Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, July 9, 2010

Ushindani wa biashara ni neema kwa wateja

`Siku hizi uwanja wa mawasiliano ni burdani na neema kwa walalahoi au mnasemaje jamani' mjamaa mmoja akasema huku akisajili namba yake ya simu. Wote tukakubalina naye kuwa kama kuna nyanja iliyo na maendeleo ya haraka ni nyanja ya mawasiliano hasa tukizungumzia simu za mikononi, achilia mbali mitandao minginekwani yote inaendana. Hii yote ni kwasababu ya ushindani wa kibiashara, wanaposhindana kuboresha huduma zao ili kuwavutia wateja ndivyo wateja wanavyowakimbilia na kwasababu wapo wengii na kila mmoja anataka chake kinunuliwe basi wanapunguza bei na hapo ndipo mlalahoii unaponeemeka. Ndio maana tukasema `panapokuwa na ushindani wa kibiashara ni neema kwa mteja.
 Hili lipo dhahiri na kila mmoja anaona, na ilikuwa kila nyanja ifanye hivyo, kwenye huduma za usafiri,  umeme, na maji kwenye huduma za matibabu kwenye elimu na hata siasa. Lakini mungu wangu kwenye siasa mhhhhh!Nashindwa kuelewa sehemu hii muhimu ya siasa hakuna kitu kama hicho, sio kwamba hakuna, ila vichwa vya watu havitaki kuelewa kutokana na mifano halisi kama hii. Hebu tuamuke kwa hili, tusing'ang'anie kula ugali tu, wakati vyakula vingine vipo kwa afya zetu. tutaishia kusota na utapia mulo wakati wengi wananeemeka kwa kula yako. Utabakia kushika tama na hata isitoshe utajiinamia kama mtotoo yatima huku hujui nini utakula kesho. Unakuwa kama mfungwa gerezani wakati haki ni yako. Amuka baba, amuka mama, amuka ndugu hakikisha una kadi yako ya kupigia kura, hiyo ndiyo hakikisho la demokrasia yako siku ikifika.

 `Bwana uwanja wa siasa kwa Tanzania, bado hatutaweza kuingia katika ushindani kirahisi kwasababu wananchi wengi hawajaelewa nini maana ya siasa. Wanachojua ni kuchagua yoyote atakayenadiwa , lakini kwanini na ili iweje sio kazi yao, wao wapoo katika kulihangaikia tumbo lao, lakini matokea ya walichochagua yanapowarudia na kuwaumiza ndipo wanapoaanza kulalamika. Na hii imekuwa kama kasumba na dawa yake sio rahisi kupatikana. Sijui labda kwa vizazi vijavyo' akasema bwana hekima.
'Inawezekana hata kesho, tatizo ni nani katika ulingo wa siasa anaweza kuwashawishi wananchi? mimi sikubaliani kuwa mageuzii ya kisiasa hayawezekani, kwasabau wanaochagua ndio sisi na tunaoumia ndio sisi , sasa kwanini tusiamue kuwa sasa tunataka wali badala ya ugali!' akasema jamaa mwingine.
'Nyie mnaweza kusema hayo na mkaelewa lakini sio asilimia kubwa ya jamii zetu hasa kijijini...mimi naona tuishie na kufaidi nyanja zilizoendelea na kutuletea neema, ngoja nikajisajili kwenye mtandao wangu kwasababu sina cha kupoteza kwahili, hawa jamaa nawakubali na hata nikikaa foleni kujiandisha najua matunda yake ni mazuri. Na nakubali kuwa ushindani wa kibishara ni neema kwetu...' akasema mama mmoja.
 Kweli hivi kuna haja ya kuingia shule ili kulielewa hili, mbona lipo wazi. Labda uwoga, labda .....sijui , ngoja niwaachie , ila nikuwaasa wenzangu kuwa kura yako ni muhimu sana unatakiwa uitafute na ukiipata uhakikishe unampa mtu unayemuamini kwa maendeleo yako ya baadaye.
From miram3

3 comments :

Anonymous said...

Unafikiri watu hawaelewi , wanaelewakabisa,lakini kuna mchezo mchafu unaoanzia sasa, wewe mwenyewe nafikiri umeuona, wapo watu wameshaanza kuwalaghai wananchi kwa pesa, na kutokana na umaikini wao wanahadaika,
Upo mchezo mchafu wa kuibiwa kura, hili lipo, sio lazima wazi kama unavyojua wewe, kuna mbinu nyingi

Anonymous said...

Unafikiri watu hawaelewi , wanaelewakabisa,lakini kuna mchezo mchafu unaoanzia sasa, wewe mwenyewe nafikiri umeuona, wapo watu wameshaanza kuwalaghai wananchi kwa pesa, na kutokana na umaikini wao wanahadaika,
Upo mchezo mchafu wa kuibiwa kura, hili lipo, sio lazima wazi kama unavyojua wewe, kuna mbinu nyingi

Anonymous said...

Sasa nyie mnafikiri nani ataiweza nchi hii, kama sio chama tawala. Wao wameshaweka mizizi toka shinani na hii sio kazi ndogo, inahitaji gharama, inahitaji busura na inahitaji usalama...sio rahisi chama kingine kikurupuke tu na kiseme kinaweza kutawala. Kitakuwa kimekubalika mjini , lakini kijijini kunahitaji busara, angalia huko Mara watu wnavyouana...unafikiri hiyo ni nini...
Mbinu lazima zitumike kwa maslahi ya nchi, kwasababu bado wananchi hawajaiva na ukiwapa wengine uongozi sasa hivi watawehuka na kuitumbukiza ncho kwenye janga...sasa muda ukifika hakuna hata kupigia debe utaona mwenyewe. Bado nchi hii changa kisiasa!