Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Monday, June 14, 2010
Ukijifanya wajua, utajulishwa...
'Kuna nini, usiniambie na wewe sasa imani ya kidini, na elimu ya Ulaya imekutoka na unataka kuamini ushirikina' nilimdadisi nikitaka kujua zaidi.
'Imani ya dini haiwezi kunitoka, na jinsi unavyojikita katika imani za kidini ndivyo majaribu yanavyokuwa mengi, unaifahamu hiyo...' alisema na kuniangalia kwa macho ya ukali. Nilimtizama naye kwa mtindo huohuo.
'Bwana unaambiwa tembea uone, na ukijifanya unajua unaweza ukajulishwa usiyoyajua. Mimi nilipohamia kwangu niliwakuta bado wenyeji waliokuwepo awali bado wapo, ingawaje sasa wamehama na kuuza maeneo yao, sasa tunaishi wakuja watupu. Hii ni ahueni kwetu, kwani walichotufanyia sie wa awali tutaendelea kuwakumbuka.
'Nilipofika awali nilikaribishwa kwa bashasha na wenyeji wakawa wananitembelea na kuniomba hiki na kile, nami sikuwa na hiana, kumbe wenzangu walikuwa wakija na mambo mengine. Siku za mwanzo tukawa tunaona maajabu, mara mapaka yanalia usiku kucha, mara mbwa mara mapanya ya ajabu. We fikiria paka au panya anapita juu ya paa unafikiri mtu anakanyaga. Sisi hatukujali tukajifanya kama hatujali, ila moyoni tukawa twajiuliza hii ikoje.
'Siku moja mtoto wetu akawa anaongea na mtoto wa jirani, mimi nilikuwa nimejipumzisha ndani, manake mchana unaweza kulala kwa raha kidogo, lakini usiku ukilala unachoka utafiri ulikuwa unabeba mizigo mizito. Wakati kausingizi kananishika nikashtuka niliposikia kauli ya yule mtoto wa jirani.
'Jana usiku tulikuwa tunasherehe na bibi, kwenye ule mti mkubwa karibu na makaburi. Wewe ulikuwa ukipiga ngoma, na mama yako alikuwa akicheza uchi huku baba yako akiwa kiti cha bibi yangu...bibi alikuwa akila nyama chafu, wanasema za wafu...mimi sikupenda lakini bibi alikuwa akitulazimisha tule. Nilipoamuka bibi aliniita akasema, ulichoona jana ukisema nitakufinya...' sautu ya yule mtoto alipenya kichwani kama sindano na kunifanya niishiwe nguvu, na mara usingizi ukanishika. Ndani ya huo usingizi nikaota ndoto ya ajabu.
Nilikuwa na upanga wa moto, upanga huo alinipa maalimu mmoa, katika ndoto akasema ukiwa nao huo hutadhurika na hakikisha unatembea nao kila siku. Basi ndani ya ndoto nikapita kwenye mti ambao upo makaburini, nikawakuta majirani zangu wamekaa, waliponiona wakaanza kunijia kwa hasira wakisema wewe sasa unaanza kuingilia mambo yetu tutakuonyesha sisi nani. Nikakumbuka ule upanga, nikauchomoa, ile kuuchomoa tu, watatu kati ya wale majirani wakaanguka chini, nikaanza kupambana nao bila huruma, niliwafyeka bila huruma na wote wakawa wamelala chini hoi. Mara nikashituka toka usingizini.
Kilichonishitua ni kelele za majirani. Nikakurupuka mbio kuelekea nje, nilipofika kwa jirani yetu nikasikia hali ni mbaya sana wanampeleke kwao kitu kama Bagamoyo, siijui ni huko au kuna mji unaofanana na huo.
Nilimuhadithia mke wangu naye akanipa kisa ye tangu awe anasoma ile dua kabla ya kulala amekuwa akipmbana na hawo watu kwenye ndoto, lakini kila akiamuka anasahau kuniambia. Na kila siku ikawa mapambano , ninawafyeka ile mbaya na haikupita muda mara huyu kahama yula kahama mapaka majirani niliowakuta awali wote wakawa wameondoka.
'Ndugu yangu, lakini vituko vilivyotokea awali ni vya kutisha na hadi siku nipozidiwa ndipo nilipomtembelea huyo maalimu akaamua kuja nyumbani na kutosema dua na maombi mbalimbali na kutuomba kila tukilala tuwe tunasoma baadhi ya dua na kuomba hifadhi ya Mungu, na kweli huoo ukawa ndio upanga wetu na huo ukawa mwisho wa mateso...' akamalizia rafiki yangu.
Mimi nilishangaa kwani rafiki ninayemuongelea ni msomi, alikuwa Ulaya na kurudii karibuni, yeye na familia yake ni kama wazungu ukienda kwao, sasa kunihadithia habari kama hii niliingiwa na wasiwasi kuhisiana na imani hizi. Kwanza nilijarinu kuwaza ni nini faida yake, na je wanaofanya hivyo hawamuogopi Mungu. Na e kwanini kama vitu hivyo vipo kama vile kutembea na ungo, kwanini wasivifanye kiutaalamu watu wakatumia usafiri huo kwa faida. Hebuu jaribu kufikiria kama watu watatembea ungo kuna haja gani ya ndege. Wabuni hizo taaluma na kuziweka kisasa, au mnasemaje wenzangu, au ...
Ninani aliwahi kukutana na hivyo vibweka?
From miram3
1 comment :
Acheni imani za kishirkina, na waoamini hayo watashindwa kwa jina la Yesu, mimi nitawaombea mapepo mabaya yawaondoke...washindwe na walegee
Post a Comment