Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, July 14, 2010

Uchungu wa mwana-3

Ili uelewe kisa kizima rejea kisa kilichopita kwa kubofya hapa: Uchungu wa mwana-2

  Hakukumbuka alikaa kwa muda gani pale nje ya lile duka, ila kilachomshitua ni kiupepo cha jioni kilichokuwa kikipuliza. Alishangaa huyu jamaa mwenye duka mbona harudi tena. Au kaamua kukimbia. . Aliamua kuondoka na kurudi shuleni. Na huko alimkuta rafiki yake akiwa na wasiwasi mwingi. Alimwambia rafiki yake nini kimemkuta na rafiki yake akamshauri wakaitoe hiyo mimba.


‘Nitoe mimba, hapana huo ni uuaji…hapana ni heri ni…’ akasema huku anaanza kulia.

‘Ukilia itasaidia nini mwenzangu, hilo limekufika, nan i jambo la kawaida, hata mimi niliteseka lakini nikaipa moyo’

‘Ina maana na wewe…’ akashangaa kumsikia mwenzake akitoa ushuhuda.

Lakini hata hivyo hakupenda kabisa wazo hilo la kutoa mimba, lakini baadaye akakubali na kesho yake kwasbabu ilikuwa siku ya jumapili waliongozana hadi hospitali moja ya mtu binafsi, ambayo wengi wao walikuwa wakienda hapo, kuna dakitaro mmoja aitwaye `chinjachinja’. Walimpa jina hilo kwa kazi yake hiyo ya kutoa mimba za wanafunzi kwa siri.

‘Simnajua malipo yake, mumejiandaaje, kwa pesa au kwa namna nyingine, na kwa namana nyingine ujue ni siku tatu na ya nne ndio namaliza kazi.’ Akasema Yule dakitari na ilibidi Yule rafiki yake amueleze mana ya malipo ya namana nyingine kuwa ni malipo ya ngono kwa siku tatu mfululuzo kwa huyo dakitari na siku ya nne ndipo kazi ya kutolewa mimba inapofanyika.

‘Hapana mimi siwezi kabisa kufanya hilo kosa tena, ni heri nimpe hela ya ada kwasababu sijalipa ,halafu nitawadanganya wazazi kuwa nimeibiwa’ akasema Yule binti.

‘Sawa, huo ni uamuzi wako, lakini kama ingekuwa mimi ningejitosa hizo siku tatu kwasababu hakuna tofauti sasa una mimba utakuwa unaogopa kupata nini tena, na hela ya ada itahitajika na sijui wazazi wataamini hilo swala la kuibiwa, lakini sawa, ngoja nikamueleze, wewe nenda jengo lile kule huko ndipo anapofanyia kazi zake’ rafiki yake akaongea kwa kujiamini akionyesha kukomaa kwa kazi hiyo.

Binti Siamini alijikongoja hadi jengo aliloambiwa akakaa kwenye benchi, aliwakuta mabinti wengine wawili ambayo kwa hisia zake alijua na wao walikuwa wakisubiria kufanyiwa kitendo hicho. Na hapo alijipa moyo, kuwa ni kitu rahisi tu. Na mara Yule dakitari alifika na nesi mmoja.
‘Hawa ndio wagonjwa wetu, nataka hii kazi tuifanye chapuchapu, na sitaki makosa’ akasema Yule dakitari akimuelezea Yule nesi ambaye alicheka bila wasiwasi. Na mara majina yakaanza kuitwa, na huyo aliyeitwa akaingia ndani, haikuchukua muda sana akatoka huku analia, na kuondoka zake, na wapili akafuatia.


Je tuendelee,

Hapana naona tukomee hapa ili tujadili kidogo hili swala la kutoa mimba , je ni haki na linafaa kama mtu hataki hiyo mimba, hatuoni kuwa huo ni uuaji. Nasemea kwa mwanafunzi kama huyo aliyepata uja uzito bila kukusudia! Tukumbuke athari zake kama kwa mfano utasema inafaa, kwa wengine itakuwa kama umewaruhusu wafanye hiyo kazi kwani mwisho wa siku likigunguluka anaitoa hiyo mimba, achilia mbali hilo gonjwa, kwani halitoleki kihivyo!

Nasubiri maoni yenu na endelea na sehemu ya nne

Emu three

1 comment :

Anonymous said...

Hii haipo kabisa etu wanafunzi waruhusiwe kutoa mimba ili waendelee na masomo hakuna kabiasa. Huo ni uuaji.
As far as this story concern, its very sad indeed, inasikitisha sana, hebu imalizie tuone itakuwaje?