Nikiwa ndani ya hospitali kubwa kabisa ya Muhimbili, nilikuja kumwangalia mgonjwa wangu, nikavutiwa na mbu wengi waliojazana dirishani, nikakumbuka taarifa za mbu wa ajabu waliozuka Muhimbili. Nilijaribu kutafakari ule uvumi, kwani wengine walifikia kusema mbu waliopo hapo Muhimbili ni wakubwa kama nzi. Lakini niliowaona pale dirishani ni mbu wa kawaida, ila cha ajabu ni kuwa ni wengi kuliko kawaida.
'Hivi hawa mbu usiku si wanatoka hapo dirishani na kupamabana na watu' nikauliza wenzangu
'We acaha tu, wanatoka kwa wingi kama unavyowaona, lakini muda huo wengi tunakuwa ndani ya neti zetu’
‘Ina maana mtu utakuwa hutoki ndani ya neti, ukitaka kujisaidi je, au hao madakitari wanatembea na neti zao?’ Nikadadisi zaidi.
Kipindi Fulani tulisikia kisanga hichi cha Mbu waklionyesha kwenye luninga, na hatukujua nini chanzo cha kuwepo kwa mbu hao hapo Muhimbili, ingawaje uvumi wa watu unadai hawo mbu walitokana na kuzaliwa katika chumba cha majaribio ya wataalamu wakiwa katika uchunguzi wao. Sina uhakikka na hilo, lakini kwa macho yangu nimewashuhudia mbu wengi wakiwa wanatembea madirishani kwenye vyumba vya wagonjwa.
Nikiwa bado natafakari hili macho yangu yalitembelea mle ndani nakuwaangalia wagonjwa mbalimbali, Wengine hali zao zilikuwa mbaya na wengine walikuwa na nafuu, na kilichonivutia zaidi ni kuona vitanda vingine vilijaa jamaa za wagonjwa kiasi kwamba mgonjwa mwenyewe huwezi kumuona kirahisi. Nikasema moyoni, huyo mgonjwa huenda ana jamaa wengi au ni mmoja kati ya watu maarufu.
Lakini vitanda vingine vilikuwa havina jamaa za wagonjwa, wagonjwa hawa walionyesha nyuso za huzuni, wakiwatizama wenzao wakisalimiwa na kuletewa hiki na kile. Roho hapa iliniuma na kujisemea moyoni, ina maana hawa hawana ndugu kabisa, au ni wagonjwa toka Mikoani, lakini kwanini watu wasijigawe angalau wasalimie hapa na pale kuliko kuwazunguka wagonjwa wachache hadi mgonjwa anakosa hewa.
Vyovyote iwavyo, unapokuwa mgonjwa unahitaji ukaribu wa ndugu, na ukiwa mgonjwa unapoona ndugu wanakujali inakupa moyo mgonjwa na kupata faraja fulani, na wakati mwingine unauuona huo ugonjwa ulio nao ni wakaida tu, lakini unapokosa jamaa wa kukutembelea unaweza ukawaza mengi, labda jamaa wamekutenga, au ndio wameona kuishi kwako kumefikia kikomo, na vitu kama hivyo.
Kwa ushauri wangu, jamaa tunapokwenda kuwaona wagonjwa mahospitalini ni vyema tukajenga tabia ya kuwapitia wagonjwa mbalimbali kuliko kujazana kwenye kitanda cha mgonjwa mmoja, ili tupate thawabu na kuwapa moyo wagonjwa wengine, huo ni upendo mzuri kwa wagonjwa. Najua kweli kila mmoja ana hamu sana ya kumuona mgonjwa wake na kuongea naye, lakini wakati mwingine watu wanajazana kwa mgonjwa mmoja kiasi kwamba hamuwezi kuongea naye wote, hilo ni wazo langu tu.
Ni mimi: emu-three
4 comments :
Mmmmmmhhhh ngoja nami nipige ziara hapo.
Bonge la Wazo Mkuu! Naamini kabisa inawezekana kusalimia wagonjwa wengine mtu akiamua.
Hivi kama Muhimbili Mbu wanatushinda je huko kwingine si tunaimba tu katika kudai tunapiga vita Malaria?
Mungu Ibariki Tanzania!
Duuuh alafu jamaniiiii Muhimbili si Hospital ya Taifa? Kweli Tanzania safari bado ni ni ndefu.
nanukuu "Kwa ushauri wangu, jamaa tunapokwenda kuwaona wagonjwa mahospitalini ni vyema tukajenga tabia ya kuwapitia wagonjwa mbalimbali kuliko kujazana kwenye kitanda cha mgonjwa mmoja, ili tupate thawabu na kuwapa moyo wagonjwa wengine, huo ni upendo mzuri kwa wagonjwa. Najua kweli kila mmoja ana hamu sana ya kumuona mgonjwa wake na kuongea naye, lakini wakati mwingine watu wanajazana kwa mgonjwa mmoja kiasi kwamba hamuwezi kuongea naye wote, hilo ni wazo langu tu." mwisho wa kunukuu :- ni wazo zuri sana hili kwani binadamu wote ni sawa tu. Ahsante kwa somo hili
Post a Comment