Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, July 12, 2010

Uchungu wa mwana

Ilikuwa siku ya Jumapili, na siku kama ya leo wafanyakazi wengi wapo majumbani mwao, na wengi wao hujivuta kitandani wakipumzisha miili yao baada ya pilikapilka za wiki nzima. Mara kilio cha mtoto wa miaka mi-nne na nusu kilisikiika kwenye chumba kimojawapo katika jengo hili kubwa ambalo ndani yake kuna ofiisi za kuwahudumia Watoto waliokosa wazazi na wazazi waliokuwa wanafunzi ambao waliofukuzwa na jamii zao kutokana na kupata uja uzito kinyume na matarajio yao.


Sauti ya mtoto Yule ilikuwa kubwa kiasi kwamba mama yake aliyelala naye ilibidi aamuke toka usingizini, hakutaka kuamuka mapema siku hii kama ya leo kwani kazi za kuhudumia jamii zilimchosha kupita kiasi, ingawaje alishazoea zile pilikapilika za kuwalea Watoto na kuwahurumia kutokana na kukosa wazazi au kuwauuguza wale wanaoumwa. Kazi hii aliifanya kwa wito kwani alijua wapo wengi kama hawo wanaoteseka kijijni bila huduma, na huenda angelikuwa mmoja wao kama asingekutana na huyu mama msamaria mwema.

Alikuwa ameajiriwa kwenye hili shirika baada ya kujifungua mtoto wake wa kiume Adam, mwanzoni aliteseka kidogo kwani maisha ya kuishi kwa mtu sio sawa na kuwa kwako, alijaribu sana kusahau machungu ya kadhia nzima ya maisha yake yaliyopita lakini haikuwa kazi rahisi, kila mara kumbukumbu zilimrejea na kutamani arudi kule shuleni na kukutana na mbaya wake na kuhakikisha kuwa kichwa cha Yule muuza duka kakiondoa kwenye kiwiliwili.

‘Ipo siku nitakutana naye, naapa nitamfanyia kitu mbaya’ akawa mara kwa mara anajisemea.

`Mimi siwezi kuzaa na mtu kama wewe, shepu gani ya kuipeleka kwa wazazi wangu, etii nikaitambulishe kuwa nimezaa na wewe. Nakuomba ten asana, kaitoe hiyo mimba kwasababu sio yangu, na siui umeipataje, na hela sasa sina, vinginevyo kanywe simu tujue moja, unasikia kafilie mbali huko’ aliyakumbuka sana Maneno haya machafu toka kwa Yule muuza duka siku alipoenda kumpa taarifa ya uja uzito huo.

Alimwangalia mwanae kuona kama kuna tatizo gani, na uso wake ulipokutana na uso wa mwanae, akakunja sura kwa hasira, halafu akambembeleza na kusema kwa uchungu, `ama kweli sasa naamini kuwa uchungu wa mwana aujuye ni mzazi, vinginevyo ungekuwa marehemu wewe, hebu lala huko’. Aliyasema hayo aneno kwa nguvu bila kujali kuwa kuna mtu anamsikia. Na kila anapomwangalia huyo mtoto anakumbuka kisa cha kumpata huyo mtoto amabaye kwake anamwita mtoto wa marehemu.

‘Wewe baba yako alikufa siku ile aliponitamkia kuwa mimba sio yake na sitaki kusikia ukiniulizia baba yako yupo wapi, baba yako amekufa’ alikumbuka siku moja mwanae alipomuuza kuwa baba yake yupo wapi.

‘Wewe usimwambia kabisa huyu mtoto Maneno kama hayo, kama baba yake yupo hai lazima siku ikifika utamwambia kwani ana haki ya kumjua’ mama msamaria mwema alimwambia kwa hasira.

‘Mama nikikuhadithia kisa changu kwa urefu unaweza kukubalina na haya maneno yangu, kwani baba yake sio mtu , ni mtu kwasababu ana sura ya kibinadamu, lakini roho yake ni ya kinyama. Yeye alikuwa kazi yake ni kuwaharibu wa watoto wa shule kutokana na hela zake halafu wakipata uja uzito anawaambia wakazitoe hizo mimba, je kama ningefanya kama alivyoniambia unafikiri huyu mtoto angekuwa wapi. Yeye kwake mtoto huyu ni marehemu, lakini kwa vile nipo naye basi yeye ndiye marehemu, ndio maana namwita huyu mtoto, mtoto wa marehemu’. Akasema huyu binti kwa hasira na hakutaka ushauri mwingine zaidi.

Mama msamaria mwema alitaka sana kujua kisa hicho kwa marefu, lakini mara nyingi alikosa muda kwasababu ya pilikapilika za kuihudumia jamii, lakini siku hiyo akaona aka echini akisikie hicho kisa ili aweze kutoa ushauri mwema kwa huyu binti.

Na hapo ndipo binti alipoanza kumhadithia Yule mama kisa kizima cha tukio hilo ambalo kwake aliuita mkosi wa maisha yake.

Tuwepo pamoja kesho kukisikia kisa hicho Mungu akipenda, soma sehemu ya pili na kwa ushauri toa maoni yako hapa au tuma kwa e-mail: miram3.com@gmail.com

Mimi
 emu-three

2 comments :

Yasinta Ngonyani said...

Ni simulizi ya kusikitisha na kusisimua nausubiri muendelezo kwa hamu kweli... eehh nimesahau kupiga hodi hodi ...hodi hodi hapo kibarazani..

emuthree said...

Karibu sana dada Yasinta, jisikie home, manake hapa nipo mpweke na nikipata mtu kama wewe najua mambo yatakuwa murua.