Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, August 30, 2010

Ni nani kuwa kiongozi wetu 3?

Watu walikuwa wanazidi kuongezeka kila muda ulivyokuwa ukipita, mpaka walizi wakakata wakashindwa
nini wafanye ili kuwazuia watu wasidi kuongezeka. Na huku Yule kichaa akizidi kupoteza muda, kama vile alikuwa akiwasubiri watu wote wafike kwenye mkutano huo, kabla hajamtaa huyo kiongozi wa matumaini.


‘Jana asubuhi alinijia mgeni nyumbani kwangu…’ Yule kichaa akaanza kusema kwa unyenyekevu na sauti ambayo ilionyesha dhamira ya kile alichokuwa akitaka kusema. Alipotamka maneno hayo watu wakaguna, wengine walishindwa kujizuia na kusema, `nyumbani kwako wapi, vibarazani mwa watu au majalalani.

‘Mgeni huyu nilipomuona tu, nikafikiria shari, kwani shari na ubabe ndio sera yake, na alipofika kwangu alisimama kama asikari akasema kwa sauti ya ukakamavu ‘mimi ndiye ninayefaa kuiongoza nchi ya matumaini, kwasababu kwanza jina langu ni `NGUVU’ na uwezo wangu unadhihiri hili, ninahistoria ndefu ya kutawala sehemu mbalimbali kwa kutumia wasifa wangu, sina haja ya kuongea mengi, kama wanataka kunichangua hawatajuta kwa hilo…’ akageuka kama askari na kuondoka zake.

Kwakweli nilitafakari sana, na kusema, hivi kweli katika dunia hii ya sasa, nyakati hizi tunahitaji `Ubabe katika uongozi, udikiteta umepitwa na wakati. Mimi naona tusubiri huenda atakuja mwingine ambaye ataendana na nyakati hizi.

‘Wakati nimekata tama ya kusubiri mara mlango ukagongwa, na sasa uligongwa mbele ya kichwa changu mpaka nikasikia ubongo kama unataka kutoka…’ aliposema haya maneno watu wakaguna, kila mmoja aliwaza lake, wengine wakasema nyumba anayozungumzia huyu kichaa, kumbe ni kichwa chake au ni huko kuchanganyikiwa nini..

‘Mgeni huyu alikuwa mtanashati, tai na kila kitu kuonyesha mpangilio wa maisha yake, nilitabasamu nilipoona tabasamu lake likiongezeka usoni. Nikamkaribisha vizuri naye bila kupoteza muda akaanza kuniambia nini kilichomleta kwangu. Alisema dunia nzima huongozwa na wasomi, watu wenye akili kama jina lake lilivyo. Yeye anaitwa AKILI, na ndiye mwenye haki ya kuitawala nchi ya matumaini. Akasema, kuwa zamani kabla ya uhuru mtawala `NGUVU’ ndiye alistahili kwasababu tulihitaji uwezo huo, vita na nguvu nyingi ili kujikomboa, lakini sasa tuna uhuru, kinachohitajika ni kuujenga uhuru wetu na wasomi ndio wanaoweza kuijenga nchi ya matumaini.

‘Huyu aliongea sana, si unajua tena ukiwapa hawa watu nafasi huongea zaidi na zaidi , mpaka nikachoka kumsikiliza. Niliwaza sana, ndio tunahitaji watu wenye `akili’ wasomi wa kila namna, lakini wasomi wengi wameididimiza hii nchi kwenye mambo ambayo huleta maendeleo lakini yana madhara kwa upande mwingine. Ina maana bado ili kuwe na matumaini kunahitajika aina Fulani zaidi ya uwezo, ili hawa wasomi, ambao nembo yao ni AKILI, wakishirikiana na walinzi, wenye nembo ya NGUVU, kuwekwa pamoja na kuleta kile tunachotaraji.

‘Sasa hivi wasomi ni wengi, je ni msomi yupi anastahili kutawala, dakitari, injinia, mkemia , mwalimu, mwanasiasa n,k. ni yupi tumpe nchi ya matumaini. Nikashindwa kupata jibu, na nikakumbuka wale madakitari waliovumbua mambomu ya kuangamiza watu, nikakumbuka wale wasomi waliotumia usomi wao kuihujumu nchi….mwisho wa siku nikaona bado sijampata kiongozi sahihi. Nikasema ngoja nivute muda, huenda akaja anayestahili.

Ilipofika jioni wakati nimekata tama, mara mlango ukakongwa. Na aliyeingia sasa hivi, alikuwa jamaa aliyechoka, nafikiri kwasababu ya safari ndefu au kuwaza sana au …nikashindwa hata kumtambua umri wake au ni mtu wa namna gani.

