Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, July 14, 2010

Happy birthday:http://miram3.blogspot.com/


                                          HAPPY BITHDAY: http://miram3.blogspot.com/


 Imeshafika mwaka sasa , nakushukuru sana dada Yasinta kwa kunikumbusha hili. Ni kweli tangu siku ile nilipoamua kuondoa uwoga na kuiweka hii blog hewani sasa ni mwaka. Ilikuwepo kabla, lakini nilikuwa nikiandika mambo yangu na kujisomea mwenyewe, lakini baadaye watu wakanishauri, kuwa namimi naweza. Na mwakaa sasa umetimia  tangu niuondoe huwo woga, namshukuru Mungu kwa kunijalia kufanikisha hili.
 Ningependa kuwashukuru nyote ambao mumenipa moyo na kushiriki pamoja nami kuifanikisha blogi hii angalau inaanza kujulikana,  kwani uzuri wa blogi nikuchangiana mawazo. Sitaweza kuwataja wote kwasababu wengi ni Anonymous

 Nia yangu kubwa ni kuandika matukio mengi iwezekanavyo na visa vingi vyenye mafunzo, kwa kupitia lugha yetu ya Kiswahili. Hii ni lugha yetu na wakuitangaza ni sisi wenyewe, kwani chako ni chako, cha mwezio sio chako. Tuipendeni lugha yetu, tuitangaze bila woga na tujivunie nayo.
 Namaliza kwa kusema karibuni nyote, na tusaidianeni wanablogi kwani njia hii ni nyepesi sana kutoa kile kilichopo moyoni mwako, ila tusivuke mpaka nakuharibu nia njema ya waliogundua upeo huu. Na katika kuandika kuna kukoseana , sisi kama tunatuliowakwaza, twaomba msamaha kwani nia yetu ni njema kabisa ya kusaidiana , na kuhurumiana.
Ahsanteni sana

mimi emu-three kwa niaba ya :


7 comments :

Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana kwa kutimiza mwaka na nakutakia kila la kheri na ujue tupo pamoja. UPENDO DAIMA!!

Simon Kitururu said...

Hongera Mkuu!

emuthree said...

Nashukuruni sana wadau na karibuni hapa ni penu, na natumai mtanisaidia pale ninapokwenda kombo, kwani nyie mlishaanza mapema au vipi?

Anonymous said...

Happy birthday blog*3 happy bith 2you! How old are you now...
Hongera sana na natumai umeiva, kwani mwaka mmoja sio haba

KKMie said...

Hongera sana kwa kufikisha mwaka mmoja. Ni hatua kubwa sana kwenye maisha ya mtandaoni.

Mungu akuzidishie nguvu na kukupa muda wa kuendelea Blog yako yenye mambo mengi mazuri.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

HONGERA SANA!!!

emuthree said...

Oh, naendelea kuwashukuru sana wote mlionipa hongera zenu, na wale walioamua kunipa hongera hizo kwa mdomo(live) lakini raha ya blog ni kupewa kwenye blog. Hata hivyo nashukuruni sana na tuendelee kutoa vitu