Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, July 8, 2010

Mpende akupendaye...

                      Mpende akupendayo( inaendelea kutoka `je ndoa ni kaburi la mapenzi)

`Mimi sijamuelewa mwenzangu na hatua aliyochukua ameharkisha sana, kwani sababu muhimu nilishamueleza kuwa kwanini nachelewa kurudi nyumbani na kwanini nimepunguza baadhi ya zawadi, na sio zawadi du hata huduma nyingine. Hii ni kutokana ha hali na gharama za kimaisha…’ alikuwa mume wa jamaa aliyeachwa na mkewe kutokana na kukosekana kile kinachoitwa `pendo’


Niliamua kumuona huyu muhusika ili kusikia zaidi, na hakupend kuliongelea swala hilo kiundani zaidi, lakini yale machache aliyonielezea yalinifanya nami niingiwe na wasiwasi kuhusiana na swala zima la ndoa na mapenzi ndani ya ndoa. Je tunaelewa kiundani maana halisi ya ndoa, kwanini kwanza watu waoane? Au ndio ndio tumelalia ule usemi usemao `mpende akupendae, siyekupenda achana naye..’

Kujibu Swali hili inahitaji kuelewe historia ya mwanadamu, na uangalie upande wa imani za kidini kwa upande mmoja na sharia na taratibu za jamii kwa upende mwingine. Lakini kabla hatujaangalia upande huo, inahitajika tujue kwa ujumla wake nini hasa maana ya mapenzi ambayo yanafikisha hadi watu kufunga ndoa. Mimi sio mtaalamu sana, lakini tunaweza kusaidiana sote kulinyambulisha kutokana na uzoefu.



Nakumbuka sana yale mashairi ya jamaa aliyosema yeye kapata ua lake waridi, limechipua vizuri bustanini, kila siku analimwagilia maji na kuliwekea mbolea, hata ikifikia kiangazi hulitengenezea mwavuli au kulivisha shada lenye unyeunyevu ilimradi lisinyauke, na kupoteza uzuri wake!

Yeye kalipenda ua, na kulifanyia kila awezalo ili lisinyauke au kupoteza umurua na uzuri wake, je ua limefanya nini kwake? Ndio limefanya kile anachotaka mwenye ua, limerembeka, limemvutia jamaa, na ndio maana anaendelea kulimwagilia maji na kuweka mbali.

Kwa kifupi kila jambo linahitaji uelewa wake ili ulifanye linavyotakiwa. Mapenzi sio tofauti na mambo mengine, nayo yanahitaji uelewa, ili yawe mapenzi ya kweli. Kwa mfano mtoto anampenda mzazi wake, kwanini? Kwasababu anapata zile huduma zake kama mtoto kutoka kwa mzazi wake kwahiyo hiyo hali ile inajijenga kihisia na hayo ni mapenzi kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto. Na hata kama mtoto atamuuzi mzazi wake sana, bado mzazi hata kata tama kuweka yale mapenzi yake kwa mwanae. Kwa mfano kama huyu mzazi angemtelekeza mwanae haya mapenzi yangekuwepo? Lazima yatayumba na kuweka chuki Fulani moyoni.

Watoto pia hupata mafunzo ya mapenzi kutoka kwa wazazi wao au jamii wanayoishi, na mara nyingi hii hujijenga na kuwa kigezo chao cha maisha yao ya baadaye. Ni kosa kubwa sana wazazi wanapogombana au kukosana wakafanyia ugomvi wao mbele ya watoto wao. Hii huwajengea taswira mbaya watoto na wakashindwa kuelewa nini kinachoendelea hususani katika swala la mapenzi na ndio maana watoto wadadisi watakuuliza swali kama hilo `nini maana ya mapenzi’ na wewe kama mzazi hutakiwi kugomba na kusema `wewe umechanganyikiwa nini unazungumza mambo gani yasiyo na heshima…’ na vitu kama hivyo. Hapo utakuwa umeshindwa kutimiza wajibu wako kama mzazi.

Mapenzi ni tunu ya ushirikiano ambayo wawili wapendanao wanashibana nayo. Inawezekana kushibana kwao kusiwe sawa na wengine lakini wamakubaliana nayo, kivitendo hata kama hawakukaa wakaongelea kuwe tufanye hivi au vile. Lakini hisia za kujaliana kuhurumiana na hata kkushirikia zimejijenga na kuleta thamani Fulani tunayoweza kuiita mapenzi. Inawezekana pia katika kufanikisha hilo mmoja akawa anafanya juhudi zaidi kuliko mwingine lakini mataraio yake ni kuwa mwishowe wote watakuwa katika mlinganyo mmoja.

Labda swali litakuja kwa mfano kama mmoja hakubaliana na utaratibu uliopo kutoka kwa mwenzake afanyeje ili waliweke penzi lao sawasawa. Hapa ndipo panapoleta tatizo. Tatizo kubwa la mawasiliano.

‘Ndugu yangu, kama kweli mlikuwa mkiishi hivi kuwa labda mwenzangu atanijua tatizo, au ataelewa nini hukipendi au hukitaki na ajirekebishe bila kuambiwa , mtakuwa mumekosea na matokeo yake ndio kama hayo, mwenzako kakimbia. Hatuwezi kujua zaidi labda kuna mengi yamemkwaza, lakini kosa kubwa ni kuwa hamkutaka kulielewa tatizo mkakaa pamoja mkaliongelea kiundani huenda mngefikia muafaka. ‘ Nilimueleza rafiki yangu lakini akawa anatingisha kichwa kutokukubaliana nami.

Je wewe ungeendelaje kumshauri huyu jamaa.

From miram3

4 comments :

Anonymous said...

Mimi ningemshauri atafute mke mwingine, yeye anahangaika nini wanawake tupo, akichoka huyu aje kwa yule akikosa aje kwangu, mimi nawashngaa sana, mapenzi mapenzi, mapenzi gani bila pesa

Anonymous said...

Maana ya mapenzi ni pana kutegemeana na mwenyewe. Unaweza ukasema mapenzi ni kujaliana na kusikilizana na kusaidiana na vyovyote unavyojua ilimradi mwisho wa siku nyote mnaridhika.
Sasa ikitokea msuguano ina maana hakuna kuridhika, ama kwa mmojawapo au kwa wote na hatimaye kama hakuna usuluhishi na kuangalia kina cha mgogoro mapenzi huyeyuka.
Kwa jamaa mkewe kamkimbia hakutaka kujishughulisha zaidi, huenda kuna sababu ya jamaa kuchelewa hapati lile tulizo la moyo kama awali au kazi nyingi au jamaa ndio wapenda wengi!
Ni vyema tukaangalia nini tunachokipenda ndani ya mapeni yetu tukaviboresha na kujaribu kile tusichokipenda tukikwepe, kwa mmoja au kwa wote
Ahsateni

Anonymous said...

Picha bwana, picha ndio mvuto, unajua kusoma nako kunachosha, ingawaje uliyoandika yana mantiki, lakini mvuto wa picha, hapo ungeweka mrembo...mmh ungeona mijamaa ikipitia pitia, siunajua hata kwenye maduka, akiwepo dada mrembo wateja kibao..
Kuhusu mapenzi mimi siyajui ila najua kupenda...eehe, najua kivitendo, muulize my darling...

Anonymous said...

Mbona humalizii uhondo, unatuacha hewani bwana, unajua ukituachia hewani tunashindwa kujua ilikuwaje baadaye, na tunabaki kuulizana ilikuwaje na mwisho wake tunatunga uwongo