Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, September 1, 2010

Je wangefanya wanawake ingekuwaje?


 Hivi kweli ingekuwa sisi wanawake tungefanya hivyo sijui ingekuwaje…’ hii ilikuwa sauti ya masikitiko ya dada mmoja ambaye sasa hivi yupo nyumbani kwa wazazi wake, baada ya kukutana na mikasa mingi iliyosababisha kumkimbia mume wake ni mikasa yenye kusikitisha na kuogofya. Nikaona nijaribu kuiweka baadhi ya mingi aliyoileta ili iwe fundisho na huenda tukijadiliana tunaweza kusaidia kitu.


‘Mume wangu nilimpenda sana, sikudhani kuwa haya yote yangetokea,na hata waliponikanya wazazi wangu wakati nilipowatamkia kuwa nataka kuolewa na mume huyu uliokuwa , sikuwaelewa, kwani pendo lilikuwa limekita kwenye mtima.

‘Mimi nina imani sana na dini yangu na mambo yakishirikina huwa siyaamini, lakini mikasa iliyonipata ilinifikisha niogope, sio kwa ajili yangu, ila kwa kiumbe hiki…’ alimuonyesha kidole mtoto wake na kutabasamu. Tabasamu lake lilifichua uzuri uliokuwa umefifia kwasababu ya huzuni, na kukonda kwa mawazo.

‘Mikasa hii ilianza pale tulipoamua kumtafuta mfanyakazi wa ndani, ingawaje nilishakumbana na mengi kabla, lakini hayo ya mwanzo yalikuwa hayanipi shida sana. Nakumbuka ipo siku niliambiwa na rafiki yangu kuwa mume wangu yupo chumba cha wageni na mwanamke mmoja wa jirani yangu, sikuamini, lakini kwa shingo upande nilifuatana na Yule aliyeniambia, na tulipofika kwenye nyumba hiyo ya wageni, tukasikia ndani watu zaidi ya mmoja wakijadili maswala yao ya biashara, nilimkasirikia sana huyu nilyemuita palepale `mbea, mvurugaji wa ndoa za watu’ nilimuita hivyo, kumbe yeye alishashuhudia vitendo vya mume wangu mara nyingi na sasa aliona imezidi kiasi.

Mfanyakazi alipoletwa tulikaa vizuri mwanzoni, lakini siku zilivyozidi kwenda nikaona kiburi cha Yule mfanyakazi kinaongezeka, na nikimsema mume wangu anaingilia kati, akisema namnyanyasa kwasababu ni mfanyakazi wa ndani, wakati mwingina ananiambia ni matatizo yangu ya ujauzito ndio maana namchukia mtoto wa watu bila sababu.

Siku moja nilirudi nyumbani nilikuwa naisikia vibaya, nilipofika nikakuta gari la mume wangu nje, wakati aliaga kuwa hatarusi leo, nikajisemea moyoni huenda safari imeahirishwa.

Nikaaingia chumbani kwangu, nikakuta kitanda, nilichotandika mwenyewe asubuhi kipo shangalabaghala, nikasema, labda mume wangu alichoka akaamua ajipumzishe, lakini hali ya hewa iliyokuwemo humo ndani haikunipa raha. Nikamuita mfanyakazi wa ndani, mara akatokea chumbani kwake akiwa na khanga moja, huku kainamisha kichwa chini.

‘Vipi mbona upo hivyo unaumwa’ nikamuuliza nay eye akasema anajisikia vibaya tu aliamua alale kidogo.

‘Mume wangu karudi saa ngapi, na mbona chumbani kwangu kupo ovyo-ovyo’ nikamuuliza kwa hasira.

‘Alirudi muda kidogo, na-na, sijui kuhusu chumbani kwako, wewe siulisema tusiingie huko…’ akasema kwa kigugumizi.

Kichwani nikasema kama sio huyu mfanyakazi wa ndani basi mume wangu aliingiza mwanamke humu ndani, na hili nilishaambiwa na majirani kuwa nikiwa kazini mume wangu anaingia na wanawake, niliwaambia huenda ni wafanyakzi wenzake. Nikaona nisiumizekichwa change bure na kwa vile najisikia vibaya, ni heri niya-ache kama yalivyo, nikijifungua nitapambana nayo mwenyewe, na huenda ni matatizo ya mimba ndio yananipa zana hizi potofu. Nikaa kwenye kiti nikamsubiri mume wangu ambaye alikuwa anaoga. Sikutaka kulala pale kitandani tena, na wakati nimeinamisha kichwa change kwenye kiti, macho yangu yakaona chupi ikiwa pembeni mwa kitanda.

Mimi sina tabia yakuweka chupi zangu ovyo , na ninauhakika niliondoka kukiwa kusafi na ile chupi ni ya kike.Nilipoikagua nikagundua ni chupi ya mafanyakazi wangu wa ndani…....

***********
Ngoja tuishie hapa kwa muda, nini kiliendelea tutaleta baadaye, tunahitaji maoni kwa wingi ili tuwekane sawa.

Imeletwa kwetu na tunawakilishwa!

2 comments :

Yasinta Ngonyani said...

Namsifu sana huyu dada kwa uvumilivu wake na pia kwa uaminifu wake. Sio wanawake wote wangeweza kuvulimia kiasi hicho hasa alipomkuta mfanyakazi wake katika hali hiyo na halafu mume wake anaoga. Ni kweli nami najiuliza je angakuwa mwanamke amefanya hivyo ingekuaje?? Najiuliza kwa nini wanaume wanatamaa sana? SIO WOTE. Nasubiri muendelezo

Anonymous said...

Mmmmmmmmmmh! Jamani hawa wanaume wetu, hawatoshekiiiiiiii? Hizi kesi za wasichana wa kazi na wa baba wenye nyumba ni nyingi mnooooo!!!1

Hebu 2subiri m3 amalizie hii stori 2one.

Lakini kosa afanye mwanamke ndio kosa, ila mwanamme ni bahati mbaya, ooh ibirisi nk. Hayaaa.