‘Najua hata wewe umenisahau, kama ilivyo dunia na walimwengu. Dunia sasa hivii inayumba kwasababu ya kukosa watu kama sisi. Dunia inatikisika kwa mabomu, uangamizi usio na faida, kwasababu ya kutumia na akili pasipoo na mapangilio. Dunia sasa hivi inahitajika kurejea enzi za watu wa zamani, watu wenye kutumia akili kwa mpangilio, watu wenye kutafakari, nini nikifanya leo kitaleta athari gani baadaye, nini nipange ili mpangilio huo usadie wote, tajiri au masikini , mkubwa au mdogo, ili kila mtu apate kile kilichomsatahili bila kuoneana. Dunia ya sasa inahitaji watu wa namna yangu…’

‘Watu hao ni nani?’ nikamuuliza kwani nilshachoka na nilidhani huyu naye anaweza kuendelea kuongea kama alivyoongea Akili.

‘Dunia hii inamuhitaji HEKIMA. Hekima ndiye kiongozi muadilifu, hekima ndiye atakayeweza kuwaunganisha wenye nguvu na dhaifu, hekima ndiye atakayeweza kuzielekeza akili zetu na elimu yetu katika mambo yenye manufaa, kuliko maangamizi. Waambie watu wako kama wanataka nchi ya matumaini basi nitakuja tushirikiane nawo na ni matumaini yangu tutafanikiwa….’ Akaondoka.

Nilipumua na kutabasamu na nikasema hatimaye tumempata kiongozi wa nchi ya matumaini, na ninawaambia, kiongozi mwenye sifa zote alizotaja mkuu wetu ni Hekima, kwasababu akiwa kwa warefu yeye ni mrefu kuliko wote, akiwa kwa wafupi yeye ni mfupi kuliko wote, akiwa kwa mijitu yenye nguvu yeye ana nguvu kuliko wao, halikadhalika, wanyonge, wasomi na wote atakuwa kama wao na kuziweka akili zao kihekima, kwani yeye hutumia hekima katika maamuzi yake. Ahsanteni.

Nderemo vifijo, vigelegele, vikatanda, hewani, kila mmoja akimkumbatia mwenzake na kusema `hatimaye tumempata kiongozi wa matumaini ‘. Hali ili iliendelea na hakuna hata mtu mmoja aliyekumbuka kwenda kumpa mkono Yule kichaa, ambaye alitoweka kiajabu na haijulikani tangu leo huyo kichaa kaenda wapi!

Ni mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

8 comments :

Anonymous said...

Hatimaye nimekupata, kama nilivyosema awali, watakaokuelewa ni wale wafikirifu, wenye uoni, vinginevyo mtuu ataona ni story ndefu isiyoeleweka.
Kwa mafikira ya kina utaona dunia ikitawaliwa na `miguvu ya mataifa makubwa, nini hatima yake, na ndani yake wapo wataalamu wasomi(AKILI), nini hatima yake.
Inaonyesha kuwa miguvu na akilii bila busara ni hakuna kitu. Ni ujumbe muria huo toka kwa emu-three, mwenye akili na utambuzi atambue, mimi nishatambua je wewe?

Anonymous said...

MMMH! NI KWELI M3. WEWE UPO JUU. CJUI WADAU WAMELIONA HILO? JAMANI MWENYE MASIKIO NAASIKIE, UJUMBE UMEFIKA WAKATI MUAFAKA. KWAHIYO WENYE MASIKIO NAWASIKIE.

EDNA said...

Kazi nzuri emu-three....

emuthree said...

Nashukuruni sana, kama kile nilichotaka kukieleza kimeeleweka, ni ujumbe kwetu sote hasa kipindi hiki cha Uchaguzi, ni vyema tukamchagua kiongozi mwenye Hekima! Kutokana na hekima hiyo ataweza kukubalika katika kundi lolote, ndio maana nikasema kiongzi huyo `atawashinda warefu wote, wafupi wote , wanene wote , wembamba wote na nk. Na hii inawezekana kama kiongozi huyo ana hekima, hekima ipo juu kwa kila jambo. Na ili jambo lifanikiwe vyema, ni lazima `hekima' itumike, hasa katika uongozi!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mh, nami ntagombea, si nina hekima?

Anonymous said...

Kamala, unaweza ukagombea mkuu, lakini naona kama umechelewa,..
Labda tutafute maana na sifa za hekima, lakini `kichaa wetu kayeyuka, tutamuuliza nani?'. Na hapa ndipo tatizo linapojitokeza kuwa tunapopata kitu tukitakacho tunaanza kusherehekea hata kabla kitu hicho hakijakidhi ile haja!
Wananchi hawa walianza kusherehekea wakijua kuwa wamempata hekima, kwao wao inatosha, ila kwetu sisi, ni je hekima ni yupi na anapatikana kweli na je tutamjuaje na kwa sifa gani?

chib said...

Makini sana emu three. Nimekufuta jasho

Anonymous said...

These are actually enormous ideas in regarding
blogging. You have touched some fastidious things here.

Any way keep up wrinting.

My weblog - cheap legal highs