Kabla hujaendelea rejea sehemu iliyopita kwa kuboya hapa:
sehemu ya nne
Halafu endelea....
Alitoka mle ndani akaelekea maeneo yenya maduka, na maduka ya dawa mengi yalifungwa, sasa akashindwa anunua dawa gani itakayomuua bila maumivu. Akaona labda sumu ya panya, au sumu gani yakunimaliza haraka. Akawa anajiuliza wakati huo akajisahau kuwa yupo katikati ya barabara. Na mara akajikuta anaelea hewa na kilo cha umeuuua, kikasikia.
Alipopata fahamu akajikuta yupo hospitalii akiwa kafungwa mabadeji usoni na mkononi. Alijaribu kukumbuka nini kilichomsibu na kabla hajapata jibu akaingia shangazii yake.Alimshangaa kumuona nay eye kafungwa mabandeji usoni, akafikiria huend naye alaipata ajali.
‘Vipi unajisikiaje?’ shangazi mtu akauliza
‘Mimi sijambo sijui wewe, mbona na wewe umefungwa mabandeji, ulipata ajali?’ akauliza
‘Aheri ningepata ajali ningejua moja, haya ni mateso uliyotuletea, lakini hayo tuyaache niambie ilikuwaje?’ Shangazi mtu akasogea kitandani kusikiliza nini kichotokea, lakini jibu alilopata sio kamwe ilivyokuwa. Mwishowe akasema kwa uchungu; ‘haya majeraha yanatokana na kipigo kutoka kwa baba yako, na sijui mama yako atakuwa katika hali gani, manake alipigwa kiasi cha ambacho sijui kama …’ ilibidi akatishe alipogundua hayo mazungumzo sio mahala paake
Siku ilikuwa ndefu na kila alilojaribu na mazunguzo yake na shangazi yalimtonesha kabisa kidonda moyoni mwake lakini hakujua nini afanye baada ya hapo. Akatafuta njia kuwasiliana rafiki yake shuleni na rafiki yake hakutaka hata kuongea naye , kwani anasema huko shukeni mambo yamekuwa mabaya mmoja wa waliotoa mimba siku ile amefariki na Yule dakitari na nesi wake wamekamatwa na haijulikani itakuwaje.
‘Huenda na mimi ningekufa, lakini ni heri ningejifilia kuliko hili balaa linaloniandama mimi na familia yangu’ akasema na kukata simu.
‘ Nimepiga simu nyumbani, kama nilivyokuambia kuwa huko niliacha balaa, mama yako hajitambui kwa kipigo alichopatya kalazwa hospitali, hatujui hali yake iatakuwaje na baba yako kakamwata yupo polisi kwa kutaka kuua…’ shangazi akasema huku kakunja uso kwa hasira. Alijua kila mtu sasa atakuwa anamchukia kwahiyo uamuzi mwingine ni kuhakikisha anaondoka kabisa eneo hilo la Morogoro, na sijui aende wapi.
Shangazi yake alip[oondoka tu, akatoroka pale hospitali na kuelekea kituo cha basi, Kituoni akapanda gari liendalo Dar-es-salaam.
Alipofika Ubungo, akahangaika mwishowe akapata mama mmoja mwenye Watoto ambaye walikuwa naye ndani ya gari akamsaidia na huyo mama akasema waende wote kwake amsaidie Watoto.
‘Twende kwangu unisaidie kubeba hii mizigo manake nimempigia simu mume wangu lakini nasikia kapata safari ya ghafla kwenda Arusha’ akasema Yule mama.
Ilikuwa Bahati ya mtende, kwani alipomuelezea Yule mama kuwa kafukuzwa na wazazi wake kwasababu ana ujauzito, kumbe Yule mama ni moja wa kiongozi wa shirika linalowasidia wanafunzi walifukuzwa shule au kutelekezwa na wazazi wao kwa uja uzito.
‘Sasa wewe tutakaa pamoja hapa kwangu usifikiri chochote kuhusu yaliyopita, utapata kila kitu , pamoja na kusoma. Hapa umefika, ila tu kwa siku hizi chache utakuwa ukinisaidia kazi za nyumbani hadi mfanyakazi wangu atakaporudi.
Hapo ikawa ndio mwanzo wa maisha mapya lakini moyoni alikuwa bado ana donda ndugu la kulipiza kisasi kwa huyu mtu aliyempa ujauzito na kumsababishia akosane na wazazi wake na hajui nini kinaendela husani mama yake. Je yupo hai au alikufa kutokana na kipigo, na je baba yake aliachiwa gerezani au anatumikia kifungo cha mauaji au kujeruhi.
Naona niishie hapa, na kama kuna watu wanataka tuendelee na hii hadithi hadi mwisho basi watoe maoni na nashindwa kuifikisha mwisho kwasababu kila kitu kinahitaji gharama, na internet café ni gharama sana. Kama tukijaliwa tutaingia sehemu ya pili ambayo itaonyesha maisha ya huyu binti na ujauzito, na nini kilitokea kijijini.
Ni mimi: emu-three
4 comments :
Yaani uanataka kutatiza eti kwasababu ya gharama, kwanini usiongee na wenye matangazo wakakufadhili kwa kuweka matangazo yako hapo, mbona vitu unavyoandika vinalipa kabisa.
Huyu aheri emekutana na mama msamaria mwema, wengine wanaishia kujiuza na kugeuka machangu, kisa kinaanzia hapohapo.
Lakini hata hivyo huyo binti alikuwa na tamaa
emu-three wewe ni mkali ile mbaya. Siwezi jua kama hii story umetunga au emetokea kweli. Kwa kweli ni story nzuri na ya mafundisho kwa pande zote mbili, wazazi na mtoto. Sitaweza sema mengi kwa sababu kisa ni cha siku nyingi nilikuwa sikukisoma, leo ndio nimepata nafasi.
Mmmmmh. wewe ni kiboko ile mbaya.
HONGERA SANA, Tupo pamoja.
Nashukuru sana kwa hongera na kisa hicho kimetokea, kama nilivyoainisha kwenye madhumuni ya hii blog ni kuandika matukio na kuyaweka katika hali ya kimafundisho.
Karibu sana na nina visa vingi vimetokea vyenye mafundisho, na kama ningepata muda na vitendea kazi basi ningeviweke hewa ili tupate mafundisho lakini ipo siku mtaviona kimoa baada ya kingine
Post a Comment