA MKE WAKO.
ITABIDI USAMEHE YOTE, NA MSHUKURU MUNGU NA KUMPENDA SANA MKE WAKO KWANI BILA YA JITIHADA ZAKE USINGEPONA. KWANI NA YEYE ALIKUWA MUWAZI KWAKO WALA HAJAKUFICHA KITU.
FUNGUENI UKURASA MPYA NA MKE WAKO NA UWAZE MAPENZI YENU UPYA. SAHAU YALIYOPITA.
Post a Comment