Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Thursday, August 12, 2010
Mungu akipenda
'Hii ilikuwa ndoto yanagu kuwa ruban1, na kweli ilitimia, sasa hivi naendesha ndege, vipi wewe mwenzangu ndoto yako ya kuwa mtu wa kuogopewa duniani imetimia' haya yalikuwa mzungumzo ya jamaa wawili waliokutana bila kutegemea baada ya kuachana shule miaka karibu kumi na tano iliyopita.
'Naweza kusema ndoto hiyo ilikuja kinyume na nilivyotarajia, kwani baada ya kuachana pale mimi nilijiunga na jeshi na huko sikukaa muda mrefu nikaacha, sasa ule ujuzi wa jeshi ukanitia mshawasha nikaanzisha kikundi cha ujambzazi...'
'Nini kikundi cha ujambazi..
'Ndio usiogope rafiki yangu, nimeachana na hiyo kazi kabisa sasa mimi ni mjasiriamali mwaminifu baada ya kutoka kifungoni, na najuta kwanini niliweka nia kama ile ya kuwa baadaye nataka kuwa mtu wa kuogopwa. Nilichoomba kilikuja kwa mtizamo mbaya badala ya kuogopwa kwa mambo mazuri, nilikuja kuogopwa kwa mambo mabaya. Hili lilinipa fundisho kuwa hata watoto wetu jaribuni kuwapa moyo wawe na matumaini ya vitu vizuri.
'Ninawashangaa wazazi wanaowatukana watoto wao kwa majina mabaya, wewe jambazi mkubwa wewe ibilisi mkubwa wewes ijui nani, haya maneno sio mazuri kwa watoto wetu wanakuja kuyavaakitari, haya yanayowajengea taswira nzuri ya baadaye, kuliko kuwakatisha tamaa pale wanapokosa. Hili nilijifunza katika maisha yangu, kwani wakati mwingi nilikuwa nikipata vipigo kwa wazazi wangu na kuniita kuwa wewe utakuwa jambazi, wewe mtoto mbaya, ...Nini matokeo yake, ndiyo hayo, nikauonja ujambazazi..licha kuwa nilibahatika kupata elimu bado nilikuwa na mawingu mabaya kichwani mwangu. Ni vyema tukawaita watoto wetu na kuwapa matumaini mazuri kuwa wewe utakuwa raisi, wewe utakuwa dakitari. .'.alisema kwa uchungu
Maisha yale yaliniweka pabaya, kwani kila tulivyofanikiwa kupora mali za watu ndivyo nilivyotamanai kufanya zaidi na watu wakaogopa hata kusikia jina langu...'
Picha juu ni enzi za shule sijui jamaa zangu hawa walifanikiwa kufikia ndoto zao, huenda walifanikiwa baadhi, lakini kila ukitumaini jambo muweke mungu wako mbele kuwa mimi napenda kuwa mtu fulani mungu akipenda.
Ni mimi: emu-three
6 comments :
du jamaa anasikitisha sana, lakini kwa upande mwingine nakubaliana na mtazamo wa kutowapa majina ya ajabu watoto wetu kwani mwisho wa siku athari yake inakuja kuonekana.
Utakuta mtu anamwita mtoto, Jalala, Majuto, Sikujua, Sikudhani, Siyawezi, Sihaba na mengineo mwishowe watoto wanakuwa na tabia zinazoendana na majina hayo
Hiyo picha kuna watu nawafahamu kidogo, niliwahi kuwaona kwenye shule moja iitwayo Umbwe, nilikuwa kidato cha nne wao wakiwa kidato cha sita, siui hawa watu wapo wapi sa hizi, nafikiri kuna baadhi nilisikia wamehsfariki dunia, siyakumbuki majina yao , lakini sura nazikumbuka kidogo, huenda wengine haream po ni wazee na sura zimebadilika.
Inawezekana wengine hapo walimeet dream zao, wengine ni Chieaf Auditor, Ma-Accountant, Ma-manager...kwasababu nakumbuka hawa walikuwa wakisomea ECA
Nakubali kuwa si vizuri kuwatukana watoto. Huwa nashangaa sana nikikuta mzazi kakasirika halafu anafurumusha matusi kwa mtoto wake kama kichaa vile.
Malezi huathiri sana watoto. Kirahisi tu unaweza kumfanya mtoto ambaye angekuwa jemadari ageuke maishani mwake yote kuwa mtu wa kutojiamini tukiachana na wale wafikiao mpaka kuwa majambazi.
Lakini TUKUMBUKE PIA inasemekana MOJA ya kitu WAZAZI hukosea katika malezi ya watoto ni kuwa na staili ya aina moja tu ya malezi kwa watoto wote.
Watoto hutofautiana. Na kama una watoto zaidi ya mmoja kumbuka kuwa STAILI unavyomlea mmoja sio lazima iwe sawa na umleavyo mwingine hasa kama unawachunguza.
Kuna watoto ambao kukaripiwa tu inatosha wakikosea na kuna ambao LABDA wanahitaji mpaka bakora pia.
Kwa hiyo unaweza kukuta unachapa mtoto ambapo angestahili kukalishwa kitako tu na kuelezwa kuwa anachofanya si sahihi na kutokana na hilo hapewi pipi mwezi huu.
Kuna mambo mengi huwa yanasaulika mzazi/mlezi anasahau kama labda huyo mtoto kafanana na yeye na anasema lione kwanza kichwa kama bundi, je amejiangalia mwenyewe?
Na hilo la kuchapa viboko wengi wanafikiri wakimchapa mtoto viboko atasikia na kuacha kumbe ndo kwanza anampa usugu. Kwa kweli kulea ni kazi...
Pichani, yupo mzee mzima Yaser, Kingu, Mzee,Muktar,...wengine nimewasahau
Duh.
Post a Comment