Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, June 16, 2010

Kila mchuma janga...

Wengi hawakuamini pale kijana mtukutu alipoanza kujenga nyumba yake, lakini wale wanaoijua tabia yake waliguna kwa mashaka, hiyo hela kaipatia wapi, au isije ikawa ndio hiyo biashara ya madawa ambayo wengi walihisi kuwa huenda anaifanya. Wenye nia njema waliwafuata wazazi wa kijana huyu na kuwaomba wamdadisi vyema kijana wao asije akaingia kwenye lindi la maangamizi.
'Nyie vipi, kijana wetu alipokuwa mitaani akihangaika na maisha mkasingizia wizi, mkamkashifu sasa ameibuka na ana hali nzuri mumebadilika na kuanza mengine, hamchoki jamanai, mwataka nini na kijana wangu..' akalalama mama mtu.
'Sio hivyo mama mtukutu, wote ni wazazi na huwa tunajali watoto wote, na pale tunapoona kuna walakini lazima tuseme , huo ndio wajibu wa kila mzazi.' akasema mama busara.
'Kwahiyo mnataka kusema nini, tumwambie aache kujenga nyumba arudie uchokoraa' akasema baba mtu.
'Hamjatuelewa na hamtaki kutuelewa, jambo jema ni kuchunguza nyendo za mwanenu, mjue kweli mali anayopata anaipata kihalali, kwasababu leo mnafurahia matunda ya mwanenu ambayo hamjui kayachumaje au kayachumia wapi, kesho mnaweza mkayajutia kwani kila mchuma janga hula na wakwao.' akasema mama busara.
 Baba mtu alitafakari kwa kina maneno yale, alikumbuka jinsi jana alivyomueleza mkewe kuhusiana na mabadiliko ya mtoto wao, walibisha sana na mkewe, na kama ujuavyo akina mama huwapenda sana watoto wao na hawapendi kuona mtoto akiambiwa ana tabia chafu. Waliishia kusema wavute subira, kwani subira huvuta heri.
 Kijana mtukutu, alijenga nyumba yake na mara akanunua gari, mara akaanzisha kampuni , mara akawa anajenga vitu vya kusaidia wasiojiweza , mara akajenga hospitali. Ikafika mahala watu wakaanza kumkubali, ila werevu waliguna wakasema, twamjua alikotoka, kwani chema hujiuza na kibaya huitembeza, mwenye kovu haambiwi kapona. Mara kijana kajiunga kwenye siasa, kaanza kampeni. Na tunavyosikia katika majina yaliyopendekezwa jina lake limo. Na huenda uchaguzi ujao atakuwa mmoja wa wagombea, na uwezekano wa kupita ni mkubwa, siunajua tena. ...
 Maongezi ya jamaa huyu yalinifanya nitafakari kuhusiana na uchagusi ujao, wengi wa wagombea tunawajua, sidhani kama ataletwa mgombea kutoka kusipojulikana, ni wakati sasa wa kuwachunguza wagombea wetu tabia zao toka utotoni, shuleni na makazini. Tabia zao za kila siku, mienendo yao ya kimaisha tunaifahamu. Nasema hivi kwasababu hizo tabia na mienendo yao ndiyo itakayotuonyesha uimara na uadilifu wa kiongozi tunayemtaka. Usidanganyike na mabadiliko ya muda mfupi, kwani tabia haijifichi, na tabia haibadiliki mara moja, na wengi huficha makucha yao wakiwa wanatafuta. Tukumbuke sana huo usemi wa `kila mchumia janga hula na wakwao...'
From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Sasa unaanza kutupa vionjo ambavyo wengi wanapenda. Unajua wapenzi wengi wa blog wanapenda picha, sio maneno sana, sijui kwanini!