Wakati nawaza hili tukawa tumefika eneo la jengo la Wamachinga, wenyewe wameamua kuliita kizungu, `Machinga Complex’ Hii Machinga haina kizungu, nasikia Machinga, imetokana na neno `maching guy’ watembea kwa miguu, eti wadau mnalijuje hilo? Hebu tuachene na hilo tuendee na kusudi la tukio hili.
‘Jamani hapa tutauza nini ili tuweze kulipa kodi’ nikasikia mama mmoja akilalamika. Yeye ni mmoja waliobahatika kupata chumba katika jengo hilo, anasema vyumba humo nividogo sana, kiasi kwamba huwezi kuweka bidhaa za kutosha ili upate faida na kulipia kodi mbalimbali.
http://www.pwaniraha.com/2009/04/machinga-complex-katika-hatua-za-mwisho.html
‘Kodi hapa inaanzia elifu sitini, na bidhaa za kuuza unapangiwa kutegemeana na eneo la chumba, bado kuna kodi ndogondogo, kama ukitoka kwenda chooni ulipie shilingi mia mbili, kuna umeme hatujui hatima yake itakuwaje manake umeme nao umekatwa kwasababu ya bilikubwa, na unavyojua tatizo la umeme nchii hii…’ huyu mama aliendeela kuongea. Nikajisemea moyoni, lini nitapata bahati ya kuingia humo ndani ili nione huo udogo wa hivyo vyumba, kwani wanadai mapana yake yanaweza yawe mikono miwili, oooh, mikono miwili , sijui watauza nini, labda wauze vitu vya thamani sana, kama dhahabu, mafuta ya urembo ili waweze kulipa kodi na faida, swali litakuja, je bei hizo zitaweza kukubalika kwa wateja? Isije wakapandisha bei hata kama bidhaa hizo, thamani yake haiendani na hiyo bei, ili angalau wapate faida!
Haya ndio maisha ya bongo bwana, kunakuwa na mikakati mizuri ambayo ina malengo mazuri. Kwa mfano kwenye mikakati mingine inapangwa mwishowe inapofika katika utekelezaji mambo yanakwama, sasa sijui tatizo nini ,ni la watendaji ! Ni kwanini basi, labda watendaji wengi wameajiriwa kutokana na kujuana tu, labda watendaji hawo wanajua kazi zao , lakini malipo wanayolipwa hayaridhishi, au labda wengine ni tamaa zao tu, hii inanikumbusha jinsi makampuni na mashirika yaliyokuwa yakimilikiwa na serikali yalivyokufa, na mengine kuchukuliwa na watu binafsi.Ni kweli kuwa tulikosa wataalamu wa kuyaendeleza?
Unajua yote hayo mwisho wa siku mzigo wote unakwenda kwa mtumiaji, au mlaji, ndiye anayebeba gharama zote hizo , thamani ya hicho kitu inakuwa haiendani kabisa na bei. Ndio maana ukitaka kununua kitu sasa hivi unatakiwa uwe makini sana!
Sasa niende wapi Kariakoo au meneo ya posta? Nitawajulisha baadaye ilikuwaje
Ni mimi: emu-three
3 comments :
Bongo hii bwana, hapo gharama iliyotumika ni kubwa saana, na sijui kama inaweza kurudi. Na kwanini wasiangalie hali halisi ya biashara, au walichukulia muuza pipi na karanga ndiye atachukua chumba, na je kodi atalipia kutoka wapi
HIli Machinga Complex lilijengwa bila utafiti wa kutosha. Sita shangaa baada ya muda likigeuka kuwa kijiwe cha wafanya biashara matajiri ambao kiuchumi wataweza kuhimili gharama za kufanya biashara humo.
Watu husahau kuwa moja ya kiwafanyao wamachinga wawe mtaani ni kuwa mtaji ni mdogo na kuwa kwao mtaani huwa wanaepuka bili za jengo kitu ambacho husaidia kuweka kafaida kidogo.
Hili ndilo tatizo la kumpa kazi ya kupanga mipango ya biashara ya kuku mtu ambaye hajawahi hata kuona kuku iwezavyo kuleta matatizo.
Wanasema Chukua Chako Mapema, hapo watu washachukua chao, sasa mnawaletea longolongo, na nyie tafuteni kwenu, vinginevyo mtabakia kulalama tu.
Post a Comment