Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, July 6, 2010

Je ndoa ni kaburi la mapenzi

`Baba eti nini maana ya mapenzi?' Swali hili lilinishitua kidogo, kwani aliyeniuliza ni mwanangu wa miaka kumi na moja, sikutegemea swali kama hili kwa umri kama wakwake, na hisia zangu zilinipeleka mbali na kutafakari sana kabla sijamjibu.
'Mapenzi??..mhhh, kwanini umeuliza hivyo mwanangu au nikuulize kwanza wewe unaelewaje neno mapenzi?' nikaona nivute muda kwa kumdadisi zaidi.
'Ndio maana nikakuliza baba, kwasababu mimi nashindwa kujua tafsiri hasa ya neno hilo, jana kwenye tamthilia watu waliuana eti kwasababu ya mapenzi, juzi jirani yetu kakimbiwa na mkewe na nimesikia eti ni kwasababu ya mapezi, kwangu nilijua kuwa mapenzi ni kitu kizuri, kuhurumiana na kupendana, sio ndio hivyo baba, lakini mbona tena nasikia tofauti, au wanakosea kuita neno mapenzi?'
 Kabla sijamjibu mwanangu taswira ya tukio la jirani yetu liliniteka akilini na kutafakari kwa kina, kwani mwanangu alivyoniuliza pia hata sisi wakubwa tunajiuliza hivyohivyo na kujifanya tunajua nini hasa maana ya mapenzi. Na ujuaji wetu ni tafsiri kutokana na utashi wetu. Kisa cha jirani yetu kilileta tafsiri potofu kuhusiana na neno mapenzi, kwani mkewe alivyoondoka aliacha barua ambayo mwishoni huyo mke aliyeondoka alihitimisha kwa kusema `ama kweli sasa nimeamini kuwa ndoa ni kaburi la mapenzi' .
 Katika maelezo yake kwenye hiyo barua alisema, kabla ya kuolewa na mumewe ambaye kipindi hicho walikuwa wakiitana wapenzi, anasema mpenzi wake kipindi hicho alikuwa anamjali na kumpenda penzi la kweli. Alikuwa akimpa kila kitu anachotaka na hata kile alichokuwa hakitaki alikipata kwa kushitukiziwa na hiyo ilimpa faraja sana. Aliendelea kusema kuwa mapenzi aliyoyapata hata nyumbani kwao kipindi  hicho hakuweza kuyapata.
'Nyumbani nilikuwa siruhusiwi kutembea ovyo, kwenda ufukweni kununua kile nikitakacho, lakini alipokuja mpenzi wangu na kutambulika kama mchumba, nikawa naruhusiwa kutoka naye, akija nyumbani tunakwenda ufukweni, tunaenda huku na huko na kuninunulia zawadi za kila namna na hata kuniahidi nyingine nyingi na ahadi ake zilikuwa sio za uongo, kinyume kabisa na walivyokuwa wakinifanyia waazi wangu, kwahiyo nilimpenda kupita kiasi na matarajio yangu yalikuwa nitazipata zaidi tukisha funga ndoa.

'Wazazi wangu waliniomba nivute subira ili nimjue mchumba wangu vyema, lakini penzi lilinifunika na pazia nyepesi usoni, nikajifanya sioni mbele. Niliwaambia wazazi wangu kama hawataki tufunge ndoa haraka basi nitatoroka. Wazazi wangu wakaona haina jinsi, mtoto akililia wembe mpe, nami nikapewa.
 Kwakweli mwanzoni niliendelea kuyapata mapenzi kama ilivyokuwa awali, lakini kila siku zilivyozidi kwenda mambo yakawa yanabadilika, hata yale maneno matamu ya mpenzi, la-azizi, na mengineyo yakawa yanapotea kidogokidogo mpaka  ikafikia nikiitwa nasikia `wewe njoo hapa...' sikuamini.
 Kilichonikwaza zaidi ni ratiba za mume wangu kubadilikabadilika, mwanzoni tulivyoona alikuwa unarudii kazini mapema, na ukija lazima uje na vizawadi na maneno matamu,ambayo yalianza kufifia kama ladha ya banzoka mdomoni, ukaanza kuchelewa na hata wakati mwingine kuamua kulala  hukohuko ukidai unakazi nyingi una mikutano unasafari za kikazi, na nikikuuliza zaidi unakuwa mkali. Je hayo ndio mapenzi mapya, na mapenzi yale ya zamani ambayo ndiyo mapenzi ya kweli yameenda wapi, je sina haki ya kukuuliza. Imefika unarudi umelewa na ukirudi hujali hata kunisemeesha unalala kama gogo, je hiyo ndiyo haki yangu ya ndoa. Nimevumilia nikaona basi kama noma na iwe noma.
 'Nakupenda sana mume wangu kwa mapenzi yale ya zamani, haya mapya mimi siyajui, nimevumilia mengi ambayo siwezi kuyaandika hapa, nimefikia tamati kuwa mapenzii yetu ya zamani yamefikia kikomo, kwani nahisi unaye unayempenda kama ulivyokuwa ukinipenda kabla hujanioa, na najua kuwa ukimuoa ataishia kama mimi, kwani mimi sasa naamini kuwa `ndoa ni kaburi la mapenzi. nakutakia maisha mema kwaheri.
 Jamani ni kweli hii kuwa ndoa ni kaburi la mapenzi?
 Hebu tujadili, pamoja kama mpo tayari kwa hili, kwani tukijadili pamoja, itakuwa rahisi kwetu kuwajibu watoto wetu , ambao wanana nitajitahidijikuta katik wakati mgumu wa kupambanua zuri na baya. Nami nitajitahidi kuelezea nionavyo mimi kwenye sehemu ya pili

From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Haya mambo ni nyeti na yanahitaji mjadala wa kiutu uzima, nitachangia baadaye