Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Thursday, July 15, 2010
Uchungu wa mwana-4
Akiwa anasubiri zamu yake mara akapitiwa na kajiu-singizi kamauzauza, na ndani ya huo usingizi akaota yupo chumba kilichojaa Watoto Wachanga. Yeye aliota kuwa ni mmoja wa wauguzi kwasababu alikuwa kavaa mavazi ya nesi, na mara akaja dakitari na kisu mkononi, akamwambia unamuona Yule pale kitanda cha mwisho, huyo ndiye mwano uliyemzaa kwa machungu makali. Aliinua uso wake kumwangalia huyo mtoto mchanga lakini sura haikuweza kuonekana vizuri, kwa sababu ya gizagiza, lakini kalikuwa katoto kachanga. Yule dakitari kwenye ndoto akamwambia.
‘Wewe siumesema mumeo hamtaki huyu mtoto, sasa chukua hiki kisu mmalize mara moja halafu tutasema mimba imeharibika’ akapewa kile kisu. Na yeye kwa hasira ambazo hakujua zimetoka wapi na zimejaa moyoni alikichukua kile kisu na kumsogelea Yule kiumbe ambaye alimwangalia kwa macho ya huruma, akakisogeza kile kisu moyoni mwa kile kiumbe, mara damu zikaanza kutoka. Mmmh, huruma ikamwingiea akakitupa kile kisu na kutoka mle odini mbio na huku nyuma akasikia kicheko cha dharau, kikisema wewe mnafiki mkubwa unajifanya una huruma sana eeeh, hapo sasa unasubiri nini, mbona unataka kukiua kiumbe kisicho na hatia’ Na mara akasikia jina lake likiitwa.
Ndoto ile fupi ilimteka mawazo akashindwa kuinuka pale alipokaa, hadi rafiki yake alipoamua kumuinua kwa nguvu, na kumwambia anapoteza muda, hapo sio sehemu ya kusubiri kwa mudamrefu. Akajizoazoa hadi chumba kiitwacho cha upasuaji. Na kweli pale mlangoni paliandikwa chumba cha upasuaji.
Alipofika mle ndani mwili ulizizima kwa woga hata wakati yule nesi anamwelekeza nini cha kufanya, alikuwa haelewi kabisa kuwa anaambiwa nini. Ile taswira na damu zikitoka mwilini mwa mtoto mchanga zilimfanya ajione muuaji . Mara alisikia Yule nesi akimwamurisha atoe nguo na apande kitandani, akafanya hivyo na alipofika pale kitandani mara ile ndoto ya Yule mtot o ikamjia akilini na kusikia sauti ya mtoto akilia akilini mwake.
Aliruka pale kitandani na kuchukua nguo zake na bila kusema kitu akasogea kwenye ile meza na kuchukua hela yake ambayo ilikuwa bado pale mezani na mbio akatoka nje, na alikuta rafiki yake anamsubiri kwa hamu, akijua mambo yameisha salama. Hakutaka hata kuongea naye akakimbilia shuleni na alipofika shueni alikusanya nguo zake na kuziweka ndani ya begi na mbio hadi kituoni cha mabasi.
‘Sasa niende wapi’ akajiuliza,.
Na mara akamkumbuka shangazi yake ambaye alikuwa akiishi maeneo ya mjini, akaona huko ndipo pa kufikia kabla hajachukua uamuzi mwingine. Alijua kabisa hata shangazzii yake hatamuelewa lakini ni heri kuliko kwenda kukutana na baba yeke ambaye sio tu atapata kipigo, lakini na mama yake itakuwa ndio mwisho wa ndoa yao.
Alipofika kwa shangazi yake alimkuta anatoka kwenye biashara zake na alikuwa hajapumzika, na haraka akampokea kwa furaha na waswasi. Na kabla hajaanza kumuelezea akaanza kuangusha kilio, na shangazi yake akakipokea kwa hisia tifauti akijua kuna mtu kafa, wakaanza kulia pamoja.
‘Shangazi mbona unashitua, niambie ukweli, nani kafa, niambia ukweli...' Alipokelewa begi la nguo na kukaribishwa ndani huku wote wanalia.Akaona asipoteze muda na kukaribisha watu wakijua kuna msiba, akaanza kumuelezea yote yaliyomsibu na shangazi mtu aliinuka kwa hasira akitaka kumzaba vibao Yule binti lakini huruma zikamjaa na kurudi kukaa. Alishindwa afanyeje, alimjua kaka yake vyema, na liogopa kabisa kwenda kumwambia, lakini sasa angefanyeje.
‘Basi wewe kaa hapa mimi kesho asubuhi na mapema nafunga safari hadi kijijini nitajaribu
kumueleza kaka, ila sidhani kama ataelewa na sijui nini kitanikuta mimi akisikia kuwa nimekupokea na upo kwangu’ Akasema huku machozi yakimtoka.
Kesho yake asubuhi na mapema shangazi akafunga safari na huku nyuma binti akabakia akimuomba sana mumngu wake amsaidie akijuta kwanini hakuitoa ile mimba kwasababu sasa kisa kimeshafika kwa wazazi wake na kitawadhuru hata wale wasiohusikia. Akasema sasa naona muda muafaka umefika wa kufanya jambo jingine. Hakutaka kabisa wazazi wake waje wamkute na kuanza kupata kupata kipigo, hakutaka kabisa ashuhudia mama yake akipata kipigo au kufukuzwa, au kuvunja ndoa ya watu, lakini sasa hayo yamkini kutokea. Akaona ni heri achukue sumu anywe.
Oh, jamaa anasema muda umeisha, kwahiyo ngoja niishie hapa na labda kwa ushauri kwa ambao kwa namna moja au nyingine yamewakuta mabalaa, sio jambo jema kukimbilia kujiua. Tusipende kukimbia matatizo kwa kuondoa uhai wetu, huo bado ni ubinafsi, na hausaidii kitu zaidi ya kuwaumiza wengine zaidi ya hivyo unavyofiukiria, Kaa chini tulia na muombe Mola, atakusaidia, kwani matatizo yapo na yameletwa kwetu kama mitihani,na wa kupambana nayo ni sisi.
Kesho tukijaliwa
Mimi wenu
emu-three
1 comment :
Kwani huyo kabila gani, mnake kuna kabla kujiua kujiua kwao sio tatizo
Post a Comment