Naomba uniwekee kero yangu hii kama hutojali!
'Jamani mimi nimechoka, karibu mwaka sasa sipati malipo yangu, kila nikija subiri malipo bado, subiri malipo bado, hivi mnataka mimi nife kwanza ili mali warithi wengine...' Huyu alikuwa jamaa mmoja niliyekutana naye ofisi za NSSF. Nilishindwa kumuelewa kwani hawa jamaa wanatoa matangazo ya mazuri sana kwenye runinga kuwa wanajali wanachama wao katika maisha ya sasa na ya baadaye. Sasa iweje wajali maisha ya baadaye zaidi nikajisemea moyoni.
'Kwani vipi mbona nasikia ukipewa ile miezi sita ya kusubiri , ikiisha basi unapata malipo yako?' tukamdadisi kwani nasi tulikuwa na shaka huenda tukawekwa kwenye tarehe za kusubiri.

'Unajua lazima kila biashara ina matangazo, huenda kweli wana nia hiyo, lakini maneno ni kitu kingine na vitendo ni kitu kingine, na wahenga walisema kizuri kitajiuza tu hata kama hakitajitangaza, au sio. Sisi wanachama hata kama tunakuwa sio haitena ndio tunaotakiwa tukisifie hiki chombo, na sio kijisifie, na sifa yao ni utendaji wao, je wanakidhi hili, au limetokea kwangu, ngoja niwasubiri wenzangu labda mimi nina gundu' Akazidi kulalamika yule jamaa.
Niliingiwa na wasiwasi kwani mimi nilishaweka malengo na vimchango vyangu hivyo, shule zimefunguliwa watoto wanataka ada, na .... Mara nikasikia jina langu likiitwa.
'Ndugu bado, malipo yako hayajawa tayari' yule dada wa hiyo ofisi akaniambia.
Nikakumbuka ile kauli ya yule jamaa, kwani tulifika naye asubuhi saa moja na nusu, tukasubiri hadi saa mbili na nusu ofisi zilipofunguliwa, tuakasaini kitabu cha wageni, tukaingia ndani tukasubiri hadi saa tatu na nusu majina yalipoaanza kuitwa, akaniambia kuwa hapa tunasubiri kupigwa tarehe, hakuna cha malipo au nini. Na kweli tarehe hiyo inakuja.
'Sasa ina maana iweje, nisubiri tena siku ishirini nyingine?' nikauliza
'Utarudii tarehe niliyokuandikia hapo' akasema nakuinagalia ile tarehe, manake nisubiri tena karibu ya mwezi mzima. Nikijumlisha na ile miezi ya nyuma, sijui itakuwa imefikia miezi mingapi. Ukipewa barua ya kwenda kijiweni na mwajiri wako unakaa nyumbani miezi sita, ndipo uende ofisi za hawa jamaa kuomba malipo yako. Fomu zilkisha pokelewa unaandikiwa tarehe mbili za kurudi, ya kwanza unakuja baada kama mwezi hivi kupita, au siku ishirini, unakuja kuangalia kuwa fomu zako hazina matatizo, kama zina mataizo utakuta jina lako ubaoni, utaenda ndani kuelezewa cha kufanya. Kama hazina mataizo unasubiri tena karibu siku 20 hivi kutegemeana na tarehe uliyoandikia, ukija unaweka fomu yako kwenye kiboksi unasubiri kuitwa, kama nilivyoitwa leo mimi hapo unapigwa tena tarehe ya siku ishirini, sijui nikirudi tena siku hiyo nitapigwa tarehe nyingine kama jamaa yangu alivyopigwa tarehe, sijui...namuomba mungu siwe hivyo, ili mafao hayo yanisaidie kwa hapa sio baadaye!
Jamani, hela yenyewe kiduchu, thamani yake inaporomoka kila siku, na unapoitafuta ujue kweli umebanwa, siunajua ubanwa, fikiria ajira zilivyo na shida, umesota nyumbani miezi sita, sasa umeona labda hiyo pesa itaniokoa, angalau nikauze pipi mitaani, unafika unapigwa tarehe, ...
Hatukatai, pesa zinahitaji umakini, lakini dunia ya sasa kila kitu kipo kwenye mtandao, ni vyema mkawa na utaratibu wa kadi kama huo mliokuwa mumebuni, kuwa pesa za mwanachama zinakuwa kama benki ya kuwa kila mwanachama akitaka kuhakiki michango yake inakwenda na kadi anaiona, na kama imefikia hatua ya kulipwa basi hakuna usumbufu tena. Pili njia mbadla ni kutumiana statement mara kwa mara, ili kama kuna mapungufu yahakikiwe mapema.
Samahanini kwa kuiweka hii habari tena, lakini inapobidi lazima tusema, huenda ni udhaifu wa watendaji wachache, huenda ni kweli kuna mapungufu ya kumbukumbu kutoka kwa muajiri, huenda kumbukumbu za muombaji hazijakamalika, lakini ni kwa kipindi gani? Mbona naona ni muda mrefu sana wa kusubiri!
Tukumbuke sana huo usemi kuwa chema huwa kinajiuza kutokana na matendo yake, hakihitaji matangazo.
Ahsanteni
Msitaafu
1 comment :
I'm a writer from Veringenstadt, Germany just sent this onto a colleague who was running a bit of research on this. And she actually ordered me lunch just because I discovered it for her... lol. Actually, allow me to reword this.... Thanks for the food... But anyway, thanx for investing all that time to write about this subject here on your site.
Feel free to visit my weblog - www.amazon.com
Post a Comment