Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Friday, July 16, 2010
`Ayaaah....'
Dereve hakumuelewa kondakta wake akasimamisha gari na wale wazungu wakapanda. Yule kondakta akaanza kulalamika kwa dereva wake, kuwa anataka kumuumbua.
'Sasa unaleta hasara, mimi hawa nitawaulizaje nauli, na hii itakula kwako, nitajifanya siwaoni, wasafiri bure, wakifika kwao waseme Tan-za-ni-a nchi zuri tuna-safiri buree' Akanisogelea pale nilipokaa akaniuliza kuwa awaulizeje nauli kwa kiingereza. Nikacheka nikamwambia aseme tu `money'. Akasema hiyo rahisi lakini najua watauliza kiasi gani hapo huoni mtihani...au..
`Ayaaah, nimeibiwa', ilikuwa sauti toka nyuma ya gari na ilikatiza kabisa mazungumzo yetu na kondakta, ikawa ni gumzo la huyo aliyeibiwa simu. Na hapo kondakta kwa ucheshi wake wa kusema ovyo akaanza kubwabwaja.
'Mimi nimewaambia kuwa kabla hujaingia ndani ya daladala kitu cha kwanza jisachi mfukoni kuhakikisha nauli ipo, na iweke mfuko wa mbele au ishikilie mkononi, simu yako utajua mwenyewe. Ukiingia ndani kama umepata siti, toa simu yako ujifanye unatuma meseji, hata kama hujui kutuma, wewe donoadonoa ti ilimradi simu yako isije ukaiacha kwenye kiti. Siunajua tena mifuko yetu haina zipu.
'Sasa kama hujapata siti, ukawa mpaka rangi, manake ukisimama ndani ya gari wewe ni sawa na mpaka rangi, mpaka rangi hakai. Wewe inabidi simu yako uiweke mfuko wa shati na hakikisha aliyeoko mbele yako unamwangalia usoni, hawezi kukuibia, kwasababu anajua unamjua. Ukishuka kitu cha kwanza kwa wewe uliyekaa kabla hujainuka kwenye kiti, shusha mikono yako yote miwili wa kushoto na wakulia, na papasapapasa pale ulipokaa, kwasababu unaweza ukaacha vijisenti vyako, na ukiiunuka haraka mwenzako ataviwahi, hakuna huruma dunia hii.
'Ukiteremka chini ya gari cha kwanza papasa mifuko yako haraka, kabla gari halijaondoka, manake mara nyingi tunapanda magari bila kuangalia namba, sasa ukigundua huna simu yako, au nauli umeshasachiwa piga kelele za nimeibiwa, na angalau kama ni simu na mwizi hajaizima utaweza kuipata, vinginevyo ...ayaaaah, hawa wazungu wanataka kushuka, sasa nijikaushe kabia kama siwaoni, manake nitawaulizaje nauli.
Wale wazungu walipoteremka, wakatoa noti ya shilingi mia tano na kuzungumza kiswahili fasaha kabisa
`Kata watu wawili, na safari njema...'
'Ayaaah, kumbe ni waswahili wenzetu, anazungumza kiswahili utafikiri wanatoka Zanzibar'!
Kwakweli abiria wote mle ndani ya gari ilibidi waangue kicheko na mmoja akasema kuwa ikipita miaka mitano, nchi yetu itajaa machotara wa mchanganyiko wa damu za kitanzania na wazungu hasa Wachina. Na kabla hajamaliza kuongea yule konda akadakia..
'Na Watanzania wote watakuwa wafupiwafupi, kama Wachina na hata mitumba itabidi ichukuliwe huko China au Japani, kwasababu wakileta toka Ulaya, nani atavaa, suruali moja inawatosha watu wawili, atavaa nani.....Ayaaah, unaona tena kile kituo kuna wazungu tena Wachina. Lakini hawo najua washajifunza kiswahili ngoja waingie.
Wazo la leo, umzanie siye anaweza kuwa ndiye.Unaposafiri usiongee ovyo kwa lugha yako, ukidhani kuwa wenzako hawasikii, unaweza ukawa unamteta mtu kwa lugha yako kumbe naye anatoka hukohuko, mwisho wa siku ukaumbuka.
Ni mimi: emu-three
No comments :
Post a Comment