Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, August 27, 2010

kufa kufaana

‘Nataka akili tatu na spidi mbili’ nikasikia mtu anaagiza vitu hivyo kwenye kibanda cha muuza kuku wa kukaanga, nafsi yangu ikataka kujua hivyo vitu ni vitu gani, mara Yule muuza nyama akachagua miguu ya kuku mitatu na vichwa viwili vya kuku, nikaamini kweli shehe wangu alichokuwa akiongea siku ile ni kweli.


Shehe wangu alisema, imefikia hatua kunguru wanaamua kunyakuwa hata chakula cha mtoto ndani kwasababu vile vitu alivyotakiwa ale havipatikani siku hizi. Zamani mtu akichinja kuku vichwa, miguu ya kuku, utumbo vinatupwa ili kunguru naye ajipatie riziki yake, sasa siku hizi havitupwi tena, hivyo ni biashara kubwa mitaani.

Sasa umezuka mtaji wa ukoko, ukoko ule ambao sehemu maarufu kama mahotelini, mashuleni au hata majumba ambapo wanapika chakula kwa wingi na vyakula kama ubwabwa lazima ukoko unabakia na mwisho wa siku huwa ni wakutupwa, siku hizi hautupwi ni biashara nzuri kwa wafanya biashara wa barabarani na kwenye vilabu. Ukoko huo huchukuliwa na kutengenezwa tena kinamna ambayo wateja wake wanautaka, hutaamini watu wanauogombea kama mpira wa kona.

Wakati nawaza haya, nikasikia watu wanaongelea maajabu mengine ya kugombea maiti. Niligeukia upande ule kusikiliza haya mazungumzo ya ajabu kabisa. Watu wamefikia kutoana ngeu kwa sababu ya kugombea maiti. Maiti kafariki karibu wiki mbili zimeshapita, pande mbili hazikubaliani wapi maiti akazikwe, kila mmoja anadai maiti akazikwe kwake!

Kisa hiki kilikuwa cha namna yake kwani marehemu huyu alifariki bila msaada wowote, kipindi anaumwa ndugu na hata mkewe ambao sasa wanamgombea hawakumjali. Ndugu walikata mguu kwasababu eti walikuwa hawajaliwi na mke wa jamaa, wakija kuwatembelea mke mtu anawadharau na kuwanyanyasa, basi wakawa hawafiki tena kwa jamaa, hata alipoumwa sana na kuhitaji huduma za kipesa , kwani kwasababu ya kuumwa aliishiwa kabisa na kwasababu ya kuishiwa hata mke mtu akawa hamjali tena.

Jamaa wa watu akawa anasaidiwa na watoto wake ambao wakitoka shule wanakwenda kuuza vitu mitaani halafu ikipatikana pesa wananunua dawa na chakula kwa ajili ya baba yao. Mke akawa hakai ndani anadai anakwenda kwenye biashara zake na anaweza akakata wiki haonekani nyumbani. Hili wanawake watasema `kwanini wao, lakini tukio hili limetokea inabidi tuliseme, kuwa kuna wachache wanakosa fadhila hasa hali mbaya inapotokea nyumbani.

Hali ikazidi kuwa mbaya na jamaa akafariki ndani ya nyumba yake nzuri tu, na baadhi ya mafremu ya biashara ambayo yalikodiwa na pesa nyingi ilishalipwa na waliokodi hizo fremu zaidi ya mikataba yao, kwani jamaa ilibidi awe anawakopa kila baada ya muda na matokeo yake wakawa wamelipa zaidi ya mikataba yao.

Ndugu waliposikia ndugu yao kafa wakaja nyumbani cha kwanza ni kudai kuwa maiti itapelekwa kwa kaka yao mkubwa nje ya mji, kwani familia yao wote huzikwa huko. Mke mtu akasema hakuna kitu kama hicho, kwani wakati anaumwa hamkuonekana na marehemu alisema atazikwa karibu na nyumba yake hapahapa. Kauli hiyo iliungwa mkono na watoto. Ndugu wakasema hilo halitawezekana kwasababu ni taratibu za familia yao wote huzikwa sehemu moja.

Ugonmvi ukawa mkubwa hadi watu kutishiana amani hadi wakuu wa dini wakaitwa, haikusaidia, jamaa wakaingia mahakamani, na kesii hiyo itasikilizwa karibuni.

Hebu jamani nisaidieni, inakuwaje watu wanagombea maiti, wakati marehemu akiwa haii hawakumjali kabisa,na tena akawa anaumwa bila msaada wowote sasa kafa wanamgombea, nini wanachotaka kutoka kwa marehemu, huo upendo umetoka wapi baada ya mtu kufa…. zaidi ni kuwa watu hawa wanatafuta upenyo wa kuwafisidi watoto wa marehemu ili wazichukue mali za marehemu na mwisho wa siku watoto wanabakia bila chochote!

Ndio jamaa akasema siku hizi kufaa kufaana, vile vya kutupwa sasa ni biashara, maiti sasa anagombewa, kwani mwisho wa siku kuna mabaki na mabaki hayatupi na mali za marehemu watu wataambulia chochote!

Huu ndio ujumbe wa ijumaa

6 comments :

Simon Kitururu said...

‘Nataka akili tatu na spidi mbili’ hahahaaa imeniua sana oda hii.

Siku hizi kila kitu mtaji. Michango ya marehemu, Kichenni Pati, harusi, Sadaka kanisani ....nk.... ukichunguza waweza kutokwa na imani ya utu wa huyu kiumbe aitwaye BINADAMU.:-(

Anonymous said...

Hii ipo kwa baadhi ya watu, wengine wanasababu kudai marehemu azikiwe mahala fulani au nyumbani kwao kwa asili, lakini wengine ni ushabiki tu, siunajua kuna watu wanapenda ushindani.
Kwa hawo inaonekana wanakitu wanakitafuta hasa kama kuna nyumba na vitu fulani wengine wanapenda msiba ukae kwao, ili michango na hatimaye utaratibu mzima wa kumiliki unakuwa mikononi mwa huyo aliyebeba dhamana ya msiba kwa ujumla.

Anonymous said...

ahaha, kweli kufa kufaana! zamani tuliamni kuwa wachanga pekee ndio wapenda fedha mbele utu nyu,a na wapare wabahili, lakini maisha ya sasa kila mtu anaangalia kile atakachopata baada ya kufanya jambo. hapo si mali pekee wanayaongalia kwanza wanaaza na rambirambi na kisha kupewa kuwa msimamizi wa miradhi kinachofuatia, hahaha

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli dunia hii sijui ni mwisho wa dunia au? Maana hii habari ya kugombea maiti nimeisikia pia kwenye ITV kuwa marehemu alitaka kuzikwa Dar na wanandugu ambao walikuwa hata hawamjali walikuwa wanataka marehemu akazikwa kwako Bukoba. Yaani hawakujali kama marehemu ana mke na watoto hapa Dar. kaazi kwelikweli sijui mwisho wake wataanza biashara ya nini?

Bennet said...

Hii ya miguu ya kuku mienichekesha sana, lakini hii ya kugombea maiti imenifutia furaha yote, ndugu wa kiafrika tuna matatizo sana

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

duh